Translate

Alhamisi, 3 Septemba 2020

200-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Ribaatw Fiy SabiliLLaah

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Fadhila Za Ribaatw  Fiy SabiliLLaah

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٢٠٠﴾

200. Enyi walioamini! Subirini na zidini kuvuta subira na bakieni imara na mcheni Allaah ili mpate kufaulu.

 

Mafunzo:

 

Baadhi Ya Maana Ya Ribaatw: 

 

Kwanza:  Kubakia kuchunga mipaka katika Jihaad fiy SabiliLLaah

Pili:          Kubakia katika ‘Ibaadah baina ya Swalaah Na Swalaah ya pili.

 

Fadhila za Ribaatw: Sahl bin Sa’ad (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ar-Ribaatw (Kubakia kuchunga mipaka) kwa ajili ya Allaah siku moja ni bora kuliko dunia na vilivyomo. Na sehemu (ndogo kabisa) ukubwa wa  kuweka fimbo ya mmoja wenu Jannah ni bora kuliko dunia na vilivyomo. Na juhudi ya kutoka jioni anakotoka mja katika njia ya Allaah au asubuhi ni bora kuliko dunia na vilivyomo.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Pia: “Ribaatw ya siku moja na usiku wake ni bora kuliko kufunga mwezi mzima na qiyaam chake (kisimamo cha kuswali usiku), na mtu akifa (akiwa katika ribaatw), ‘amali zake zitaendelea kuandikwa na riziki yake ataendela kupata na atasalimika na fitnah (za kaburi).”  [Muslim].

 

 

 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...