Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
45-Amepewa Al-Wasiylah (Heshima Maalum)
Na Al-Maqaam Al-Mahmuwd (Cheo Cha Kusifika) Siku Ya Qiyaamah
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ﴿٧٩﴾
Na katika usiku, amka uswali (tahajjud) kuisoma (Qur-aan); ni ziada ya Sunnah kwako Asaa Rabb wako Akakuinua cheo kinachosifika. [Al-Israa: 79]
Nayo ni Ash-Shafaa’ah (Uombezi) Siku ya Qiyaamah baada ya kisimamo kirefu mno cha watu katika mkusanyiko wa viumbe wote. Watu watamwendea Nabiy Aadam, Nuwh, Ibraahiym, Muwsaa na ‘Iysaa (عليهم السلام) wawaombe Ash-Shafaa’ah lakini kila mmoja atakataa kwa kutoa udhuru wake, na kila mmoja atawaambia Ummah wake wapeleke ombi kwa Nabii mwenginewe mpaka watu wamfikie Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) wamuombe, na hapo ndipo atakapoinama kusujudu na kumuomba Rabb Wake Ash-Shafaa’ah, na Allaah (عز وجل) Atamkubalia Shafaa yake, basi mahali hapo ndipo pakaitwa “Al-Maqaam Al-Mahmuwd” [Cheo cha Kusifika] kwa kuwa viumbe wote watamsifu Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa sababu Shafaa’ah yake ndio sababu yao kufanyiwa wepesi kisimamo chao kirefu mno Siku hiyo ya Mkusanyiko. Hadiyth ifutayo inathibitisha:
عن ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا يَقُولُ : ( إِنَّ النَّاسَ يَصِيرُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ جُثًا ، كُلُّ أُمَّةٍ تَتْبَعُ نَبِيَّهَا يَقُولُونَ : يَا فُلانُ اشْفَعْ ، يَا فُلانُ اشْفَعْ ، حَتَّى تَنْتَهِيَ الشَّفَاعَةُ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَذَلِكَ يَوْمَ يَبْعَثُهُ اللَّهُ الْمَقَامَ الْمَحْمُودَ ) رواه البخاري
Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما) amesema: Watu watasubiri wakiwa watapiga magoti Siku ya Qiyaamah, na kila Ummah utamfuata Nabiy wake wakisema: “Ee fulani tuombee Ash-Shafaa’ah (kwa Allaah), mpaka ombi la Ash-Shafaa’ah litamfikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na hiyo ndio siku ambayo Allaah Atamuinua katika Al-Maqaam Al-Mahmuwd (Cheo Cha Kusifika) [Al-Bukhaariy]
Miongoni mwa amali zikatazosababisha kupata Ash-Shafaa’ah ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
1-Kuitikia Mwadhini na kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " إذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوامِثْلَ مَا يَقُولُ ، ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ ، فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا . ثُمَّ سلُوا اللَّه لي الْوسِيلَةَ ، فَإِنَّهَا مَنزِلَةٌ في الجنَّةِ لا تَنْبَغِي إِلاَّ لعَبْدٍ منْ عِباد اللَّه وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُو ، فَمنْ سَأَل ليَ الْوسِيلَة حَلَّتْ لَهُ الشَّفاعَةُ
‘Abdullaah bin ‘Amruw (رضي الله عنهما) kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akisema: ((Mtakapomsikia muadhini basi semeni kama anavyosema, kisha niswalieni, kwani mwenye kuniswalia mara moja Allaah Atamswalia mara kumi, na kisha niombeeni (kupata) ‘wasiylah’ ambayo ni manzila (heshima maalum) huko Jannah. Haitomstahikia isipokua mja mmoja katika waja wa Allaah, nami ninatarajia kuwa mja huyo, na mwenye kuniombea “Al-Wasiylah” atapata uombezi (wangu Siku ya Qiyaamah)) [Muslim (1/288)
2-Kuitikia Mwadhini na kumuombea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) du’aa iliyothibiti:
وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : {مَنْ قَالَ حِينَ يَسْمَعُ اَلنِّدَاءَ : اَللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ، وَالصَّلَاةِ اَلْقَائِمَةِ، آتِ مُحَمَّدًا اَلْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ، وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا اَلَّذِي وَعَدْتَهُ، حَلَّتْ لَهُ شَفَاعَتِي يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ} أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kusoma anaposikia Adhana:
اَللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ اَلدَّعْوَةِ اَلتَّامَّةِ، وَالصَّلَاةِ اَلْقَائِمَةِ، آتِ مُحَمَّدًا اَلْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ، وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا اَلَّذِي وَعَدْتَهُ
Allaahumma Rabba haadhihid-dda’watit-ttaamah, wasw-Swaalaatil qaaimah, aati Muhammada al-wasiylata wal fadhwiylah, wab-‘ath-hu maqaaman mahmuwdan alladhiy wa’adtah.
(Ee Allaah, Rabb wa mwito huu uliotimia, na Swalaah iliyosimama, mpe (Nabiy) Muhammad al-Wasiylah (cheo, heshima maalumu, daraja), na fadhila, na mfikishe daraja yenye kuhimidiwa, ambayo Umemuahidi).
Ash-Shafaa’ah (Uombezi) wangu umehalalika kwake Siku ya Qiyaamah.” [Imetolewa na Al-Arba’ah]
3-Kuimarika katika Tawhiyd ya Allaah (عز وجل)
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّهُ قَالَ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ : مَنْ أَسْعَدُ اَلنَّاسِ بِشَفَاعَتِكَ؟ قَالَ: ((مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ خَالِصًا مِنْ قَلْبِهِ))
Abuu Hurayrah (رضي اَللَّهُ عَنْهُ) alimesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) “Nani atakayefanikiwa zaidi na shafaa’ah yako? Akajibu: ((Atakayesema
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ
Laa ilaaha illa-Allaah
hali ya kuwa na niyyah safi moyoni mwake)) [Al-Bukhaariy]
4-Kuzidishia Kusujudu (Kuswali Nawaafil):
Imehadithiwa na mmoja wa Mtumishi wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba:
كان ممَّا يقولُ للخادمِ : ألكَ حاجةٌ ؟ قال : حتى كان ذاتَ يومٍ فقال : يا رسولَ اللهِ ! حاجتي ، قال : و ما حاجتك ؟ قال : حاجَتي أن تشفعَ لي يومَ القيامةِ قال : و من دلَّكَ على هذا ؟ قال : ربِّي ، قال : أما لا ، فأعنِّي بكثرةِ السجودِ
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akimwambia Mtumishi wake: “Je unahitaji lolote?” Hadi siku moja (Mtumishi) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah nina haja!” Akauliza: “Nini haja yako?” akasema: “Haja yangu uniombee Shafaa Siku ya Qiyaamah.” Akamuuliza: Nani aliyekuongoza kuomba hilo?” Akasema: “Rabb Wangu.” Akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Basi nisaidie kwa kuzidisha kusujudu (kuswali)” [As-Silsilah Asw-Swahiyha 2102], Swahiyh Al-Musnad (1497])
Pia,
عن أبي فراس رَبِيعَة بْن كَعْبٍ الْأَسْلَمِيُّ رضي الله عنه خادم رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: كُنْتُ أَبِيتُ مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَتَيْتُهُ بِوَضُوئِهِ وَحَاجَتِهِ، فَقَالَ لِي: ((سَلْني)) فَقُلْتُ: أَسْأَلُكَ مُرَافَقَتَكَ فِي الْجَنَّةِ، قَالَ: ((أَوْ غَيْرَ ذَلِكَ؟)) قُلْتُ: هُوَ ذَاكَ، قَالَ: ((فَأَعِنِّي عَلَى نَفْسِكَ بِكَثْرَةِ السُّجُودِ)) رواه مسلم في صحيحه
Kutoka kwa Abuu Firaas Rabiy'ah bin Ka'ab Al-Aslamiy mtumishi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye amesema: "Nililala na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) usiku mmoja nikamletea maji ya kutawadha, akaniambia: ((Niombe utakacho)) Nikasema: "Nataka kuandamana na wewe Jannah. Akasema: ((Hutaki lolote lingine?)) Nikasema: "Ni hilo tu." Akasema: ((Basi nisaidie (ili hilo liwezekane) kwa kuzidisha kusujudu [Kuswali])) [Muslim katika Swahiyh yake]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni