Translate

Alhamisi, 17 Septemba 2020

08-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Njaa Ilimtoa Nje

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

08-Zuhd Yake: Njaa Ilimtoa Nje

 

Alhidaaya.com

 

 

Siku moja au usiku mmoja, pindi njaa ilipomzidi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka nje, akakutana na Swahaba zake ambao nao pia wametoka nje kwa sababu ya kubanwa na njaa:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ أَوْ لَيْلَةٍ فَإِذَا هُوَ بِأَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ فَقَالَ ‏"‏ مَا أَخْرَجَكُمَا مِنْ بُيُوتِكُمَا هَذِهِ السَّاعَةَ ‏"‏ ‏.‏ قَالاَ الْجُوعُ يَا رَسُولَ اللَّهِ ‏.‏ قَالَ ‏"‏ وَأَنَا وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لأَخْرَجَنِي الَّذِي أَخْرَجَكُمَا قُومُوا ‏"‏ ‏.‏ فَقَامُوا مَعَهُ فَأَتَى رَجُلاً مِنَ الأَنْصَارِ فَإِذَا هُوَ لَيْسَ فِي بَيْتِهِ فَلَمَّا رَأَتْهُ الْمَرْأَةُ قَالَتْ مَرْحَبًا وَأَهْلاً ‏.‏ فَقَالَ لَهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ أَيْنَ فُلاَنٌ ‏"‏ ‏.‏ قَالَتْ ذَهَبَ يَسْتَعْذِبُ لَنَا مِنَ الْمَاءِ ‏.‏ إِذْ جَاءَ الأَنْصَارِيُّ فَنَظَرَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَصَاحِبَيْهِ ثُمَّ قَالَ الْحَمْدُ لِلَّهِ مَا أَحَدٌ الْيَوْمَ أَكْرَمَ أَضْيَافًا مِنِّي  قَالَ - فَانْطَلَقَ فَجَاءَهُمْ بِعِذْقٍ فِيهِ بُسْرٌ وَتَمْرٌ وَرُطَبٌ فَقَالَ كُلُوا مِنْ هَذِهِ ‏.‏ وَأَخَذَ الْمُدْيَةَ فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ إِيَّاكَ وَالْحَلُوبَ ‏"‏ ‏.‏ فَذَبَحَ لَهُمْ فَأَكَلُوا مِنَ الشَّاةِ وَمِنْ ذَلِكَ الْعِذْقِ وَشَرِبُوا فَلَمَّا أَنْ شَبِعُوا وَرَوُوا قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لأَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ ‏"‏ وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَتُسْأَلُنَّ عَنْ هَذَا النَّعِيمِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَخْرَجَكُمْ مِنْ بُيُوتِكُمُ الْجُوعُ ثُمَّ لَمْ تَرْجِعُوا حَتَّى أَصَابَكُمْ هَذَا النَّعِيمُ ‏"‏ ‏.‏ مسلم

 

Amehadithia Abuu Hurayrayh (رضي الله عنه) kwamba: Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka mchana mmoja, au usiku, akakutana na Abuu Bakr na ‘Umar (رضي الله عنهما) akawauliza: “Jambo gani lililokutoeni majumbani mwenu wakati huu?”  Wakasema: “Ni njaa ee Rasuli wa Allaah!” Akasema: “Nami naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, nami pia lililonitoa ni kama lililowatoa nyinyi. Twendeni!”  Wakafuatana naye hadi nyumbani kwa mtu miongoni mwa Answaariy, lakini hawakumkuta nyumbani kwake. Mkewe alipomuona (Rasuli wa Allaah) alimwambia: “Marhaban wa Ahlan” (Karibu). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Yuko wapi fulani?” Akajibu: Amekwenda kututafutia maji matamu.” Mara yule Answaariy akaja akamtazama Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake akasema: “AlhamduliLLaah! Leo hakuna mwenye wageni watukufu kama mimi!” Akaondoka kisha akarudi na kichala cha tende tosa, tende kavu na tende mbivu, Akwaambia: “Kuleni!” Akachukua kisu lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Usichinje mbuzi wa maziwa.” Akawachinjia wakala mbuzi yule na wakala katika kile kichala cha tende na wakanywa. Waliposhiba na wakamaliza kiu chao, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akawaambia Abuu Bakar na ‘Umar (رضي الله عنهما): “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, mtaulizwa Siku ya Qiyaamah juu ya neema hii. Njaa imewatoa majumbani mwenu, kisha hamkurejea mpaka mkapata neema hii.” [Muslim]

 

Na alifundisha du’aa ya kumumobea mtu anayekupa chakula au kinywaji useme:

 

اللّهُـمَّ أَطْعِمْ مَن أَطْعَمَني، وَاسْقِ مَن سَقانِي

Allaahumma Atw-’im man atw-’amaniy Wasqi man saqaaniy

Ee Allaah Mlishe aliyenilisha na Mnywishe aliyeninyweisha  [Hadiyth ya Al-Miqdaad bin Al-Aswad  (رضي الله عنه) - Muslim (3/126) [2055], Ahmad]

 

 

 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...