Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
43-Unyenyekevu Wake Anapokutana Na Mtu Na Kusalimiana Naye
Na Anapoketi Na Mtu
Miongoni mwa khulqa zake njema (صلى الله عليه وآله وسلم) na unyenyekevu wake, hakuwa akimgeuzia mtu uso wake mpaka yule mtu ageuke kwanza, na pindi mtu anapompa mkono kumsalimia, hakuwa akiondosha mkono wake hadi yule mtu aondoshe mkono wake, na pia hakuwa akiketi kwa magoti mbele ya mtu aliyeketi kwa magoti:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا لَقِيَ الرَّجُلَ فَكَلَّمَهُ لَمْ يَصْرِفْ وَجْهَهُ عَنْهُ حَتَّى يَكُونَ هُوَ الَّذِي يَنْصَرِفُ، وَإِذَا صَافَحَهُ لَمْ يَنْزِعْ يَدَهُ مِنْ يَدِهِ حَتَّى يَكُونَ هُوَ الَّذِي يَنْزِعُهَا، وَلَمْ يُرَ مُتَقَدِّمًا بِرُكْبَتَيْهِ جَلِيسًا لَهُ قَطُّ - ابن ماجه
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema: “Pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anapokkutana na mtu, huwa hamgeuzii uso wake hadi yule mtu awe ndiye mwenye kugeuza uso wake. Na pindi anapompa mtu mkono, alikuwa hauondoshi hadi yule mtu auondoshe mwenyewe. Na hakuwa akionekana kamwe ameketi kwa magoti yake mbele ya magoti ya yule aliyekuwa amekaa kando yake. [Ibn Maajah
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni