Translate

Alhamisi, 3 Septemba 2020

075-Asbaab Nuzuwl: An-Nahl - Allaah Amepiga Mfano Wa Mja Aliyemilikiwa Hana Uwezo...

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

016-Suwrah An-Nahl Aayah 75 - 76

 

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَمَن رَّزَقْنَاهُ مِنَّا رِزْقًا حَسَنًا فَهُوَ يُنفِقُ مِنْهُ سِرًّا وَجَهْرًا ۖ هَلْ يَسْتَوُونَ ۚ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٧٥﴾

Allaah Amepiga mfano wa mja anayemilikiwa hana uwezo juu ya chochote na (mwengine) ambaye Tumemruzuku kutoka Kwetu riziki nzuri; naye anatoa katika humo kwa siri na dhahiri. Je, wanalingana sawa? AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah!). Bali wengi wao hawajui.

 

 

وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَاهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ ۖ هَلْ يَسْتَوِي هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ ۙ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٧٦﴾

Na Allaah amepiga mfano (mwingine) wa watu wawili; mmoja ni bubu asiye na uwezo juu ya chochote naye ni mzigo kwa bwana wake, popote unapomuelekeza haleti khayr. Je, analingana sawa yeye na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko juu ya njia iliyonyooka? [An-Nahl: 75-76]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

عن ابن عباس في قوله عز وجل ((ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلاً عَبْداً مَمْلُوكاً ..))  قال: نزلت في رجل من قريش وعبده، وفي قوله ((مَثَلًا رَجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لا يَقْدِرُ عَلَى شَيْءٍ)) إلى قوله ((وَهُوَ عَلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ)). قال هو عثمان بن عفان، قال: والأبكم الذي أينما يوجهه لا يأتي بخير، ذاك مولى عثمان بن عفان كان عثمان ينفق عليه ويكفله ويكفيه المؤونة، وكان الآخر يكره الإسلام ويأباه، وينهاه عن الصدقة والمعروف فنزلت فيهما.

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kuhusu Kauli ya Allaah:

ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا  

Allaah Amepiga mfano wa mja anayemilikiwa…

 

Amesema imeteremka kuhusu mtu katika Quraysh na mtumwa wake. 

 

Na kuhusu Kauli Yake:

مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ

Mfano (mwingine) wa watu wawili; mmoja ni bubu asiye na uwezo juu ya chochote…

 

mpaka kauli Yake:

وَهُوَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ

naye yuko juu ya njia iliyonyooka.

 

Amesema: “(Aaliyekusudiwa) huyo ni ‘Uthmaan bin ‘Affaan.”

 

Akasema pia: “Na bubu ambaye popote unapomuelekeza haleti khayr, huyo ni mtumwa wa ‘Uthmaan, alikuwa ‘Uthmaan akimhudumia matumizi yake na kumdhamini, na kumtosheleza chakula chake. Na yule (mtumwa) mwengine (wa Aayah iliyotangulia) alichukia Uislamu na akaukanusha na akimzuia (bwana wake) asitoe Swadaqah na kutokufanya wema, zikateremka (Hizo Aayah) kuhusu wao wawili:

 

[Imaam Al-Muqbil amerekodi Ibn Jariyr (4/151) na watu wake ni watu Swahiyh]

 

Na pia,

 

عن إبراهيم، عن عكرمة، عن ابن عباس قال: نزلت هذه الآية ((ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلاً عَبْداً مَمْلُوكاً لا يَقْدِرُ عَلَى شَيْءٍ )) في هِشَامِ بْنِ عَمْرٍو، وَهُوَ الَّذِي يُنْفِقُ مَالَهُ سِرًّا وَجَهْرًا، وَمَوْلَاهُ أَبُو الْجَوْزَاءِ الَّذِي كَانَ يَنْهَاهُ وَنَزَلَتْ (( وَضَرَبَ اللَّهُ مَثَلاً رَجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لا يَقْدِرُ عَلَى شَيْءٍ )) فَالْأَبْكَمُ مِنْهُمَا الْكَلُّ عَلَى مَوْلَاهُ هُوَ أُسَيْدُ بْنُ أَبِي الْعِيصِ، وَالَّذِي يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَهُوَ عَلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ هُوَ عُثْمَانُ بْنُ عَفَّانَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ

Kutoka kwa Ibraahiym kutoka kwa Ikrimah kutoka kwa Ibn ‘Abbaas amesema: Zimeteremka Aayah hizi mbili:

ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ

Allaah Amepiga mfano wa mja anayemilikiwa hana uwezo juu ya chochote…

 

Kumhusu Hishaam ambaye alikuwa akitoa mali yake kwa siri na kwa dhahiri na  mtumwa wake Abu Al-Jawzaaiy alimzuia asifanye hivyo, basi ikateremka:

 

وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَاهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ ۖ هَلْ يَسْتَوِي هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ ۙ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٧٦﴾

Na Allaah amepiga mfano (mwingine) wa watu wawili; mmoja ni bubu asiye na uwezo juu ya chochote naye ni mzigo kwa bwana wake, popote unapomuelekeza haleti khayr. Je, analingana sawa yeye na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko juu ya njia iliyonyooka? [An-Nahl: 75-76]

 

Na aliyekuwa bubu ni mmojawapo kati ya wawili, na aliye mzigo kwa bwana wake ni Asyad bin Abiy Al-‘Iysw. Na yule ambaye anaamrisha uadilifu naye yuko juu ya njia ya kunyooka ni ‘Uthmaan bin ‘Affaan (رضي الله عنه).

[Abul-Hasan ‘Aliy Ibn Ahmad Al-Waahidi An-Naysaaburiy]

 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...