إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ
Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!
06- Shirki Ni Miongoni Mwa Al-Kabaair (Madhambi Makubwa)
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾
Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu. [An-Nisaa: 48]
Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا﴿١١٦﴾
Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali. [An-Nisaa: 116]
Na Hadiyth za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam):
((ألاَ أُنبِّئكم بأكبرِ الكبائر؟ الإشراك بالله)) متفق عليه.
((Je, hivi nikujulisheni madhambi makubwa kabisa? Ni kumshirikisha Allaah)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na pia Hadiyth:
عَنْ أبي أيوب الأنصاري رضي الله عنه انَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَنْ جَاءَ يَعْبُدُ اللَّهَ وَلاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا وَيُقِيمُ الصَّلاَةَ وَيُؤْتِي الزَّكَاةَ وَيَجْتَنِبُ الْكَبَائِرَ كَانَ لَهُ الْجَنَّةُ)). فَسَأَلُوهُ عَنِ الْكَبَائِرِ فَقَالَ: ((الإِشْرَاكُ بِاللَّهِ وَقَتْلُ النَّفْسِ الْمُسْلِمَةِ وَالْفِرَارُ يَوْمَ الزَّحْفِ)).
Imepokelekewa kutoka kwa Abuu Ayyuwb Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayekuja akiwa anamwambudu Allaah wala hamshirikishi na chochote, na anasimamisha Swalaah, na anatoa Zakaah, na anajiepusha na Al-Kabaair (madhambi makubwa) atapata Al-Jannah)) Wakamuuliza kuhusu Al-Kabaair akasema: ((Kumshirkisha Allaah na kumuua Muislamu, na kukimbia (vita) siku ya mapambano (vita).)) [An-Nasaaiy (4009) na ameisahihisha Al-Albaaniy]
Na shirki ni katika mambo saba yanayoangamiza:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه (عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ)) قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا هُنَّ؟ قَالَ: ((الشِّرْكُ بِاللَّهِ وَالسِّحْرُ وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَأَكْلُ الرِّبَا وَأَكْلُ مَالِ الْيَتِيمِ وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ وَقَذْفُ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ الْغَافلاَتِ)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jiepusheni na mambo saba yanayoangamiza!)) Wakauliza: Ni yepi hayo ee Rasuli wa Allaah? Akawaambia: ((Ni kumshirikisha Allaah, sihri [uchawi], kuua nafsi Aliyoiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki, kula ribaa, kula mali ya yatima, kukimbia wakati wa vita na kuwatuhumu uzinifu wanawake Waumini waliohifadhika walioghafilika.)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni