Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
44-Aliposhauri Jambo Katika Mas-ala Ya Kidunia Kwa Kutumia Rai Yake Ya Kibinafsi
Alikiri Kuwa Yeye Ni Bin Aadam
Swahaba (رضي الله عنهم) waliheshimu ushauri wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika mas-ala ya Dini yao na dunia yao. Basi pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipowashauri jambo kwa fikra yake ya ki binafsi kuhusu jambo katika mambo ya kidunia, walifuata ushauri wake. Lakini ilipokuja kutambulika kuwa ushauri ule haukuwa wenye kunufasiha jambo hilo la ki dunia, basi alikiri kuwa yeye ni mwana Aadam huenda ukawa ushauri wake si wa kuwanufaisha jambo hilo, kwa hiyo akawanasihi anapowashauri au kuwaamrisha jambo katika mas-ala ya Dini wafuate, lakini katika mas-ala ya ushauri kutokana na fikra zake za kibinafsi, basi wafuate jambo ambalo wana ujuzi nalo zaidi wenyewe. Mfano ni kama huu uliosimuliwa katika Hadiyth kuhusu namna ya upandikizaji na uzalishajia wa mitende.
رَافِعُ بْنُ خَدِيجٍ، قَالَ قَدِمَ نَبِيُّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم الْمَدِينَةَ وَهُمْ يَأْبُرُونَ النَّخْلَ يَقُولُونَ يُلَقِّحُونَ النَّخْلَ فَقَالَ " مَا تَصْنَعُونَ " . قَالُوا كُنَّا نَصْنَعُهُ قَالَ " لَعَلَّكُمْ لَوْ لَمْ تَفْعَلُوا كَانَ خَيْرًا " . فَتَرَكُوهُ فَنَفَضَتْ أَوْ فَنَقَصَتْ - قَالَ - فَذَكَرُوا ذَلِكَ لَهُ فَقَالَ " إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ إِذَا أَمَرْتُكُمْ بِشَىْءٍ مِنْ دِينِكُمْ فَخُذُوا بِهِ وَإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِشَىْءٍ مِنْ رَأْىٍ فَإِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ " . قَالَ عِكْرِمَةُ أَوْ نَحْوَ هَذَا . قَالَ الْمَعْقِرِيُّ فَنَفَضَتْ . وَلَمْ يَشُكَّ .
Raafi’ bin Khadiyj (رضي الله عنه) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuja Madiyna na watuu walikuwa wakipandikiza na kuzalisha mitende. Akasema: “Je, mnafanya nini?” Wakajibu: “Tunaipandikiza.” Akasema: “Labda msingelifanya hivyo hiyvo ingelikuwa bora.” Wakaacha (kupandikiza na kuchipuza au kuzalisha mitende kwa njia zao), lakini matokeo yake yakawa ni kupatikana uchache wa mazao. Wakamtajia hilo, hapo akasema: “Mimi ni mwana Aadam, nnapokuamrisheni jambo la kuhus Dini yenu basi lipokeeni na fuateni, lakini nnapokuamrisheni jambo la rai yangu, basi hakika mimi ni mwana Aadam.” Ikirmah amesema: “Alisema jambo kama hivyo.” [Muslim]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni