إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ
Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!
14 -Kuvaa Kitu Kwa Ajili Ya Kinga
Itikadi za watu kuvaa vitu au kujifunga navyo mwilini kwa kuepusha au kujikinga na kijicho, husda na madhara mengineyo. Jambo hili halijuzu kwa sababu hivyo vitu havina uwezo wa hayo wala hakuna atakayeweza kumuondoshea mtu madhara isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Anasema:
وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧﴾
Na Allaah Akikugusisha kwa dhara, basi hakuna yeyote wa kukuondolea hiyo isipokuwa Yeye; na Akikugusisha khayr, basi Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. [Al-An’aam: 17]
Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameharamisha hayo katika Hadiyth mbali mbali:
عَنْ قَيْسِ بْنِ السَّكَنِ الأَسَدِيِّ قَالَ: دَخَلَ عَبْدُ اللهِ بْنُ مَسْعُودٍ رضي الله عنه عَلَى امْرَأَةٍ، فَرَأَى عَلَيْهَا خَرَزًا مِنَ الحُمْرَةِ، فَقَطَعَهُ قَطْعًا عَنِيفًا، ثُمَّ قَالَ: إِنَّ آلَ عَبْدِ اللهِ عَنِ الشِّرْكِ أَغْنِيَاءُ، كَانَ مِمَّا حَفِظْنَا عَنِ النَّبِيِّ صلّى الله عليه وسلّم: ((إِنَّ الرُّقَى وَالتَّمَائِمَ وَالتِّوَلَةَ شِرْكٌ)) رواه الحاكم وقال: " صحيح الإسناد "، ووافقه الذّهبي والألبانيّ في "الصّحيحة" (برقم 331).
Imepokelewa kutoka kwa Qays bin As-Sakan Al-Asadiyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Abdullaah bin Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliingia kwa mwanamke ambaye alivaa shanga nyekundu, akazikatilia mbali kisha akasema: “Hakika ahli ya ‘Abdullaah hawahitaji shirki!”. Akasema pia: “Katika ambayo amehifadhi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni: ((Hakika Ar-Ruqaa (zisizothibiti), At-Tamaaim, At-Tiwaalah ni shirki).)) [Al-Haakim amesema Isnaad Swahiyh na ameikubali Adh-Dhahabiy na Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah (331)]
At-Tamaaim: Wanachofungwa watoto (kama kitambaa cheusi au nyuzi n.k.) shingoni (au mkononi) kukinga jicho baya.
Ar-Ruqaa au Al-‘Azaaim: Ni tabano au azima inayosomwa. Imeruhusiwa tu inapokuwa haina shirki. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameiruhusu inapokuwa hali ya kudonelewa na mdudu sumu au anapopatwa mtu na jicho baya (au husda) au homa.
At-Tiwaalah (mvuto wa ndere): Kinachodaiwa kuwa kinasababisha mwanamke apendwe zaidi na mumeme au mume apendwe zaidi na mkewe.
Hadiyth nyenginezo zinazoharamisha kuvaa vitu kwa ajili ya kinga ni zifuatazo:
عَنْ أَبِي بَشِيرٍ الأَنْصَارِيِّ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) أَنَّهُ كَانَ مَعَ رَسُولِ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي بَعْضِ أَسْفَارِهِ، فَأَرْسَلَ رَسُولاً, أَنْ ((لاَ يَبْقَيَنَّ فِي رَقَبَةِ بَعِيرٍ قِلادَةٌ مِنْ وَتَرٍ أَوْ قِلادَةٌ إِلاَّ قُطِعَتْ)).
Imepokewa kutoka kwa Abu Bashiyr Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba alikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika safari mojawapo. Akamtuma mjumbe kuamrisha kwamba: ((Kusiachwe kidani cha uzi au kidani chochote katika shingo za ngamia isipokuwa kikatwe)). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Pia:
رَوَى أَحْمَدُ عَنْ رُوَيْفِعٍ قَالَ؛ قَالَ لِي رَسُولُ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((يَا رُوَيْفِعُ، لَعَلَّ الْحَيَاةَ سَتَطُولُ بِكَ؛ فَأَخْبِرِ النَّاسَ أَنَّ مَنْ عَقَدَ لِحْيَتَهُ، أَوْ تَقَلَّدَ وَتَرًا، أَوِ اسْتَنْجَى بِرَجِيعِ دَابَّةٍ أَوْ عَظْمٍ؛ فَإِنَّ مُحَمَّدًا بَرِيءٌ مِنْهُ))
Ahmad amepokea kutoka kwa Ruwayfi’ ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameniambia: ((Ee Ruwayfi’! Huenda ukaishi zaidi baada yangu. Kwa hiyo wajulishe watu kwamba: Yeyote atakayefunga fundo ndevu zake, au akaweka nyuzi au mshipi shingoni mwake [kuwa ni talasimu] au akastanji na mkojo wa mnyama au mfupa, basi Muhammad amejitenga naye)). [Ahmad, Abuu Daawuwd]
Vitu ambavyo aghlabu hutumiwa na watu kuvivaa au kujifunga wakiamini vinawakinga:
a) Hirizi za vitambaa vyenye maandishi ndani ikiwa ya Quraan au mengineyo.
b) Mtoto mchanga kupakwa masinzi au wanja usoni au kuandikwa Jina la Allaah!
c) Kuwapaka watoto wachanga wanja usoni na nakshi za nyota na mwezi, kwa kuamini ule wanja unazuia 'ayn (kijicho).
d) Anapolazwa mtoto mchanga kukiwa chini ya mto wake vitu kama kisu, ndimu n.k.
e) Kuvalishwa vyuma mkononi.
f) Kuvalishwa mtoto mchanga au hata wakubwa, kidani chenye lakti ya Aayatul-Kursiy au Jina la Allaah! Ni jambo linalotendwa na wengi! Hakika ni kosa kubwa kwani ni kudhihirisha kutokumadhimisha Allaah kwa sababu kidani hicho anaingia nacho mtu chooni. Juu ya hivyo ni kuitakidi kuwa kinamkinga mtu na shari, uhasidi, jicho n.k. Imeshatangulia Hadiyth mbali mbali na Fataawa za ‘Ulamaa kukataza haya, na rejea mlango wa “Kutundika vitu”.
g) Kuvalishwa kitambaa cheusi mkononi wengine wanatia mvuje ndani yake yenye harufu mbaya kuepusha majini.
h) Mapambo yenye kuandikwa Aayah za Qur-aan:
i) Mapambo ya vijiwe vya rangi ya buluu, vinginevyo vina jicho.
j) Kuvaa pete au mapambo yenye vito rangi kadhaa kwa kuitakidi rangi hizo zina maana ya wanachoita ‘bahati nzuri’ au kuleta hali fulani njema kutokana na tarehe au miezi ya kuzaliwa:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni