Translate

Jumatatu, 8 Juni 2020

Habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo

Habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo

MAFUTA YA HABBAT SODA NI DAWA KWA KILA UGONJWA ISIPOKUWA KIFO

Hii ni orodha ya magonjwa 89 kwanza

Inapotokea wafalme wa Misri, Malkia wa Ulaya, Mitume na wanasayansi wa kisasa wanakuja na kukubaliana katika jambo moja, ni mhimu kudadisi juu ya jambo hilo.

Ingawa nyakati za sasa tunazungukwa na taarifa na elimu nyingi kuliko katika wakati mwingine wowote, bado tunahitaji kujifunza vitu kutokana na historia na maisha ya kale.

Kutoka kwa baba wa sayansi ya matibabu katika nchi za magharibi Hippocrates kwenda mpaka kwa kiongozi wa mfumo wa mwisho wa kifarao Cleopatra hadi kwa mfalme Tut na jamii iliyofuata, kitu cha pekee ambacho walikuwa wakifanana viongozi hawa kwa pamoja ilikuwa ni thamani waliyoiona katika mtishamba fulani.

Mtishamba au mmea huo ambao viongozi hao walikutana pamoja si mwingine bali ni habbat soda. Habbat soda ndilo jina linalotumika zaidi mashariki ya kati na huko ulaya hujulikana zaidi kama ‘black seeds’.

Kwahiyo niliamua kuchukua muda kusoma na kupeleleza zaidi kuhusu habbat soda kwa ajili yangu mwenyewe na ya wasomaji wangu ili hatimaye niweze kukuletea mwanga kamili juu ya mengi yanayosemwa kuhusu mafuta ya habbat soda.

Unaweza kuwa umesikia majina tofauti tofauti ya habbat soda kutegemea na sehemu gani ya dunia ulipo.

Haya ni moja ya majina yake:

*Kalonji Oil
*Black Cumin Seed Oil
*Nigella Seeds
*Graine De Nigelle
*Black Onion Seeds
*Schwarzkummel

Mafuta ya habbat soda yanatokana na mbegu za habbat soda na mbegu hizi huwa ni nyeusi na ndiyo maana kwa kiingereza wanaita ‘black seed’.

Kuna mashine nyingi za nyumbani unazoweza kutumia kutengeneza mafuta yako mwenyewe kutoka katika mbegu za habbat soda ingawa bado nakushauri ununuwe yale ambayo yameandaliwa tayari.

Habbat soda ina sifa hizi:

*Huondoa bakteria mwilini
*Huondoa uvimbe
*Huondoa sumu mwilini
*Inaondoa fangasi
*Inatibu kansa
*Inatibu pumu
*Inadhibiti kazi za histamini
*Inaua virusi
*Inazuia damu kuganda

Vitu viwili mhimu zaidi ambavyo mafuta haya yanavyo ni ‘thymoquinone’ na ‘thymohydroquinone’.

Vimeng’enya hivi viwili ndivyo vinaweza kusemwa kuwa ndiyo sababu ya mafuta haya kuwa ni dawa kwa kila ugonjwa. Vinaimarisha moja kwa moja kinga yako ya mwili na kuifanya ipatikane wakati wowote itakapohitajika na mwili.

Vimeng’enya hivi viwili ndivyo inaaminika ndiyo sababu mfalme Tut alipatikana na chupa ya mafuta ya habbat soda kwenye kaburi lake akitumaini kuyachukua na kuyatumia atakapofufuka!

Mtume Muhammad (S.A.W) amewahi kunukuliwa akisema ‘Mafuta ya habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo’

Mbegu za habbat soda zinatoka katika majani ya mmea ujulikanao kama ‘Nigella Sativa’ na unalimwa karibu katika kila pembe ya dunia kwa sasa. Asili yake ni Afrika kaskazini, mediterania/ulaya na Asia na kutoka hapo umesambaa kila sehemu ya dunia.

Habbat soda inachukuliwa kama moja ya dawa za asili bora zaidi kuwahi kutokea.

Nini yanachoweza kufanya mwilini haya mafuta ya habbat soda? kuna matumizi mengi ya habbat soda katika kutibu na kukinga magonjwa mbalimbali.

Hapa nimejaribu kukusanya baadhi ya magonjwa 89 ambayo unaweza kujitibu kwa kutumia habbat soda.

Kama kawaida unapewa angalizo kutotumia dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa daktari

MAFUTA YA HABBAT SODA NI DAWA KWA KILA UGONJWA ISIPOKUWA KIFO

Mafuta ya habbat soda

Magonjwa 89 yanayoweza kutibika na habbat soda ni pamoja na:

1. Yanaimarisha afya ya moyo

Afya mbovu ya moyo inaweza kuwa ni matokeo ya sababu nyingi lakini sababu zote chanzo chake kikuu ni matokeo ya kutokuupa moyo virutubishi unavyovihitaji.

Mafuta ya habbat soda yana asidi mafuta safi na yenye Omega 6 na 9, pia yana kirutubishi kingine mhimu zaidi kijulikanacho kama “phytosterols” ambacho husaidia kulazimisha kusinyaa na kutanuka kwa mishipa ya damu na hivyo kusaidia kuzuia damu kuganda na kujikaza katika ateri.

Viinilishe hivi pia husaidia kushusha lehemu kwenye damu na kiasi cha damu sukari.

Kwa karne nyingi mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kutibu matatizo mengi yanayohusiana na moyo.

2. Hupigana na maambukizi ya fangasi

Maambukizi ya fangasi yanatokea wakati bakteria wanapozidi juu ya ngozi yako na kupelekea kutokea kwa magonjwa mengi ikiwemo miwasho, upele na ukurutu.

Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda ni mazuri kwa tiba karibu kwa kila aina ya fangasi kitu kinachopelekea wanasayansi wengi kuamini kuwa habbat soda ni dawa ya asili na mbadala mhimu zaidi kwa kila mtu kuwa nayo nyumbani.

3. Hudhibiti Aleji (mzio)

Wengi wetu tunapatwa na aleji na kutokewa na chafya au mafua yasiyoisha na kupelekea kushuka kwa kinga yetu ya mwili. Kutumia mafuta asili ya habbat soda kwa ajili ya kutibu aleji kunaweza kuleta matokeo mazuri bila gharama kubwa.

Na siyo kwamba mafuta haya yatakupa nafuu kwa haraka sana dhidi ya aleji tu, bali pia yatakufanya kujisikia nafuu haraka zaidi kuliko dawa nyingine nyingi za kutibu aleji za viwandani zilizopo sokoni leo.

4. Ni mafuta mazuri kwa ajili ya ngozi yako

Iwe ni muonekano au afya ya ngozi kwa ujumla, ipo sababu kwanini watu wanapenda kuwa na ngozi ya kupendeza na yenye afya.

Mafuta ya habbat soda yana asidi mafuta mhimu zaidi, yana vitamini nyingi, yana viondoa sumu vya kutosha na asidi amino mhimu ambazo miili yetu huzihitaji.

Mafuta ya habbat soda ni mafuta safi ya ngozi kwa nyakati zote za siku na kwa siku zote. Mafuta haya pia yanasaidia ngozi kutokuungua moja kwa moja na miale ya jua huku yakizuia usizeeke haraka kwa kuondoa mikunjo yoyote kwenye ngozi yako.

5. Hutibu kansa ya ngozi (Melanoma)

Kansa ni matokeo ya kinasaba cha damu (DNA) kujizidisha au kujizalisha mara nyingi na kwa haraka zaidi dhidi ya uwezo wa kinga ya mwili. Mara nyingi kansa hutokeza vivimbe sehemu mbalimbali mwilini.

Mafuta ya habbat soda yana virutubishi vingine viwili ambavyo ni ‘thymoquinone’ na ‘thymohydroquinone’ ambavyo utafiti unaonyesha huwa vina uwezo wa kudhibiti kansa kwenye ngozi na kansa nyingine mbalimbali mwilini.

Hii ni kutokana na sifa yake ya haya mafuta katika kuzuia uvimbe na bakteria, sifa kuu mbili za habbat soda.

Habbat soda hufanya hivyo kwa kuzilenga seli zako nyeupe za damu kwa kuziongezea kinga ya mwili na hivyo kuua seli za kansa.

6. Hutibu chunusi

Chunusi ni matokeo ya moja kwa moja ya vivimbe kwenye ngozi hasa ya paji la uso na usoni kwa ujumla.

Mafuta haya yanaondoa uvimbe wa aina yoyote kwenye ngozi na kuitengeneza upya ngozi huku yakiiacha nyororo na muonekano wake wa asili.

Mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kwa ajili hii ya kutunza na kutibu maradhi mbalimbali ya ngozi na wafalme na malkia wengi katika historia yote ya dunia.

7. Hutibu maambukizi

Maambukizi ya aina yote hupigwa na kinga ya mwili hasa na seli nyeupe za damu ndizo zinazohusika na kazi hiyo.

Kwa kuiongezea nguvu kinga ya mwili moja kwa moja, mafuta ya habbat soda yanausaidia mwili wako kupigana na maambukizi kutoka kwenye nywele kichani mpaka kwenye kucha.

Hii ni sifa ya pekee ya habbat soda ambayo imekuwa ikijulikana kuwa nayo katika historia yote ya dunia tangu enzi hata leo bado ni moja ya dawa za asili zenye nguvu ya kupigana na maambukizi ya aina nyingi ya mwili.

8. Hutibu tatizo la ugumba

Ugumba unaweza kutokea kutokana na sababu nyingine nyingi, ingawa imethibitishwa pasipo na shaka kwamba mafuta ya habbat soda yamewasaidia wengi kuimarisha afya zao za uzazi.

Kwa wale wote wenye tatizo la uzazi au ugumba tambueni kuwa mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kutibu matatizo ya ugumba kwa zaidi ya miaka 2000 sasa.

Mpaka leo bado mafuta ya habbat soda yanaendelea kuripotiwa kama ndiyo dawa bora zaidi ya asili kwa ajili ya kurekebisha tatizo la ugumba kwa watu wa jinsia zote mbili.

Wakati huo huo mafuta ya asili ya habbat soda yamethibitika kuwa dawa bora zaidi ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake na hutibu tatizo la nguvu za kiume hata kama mwanaume utakuwa na umri wa miaka 120.

Unachohitaji ni kuyatumia kwa kipindi kirefu hata miezi miwili au hata zaidi mfululizo kama tatizo limekuwa sugu sana.

Ni mhimu vile vile kufanya vipimo kutambua ni nini hasa chanzo cha wewe kutopata ujauzito kabla hujaamua kujaribu dawa hii.

9. Huotesha nywele

Moja ya matumizi makubwa ya mafuta haya ni kuotesha nywele. Bidhaa nyingi sokoni zinazotumika kwa ajili ya kuotesha nywele zinaacha madhara makubwa zaidi kwa mtumiaji kuliko faida zake.

Kwahiyo kwa wale wenye tatizo la upala, nywele zisizokuwa na kwa wale ambao nywele zao hazina afya mnashauriwa kuchagua mafuta haya kwa matatizo haya yote.

Ingawa haieleweki ni kwa namna gani mafuta haya yanakuza nywele lakini wanasayansi wanaamini haya yanaweza kuwa ni matokeo ya uwezo wake mkubwa wa kuondoa sumu na protini nyingi ndani yake.

Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya nywele yenyewe ni meusi kabisa kabisa na huwa mazito kidogo tofauti na yale ya kunywa na kupakaa mwilini na hayatumiki kwa shughuli nyingine zaidi ya nywele.

10. Hutibu mafua na homa

Mafua na homa ni matokeo ya kushuka kwa kinga ya mwili na kadri unavyoendelea kuyavumilia magonjwa kama haya ndivyo unavyozidi kuidhoofisha zaidi kinga yako ya mwili.

Kama tulivyoona kabla kuwa mafuta ya habbat soda huongeza kwa haraka sana kinga ya mwili, huondoa haraka sumu mwilini na bakteria mbalimbali na hivyo kufanya kuwa ndiyo dawa nzuri ya asili dhidi ya mafua na homa za mara kwa mara.

11. Hutibu majipu

Liwe ni jipu moja au majipu mengi kwa pamoja, mafuta ya habbat soda ndiyo dawa nzuri kukupatia nafuu ya haraka. Hii ni kwa sababu kwa sehemu kubwa majipu ni matokeo ya maambukizi ya bakteria na mchafuko wa damu.

Na mafuta ya habbat soda ni wakala mzuri wa kuondoa bakteria na kusafisha damu na hivyo kuwezesha majipu kuwa chini ya ulinzi.

Unaweza kupakaa mafuta haya juu ya jipu moja kwa moja na wakati huo huo mengine unywe kama utakavyoelekezwa na Tabibu.

Hata hivyo ikiwa jipu ni kubwa sana na huoni nafuu hata baada ya kujaribu mafuta haya muone daktari kwa msaada zaidi.

12. Hutibu kikohozi na Pumu

Ile sifa yake kuu ya kuondoa vivimbe kwenye tyubu za koo, kitendo chake cha kuongeza kinga ya mwili, kuua bakteria na virusi ndiyo sababu za mafuta haya kutumika kutibu kikohozi na pumu.

Imeandikwa katika historia kuwa mababu wa zamani wa Misri walikuwa wakitumia mafuta ya habbat soda hasa kwa ajili ya kuimarisha afya ya mfumo mzima wa upumuwaji.

13. Hutibu kuharisha

Mara nyingi kuharisha ni matokeo ya maambukizi ya virusi na bakteria na kama tulivyoona mafuta ya habbat soda hudhibiti bakteria na virusi mbalimbali mwilini na hivyo kufanya ndiyo dawa nzuri mbadala kwa ajili ya kutibu au kuzuia kuharisha.

Huweka sawa mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na tumbo kwa ujumla na hivyo kuzuia mwili wako kupatwa na tatizo la kufunga choo.

14. Hutibu shinikizo la juu la damu

Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya shinikizo la juu la damu ni moja kati ya matumizi makubwa ya mafuta haya kwa sasa.

Ingawa haijathibitishwa rasmi kama dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu lakini wagonjwa wengi wa shinikizo la juu la damu wameripoti kushuka kwa kiwango kikubwa cha mashinikizo yao ya damu wakati wanapotumia mafuta haya ya habbat soda.

Tafiti kadhaa zimepelekea wengi kuanza kutumia mafuta ya habbat soda kama dawa ya asili kwa ajili ya kutibu shinikizo la juu la damu.

Pia hakikisha unakuwa na uzito sawa kulingana na urefu wako. BP ya juu inaweza kuchelewa kupona ikiwa uzito wako upo juu ya inavyotakiwa uwe nao.

15. Huondoa tatizo la kukosa usingizi

Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda ni dawa nzuri ya asili dhidi ya tatizo la kukosa usingizi na matatizo mengine kama hayo ya kuvuruga utulivu wa usingizi kwa ujumla.

Watu wengi wameripoti kupata usingizi mororo na utulivu kwa ujumla kwa kutumia habbat soda.

16. Huzuia mishtuko na kukakamaa kwa mishipa

Mafuta ya habbat soda ni dawa nzuri ya kuzuia kukakamaa na mishtuko mbalimbali kwenye mishipa. Unaweza kuyanywa mdomoni au unaweza kupakaa na kuchua moja kwa moja sehemu ya mishipa yenye matatizo kwa ajili ya matokeo mazuri ya haraka.

17. Huondoa kichefuchefu na mvurugiko wa tumbo

Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya kuondoa kichefuchefu na kuvurugika wa tumbo ni moja ya sifa nyingine kubwa ya mafuta haya.

Uwezo wa mafuta haya kutibu haya matatizo mawili unatokana na nguvu yake kuhamasisha vimeng’enya vyakula vya mwili wako na kuondoa gesi tumboni.

18. Dawa bora kwa matatizo ya meno

Dawa nyingine nzuri kwa matatizo ya meno kama jino kuuma, kuoza, kutoboka, kulegea nk ni mafuta ya asili ya habbat soda.

19. Huua seli za kansa ya damu

Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda yanacho kitu mhimu sana kiitwacho kwa kitaalamu kama “thymoquinone” ambacho huziua seli za kansa ya damu (leukemia HL-60 cells).

20. Hutibu saratani ya matiti

Mafuta ya habbat soda yana uwezo wa kuzuia seli za saratani ya titi kuendelea kujizalisha na inashauriwa kwa ajili ya kutibu saratani ya titi yatumike kwa kipindi kirefu miezi hata miwili au zaidi.

21. Hutibu saratani ya utumbo mpana

Kimeng’enya kiitwacho ‘thymoquinone’ kilichomo kwenye mafuta ya habbat soda na sifa yake kubwa ya kuondoa sumu ndivyo vitu viwili vinavyoyawezesha mafuta ya habbat soda kuzishambulia na kuziua seli za saratani ya utumbo mpana (colon cancer).

Yanabaki kuwa ndiyo dawa mbadala bora zaidi kwa saratani ya utumbo mpana inayosumbua watu wengi miaka ya karibuni.

Habbat soda si dawa ya magonjwa mengine mengi tu bali pia ni moja ya vitu mhimu sana katika kuzuia kukua, kujizidisha au kujizalisha upya kwa seli mbalimbali za kansa.

Uwezo wa mafuta ya habbat soda kudhibiti uongezekaji wa seli za kansa unashawishi sana kiasi kwamba madaktari wengi wamekiri kuwa ni dawa moja bora sana mbadala dhidi ya saratani ya kwenye utumbo mpana.

22. Hutibu fangasi ya ngozi na mapunye

Fangasi, mapunye, ukurutu na magonjwa mengi ya ngozi yanaweza kutibika kwa kutumia mafuta ya habbat soda.

Fangasi na mapunye ni tatizo linalowapata watu wengi karibu kila sehemu katika nchi tajiri hata katika nchi maskini pia.

Unaweza kuyanywa mdomoni na wakati huo huo ukapaka moja kwa moja juu ya ngozi sehemu yenye tatizo kwa majuma kadhaa kama utakavyoelekezwa na Tabibu.

23. Husaidia kupunguza uzito

Uwezo wa mafuta ya habbat soda kushusha uzito unatokana na sifa yake ya kuweza kupunguza sukari katika damu.

Zaidi ya kuwa ni wakala muondoa sumu mwilini wa asili, mafuta ya habbat soda husaidia pia kuongeza nguvu katika mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kupunguza kiasi chako cha njaa.

Hii ya kudhibiti kiasi cha njaa ni mhimu sana hasa wakati unataka kudhibiti mfumo wa vyakula unavyokula.

24. Hutibu Kisukari

Kitu gani kimeyafanya mafuta ya habbat soda kuwa ndiyo dawa nzuri ya asili dhidi ya Kisukari? Ni ule uwezo wake mkubwa wa kushusha shinikizo la damu na kusaidia wagonjwa wa Kisukari wote ambao ni tegemezi au si wategemezi wa insulin.

Ni dawa nzuri kwa watu wote wenye kisukari aina ya kwanza na kisukari aina ya pili kwa wakati mmoja.

Pia huboresha kwa ujumla AFYA ya damu yako.

25. Hutibu kifafa na mishtuko ya moyo

Dawa nyingi za kisasa zinazotumika kutibu kifafa na mishtuko ya moyo huwa zina orodha ndefu ya madhara mabaya (negative side effects) pia.

Bahati nzuri kwa upande wako wewe unayesoma makala hii ni kuwa mafuta ya asili ya habbat soda (black seed oil) ni dawa nzuri ya kutuliza kifafa na matokeo yaletwayo na kifafa.

Baadhi ya tafiti zimeonyesha watu wenye kifafa na mishtuko ya moyo waliacha kuonyesha tabia au dalili za kifafa au mishtuko ya moyo walipotumia mafuta ya habbat soda kwa wiki 4 hadi 6 huku wakitumia sambamba na dawa walizopewa hospitalini.

Watafiti wengi wanasema hii ni kutokana na kiinilishe mhimu kilichomo kwenye mafuta haya kijulikanacho kama ‘thymoquinione’.

26. Hutibu vidonda vya kooni

Mafuta ya habbat soda yamethibitishwa kutibu vidonda vya kooni (tonsils) na kuondoa kila aina ya maumivu kooni na kuondoa uhitaji wa dawa za kuondoa maumivu (pain killers).

27. Hutibu kidonda ndugu (MRSA)

Kidonda ndugu au kama kinavyojulikana kwa kitaalamu kama ‘Methicillin resistant Staphylococcus aureus (MSRA)’ ni ugonjwa unaoendelea kuwasumbua wataalamu wengi katika mahospitali maeneo mengi duniani.

Mara nyingi hutokea kama matokeo ya kudhoofika kwa kinga ya mwili. Uwezo wa kuondoa uvimbe na sumu wa mafuta haya unayafanya kuwa dawa mbadala yenye ufanisi zaidi katika kutibu kidonda ndugu.

Mafuta ya habbat soda yatakusaidia kutibu kidonda cha aina hii bila shida yoyote, yatazuia pia kuendelea kuongezeka au kusambaa zaidi kwa kidonda hiki.

Kama kuna matumizi mhimu sana ya dawa hii basi ni hili la kutibu vidonda mbalimbali ikiwemo kidonda ndugu kidonda ambacho huletwa na bakteria na kuwa sugu kutibika kwa dawa nyingi za kawaida.

28. Huondoa utegemezi wa madawa ya kulevya

Kutumia mafuta ya habbat soda kuondoa utegemezi (uteja) kwa madawa ya kulevya na vilevi vingine ni moja ya kazi nyingine zilizothibitika kufanywa na mafuta haya.

Katika majaribio, mafuta ya habbat soda yameonyesha kuwa msaada mkubwa kutuliza hali ya kujisikia vibaya na mauzauza mengine yatokanayo na kuacha kutumia dawa za kulevya na wakati huo huo yameonyesha kudhibiti hamu ya kutaka kurudia tena matumizi ya madawa ya kulevya baada ya mtu kuamua kuacha.

29. Huondoa makovu

Iwe ni makovu ya upasuaji uliopita au ni makovu mengine yoyote, mafuta ya habbat soda ndiyo dawa nzuri kwa ajili ya kuondoa makovu. Ni moja kati ya dawa mbadala chache ambazo zimethibitishwa kuondoa na kutibu makovu moja kwa moja.

30. Hutibu kansa ya mlango wa kizazi

Kansa nyingine ambayo mafuta ya habbat soda yamethibitika kuitibu ni kansa ya mlango wa kizazi (cervical cancer).

Hii tena inawezekana kutokana na kimeng’enya ‘thymoquinione’ kipatikanacho kwenye haya mafuta, tafiti zinaonyesha kuwa husaidia pia kwa kuziongezea nguvu na idadi seli nyeupe za damu na kuzidhibiti seli za kansa kuendelea kujizalisha.

31. Huzuia madhara ya miale ya jua

Tafiti zinaonyesha kuwa watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda na kukaa kwenye jua masaa mengi walipatwa na madhara machache ya miale ya jua kulingalisha na wale ambao walikaa juani muda mrefu bila kutumia habbat soda.

Kiasi kikubwa cha kinga ya mwili kilionekana kwa watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda.

Kuna tafiti pia zinazothibitisha habbat soda kuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wa kansa walio kwenye matibabu ya mionzi.

32. Huzuia na kutibu athari za sumu ya risasi

Sumu ya risasi (lead) ndiyo moja ya sumu zinazowapata watu wengi dunia nzima sababu ya maendeleo ya viwanda na matumizi ya madawa ya mashambani.

Risasi inaweza kuleta shida na mambo mengi kuhusiana na kazi za mwili wako kwa ujumla na kuleta matatizo katika moyo, tumbo, figo, mfumo wa fahamu, mifupa na hata katika mfumo wako wa uzai.

Tafiti zimeonyesha kwamba mafuta ya habbat soda kuwa na uwezo mkubwa kuzuia na kurekebisha madhara katika ubongo yaliyotokana na sumu ya risasi.

33. Huimarisha ukuwaji wa ndevu

Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda yanaweza kuhamasisha ubora na ukuwaji wa ndevu kidevuni.

Ingawa hii siyo kazi yake hasa ya msingi, unaweza kupakaa moja kwa moja mafuta ya habbat soda ya nywele juu ya kidevu chako na utaona ndevu zinakuwa na afya nzuri, zinakuwa haraka na kuziacha zenye unyevunyevu pia.

34. Hutibu maumivu ya kuumwa na nyuki na nyigu

Unga wa habbat soda ukichanganywa na maji kidogo ni dawa nzuri kabisa ya asili kwa maumivu au uvimbe kutokana na kuumwa na wadudu kama nyigu na nyuki. Chua sehemu iliyoathiriwa na mchanganyiko huu kama utakavyoelekezwa na Tabibu.

35. Huondoa msongamano kifuani

Mwagia na uchue kwa dakika kadhaa juu ya kifua chako na mafuta ya habbat soda kuondoa msongamano (makohozi, gesi nk) kifuani.

Utapata matokeo mazuri zaidi kama utachanganya mafuta haya na asali kwa ajili ya hili zoezi.

Unaweza pia kuamua kunywa mdomoni kijiko kidogo kimoja cha chai kila siku badala ya kupaka juu ya kifua.

36. Hutibu maumivu ya sikio

Mafuta ya habbat soda yakichanganywa na mafuta ya zeituni yanaweza kutibu maumivu ya sikio na miwasho mingine masikioni.

37. Dawa nzuri ya magonjwa ya macho na kuona

Mafuta ya habbat soda yanaweza kutumika pia kutibu maambukizi ya kwenye macho na wakati huo huo kuongeza uwezo wa macho kuona (eyesight and vision).

Yametumika pia na watu wengi kutibu maambukizi ya kwenye macho yao ambayo hupelekea macho kuwa mekundu.

Ili kutibu hayo unaweza utapakaa mafuta haya sehemu zinazozunguka jicho lako kabla ya kwenda kulala na unaweza kufanya zoezi hili kila siku au kadri utakavyoelekezwa na Tabibu.

38. Hutibu kiharusi

Unapougua kiharusi hasa usoni, mafuta ya habbat soda yanaweza kuleta nafuu haraka.

39. Huondoa msongamano puani

Habbat soda pia hutumika kuzibua na kuondoa msongamano puani. Hii ni moja ya kazi ambayo mafuta haya yanazifanya vizuri zaidi.

40. Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo

Kutumia mafuta ya habbat soda kwa ajili ya kuondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo ni njia nzuri ya kuondoa maumivu na mawe katika kibofu cha mkojo kwa pamoja.

Uwezo mkubwa ulionayo mafuta haya katika kuondoa vivimbe na sifa yake ya kuondoa sumu ndivyo vitu vinavyoyafanya mafuta haya kuwa dawa bora ya asili ya kuondoa mawe katika kibofu cha mkojo.

41. Huondoa mawe katika Ini

Kama ilivyo kwa mawe katika kibofu cha mkojo, mawe katika ini pia yanaweza kusababisha maumivu na madhara mengine makubwa wakati ukijitibu kwa kutumia dawa za viwandani.

Sifa za mafuta ya habbat soda huondoa mawe katika ini kwa hali ya mwendelezo mpaka yatakapoondoka yote.

Kunywa mafuta haya yakichanganywa na asali hutoa matokeo mazuri zaidi.

42. Huondoa gesi tumboni

Mafuta ya habbat soda huusaidia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula na hivyo kukusaidia kuondoa gesi. Pia yamethibitika kuondoa mvurugiko wa tumbo na takataka nyingine tumboni kwa haraka zaidi.

43. Hutibu bawasiri

Dawa nyingi zinazotumika kutibu bawasiri zina madhara mengine mabaya na nyingi ya hizo hazitibu kabisa bawasiri na kulazimisha wengine kufanya upasuaji.

Mafuta ya habbat soda kwa upande wake yanatoa suluhu ya haraka katika kutibu bawasiri zote ya nje nay a ndani na tafiti zinaonyesha yanao uwezo wa kuzuia kusambaa au kuongezeka kwa ugonjwa huu.

44. Huondoa maumivu ya kichwa

Faida nyingine mhimu ya mafuta ya habbat soda ni uwezo wake katika kutibu maumivu ya kichwa na kipanda uso. Kwa karne nyingi Waarabu na Wazungu wamekuwa wakitumia mafuta haya kwa kupaka maeneo ya karibu na pua, macho na sehemu ya mbele ya kichwa pia kuyanywa ili kuondoa maumivu ya kichwa.

Pia yale meusi kwa ajili ya nywele nayo yanaondoa maumivu ya kichwa na hili nimelishuhudia mimi mwenyewe nilikuwa na tatizo la kuumwa kichwa mara kwa mara sababu ya kukaa kwenye computer masaa mengi lakini tangu nianze kutumia mafuta haya sijawahi kuumwa kichwa tena.

45. Huongeza kinga ya mwili

Unaweza kutumia mafuta ya habbat soda kuimarisha kinga yako ya mwili kwa ujumla na hivyo kuongeza ulinzi wa mwili wako dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo dhidi ya bakteria na virusi.

Mafuta ya habbat soda ndiyo bidhaa pekee ya asili iwezayo kuimarisha kinga yako ya mwili kwa muda mfupi.

Unaweza kutumia pia mafuta haya hata kama huumwi chochote.

46. Husaidia mama anayenyonyesha

Mafuta ya habbat soda yakitumika na mama anayenyonyesha husaidia kuongezeka kwa uzalishwaji wa maziwa.

47. Huongeza kumbukumbu

Utafiti unaonyesha kuwa mafuta ya habbat soda yana uwezo wa kuongeza uwezo wako wa kumbukumbu, ufahamu na umakini.

Karibuni imethibitika habbat soda yanaweza kuongeza uwezo wa kukumbuka vitu kwa haraka vikiwemo vya muda mfupi na hata vile vya muda mrefu.

48. Huondoa madoa meusi kwenye ngozi

Moja ya kazi za mafuta ya habbat soda ambazo wengi hawazijuwi ni hii ya kuondoa madoadoa au mabaka meusi juu ya ngozi.

Unachohitaji ni kuyatumia mafuta haya na hutachelewa kuona matokeo.

49. Huondoa maumivu ya kung’atwa na wadudu

Wadudu kama mbu na wengine wanapokuuma huacha pia maumivu fulani na hata uvimbe.

Kupaka mafuta haya juu ya eneo lililoathirika kutasaidia kuondoa maumivu na uvimbe au muwasho wowote sababu ya wadudu hao.

50. Hutibu kukauka kwa midomo (Lips)

Tatizo hili la midomo ya nje (lips) kukauka limepelekea kutengenezwa kwa bidhaa nyingi za viwandani kwa ajili hiyo na wanawake ndiyo wanaonekana kuzitumia zaidi huku baadhi ya bidhaa hizo zikiripotiwa kusababisha baadhi ya saratani.

Mafuta mhimu (essential oils) yapatikanayo katika mafuta ya habbat soda yanaweza kuzuia kukauka kwa mdomo na kuzalisha upya ngozi kwenye sehemu za nje ya mdomo (lips) na kukuachia rangi safi ya asili ya lips zako bila madhara yoyote mabaya hapo baadaye.

51. Yanatibu kufunga choo

Kama vile yanavyokusaidia katika mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula ndivyo yanavyokusaidia pia kwa tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

Kuna watu wengine asipopata choo hata siku mbili haoni kama ni tatizo kwake na mwingine amezoea kupata choo kigumu kila siku na anaona ni kawaida tu.

Kufunga choo au kupata choo kigumu sana kila mara ni ishara mbaya kuhusu afya yako.

Mafuta ya habbat soda yanatibu tatizo la kufunga choo (constipation) bila shida yoyote.

52. Hutibu maumivu ya mgongo na mishipa

Unaweza kupunguza mahitaji ya dawa za kuondoa maumivu ya mgongo na mishipa kwa kupaka au kujichua na mafuta ya habbat soda sehemu yenye maumivu moja kwa moja.

Hutakawia kuona nafuu kwa haraka.

53. Husaidia kuondoa maumivu ya tumbo

Kwa matatizo mengi ya tumbo, mafuta ya habbat soda yanaweza kuwa msaada mkubwa wa kukupa nafuu kwa haraka.

Kuondoa maumivu ya tumbo ni moja ya kazi kubwa inayotambulika na wengi ya mafuta ya habbat soda.

54. Huondoa maambukizi kwenye fizi

Maumivu na maambukizi kwenye fizi za meno vinaweza kuondolewa kwa kutumia mafuta ya habbat soda.

Uwezo wake wa kuondoa sumu na uvimbe ndiyo sababu ya madaktari wengi kupendekeza itumike kutibu maambukizi kwenye fizi.

55. Hutibu U.T.I

Maambukizi na matatizo mengi kwenye kibofu cha mkojo na njia ya mkojo kwa ujumla yanatibika na mafuta ya habbat soda ikiwemo ugonjwa wa U.T.I (yutiai) unaowasumbua watu wengi miaka ya karibuni.

56. Huzuia mdomo kukauka

Kutibu tatizo la mdomo kukauka chukua kijiko kidogo kimoja cha mafuta haya na weka mdomoni kwa sekunde 30 hivi.

Jigeuzegeuze kichwa na mdomo kuhakikisha mafuta yanagusa kila sehemu za mdomo wako kabla ya kutema au unaweza hata kuyameza.

Kisha safisha mdomo na kinywaji kingine kitamu kama juisi hivi au asali kuondoa radha yake ya ukakasi.

57. Huzuia pua kuvuja damu

Haya ni moja ya matumizi ya asili ya mafuta ya habbat soda nyakati za joto katika majira ya kiangazi katika jamii nyingi mashariki ya kati.

58. Huondoa majeraha ya kuungua moto

Kupaka mafuta ya habbat soda juu ya majeraha ya kuungua kwa moto au maji ya moto kumethibitika kuponya majeraha hayo na kuzalisha upya ngozi.

Ukiacha Kuondoa majeraha, mafuta ya asili ya habbat soda huondoa pia maumivu haraka na kuizalisha upya ngozi yako.

59. Hutibu mba kichwani

Mafuta haya si mazuri kwa ajili ya kukuza au kuotesha nywele zako tu, bali pia huhamasisha ukuwaji wa vinyweleo vya ngozi na hata kuzuia na kutibu mba.

Na mafuta haya unapoweka kichwani yanadondoka kidogo kidogo hadi kwenye ubongo na utaona vitu kama maumivu ya kichwa vinaanza kuisha taratibu.

60. Huondoa maumivu kwenye maungio

Moja ya matumizi yanayojulikana na wengi zaidi ya mafuta ya habbat soda ni kutibu maumivu ya kwenye maungio (joints) mbalimbali mwilini.

Utapata nafuu ya haraka ukitumia mafuta haya kuondoa maumivu katika maungio.

61. Huzuia kudhurika kwa figo kama matokeo ya Kisukari

Ukiacha ukweli kwamba mafuta ya habbat soda ni dawa mbadala nzuri kabisa ya kutibu Shinikizo la juu la damu na Kisukari pia ni dawa ya kuzuia kudhurika kwa figo kama matokeo ya kuugua ugonjwa wa kisukari.

Sababu ya hili ni kutokana na viinilishe mhimu sana vilivyomo kwenye habbat soda ambayo hujulikana pia kama ‘nigella sativa’ au ‘black seeds’.

62. Huweka sawa mzunguko wa hedhi

Mafuta haya yana kazi mhimu sana linalopokuja suala la kulinda na kutibu matatizo mbalimbali ya uzazi.

Matatizo karibu yote ya uzazi kama maumivu ya tumbo chini ya kitovu, siku za mwezi zisizoeleweka au kutokuwa na mzunguko maalumu, kukosa hedhi, matatizo katika mfuko wa uzazi na hata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Ni dawa nzuri kutumika hata kwa wamama wakubwa wanaopatwa na matatizo kutokana na kusimama kuona siku zao.

63. Mazuri wakati wa ujauzito

Inasisitizwa kuwasiliana na daktari wako wakati wa ujauzito kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote.

Hata hivyo mafuta ya habbat soda yameonyesha matokeo chanya hata yakitumika wakati wa ujauzito ingawa bado hakuna hitimisho la jumla ikiwa yatumike kwa mama mjamzito au yasitumike sababu katika baadhi ya kesi yanaonyesha kupunguza kukazika kirahisi kwa misuli ya mfuko wa nyumba ya uzazi.

Mhimu: usitumie habbat soda kama mjamzito bila uangalizi wa karibu wa Tabibu.

64. Hutibu baridi yabisi (Arthritis)

Mafuta ya habbat soda yamethibitika kuwa dawa bora dhidi ya ugonjwa wa baridi yabisi, maumivu kwenye mishipa na hali ya mwili kuwaka moto kwa ujumla.

65. Hutibu vidonda vya tumbo

Ni moja ya dawa za asili chache zinazoweza kutibu vidonda vya tumbo moja kwa moja.

Tafiti nyingi zinathibitisha mafuta ya habbat soda yanatibu aina zote za vidonda vya tumbo!

Kumbuka pia kunywa maji mengi ya kutosha kila siku, epuka pia vinywaji na vyakula vyenye asidi nyingi.

66. Yanaondoa maumivu mbalimbali

Mafuta ya habbat soda yanaondoa mahitaji yako kwa dawa nyingi za kuondoa maumivu (painkillers) mbalimbali mwilini.

Katika kesi nyingi mafuta ya habbat soda yanaweza kuondoa kabisa mahitaji ya dawa za kuondoa maumivu.

Uwezo wake wa kuondoa vivimbe unayafanya kuwa chaguo zuri zaidi katika kutibu maumivu yote ya mwili wako kutoka kwenye nywele mpaka kwenye kucha.

67. Hutibu kansa ya Ubongo

Mafuta ya habbat soda ni msaada mkubwa katika kudhibiti na kusambaratisha vivimbe kwenye ubongo na seli za kansa kwenye ubongo wako.

Makundi kadhaa ya watafiti wamehitimisha kuwa mafuta ya habbat soda ni dawa halali ya asili kwa ajili ya kutibu kansa ya ubongo na uvimbe katika ubongo.

68. Yanapunguza wasiwasi (Anxiety)

Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda kuwa msaada mkubwa katika kudhibiti tabia za kuhamaki na wasiwasi na hivyo kukuwezesha kujisikia vizuri kila mara.

Na utaona matokeo haya baada ya matumizi ya habbat soda kwa siku 30 hivi.

69. Huondoa huzuni na mfadhaiko (stress)

Tafiti kadhaa zimeonyesha watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda wanakuwa ni watu wenye furaha ya asili na kuwa si wepesi kuwa na huzuni au kufadhaika.

Kazi hii ya mafuta ya habbat soda ndiyo mhimu kuliko zote sababu mamilioni ya watu wanakabiliwa na tatizo la kuwa na huzuni au stress na mifadhaiko ya akili kitendo ambacho kinaweza kuharibu kinga zao za mwili na maisha kwa ujumla.

Ni vigumu sana kupata mtishamba ambao unaweza kutibu matatizo yanayohusiana na saikolojia moja kwa moja lakini mafuta ya habbat soda yanaweza kutumika kwa dhumuni hili la kutuliza, kupunguza na kutibu tatizo la huzuni au kufadhaika kwa akili.

70. Hutibu kizunguzungu

Historia nyingine katika matumizi ya mafuta ya habbat soda ni katika kutibu kizunguzungu.

71. Hutibu Kiungulia

Faida nyigine kubwa ya mafuta ya habbat soda ni kuwa ni dawa ya asili dhidi ya kiungulia. Ingawa kuna tafiti chache zinazoweza kuthibitisha hili, bado historia inaonyesha mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kutibu kiungulia kwa karne nyingi.

72. Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu

Kumekuwa na tafiti nyingi hivi karibuni ambazo zimeonyesha mafuta ya habbat soda kuwa msaada mkubwa kwa kuzuia na kupunguza kuongezeka kwa dalili za ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

73. Hutibu homa ya uti wa mgongo

Nguvu za mtishamba huu zimethibitika kuwa msaada mkubwa katika kutibu homa ya uti wa mgongo (meningitis).

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa mafuta ya habbat soda ni moja ya tiba asili nzuri zaidi kwa ajili ya homa ya uti wa mgongo inayoaminiwa hadi sasa.

74. Huongeza afya ya figo

Kuanzia kwenye ugonjwa wa figo hadi kwenye mawe ya kwenye figo, mafuta ya habbat soda yamethibitika kuwa msaada mbadala kwa matatizo ya figo.

75. Huimarisha afya ya mbegu za kiume

Ukiacha uwezo wake katika kuongeza stamina na nguvu kwa wanaume na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake, mafuta haya pia hutumika kutibu tatizo la afya dhaifu la mbegu za kiume na kuongeza wingi wake kwa ujumla (semen count).

Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali, mbegu za kiume zinaonekana kuimarika na kuwa nyingi za kutosha baada ya kutumia dawa hii kwa miezi miwili kila siku.

76. Huimarisha mifupa

Tafiti zimeonyesha kuwa mafuta ya habbat soda yanaongeza ukuwaji wa seli za uboho wa kwenye mifupa kwa asilimia 150 yanapotumika. Hii ni kwa mjibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa kwa watu wengi mbalimbali.

Kile kinashangaza zaidi ni kuwa mafuta haya yameonekana kuwa na uwezo wa kuzuia uongezekaji wa vivimbe mbalimbali walau kwa zaidi ya asilimia 50.

77. Tiba asili ya chango kwa watoto

Ukiwa na mtoto anayesumbuliwa na chango au msokoto wa tumbo linaweza kuwa ni jambo linalokupa msongo wa mawazo maishani.

Ingawa visababishi vya chango kwa watoto bado havijulikani bayana, kile ambacho kimethibitishwa ni kuwa mafuta ya habbat soda ni tiba asili kwa chango au msokoto wa tumbo kwa watoto.

Mhimu: Usimpe mtoto dawa yoyote bila maelezo na uangalizi wa karibu wa Tabibu.

78. Hurekebisha matatizo katika tezi dume

Afya ya tezi dume ni ishu kwa wanaume wengi duniani kote na kupata dawa ya asili nzuri kwa ajili hiyo inaweza kuwa mtihani kwa wengi.

Kwa bahati nzuri mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kwa ajili ya kuimarisha afya ya tezi dume kwa karne nyingi sasa.

Tafiti zinaonyesha kuwa ni dawa nzuri hata kwa saratani ya tezi dume.

79. Huondoa udhaifu wa mwili kwa ujumla (lethargy)

Wengi wetu tunapatwa na kupungukiwa na nguvu za mwili na wakati fulani nguvu zote za mwili kwa ujumla na nguvu za ubongo na za kiroho pia.

Kwa ajili ya matatizo ya udhaifu wa mwili iwe kimwili, kiakili na hata kiroho hakuna dawa nyingine ya asili iwezayo kurekebisha hali hizo kama yawezavyo kufanya hivyo mafuta asili ya habbat soda.

80. Huondoa uchovu sugu

Kutoka kwenye maelezo yaliyotangulia hapo juu, mafuta haya pia yamethibitika kuondoa uchovu sugu wa aina zote na kuupa nguvu mpya mwili.

81. Huhamasisha uzalishwaji wa mkojo

Faida nyingine kubwa ya mafuta ya habbat soda ni uwezo wake wa kuhamasisha uzalishwaji wa mkojo.

Matatizo mengi ya kibofu cha mkojo na tezi dume yamekuwa yakitibiwa kwa kutumia mafuta ya habbat soda kwa zaidi ya miaka 2000 sasa na tafiti zimethibitisha hivi karibuni faida hizi za mafuta ya habbat soda katika majaribio ya kimaabara yakionyesha kuimarisha sana kwa afya ya tezi dume na kazi zake kwa ujumla.

82. Huzuia madhara yatokanayo na shambulio la moyo

Kama tulivyoona pale mwanzo kabisa kuwa mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika miaka mingi kutibu matatizo mbalimbali ya moyo, vivyo hivyo yameonekana kuzuia madhara ya pili yatokanayo na shambulio la moyo (heart attack) na magonjwa mengine kwenye mfumo wa upumuwaji kwa ujumla.

83. Husaidia kuongeza damu mwilini

Wengi wetu tunakumbwa na tatizo la kupungukiwa damu (anemia) na hili linaweza kuiweka miili yetu katika hali ya hatari zaidi. Kwa mara nyingine tena mafuta ya habbat soda yanaonekana kuokoa tatizo hili baya la kiafya.

Yamethibitika kutibu tatizo la upungufu wa damu moja kwa moja.

84. Huondoa vimelea vya magonjwa

Mafuta ya habbat soda ni kinga dhidi ya vimelea (parasites) vingi vya magonjwa na huvitafuta na kuviua vimelea hivi popote vitakapokuwa ndani ya mwili.

Hufanya kazi hii kwa kuvilevya hivyo vimelea na kuupa urahisi mwili kuviangamiza.

85. Husaidia kupunguza uzito

Kwa sababu uzito na unene kupita kiasi huhusiana pia na matatizo mengine ya kutofanya kazi kwa kinga ya mwili, ukaidi wa insulin, kansa na matatizo mengi katika mfumo wa upumuwaji, ndipo mafuta ya habbat soda yanapokuja kuwa mhimu kwa ajili ya kupunguza uzito na unene kupita kiasi.

Mafuta ya habbat soda yamethibitika na watafiti wengi kote duniani kuwa msaada mkubwa kwa wale wanaotaka kupunguza uzito.

86. Huziua seli za kansa za aina nyingi

Hutibu na kuziua seli za karibu kansa za aina zote, kansa ya mdomoni, kansa ya ini, kansa ya kongosho nk.

Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda kuwa dawa nzuri dhidi ya kansa mbalimbali mwilini kwa kuzuia uongezekaji wa seli za kansa na kusambaratisha kansa zenyewe katika baadhi ya kesi.

Hufanya kazi hii kwanza kwa kuiimarisha kinga yako ya mwili na kuziua seli zenyewe za kansa moja kwa moja.

87. Huongeza afya ya ini

Mafuta ya habbat soda yanaimairisha afya ya ini kwa ujumla na kuimarisha kinga ya mwili. Ni dawa nzuri kutibu matatizo mengi ya ini hata kama familia yenu wote mna historia ya kuugua ugonjwa wa ini.

88. Huondoa sumu mwilini

Tatizo la mwili kuwa na sumu ni tatizo kubwa kwa watu wengi miaka ya karibuni na kupata mtishamba au dawa ya asili kwa ajili ya kuondoa sumu bado ni mtihani kwa watu wengi. Kwa bahati nzuri kwa upande wako umepata mafuta ya habbat soda.

Mafuta ya habbat soda yamethibitika kuondoa sumu kila sehemu ya mwili yanapotumika.

89. Huondoa hali ya kuchanganyikiwa (Schizophrenia)

Kutokana na sifa yake ya kuondoa vivimbe na sumu mwilini mafuta ya habbat soda yanaweza kutumika pia kutibu ishara na dalili za kuchanganyikiwa.

Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda yakitumiwa na watu wenye kuchanganyikiwa wanapata nafuu haraka ya tatizo hilo ukilinganisha na wale wasiotumia mafuta haya.

MHIMU: Usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa Tabibu.

Hitimisho:

Ni rahisi kuelewa kuwa faida nyingi ambazo mafuta ya habbat soda inazo zinawashangaza bado watu wengi.

Unaweza kudhani hayo hayawezekani kwa mtishamba wa asili kutoa tiba kwa magonjwa mengi namna hiyo! Kile ninachojuwa ni kuwa ukweli hujieleza wenyewe.

Kiasi cha faida kinachopatikana katika mafuta haya ukilinganisha na bei yake ndicho kinachowafanya watu wengi wabaki na mshangao usioisha!

Watu wengi wanashangaa ni kwanini makampuni mengi ya madawa yatumie mabilioni ya pesa kutengeneza dawa mbalimbali kwa magonjwa mengi ambayo yangeweza kutibika kwa kutumia mafuta ya habbat soda tu kama tulivyoona hapo juu.

Ukiacha hayo, kupata hospitali na ukapata matibabu sahihi na kwa gharama nafuu bado ni changamoto katika nchi nyingi maskini na nyingi ya dawa zinakulazimu kuendelea kuzitumia kwa kipindi kirefu na pengine bila hata uhakika wa wewe kuja kupona.

Bahati nzuri kwa wewe ambaye umebahatika kupata habari hizi za habbat soda na umeweza kuona ni magonjwa mangapi unaweza kutumia kujikinga na kujitibu nayo.

Na jambo zuri kuliko yote ni kuwa huhitaji kutoka hata jikoni kwako ili kupata nafuu ya ugonjwa wowote ukiwa na mafuta ya habbat soda karibu yako.

Mtishamba huu wa ajabu utaendelea kubaki kwenye vitabu vizazi na vizazi vingi vijavyo kama moja ya tiba asili mhimu zaidi iliyowahi kujulikana na binadamu.

Unahitaji mafuta ya asili ya habbat soda au unga wa habbat soda? Niachie ujumbe WhatsApp +255714800175. Mimi Napatikana TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam., naweza pia kukuletea ulipo bure ndani ya Dar na natuma pia popote ulipo nje ya Dar..

Elewa mafuta haya na hata unga wake ni vitu visivyopatikana kirahisi na ni vitu visivyojulikana na watu wengi, usipokuwa makini utauziwa feki. Vile vile siwajibiki na lolote juu ya matumizi au mambo yanayokutokea wakati unatumia dawa hii ikiwa hujanunua kutoka kwangu moja kwa moja.

SHARE post hii kwa ajili ya wengine

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 8

Imehaririwa mwisho

Let's block ads! (Why?)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...