MADHARA YA UZITO NA UNENE KUPITA KIASI
Magonjwa hatari unayoweza kupata kutokana na uzito wako kuwa mkubwa ni pamoja na yafuatayo:
1. Magonjwa ya moyo.
2. Shinikizo la juu la damu
3. Kiharusi (Stroke)
4. Kisukari aina ya pili
5. Baadhi ya aina za saratani
6. Ugumba
7. Msongo wa mawazo (Stress)
8. Matatizo ya mifupa
9. Maumivu ya mgongo
10. Kuishiwa nguvu za tendo la ndoa (kwa wanaume)
Nini hupelekea kuongezeka kwa uzito mwilini au kuwa mnene?
Uzito uliopitiliza hutokana na kuongezeka kwa nishati mwilini, vyakula tunavyo kula kila siku hutengeneza nishati ambayo hutumika katika shughuli mbalimbali za mwili.
Kwahiyo uzito kupitiliza au unene hutegemeana na kiwango cha nishati ambacho hupatikana katika vyakula na vinywaji ambavyo tumekula na kiasi kinacho tumiwa na mwili.
Kwahiyo ili usiwe na uzito mkubwa wala mdogo ni lazima kiwango cha nishati kinachoingia mwilini kilingane na mahitaji ya mwili wako hivyo basi uzito mkubwa hutokana na kula kiwango kikubwa cha nishati ikiwa matumizi ya nishati hiyo mwilini ni kidogo.
Zifuatazo ni sababu zinazopelekea kuwa na uzito mkubwa au unene nazo ni.
1. Msongo wa mawazo.
Katika hali ya kawaida msongo wa mawazo huathiri au huvuruga mfumo wa vichocheo vya mwili ivyo kupelekea kuvurugika kwa utendaji kazi wa mwili.
Kichocheo cha cortisol hufanya kazi ya kuweka uwiano sawa wa nishati mwilini, hivyo Kuvurugika kwa kichocheo hiki hufanya mtu ahisi njaa muda wote jambo ambalo litapelekea kula zaidi na nishati kuhifadhiwa mwilini kwa wingi jambo ambalo hupelekea uzito kuongezeka.
2. Kukosa usingizi.
Kukosa usingizi huongeza athari ya mtu kuwa na uzito mkubwa, kwasababu usingizi husababisha kuwa na ulinganisho au uwiano kati ya vichocheo ambavyo vinamfanya mtu ahisi njaa na vile ambavyo vina mfanya mtu asihisi njaa.
Vichocheo ambavyo humfanya mtu ahisi njaa huitwa Ghrelin navichocheo ambavyo humfanya mtu asihisi njaa huitwa Leptin.
Kwaiyo kukosa usingizi husababisha kuvurugika kwa uwiano mzuri uliopo katika vichocheo ivyo kusababisha kupanda kwa kichocheo(ghrelin) ambacho kinamfanya mtu ahisi njaa na kushuka kwa uzalishwaji wa kichocheo (leptin) ambacho humfanya mtu asihisi njaa hali hii hupelekea mtu ale zaidi na kusababisha nishati kuhifadhiwa kwa kiwango kikubwa na matokeo yake ni kuongezeka uzito.
Pia kutokana na kuongezeka kwa uhitaji wa chakula mwilini hupelekea kuathirika kwa utendaji kazi wa kichocheo (insulin) hali hii humfanya mtu awe katika hatari ya kuugua ugonjwa wa kisukari ambao hutokana na jinsi mtu anavyo ishi maisha ya kila siku.
3. Kutokufanya mazoezi.
Ili uwe na afya bora mazoezi ni muhimu kwasababu husaidia kutoa taka mwili,huimarisha viungo vya mwili, huongeza kiwango cha msukumo wa damu, vile vile husaidia kupunguza uzito au unene.
Kutokufanya mazoezi huufanya mwili kushindwa kutumia nishati inayopatikana katika chakula ulichokula jambo ambalo husababisha kuwepo kwa uwingi wa nishati mwilini nahivyo kupelekea nishati iyo ihifadhiwe kama mafuta mwilini jambo ambalo litapelekea uzito kuongezeka.
4. Unywaji wa pombe na ulaji wa vyakula vya viwandani.
Kuna makampuni mengi sana siku hizi ambayo hutengeneza vyakula na vinywaji katika viwanda vyao.Makampuni haya hutumia gharama kubwa kufanya matangazo ya bidhaa zao, Kutokana na ushawishi mkubwa wa matangazo yao na bei nafuu ya bidhaa zao watu wengi hujikuta wanatunia bidhaa za makampuni kuachana na zile za kuandaa wenyewe.
Vyakukula na vinywaji hivi vimetengeneza kwa kiwango kikubwa cha nishati.Pindi mtu anavyo tumia bidhaa hizi kwa wingi husababisha nishati kubwa iendelelee hifadhiwa mwilini wakati matumizi ya mwili ni madogo matokeo yake uzito huongezeka.
5. Kutokuzingatia lishe sahihi.
Wakati mwingine unaweza kuongeza uzito kwasababu ya kutokula mlo sahihi,na kwa kiwango ambacho siyo sahihi na wakati ambao siyo sahihi.
Baadhi ya watu uzito wao huongezeka japo wanakula kiwango kidogo cha chakula lakini wapo wengine hubaki na uzito ule ule japo wanakula mlo anbao ni sawa.
Hii inaweza kuoanishwa na kiwango tofauti cha shughuli za kikemikali mwilini au aina ya chakula ambacho mtu anakula na haina mahusiano na kiwango cha chakula ambacho mtu anakula isipo kuwa ni ubora wa chakula chenyewe hii humaanisha unaweza ukala chakula kidogo ukaongezeka uzito na mwingine akala chakula kile kile na akaongezeka uzito.
6. Matumizi ya madawa.
Dawa zimetengenezwa kwa kutumia kemikali.
Tunatumia dawa kwa lengo la kutibu au kupata suluhu ya ugonjwa ambao unakusumbua.
Dawa hizi huleta matokeo tofauti pamoja na kutibu tatizo ambalo lina kusumbua.Mbali na kutibu tatizo ambalo linakusumbua dawa hizi huleta maudhi madogo madogo na mahudhi hayo hutofautiana kati ya dawa na dawa na mtu na mtu na hii ni kutokana na vile tumeumbwa.
Baadhi ya dawa mfano dawa za kisukari , dawa za kutuliza mihemuko (ant depressant) mbali na kushusha sukari dawa hizi husababisha kuongezeka kwa uzito.
7. Ulaji wa vyakula vya wanga na sukari kwa wingi.
Ulaji wa vyakula hivi kwa wingi huchochea deli za kuhifadhi mafuta ziendelee kuhifadhi mafuta zaidi na matokeo yake in kuwa mnene au kuwa na uzito mkubwa.
8. Urithi.
Unene au uzito mkubwa unaweza ukarithiwa kutoka kwa moja kati ya wazazi na hii ni kutokana na tafiti ambazo zmefanywa.
Pia endapo mama mjamzito atakula sana au hatokula sana hupelekea kubadilika kwa DNA ya mtoto na kusababisha athari katika utumiaji wa mafuta mwilini kwa baadae.
Imehaririwa mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni