Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
42-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Kigezo Kizuri Kwa Anayetaka Kufaulu Aakhirah
Allaah (سبحانه وتعالى) Amemjaalia Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa na tabia njema zilokamilika nazo ni kigezo kwa yeyote yule anayetaka kufuzu Aakhirah kwa kuingizwa Jannah (Peponi) na kuepushwa na Moto. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ
Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Rasuli wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho [Al-Ahzaab: 21]
Imaam As-Sa’dy (رحمه الله) amesema kuhusu kauli hiyo ya Allaah (سبحانه وتعالى):
“Mwenye kufuata kigezo chake amefuata njia ya kumfikisha katika Utukufu wa Allaah na hiyo ndio Njia Iliyonyooka. Na kigezo hicho kizuri hukifuata na kupata tawfiyq kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho, kwa sababu ya kuwa kwake na iymaan, khofu ya Allaah, kutaraji thawabu na khofu ya adhabu Yake, basi hujihimiza kufuata kigezo cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).” [Tafsiyr As-Sa’dy]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni