إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ
Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!
07-Shirki Ni Kuharamishwa Kuingia Jannah Na Badala Yake Kuingizwa Motoni
Mwenye kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) atakosa kuingia Jannah bali makazi yake yatakuwa ni ya kudumu Motoni kwa dalili zifuatazo:
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾
Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.” [Al-Maaidah: 72]
Na Hadiyth zifuatazo:
عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَدْعُو مِنْ دُونِ اللهِ نِدَّاً دَخَلَ النَّارَ )) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Mas-‘uwd (Radhwiya Alaahu ‘anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayekufa akiwa katika hali ya kumuomba asiyekuwa Allaah kumfanyia mlinganishi (mshirika) ataingia Motoni)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na pia:
عن ابن مسعود رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ مَاتَ يُشْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا دَخَلَ النَّارَ))
Kutoka kwa Ibn Mas‘uwd pia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayefariki akiwa katika hali ya kumshirikisha Allaah kwa chochote ataingia Motoni)) [Al-Bukhaariy 1238, Muslim 92]
Pia:
عن جابر رضي الله عنه: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((مَنْ لَقِي اللهَ لاَ يُشْرِك بِهِ شَيْئاً دَخَلَ الْجَنَّة، وَمَنْ لَقِيَه يُشْرِك بِهِ شَيْئاً دَخَلَ النَّار))
Imetoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Atakayekutana na Allaah akiwa hamshirikishi na chochote Ataingia Jannah, na atakayekutana Naye akiwa anamshirikisha na chochote ataingia Motoni)) [Muslim 94.]
Na pia:
عَن أَبي ذَرٍّ رضي الله عنه عنِ النَّبيِّ صلَّى اللَّهُ عليهِ وسلَّمَ؛ أنَّهُ قالَ: ((أتاني جبريلُ عليهِ السَّلامُ فبشَّرَني أنَّهُ من ماتَ من أمَّتِكَ لا يشرِكُ باللَّهِ شيئًا دخلَ الجنَّةَ)) قلتُ: وإن زنَى وإن سرقَ؟ قالَ: ((وإن زنَى وإن سرقَ))
Kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Amenijia Jibriyl ‘alayhis-salaam akanibashiria kwamba atakayefariki katika Ummah wangu akiwa hamshirikishi Allaah kwa chochote ataingia Jannah)). Nikasema: “Je hata akizini au akiiba?” Akasema: ((Hata akizini au akiiba)) [Al-Bukhaariy 1237, Muslim 94]
Na Hadiyth ya Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لاَ يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هَذِهِ الأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلاَ نَصْرَانِيٌّ ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ إِلاَّ كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ
((Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, hasikii yeyote kuhusu mimi (kutumwa kwangu ujumbe) katika Ummah wa (Da’wah) Myahudi au Mnaswaara kisha afariki akiwa hayamini yale niliyotumwa nayo, isipokuwa atakuwa miongoni kwa watu wa Motoni)) [Muslim (1/80) Mlango wa Iymaan – Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu)]
Pia:
عَن عبدالله بن عمر جاءَ أعرابيٌّ إلى النَّبيِّ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ فقالَ: يا رسولَ اللَّهِ إنَّ أبي كانَ يصِلُ الرَّحمَ وَكانَ وَكانَ فأينَ هوَ؟ قالَ: ((في النَّارِ)) قالَ فَكأنَّهُ وجدَ من ذلِكَ فقالَ: يا رسولَ اللَّهِ فأينَ أبوكَ قالَ رسولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ: ((حيثُما مررتَ بقبرِ مشرِكٍ فبشِّرْهُ بالنَّارِ)) قالَ: فأسلمَ الأعرابيُّ بعدُ وقالَ: لقد كلَّفني رسولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ تعبًا ما مررتُ بقبرِ كافرٍ إلَّا بشَّرتُهُ بالنَّارِ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Bedui mmoja alikuwa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Baba yangu alikuwa akiunga undugu na alikuwa akifanya kadhaa wa kadhaa, je yuko wapi?” Akasema: (Motoni)). Ikawa kama kwamba lilikuwa jambo zito kwake. Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, baba yako yuko wapi?” Akasema: ((Utakapopita kaburi la Mushrik yeyote mbashirie Moto)). Bedui akasilimu baada ya hapo kisha akasema: “Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): amenitwika jukumu gumu kwamba kila nikipata kaburi la kafiri nimbashirie Moto.” [Swahiyh Ibn Maajah 1288]
Wala haifai kuwaombea wazazi makafiri wakafariki wakiwa katika hali ya ukafiri kwa kuwa imeshabainika kuwa ni watu wa Motoni, tena hata kama ni wazazi, ndugu au jamaa wa karibu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ﴿١١٣﴾
Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa moto uwakao vikali mno. [At-Tawbah: 113]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni