Translate

Ijumaa, 11 Septemba 2020

103-Asbaab Nuzuwl: An-Nahl: Kwa Yakini Tunajua Wasemayo Kuwa Kuna Mtu Anamfundisha...

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

016- Suwrah An-Nahl Aayah: 103

 

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ ۗ لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ﴿١٠٣﴾

Na kwa yakini Tunajua kwamba wao wanasema: Hakika hapana isipokuwa mtu anamfundisha (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم Qur-aan). Lisani wanayomnasibishia nao ni ya kigeni, na hii ni lisani ya Kiarabu bayana. [An-Nahl: 103]

 

 

Sababun-Nuzuwl:   

 

 

عَنْ عَبْد اللَّه بْن مُسْلِم الْحَضْرَمِيّ قال:  كَانَ لَنَا غُلَامَانِ نَصْرَانِيَّانِ مِنْ أَهْلِ عَيْنِ التَّمْرِ، اسْمُ أَحَدِهِمَا يَسَارٌ وَاسْمُ الْآخَرِ جَبْرٌ ، وَكَانَا يَقْرَآنِ كِتَابًا لَهُمْ. (التَّوْرَاةَ) فَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم  يَمُرُّ بِهِمَا وَيَسْمَعُ قِرَاءَتَهُمَا، وَكَانَ الْمُشْرِكُونَ يَقُولُونَ: يَتَعَلَّمُ مِنْهُمَا، فَأَنْزَلَ اللَّهُ هَذِهِ الْآيَةَ:

لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ﴿١٠٣﴾

 

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Muslim Al-Hadhwramiyy amesema:  Tulikuwa na  vijana wawili Manaswara kutoka Watu wa ‘Ayn At-Tamar, mmojawapo akiitwa Yasaar na mwenginewe Jabr, na walikuwa wakiwasomea Kitabu (Tawraat) na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiwapitia na kuwasikia Qiraa chao, basi washirikina wakawa wanasema:  “Anajifunza kutoka kwa hao wawili.”  Hapo Allaah Akateremsha:

 لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ﴿١٠٣﴾

Lisani wanayomnasibishia nao ni ya kigeni, na hii ni lisani ya Kiarabu bayana.

 

[Qurtwubiy – Jaami’ Ahkaam Al-Qur-aan, Ibn Jariyr]

 

 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...