SWALI:
Nini shari'ah ya kiislamu kwa wanawake kuvaa nguo za wazi kabisa wanapohudhuria harusi, Kama kanzu fupi zinazoonyesha miguu au mikono yote kuwa wazi au kuvaa bega na moja liko wazi, baadhi ya au kifua kuwa wazi, au kanzu kumbana (tight) hadi mwili wote viungo vyake vinaonekana, au mgongo kuwa wazi n.k. Je inaruhusiwa kwa vile wako mbele ya wanawake wenzao? ipi mipaka ya mavazi baina Yao?
Ni kweli kwamba 'awrah ya wanawake mbele ya wanawake wengine ni kutoka kitovu cha magoti?
Tumesikia kwamba 'awrah (uchi) wa mwanamke mbele ya wanawake wengine ni kutoka kitovu na magoti. Je hili ni sahihi?
Haswa katika makumbi ya sherehe tunaona wanawake wanaokuja –Tunamuomba Allaah Atulinde na Atupe afya– wanakuja huku wamevaa nguo fupi au mtu anaona vuliomo ndani ya nguo, au mavazi na miundo ya kukatwa ambazo inaonyesha ndama zao, au wao wanavaa nguo za kuonyesha mwili ndani kabisa, au vazi linaloonyesha sehemu ya kifua au sehemu ya nyuma wazi... Hivyo wanawake Waislamu wanatoka nje na wanaonekana kama wachezaji sinema katika nchi za kikafiri au mavazi mabaya kwenye sinema na televisheni. Na tunawaambia kutofanya hivyo, wanasema hakuna ubaya wowote kwa hilo, kwa kuwa 'awrah ya wanawake ni kutoka kitovu hadi magoti. Hayaa imetoweka kabisa na wanawake wamekuwa wanawaiga makafiri, na tatizo hili limefikia kiwango kikubwa mno. Tafadhali tunaomba ushauri wenu, Allaah Awalipe.
JIBU:
AlhamduliLLaah,
Mwanamke yeye wote (mwili wake wote) ni 'awrah mbele ya wanaume ambao si Mahram zake (anayeweza kumuoa), na haijuzu kwake kuonekana mbele ya wanaume hata kama atakuwa ni mwenye kujisitiri, kwa kuhofia fitnah kwa kumuangalia na kuona jinsi ni alivyo na jinsi anavyotembea. Kuhusiana na lililosemwa kuhusu 'awrah ya mwanamke mbele ya wanawake wenziwe kuwa ni kutoka kitovu hadi magoti, hii inatumika tu wakati atakuwa kwenye nyumba yake miongoni mwa dada zake na wanawake ambao anaishi nao.
Kanuni za msingi bado zinasisitiza asitiri mwili wake wote ili achukuliwe kama kiigizo bora na haya mazoea maovu yameenea miongoni mwa wanawake. Vile vile, anapaswa kusitiri uzuri wake mbele ya mahram wake na wanawake wageni ili baadhi ya mahram wake wavutiwe (waathirike) nae kitabia na adabu, au ili baadhi ya wanawake wasije kwenda kumuelezea yeye wasifu wake kwa wengine (wanaume). Imeripotiwa katika Hadiyth kuwa Mtume (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:
"Haitakiwi mwanamke kumuelezea mwanamke mwengine kwa mume wake, hivyo ni kama (mumewe) anamuona yeye" Kinachomaanishwa ni kuwa uzuri wake, kama vile kifua chake, mabega yake, tumbo lake, nyuma, mikono yake, shingo yake na ndama yake inakuwa wazi, kila mtu anaona kwamba ni jambo lisiloweza kuepukwa, mtu kuwa na hisia yake.
Na ni kawaida wanawake huelezea juu wa waliyoyaona kwa familia zao, sawa wanamume na wanawake. Hivyo mwanamke anaweza kutaja hayo mbele ya watu ambao si Mahram wake, kwa namna ambayo inaweza kuwafanya wao kuvutiwa kwake [huyo mwanamke], au ambayo inaweza kusababisha watu wabaya kutafuta njia kuanzisha uhusiano naye.
Kwa sababu hii, wanawake wanatakiwa kufunika 'awrah [sehemu zisizotokiwa kuonekana katika miili] yao - kama vile vifua vyao, migongo, mikono, ndama, n.k, - vile vile hata mbele ya mahram wake na wanawake wengine.
Kujisitiri huku kunakuwa muhimu zaidi katika sehemu za makundi, maeneo ya sherehe, hospitali, na mashule, hata kama kutakuwepo wanawake tu, kwa sababu baadhi ya wanaume ambao si Mahram na hata vijana wanaweza kuwaona au kuwachukua picha hali ya kuwa hawana stara zao kamili, na hiyo itakuwa ni sababu ya fitnah kwa wale wanaowaona.
Onyo kali imetolewa kwa wale [wanawake] ambao wanajionyesha na wavaao nguo za kuonyesha au za kubana, wakati Mtume (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam) aliposema:
”Aina mbili za watu wa motoni siwaoni... Wanawake ambao wamevaa lakini wako uchi, wanawashawishi wanaume wawatongoze, na wanaelekea kwao (kwa kuwa warahisi). Vichwa vyao kama nundu za ngamia zinazoyumba (aina ya msuko wa nywele wanaosuka wanawake). Hawataingia Peponi wala hawatasikia harufu yake ingawa harufu yake inaweza kunuswa kutoka masafa kadhaa na kadhaa” [Muslim]
Kinachomaanishwa ni kwamba wamevaa nguo za kuonyesha au nguo za kubana ambazo zinaonyesha maumbile yao, au kunapokuwepo fursa ya ajira kwenye kampuni ambayo [mavazi yao] huonyesha vifua vyao, matiti yao na sehemu zingine zisizofaa kabisa kuonekana. Hili limeenea katika makundi na katika mikusanyiko ya ujumla yote. Na Allaah Anajua zaidi.
[Shaykh 'Abdullaah bin 'Abdir-Rahmaan al-Jibriyn]
Na Allaah anajua zaidi
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2TM7Sp8
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni