Aayah Na Mafunzo
An-Nisaa Aayah 17-18
Kukimbilia Kuomba Tawbah Kabla Ya Mauti
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلَى اللَّـهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَأُولَـٰئِكَ يَتُوبُ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٧﴾
Hakika tawbah inayokubaliwa na Allaah ni ya wale wanaofanya uovu kwa ujahili kisha wakatubia haraka, basi hao Allaah Anapokea tawbah yao. Na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.
وَلَيْسَتِ التَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ حَتَّىٰ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ إِنِّي تُبْتُ الْآنَ وَلَا الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٨﴾
Lakini tawbah si kwa wale wanaofanya maovu mpaka mauti yanapohudhuria kwa mmoja wao husema: “Hakika mimi sasa nimetubu.” Na wala wale wanaokufa na hali wao ni makafiri. Hao Tumewaandalia adhabu iumizayo. [An-Nisaa: 17-18]
Mafunzo:
Umuhimu wa kuomba tawbah kabla ya kufika wakati wa kutokupokelewa: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Huikubali tawbah ya mja Wake kabla ya roho kufika kwenye mkoromo wa mauti.” [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na wengineo; Swahiyh At-Tirmidhiy (3537), Swahiyh Ibn Maajah (3449)].
Na pia. “Atakayetubu kabla ya kuchomoza jua upande wa Magharibi, Allaah Atamkubalia tawbah yake.” [Muslim].
Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida ziyada:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni