Swali: Niliingia msikitini na imamu ndio punde ameinuka kutoka kwenye Rukuu´ ambapo nikasema “Allaahu Akbar” kisha nikarukuu na kukamilisha swalah yangu pamoja na imamu na nikatoa salamu. Ni kipi kinachonilazimu?
Jibu: Ni lazima kwako kuirudi swalah yako mwanzo. Hakuiwahi Rukuu´. Mwenye kupitwa na Rukuu´ basi amekwishapitwa na Rakaa´. Mwanamke huyu – kwa mujibu wa swali lake – hakuswali swalah kamilifu. Kwa sababu Rakaa´ ambayo hakuwahi Rukuu´ yake hakuiwahi. Ni wajibu kwake kuirudi swalah yake.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2RA6j0O
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni