Lu-ulu-un-Manthuwrun
(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)
Hadiyth Ya 44
Allaah Akimpenda Mja Anamnadia Jibriyl Na Kumuamrisha Ampende Pamoja Na Wote
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِذَا أَحَبَّ اللَّهُ الْعَبْدَ نَادَى جِبْرِيلَ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ فُلاَنًا فَأَحْبِبْهُ، فَيُحِبُّهُ جِبْرِيلُ، فَيُنَادِي جِبْرِيلُ فِي أَهْلِ السَّمَاءِ: إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ فلاَنًا فَأَحِبُّوهُ، فَيُحِبُّهُ أَهْلُ السَّمَاءِ ثُمَّ يُوضَعُ لَهُ الْقَبُولُ فِي الْأَرْضِ)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:((Allaah Anapompenda mja, Humnadia Jibriyl: Hakika Allaah Anampenda fulani, nawe mpende. Basi Jibrily humpenda. Naye Jibriyl anawanadia watu wa mbinguni [Malaika]: “Hakika Allaah Anampenda fulani, nanyi mpendeni. Basi nao walioko mbinguni humpenda, halafu huwekwa kabuli katika ardhi [watu wampende])). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Mafunzo Na Mwongozo:
1. Fadhila kubwa mno kupendwa na Allaah (سبحانه وتعالى) kama Alivyotubashiria kwamba watakuwa hawana khofu, wala huzuni wala baya au dhiki yoyote ile. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٦٢﴾
Tanabahi! Hakika vipenzi wa Allaah hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.
الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿٦٣﴾
Ambao wameamini na wakawa wana taqwa.
لَهُمُ الْبُشْرَىٰ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۚ لَا تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٦٤﴾
Watapata bishara katika uhai wa dunia na wa Aakhirah. Hakuna mabadiliko katika Maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu adhimu. [Yuwnus (11: 62-64)]
2. Mapenzi yako baina wana Aadam kama baina ya mume na mke, familia, marafiki, mwalimu na mwanafunzi n.k, lakini mapenzi yaliyo muhimu zaidi ni mapenzi ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).
3. Apataye mapenzi ya Allaah (سبحانه وتعالى) atakuwa katika ulinzi wa Malaika, kwani wao wameamrishwa wampende na wamlinde mja huyo duniani na Aakhirah kuna ziada. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ﴿٣٠﴾
Hakika wale waliosema: “Rabb wetu ni Allaah.” Kisha wakathibitika imara; Malaika huwateremkia: (kuwaambia): “Msikhofu, na wala msihuzunike, na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa.”
نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ﴿٣١﴾
“Sisi ni rafiki zenu walinzi katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Na mtapata humo yale yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale mtakayoomba.
نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ﴿٣٢﴾
“Ni mapokezi ya takrima kutoka kwa Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu.” [Fusw-Swilat (41: 30-32)].
4. Waja wema wanapendeza machoni mwa watu baada ya kuwekewa na Allaah (سبحانه وتعالى) kabuli ardhini.
5. Hima ya kutenda mema yatakayosababisha kupata mapenzi ya Allaah (سبحانه وتعالى).
[Hadiyth Al-Qudsiy: ((Yeyote yule atakayefanya uadui kwa walii Wangu, basi Nitatangaza vita dhidi yake. Mja Wangu hanikaribii na kitu chochote Ninachokipenda kama ‘amali Nilizomfaridhishia, na mja Wangu huzidi kunikaribia kwa ‘amali njema za Sunnah ili Nimpende. Ninapompenda, Huwa masikio yake yanayosikilizia, macho yake anayoonea, mikono yake anayopigania, miguu yake anayotembelea nayo, lau angeniomba kitu, bila shaka Ningempa, lau angeniomba himaya bila shaka Ningelimkinga, na Sisiti juu ya kitu chochote kama Ninavyosita [kuichukua] roho ya mja Wangu Muumin, anachukia mauti, Nami Nachukia kumdhuru)). [Al-Bukhaariy]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni