أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
016-Asbaab Nuzuwl An-Nahl Aayah : 126
Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى)
وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِ ۖ وَلَئِن صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِّلصَّابِرِينَ﴿١٢٦﴾
Na mkilipiza, basi lipizeni kulingana na vile mlivyoadhibiwa. Na mkisubiri, basi bila shaka hivyo ni bora kwa wenye kusubiri. [An-Nahl: 126]
Sababun-Nuzuwl:
حَدَّثَنَا أَبُو عَمَّارٍ الْحُسَيْنُ بْنُ حُرَيْثٍ، حَدَّثَنَا الْفَضْلُ بْنُ مُوسَى، عَنْ عِيسَى بْنِ عُبَيْدٍ، عَنِ الرَّبِيعِ بْنِ أَنَسٍ، عَنْ أَبِي الْعَالِيَةِ، قَالَ حَدَّثَنِي أُبَىُّ بْنُ كَعْبٍ، قَالَ لَمَّا كَانَ يَوْمُ أُحُدٍ أُصِيبَ مِنَ الأَنْصَارِ أَرْبَعَةٌ وَسِتُّونَ رَجُلاً وَمِنَ الْمُهَاجِرِينَ سِتَّةٌ فِيهِمْ حَمْزَةُ فَمَثَّلُوا بِهِمْ فَقَالَتِ الأَنْصَارُ لَئِنْ أَصَبْنَا مِنْهُمْ يَوْمًا مِثْلَ هَذَا لَنُرْبِيَنَّ عَلَيْهِمْ قَالَ فَلَمَّا كَانَ يَوْمُ فَتْحِ مَكَّةَ فَأَنْزَلَ اللَّهُ ((وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُمْ بِهِ وَلَئِنْ صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِلصَّابِرِينَ)) فَقَالَ رَجُلٌ: لاَ قُرَيْشَ بَعْدَ الْيَوْمِ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم :" كُفُّوا عَنِ الْقَوْمِ إِلاَّ أَرْبَعَةً " . قَالَ هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ مِنْ حَدِيثِ أُبَىِّ بْنِ كَعْبٍ
Ametuhadithia Abuu ‘Ammaar Al-Husayn bin Hurayth, ametuhadithia Al-Fadhwl bin Muwsa kutoka kwa ‘Iysaa bin ‘Ubayd, kutoka kwa Ar-Rabi’y bin Anas, kutoka kwa Abuu Al-‘Aaliyah amesema: amenihadithia Ubayy bin Ka’b ambaye amesema: Siku ya vita vya Uhud, watu sitini na nne katika Answaariy waliuawa, na sita kutoka kwa Muhaajiriyn. Mmoja wao alikuwa ni Hamzah, wakamtumbua basi Answaariy wakasema: “Ikiwa (siku za mbele) tukijaaliwa kupigana nao (tukawaua) siku kama hii, nasi tutawatumbua baadhi yao mara mbili yake (kama walivyowatumbua baadhi yetu).” Akasema: Basi siku ya Fat-h Makkah Allaah Akateremsha:
وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِ ۖ وَلَئِن صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِّلصَّابِرِينَ﴿١٢٦﴾
Na mkilipiza, basi lipizeni kulingana na vile mlivyoadhibiwa. Na mkisubiri, basi bila shaka hivyo ni bora kwa wenye kusubiri. [An-Nahl: 126]
Mtu mmoja akasema: “Hakutakuwa na Quryash tena baada ya leo.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Waacheni watu isipokuwa wanne tu.” [At-Tirmidhiy, amesema Hii Hadiyth Hasan Ghariyb katika Hadiyth za Ubayy bin Ka’ab]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni