أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
016- Suwrah An-Nahl Aayah: 110
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُوا مِن بَعْدِ مَا فُتِنُوا ثُمَّ جَاهَدُوا وَصَبَرُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٠﴾
Kisha hakika Rabb wako, kwa wale waliohajiri baada ya kutiwa katika mitihani, kisha wakafanya jihaad na wakasubiri; hakika Rabb wako baada ya hayo bila shaka ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [An-Nahl: 110]
Sababun-Nuzuwl:
عن ابن عباس قال: كان قوم من أهل مكة أسلموا وكانوا يستخفون بالإسلام، فأخرجهم المشركون يوم بدر معهم، فأصيب بعضهم وقتل بعض، فقال المسلمون: كان أصحابنا هؤلاء مسلمين وأكرهوا فاستغفروا لهم فنزلت ((إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلائِكَةُ ظَالِمِي أَنْفُسِهِمْ)) إلى آخر الآية. قال: وكتب إلى من بقي بمكة من المسلمين هذه الآية لا عذر لهم قال: فخرجوا فلحقهم المشركون فأعطوهم الفتنة فنزلت هذه الآية ((وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّهِ فَإِذَا أُوذِيَ فِي اللَّهِ جَعَلَ فِتْنَةَ النَّاسِ كَعَذَابِ اللَّهِ)) إلى آخر الآية. فكتب المسلمون إليهم بذلك فخرجوا وأيسوا من كل خير ثم نزلت فيهم ((ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُوا مِنْ بَعْدِ مَا فُتِنُوا ثُمَّ جَاهَدُوا وَصَبَرُوا إِنَّ رَبَّكَ مِنْ بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَحِيمٌ)) فكتبوا إليهم بذلك إن الله قد جعل لكم مخرجا ، فخرجوا فأدركهم المشركون فقاتلوهم ثم نجا من نجا وقتل من قتل.
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba kulikuwepo watu wa Makkah waliosilimu wakawa wanaficha Uislamu wao. Washirikina wakawatoa siku ya vita vya Badr pamoja nao, na wakajeruhiwa baadhi yao na wengineo wakauawa. Waislamu wakasema: “Hawa walikuwa marafiki zetu wa Kiislamu.” Basi walilazimishwa (kutoka kupigana), wakawaombea maghfirah ikateremka:
إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿٩٧﴾
Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamejidhulumu nafsi zao; (Malaika) watawaambia: Mlikuwa katika hali gani? Watasema: Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi. (Malaika) Watasema: Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni Jahannam, na uovu ulioje mahali pa kuishia [An-Nisaa: 97]
Akasema: Ikatolewa hukumu kwa Waislamu waliobakia Makkah kuwa hawana udhuru kutokana na Aayah hii. Wakatoka, wakakutana na washirikina wakawatia katika fitnah (mitihani) ikateremka Aayah ifuatayo:
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ فَإِذَا أُوذِيَ فِي اللَّـهِ جَعَلَ فِتْنَةَ النَّاسِ كَعَذَابِ اللَّـهِ وَلَئِن جَاءَ نَصْرٌ مِّن رَّبِّكَ لَيَقُولُنَّ إِنَّا كُنَّا مَعَكُمْ ۚ أَوَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَعْلَمَ بِمَا فِي صُدُورِ الْعَالَمِينَ ﴿١٠﴾
Na miongoni mwa watu wako wasemao: Tumemwamini Allaah; lakini wanapoudhiwa kwa ajili ya Allaah, hufanya fitnah za watu kama kwamba ni adhabu ya Allaah. Na inapowajia nusura kutoka kwa Rabb wako husema: Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi. Je, kwani Allaah Hayajui yale yaliyomo katika vifua vya walimwengu? [Al-‘Ankabuwt: 10]
Wakaandikiwa hukumu Waislamu kwa hayo, wakatoka na wakaacha kufanya kheri zote ikawateremkia:
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُوا مِن بَعْدِ مَا فُتِنُوا ثُمَّ جَاهَدُوا وَصَبَرُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٠﴾
Kisha hakika Rabb wako, kwa wale waliohajiri baada ya kutiwa katika mitihani, kisha wakafanya jihaad na wakasubiri; hakika Rabb wako baada ya hayo bila shaka ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [An-Nahl: 110]
Wakaandikiwa hukumu kwa hiyo kwamba Allaah Amekujaalieni njia. Wakatoka wakakutana na washirikina wakapigana, na baadhi kuuwawa na baadhi kupona.
[Ibn Jariyr]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni