Translate

Jumanne, 1 Januari 2019

79. Matamshi ya pili ya kumswalia Mtume

2-

اللهم صل على محمد و على آل محمد كما صليت على [إبراهيم و على]آل إبراهيم، إنك حميد مجيد. اللهم بارك على محمد و على آل محمد كما باركت على [إبراهيم و على]آل إبراهيم، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyomsifu [Ibraahiym na] [1] jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa. Ee Allaah! Mbariki Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki [Ibraahiym na] jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”[2]

[1] Nyongeza hizi mbili zimethibiti kwa al-Bukhaariy, al-Bayhaqiy, Ahmad na an-Nasaa’iy. Wamezitaja pia katika mapokezi mengine, kama ilivyo katika lile tamko la tatu na la saba yanayokuja huko mbele. Hivyo usidanganyike na maneno ya Ibn-ul-Qayyim katika ”Jalaa’-ul-Afhaam” akifuata maoni ya mwalimu wake Ibn Taymiyyah katika “Majmuu´-ul-Fataawaa” (16/01):

“Hakukupokelewa Hadiyth yoyote Swahiyh ambayo imetaja “Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym” kwa pamoja.” (Uk. 198)

Hivi sasa nimekutajia Hadiyth Swahiyh juu ya hilo. Hilo ni miongoni mwa faida za kitabu hiki. Ndani yake kimeyaandama mapokezi na matamshi kwa umakini kabisa na kuoanisha baina yake. Uandamaji kama kama huo haujawahi kufanywa hapo kabla,ni fadhilah kutoka kwa Allaah (Ta´ala). Kitu kinachothibitisha kosa la Ibn-ul-Qayyim ni kwamba yeye mwenyewe amesahihisha tamko la saba linalokuja huko mbele na akakataa baadhi ya mambo ndani yake.

[2] Ahmad, an-Nasaa’iy na Abu Ya´laa katika ”al-Musnad” (2/44) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2F161th
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...