Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.”[Al-Maaidah: 72]
Na Hadiyth zifuatazo:
عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَدْعُو مِنْ دُونِ اللهِ نِدَّاً دَخَلَ النَّارَ )) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Mas-‘uwd (Radhwiya Alaahu ‘anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayekufa akiwa katika hali ya kumuomba asiyekuwa Allaah kumfanyia mlinganishi (mshirika) ataingia Motoni))[Al-Bukhaariy na Muslim]
Kutoka kwa Ibn Mas‘uwd pia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayefariki akiwa katika hali ya kumshirikisha Allaah kwa chochote ataingia Motoni))[Al-Bukhaariy 1238, Muslim 92]
Pia:
عن جابر رضي الله عنه: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((مَنْ لَقِي اللهَ لاَ يُشْرِك بِهِ شَيْئاً دَخَلَ الْجَنَّة، وَمَنْ لَقِيَه يُشْرِك بِهِ شَيْئاً دَخَلَ النَّار))
Imetoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Atakayekutana na Allaah akiwa hamshirikishi na chochote Ataingia Jannah, na atakayekutana Naye akiwa anamshirikisha na chochote ataingia Motoni)) [Muslim 94.]
Na pia:
عَن أَبي ذَرٍّ رضي الله عنه عنِ النَّبيِّ صلَّى اللَّهُ عليهِ وسلَّمَ؛ أنَّهُ قالَ: ((أتاني جبريلُ عليهِ السَّلامُ فبشَّرَني أنَّهُ من ماتَ من أمَّتِكَ لا يشرِكُ باللَّهِ شيئًا دخلَ الجنَّةَ)) قلتُ: وإن زنَى وإن سرقَ؟ قالَ: ((وإن زنَى وإن سرقَ))
Kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Amenijia Jibriyl ‘alayhis-salaam akanibashiria kwamba atakayefariki katika Ummah wangu akiwa hamshirikishi Allaah kwa chochote ataingia Jannah)). Nikasema: “Je hata akizini au akiiba?” Akasema: ((Hata akizini au akiiba)) [Al-Bukhaariy 1237, Muslim 94]
Na Hadiyth ya Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, hasikii yeyote kuhusu mimi (kutumwa kwangu ujumbe) katika Ummah wa (Da’wah) Myahudi au Mnaswaara kisha afariki akiwa hayamini yale niliyotumwa nayo, isipokuwa atakuwa miongoni kwa watu wa Motoni))[Muslim (1/80) Mlango wa Iymaan – Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu)]
Pia:
عَن عبدالله بن عمر جاءَ أعرابيٌّ إلى النَّبيِّ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ فقالَ: يا رسولَ اللَّهِ إنَّ أبي كانَ يصِلُ الرَّحمَ وَكانَ وَكانَ فأينَ هوَ؟ قالَ: ((في النَّارِ)) قالَ فَكأنَّهُ وجدَ من ذلِكَ فقالَ: يا رسولَ اللَّهِ فأينَ أبوكَ قالَ رسولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ: ((حيثُما مررتَ بقبرِ مشرِكٍ فبشِّرْهُ بالنَّارِ)) قالَ: فأسلمَ الأعرابيُّ بعدُ وقالَ: لقد كلَّفني رسولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ تعبًا ما مررتُ بقبرِ كافرٍ إلَّا بشَّرتُهُ بالنَّارِ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Bedui mmoja alikuwa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Baba yangu alikuwa akiunga undugu na alikuwa akifanya kadhaa wa kadhaa, je yuko wapi?” Akasema: (Motoni)). Ikawa kama kwamba lilikuwa jambo zito kwake. Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, baba yako yuko wapi?” Akasema: ((Utakapopita kaburi la Mushrik yeyote mbashirie Moto)). Bedui akasilimu baada ya hapo kisha akasema: “Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): amenitwika jukumu gumu kwamba kila nikipata kaburi la kafiri nimbashirie Moto.” [Swahiyh Ibn Maajah 1288]
Wala haifai kuwaombea wazazi makafiri wakafariki wakiwa katika hali ya ukafiri kwa kuwa imeshabainika kuwa ni watu wa Motoni, tena hata kama ni wazazi, ndugu au jamaa wa karibu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa moto uwakao vikali mno.[At-Tawbah: 113]
Na katika usiku, amka uswali (tahajjud) kuisoma (Qur-aan); ni ziada ya Sunnah kwako Asaa Rabb wako Akakuinua cheo kinachosifika.[Al-Israa: 79]
Nayo ni Ash-Shafaa’ah (Uombezi) Siku ya Qiyaamah baada ya kisimamo kirefu mno cha watu katika mkusanyiko wa viumbe wote. Watu watamwendea Nabiy Aadam, Nuwh, Ibraahiym, Muwsaa na ‘Iysaa (عليهم السلام)wawaombe Ash-Shafaa’ah lakini kila mmoja atakataa kwa kutoa udhuru wake, na kila mmoja atawaambia Ummah wake wapeleke ombi kwa Nabii mwenginewe mpaka watu wamfikie Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) wamuombe, na hapo ndipo atakapoinama kusujudu na kumuomba Rabb Wake Ash-Shafaa’ah, na Allaah (عز وجل) Atamkubalia Shafaa yake, basi mahali hapo ndipo pakaitwa “Al-Maqaam Al-Mahmuwd” [Cheo cha Kusifika] kwa kuwa viumbe wote watamsifu Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa sababu Shafaa’ah yake ndio sababu yao kufanyiwa wepesi kisimamo chao kirefu mno Siku hiyo ya Mkusanyiko. Hadiyth ifutayo inathibitisha:
Ibn ‘Umar(رضي الله عنهما)amesema: Watu watasubiri wakiwa watapiga magoti Siku ya Qiyaamah, na kila Ummah utamfuata Nabiy wake wakisema: “Ee fulani tuombee Ash-Shafaa’ah (kwa Allaah), mpaka ombi la Ash-Shafaa’ah litamfikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na hiyo ndio siku ambayo Allaah Atamuinua katika Al-Maqaam Al-Mahmuwd (Cheo Cha Kusifika)[Al-Bukhaariy]
Miongoni mwa amali zikatazosababisha kupata Ash-Shafaa’ah ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
1-Kuitikia Mwadhini na kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ "إذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوامِثْلَ مَا يَقُولُ ، ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ ، فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا . ثُمَّ سلُوا اللَّه لي الْوسِيلَةَ ، فَإِنَّهَا مَنزِلَةٌ في الجنَّةِ لا تَنْبَغِي إِلاَّ لعَبْدٍ منْ عِباد اللَّه وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُو ، فَمنْ سَأَل ليَ الْوسِيلَة حَلَّتْ لَهُ الشَّفاعَةُ
‘Abdullaah bin ‘Amruw (رضي الله عنهما) kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akisema: ((Mtakapomsikia muadhini basi semeni kama anavyosema, kisha niswalieni, kwani mwenye kuniswalia mara moja Allaah Atamswalia mara kumi, na kisha niombeeni (kupata) ‘wasiylah’ ambayo ni manzila (heshima maalum) huko Jannah. Haitomstahikia isipokua mja mmoja katika waja wa Allaah, nami ninatarajia kuwa mja huyo, na mwenye kuniombea “Al-Wasiylah” atapata uombezi (wangu Siku ya Qiyaamah))[Muslim (1/288)
2-Kuitikia Mwadhini na kumuombea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) du’aa iliyothibiti:
(Ee Allaah, Rabb wa mwito huu uliotimia, na Swalaah iliyosimama, mpe (Nabiy) Muhammad al-Wasiylah (cheo, heshima maalumu, daraja), na fadhila, na mfikishe daraja yenye kuhimidiwa, ambayo Umemuahidi).
Ash-Shafaa’ah(Uombezi) wangu umehalalika kwake Siku ya Qiyaamah.”[Imetolewa na Al-Arba’ah]
3-Kuimarika katika Tawhiyd ya Allaah (عز وجل)
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّهُ قَالَ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ :مَنْ أَسْعَدُ اَلنَّاسِ بِشَفَاعَتِكَ؟ قَالَ: ((مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ خَالِصًا مِنْ قَلْبِهِ))
Abuu Hurayrah (رضي اَللَّهُ عَنْهُ) alimesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) “Nani atakayefanikiwa zaidi na shafaa’ah yako? Akajibu: ((Atakayesema
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ
Laa ilaaha illa-Allaah
hali ya kuwa na niyyah safi moyoni mwake))[Al-Bukhaariy]
4-Kuzidishia Kusujudu (Kuswali Nawaafil):
Imehadithiwa na mmoja wa Mtumishi wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba:
كان ممَّا يقولُ للخادمِ : ألكَ حاجةٌ ؟ قال : حتى كان ذاتَ يومٍ فقال : يا رسولَ اللهِ ! حاجتي ، قال : و ما حاجتك ؟ قال : حاجَتي أن تشفعَ لي يومَ القيامةِقال : و من دلَّكَ على هذا ؟ قال : ربِّي ، قال : أما لا ، فأعنِّي بكثرةِ السجودِ
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akimwambia Mtumishi wake: “Je unahitaji lolote?” Hadi siku moja (Mtumishi) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah nina haja!” Akauliza: “Nini haja yako?” akasema: “Haja yangu uniombee Shafaa Siku ya Qiyaamah.” Akamuuliza: Nani aliyekuongoza kuomba hilo?” Akasema: “Rabb Wangu.” Akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Basi nisaidie kwa kuzidisha kusujudu (kuswali)”[As-Silsilah Asw-Swahiyha 2102], Swahiyh Al-Musnad (1497])
Pia,
عن أبي فراس رَبِيعَة بْن كَعْبٍ الْأَسْلَمِيُّ رضي الله عنه خادم رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: كُنْتُ أَبِيتُ مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَتَيْتُهُ بِوَضُوئِهِ وَحَاجَتِهِ، فَقَالَ لِي: ((سَلْني)) فَقُلْتُ: أَسْأَلُكَ مُرَافَقَتَكَ فِي الْجَنَّةِ، قَالَ: ((أَوْ غَيْرَ ذَلِكَ؟)) قُلْتُ: هُوَ ذَاكَ، قَالَ: ((فَأَعِنِّي عَلَى نَفْسِكَ بِكَثْرَةِ السُّجُودِ))رواه مسلم في صحيحه
Kutoka kwa Abuu Firaas Rabiy'ah bin Ka'ab Al-Aslamiy mtumishi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye amesema: "Nililala na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) usiku mmoja nikamletea maji ya kutawadha, akaniambia: ((Niombe utakacho)) Nikasema: "Nataka kuandamana na wewe Jannah. Akasema: ((Hutaki lolote lingine?)) Nikasema: "Ni hilo tu." Akasema: ((Basi nisaidie (ili hilo liwezekane) kwa kuzidisha kusujudu [Kuswali])) [Muslim katika Swahiyh yake]
Juu ya kuwa yeye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ndiye mtu mtukufu kabisa mbele ya Swahaba zake, na ndio kiongozi wao, lakini hali na maisha yake yalikuwa ni ya Zuhd ya ajabu; kwani ukitambua jinsi alivyoishi katika nyumba duni kabisa na kutokuwa na vifaa na fanicha za kifakhari nyumbani mwake, au kutokuwa na nguo za kifakhari, au kutokuwa na mali yoyote ile hadi kufariki kwake. Bali la ajabu zaidi ni kufikia hadi miezi ya kutokuwa na chakula nyumbani mwake, basi ajabu iliyoje hakika sifa hii kuimiliki mtu kama yeye, kwani hivyo ni ilikuwa ni tofauti kabisa na maisha ya viongozi wenginewe wa zama zake.
Na hayo ni mafunzo na kigezo kizuri kwetu katika zama hizi kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitambua lengo la kuumbwa kwake, kwahiyo akaelewa kuwa nyenzo hizo ni za kumpelekea yeye kumwabudu Rabb wake na kutafuta Aakhirah yake, na wala havikuwa ni vitu vya kuvipapia na kuvikusanya katika maisha ya dunia. Na ndio maana katikakauli zake kuhusu Zuhd, amedhihirisha na kufundisha kuwa maisha haya ya duniani ni ya muda mfupi tu wa kupita, hivyo hajataka kumiliki mafao au vitu vya kumstarehesha wala hakutaka anasa za maisha mafupi ya dunia bali alipendelea maisha ya Aakhirah ambayo ndio ya maisha ya kudumu milele. Akaamini na kufuata kauli kadhaa za Rabb Allaah (سبحانه وتعالى) wake Anazosema:
Na huu uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni pumbao na mchezo; na hakika Nyumba ya Aakhirah bila shaka hiyo ndiyo yenye uhai wa kweli hasa (wa milele), lau wangelikuwa wanajua![Al-‘Ankabuwt: 64]
Jueni kwamba uhai wa dunia ni mchezo na pumbao na mapambo, na kufakharishana baina yenu na kushindana kukithiri katika mali na watoto; ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha yananyweya, basi utayaona yamepiga manjano, kisha yanakuwa mabua yaliyonyauka na kupondekapondeka. Na Aakhirah kuna adhabu kali, na maghfirah kutoka kwa Allaah na radhi. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni sterehe fupi za kughuri.[Al-Hadiyd: 20]
Yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya Aakhirah Tunamzidishia katika mavuno yake; na yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya dunia, Tutampa humo, lakini Aakhirah hatokuwa na fungu lolote.[Ash-Shuwraa (42: 20)]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿١٦﴾
Bali mnakhiari uhai wa dunia.
وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿١٧﴾
Na hali Aakhirah ni bora zaidi ya kudumu.[Al-A’laa (87: 16-17).
Na chochote mlichopewa katika vitu, basi ni starehe za uhai wa dunia na mapambo yake. Na yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi na yakubakia. Je, basi hamtii akilini?[Al-Qaswasw (28: 60)]
Yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya Aakhirah Tunamzidishia katika mavuno yake; na yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya dunia, Tutampa humo, lakini Aakhirah hatokuwa na fungu lolote.[Ash-Shuwraa (42: 20)]
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alilala kwenye jamvi la mtende likamfanyia alama ubavuni mwake tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Tukufanyie godoro laini? Akasema: ((Mimi na dunia wapi? Mfano wangu na dunia ni kama mpandaji (anayesafiri kwa mnyama) aliyepumzika kivulini chini ya mti, [muda mfupi tu] kisha akaondoka na kukiacha)).[At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]
Na pia,
عن المُسْتَوْرِد بن شَدَّادرضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رسول اللهصلى الله عليه وسلم: (( مَا الدُّنْيَا في الآخِرَةِ إِلاَّ مِثْلُ مَا يَجْعَلُ أَحَدُكُمْ أُصْبُعَهُ في اليَمِّ، فَلْيَنْظُرْ بِمَ يَرْجِعُ ! ))رواه مسلم.
Imepokewa kutoka kwa Al-Mustawrid bin Shaddaad(رضي الله عنه) kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Dunia si chochote katika Aakhirah isipokuwa ni kama mfano wa mtu anayetia kidole chake(Yahyaa aliashiria kidole cha Shahaada)katika bahari, basi naangalie kiasi gani cha maji kimechota."[Muslim na wengineo. Hadiyth imesimuliwa kwa Isnaad mbalimbali na zote zimesimuliwa na Al-Mustawrid bin Shaddaad ndugu wa Baniy Fihr]
Na pia,
عن أنسرضي الله عنه : أن النبيصلى الله عليه وسلم، قَالَ: (( اللَّهُمَّ لاَ عَيْشَ إِلاَّ عَيْشَ الآخِرَةِ ))متفقٌ عَلَيْهِ .
Na imepokewa kutoka kwa Anas(رضي الله عنه) kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ee Allaah! Hakuna maisha isipokuwa maisha ya Aakhirah [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na pia,
عن جابررضي الله عنه : أنَّ رسول اللهصلى الله عليه وسلم مَرَّ بالسُّوقِ وَالنَّاسُ كَنَفَتَيْهِ ، فَمَرَّ بِجَدْيٍ أَسَكَّ مَيِّتٍ ، فَتَنَاوَلَهُ فَأَخَذَ بِأُذُنِهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( أَيُّكُم يُحِبُّ أنْ يَكُونَ هَذَا لَهُ بِدرْهَم ؟ )) فقالوا : مَا نُحِبُّ أنَّهُ لَنَا بِشَيْءٍ وَمَا نَصْنَعُ بِهِ ؟ ثُمَّ قَالَ : (( أَتُحِبُّونَ أَنَّهُ لَكُمْ ؟ )) قَالُوا : وَاللهِ لَوْ كَانَ حَيّاً كَانَ عَيْباً ، إنَّهُ أسَكُّ فَكَيْفَ وَهُوَ ميِّتٌ ! فقال : (( فوَاللهِ للدُّنْيَا أهْوَنُ عَلَى اللهِ مِنْ هَذَا عَلَيْكُمْ ))رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir(رضي الله عنه) kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipita sokoni pamoja na Swahaba zake alimuona mbuzi mdogo amekufa na masikio yake yamekatwa. Alikishika katika masikio na kuuliza: "Nani anayemtaka (huyu mbuzi aliyekufa) kwa dirhamu moja?" Wakasema: "Hatutaki huyo awe ni wetu kwa chochote (hata bure). Na je, tutamfanya nini? " Kisha akasema: "Je, mngependa awe wenu bure?" Wakasema: "Wa-Allaahi! Hata kama angekuwa hai angekuwa na kasoro, vipi akiwa maiti?" Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم) "Wa-Allaahu! dunia ni duni zaidi mbele ya Allaah kuliko huyu juu yenu."[Muslim]
Na pia,
عن أَبي العباس سهل بن سعد الساعديرضي الله عنه ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النبيصلى الله عليه وسلم ، فقال : يَا رسولَ الله ، دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أحَبَّنِي اللهُ وَأحَبَّنِي النَّاسُ ، فقال : (( ازْهَدْ في الدُّنْيَا يُحِبّك اللهُ ، وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبّك النَّاسُ ))حديث حسن رواه ابن ماجه وغيره بأسانيد حسنة .
Imepokewa kutoka kwa Abu Al-'Abbaas Sahl bin Sa'd As-Saa'idiy(رضي الله عنه) kuwa: Alikuja mtu kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Ee Rasuli wa Allaah, nijulishe mimi amali ambayo nikiifanya Allaah atanipenda na watu watanipenda." Akasema: "Kuwa na Zuhd (Upe nyongo ulimwengu) atakupenda Allaah, na vipe nyongo viliomo mikononi mwa watu watakupenda watu."[Hadiyth Hasan - Ibn Maajah na wengineo kwa Isnaad nzuri]
Na pia,
عن سهلِ بن سعد الساعديرضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول اللهصلى الله عليه وسلم: (( لَوْ كَانَت الدُّنْيَا تَعْدِلُ عِنْدَ الله جَنَاحَ بَعُوضَةٍ ، مَا سَقَى كَافِراً مِنْهَا شَرْبَةَ مَاءٍ ))رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'ad As-Saa'idiy(رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Lau kama uliwengu ungekuwa na thamani sawa na bawa la mbu mbele ya Allaah, hangempatia kafiri maji ya kunywa hata kiasi cha mkono mmoja."[At-Tirmidhy, na akasema ni Hadiyth Hasan Sahiyh]
Na pia,
عن عبد الله بن مسعودرضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول اللهصلى الله عليه وسلم: (( لاَ تَتَّخِذُوا الضَّيْعَةَ فَتَرْغَبُوا في الدُّنْيَا ))رواه الترمذي ، وقال : (( حديثٌ حسنٌ )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas-'uwd(رضي الله عنه)kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msiwe ni wenye kupapia raslimali (zisizohamishika) na hivyo kupendelea dunia."[At-Tirmidhy, na akasema ni Hasan]
Akawakhofia sana Swahaaba zake wasije kughilibiwa na anasa za dunia wakaacha Zuhd:
عن أَبي سعيد الخدريرضي الله عنه ، قَالَ : جلس رسولُ اللهصلى الله عليه وسلم عَلَى الْمِنْبَرِ ، وَجَلَسْنَا حَوْلَهُ ، فقال : (( إنَّ ممَّا أخَافُ عَلَيْكُمْ مِنْ بَعْدِي مَا يُفْتَحُ عَلَيْكُمْ مِنْ زَهْرَةِ الدُّنْيَا وَزِينَتِهَا ))متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd al-Khudriy(رضي الله عنه) amesema: Alikaa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwenye mimbar nasi tukakaa duara (tukiwa tumemzunguka), akasema: "Kwa hakika yale ninayowaogopea nyinyi baada yangu ni kufunguliwa kwenu utajiri na kuvutiwa na dunia na mapambo yake."[Al-Bukhaariy na Muslim]
Wanafurahia kwa Aliyowapa Allaah kwa fadhila Zake na wanawashangilia ambao hawajaungana nao, walio nyuma yao, kwamba: “Hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.”
Wanashangilia kwa neema za Allaah na fadhila na kwamba Allaah Hapotezi ujira wa Waumini.[Aal-'Imraan: 169-171]
Mafunzo:
Fadhila za kufa shahidi: Ibn ‘Abbaas(رضي الله عنهما)amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Palewalipopatwa ndugu zenu wa Uhud, Allaah Alijaalie roho zao kuwa katika maumbile ya ndege wa kijani ambao wanakunywa katika mito ya Jannah na wanakula katika matunda ya Jannah na hurukia na hustarehe kwenye kandili ya dhahabu chini ya kivuli cha ‘Arshi ya Allaah. Kisha roho hizo zilipopatwa na utamu wa kunywa na kula katika neema za humo ndani ya Jannah na uzuri wa makazi na marejeo yao wakasema: Laiti wangelifahamu ndugu zetu yale Allaah Aliyotufanyia sisi ili wasipuuze jambo la jihaad na wala wasirejee na kuogopa vita. Basi hapo Allaah Akasema: “Mimi ninayafikisha hayo kutoka kwenu!” Ndipo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:“Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Rabb wao wanaruzukiwa…(mpaka Aayah (3: 169-171”[Imaam Ahmad].
Pia ...
Jaabir bin ‘Abdillaah(رضي الله عنه)amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikutana nami siku moja akaniambia: “Ee Jaabir! Unanini nakuona una huzuni?” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Baba yangu amekufa shahidi na ameacha nyuma madeni na watoto. Akasema: “Je, nikujulishe kuwa Allaah Hajapata kuongea na mtu yeyote sipokuwa nyuma ya pazia? Lakini Amemhuisha baba yako na akazungumza naye moja kwa moja. Akasema: Tamani (lolote) Nikupe! Akasema: Yaa Rabb! Nihuishe (nirudi duniani) ili niuliwe tena kwa ajili Yako! Akasema Rabb(تبارك وتعالى): Nimeshatanguliza kauli kwamba wao hawatorudi tena (maisha ya dunia). Akasema: Yaa Rabb! Basi nifikishie khabari kwa nilioawaacha nyuma. Kisha Allaah Akateremsha:“Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Rabb wao wanaruzukiwa…(3: 169-171) [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Swahiyh At-Targhiyb (2276), Swahiyh At-Targhiyb (1361)].
Tanabahi! Hakika wao wanageuza vifua vyao ili wamfiche (Allaah). Tanabahi! Wanapojigubika nguo zao, Anajua wanayoyafanya siri na wanayoyatangaza. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.[Huwd: 5]
Amenihadithia Ibraahiym bin Muwsaa, Ametujulisha Hishaam kutoka kwa Ibn Jurayj na amenijulisha Muhammad bin ‘Abbaad bin Ja’far kwamba Ibn ‘Abbaas alisoma:
Kutoka kwa Abuu Barzah Al-Aslamiyy(رضي الله عنه) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Nyayo za mja hazitoondoka [Siku ya Qiyaamah] mpaka aulizwe juu ya umri wake alivyoumaliza, elimu yake alivyoifanyia, mali yake ameichuma kutoka wapi na ameitumia kwa mambo gani, na mwili wake aliutumia kwa kazi gani)).[At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]
Mafunzo Na Mwongozo:
1. Hima ya Muislamu kutumia umri wake katika yale yanayomridhisha Allaah (سبحانه وتعالى).
2. Mambo manne hayo ni miongoni mwa neema nyingi za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa mja, anapaswa kushukuru kwa yakini, kauli na vitendo, na ataulizwa kuhusu neema hizo kama Anavyosema:
Kisha bila shaka mtaulizwa Siku hiyo kuhusu kuhusu neema.[At-Takaathur: 8]
3. Himizo la kuchuma mali kutoka njia za halali na kuitumia katika yanayomridhisha Allaah (سبحانه وتعالى) pamoja na kuitolea Zakaah na sadaka na tahadharisho la chumo la haramu. [Rejea: Al-Baqarah (2: 168), Twaahaa (20: 81].
4. Kuuhifadhi mwili usitende yaliyo haramu na kuutiisha pamoja na kuutumikia katika utiifu wa Allaah (سبحانه وتعالى), na kufanya ‘Ibaadah kwa wingi.
5. Kujifunza elimu iliyo na manufaa na aifanyie kazi kwa ikhlaasw anufaike nayo na anufaishe wengineo.
6. Tanabahisho kwa Muislamu kuwa na ikhlaasw katika ‘amali azitendazo. Rejea: [Al-Kahf : 110].
7. Mambo manne hayo ni majukumu ya kila mtu Siku ya Qiyaamah. Hakuna atakayeondoka mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) bila kuulizwa.
8. Hadiyth hii ni tahadharisho la kujirekebisha, kwa mtu anayekwenda kinyume na yanayomridhisha Allaah (سبحانه وتعالى).
9. Uhai na maisha ya dunia ni kama madrasa anayosoma mtu na kufanya juhudi, kisha mtihani wake na malipo ni Siku ya Qiyaamah. Atakayefanya kinyume chake, atapata khasara huko Aakhirah ambako kwenye maisha ya milele. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
Yeyote anayetaka (starehe za dunia) ipitayo upesi upesi Tunamharakizia humo Tuyatakayo, na kwa Tumtakaye. Kisha Tutamjaalia Jahannam aingie na kuungua hali ya kuwa mwenye kushutumiwa kufukuziliwa mbali (na rahmah ya Allaah).
Wote hao Tunawakunjulia; hawa na hao katika hiba za Rabb wako. Na hazikuwa hiba za Rabb wako zenye kuzuiliwa.[Al-Israa (17: 18-20)]
Na pia Rejea: [Ash-Shuwraa (42: 20)].
10. Umuhimu wa kufanya kazi, na mtu achunge sana kazi atakayofanya, kwa sababu chumo la haramu litampeleka mtu pabaya.
11. Muislamu anatakiwa katika Shariy’ah achume chumo la halali na alitumie kwa njia za halali.
12. Katika riwaayah nyengine ya at-Tirmidhiy badala ya mwili inataja ujana umetumiwe vipi, kumaanisha kuwa kipindi hicho ni muhimu sana katika maisha ya mwana Adamu na ni wakati wa kuchuma mema mengi.
Mwanzoni mwa miaka ya 1980 wakati madaktari na watu wengine wote walipokuwa wakiwaambia watu kwamba vidonda vya tumbo vilikuwa vinasababishwa na msongo wa mawazo (stress) na vyakula vyenye kusisimua (vyenye pilipili – spiced foods), wanasayansi wawili kutoka Australia wakagundua kwamba pamoja na hayo kisababishi kikuu kingine cha vidonda vya tumbo ni bakteria ajulikanaye kama ‘Helicobacter pylori’.
Ugunduzi huo wa hawa wanasayansi wawili ndiyo ukawawezesha kupata tuzo ya Nobel ya mwaka 2005 na kukaanza zama za kutibu vidonda vya tumbo kwa kutumia antibiotiki.
Pamoja na hayo yote bado jinamizi la vidonda vya tumbo limeendelea kusumbuwa mamilioni ya watu kote duniani mwaka hadi mwaka.
Inakadiriwa katika kila watu watatu mtu mmoja ana vidonda vya tumbo na wengi wa hawa wagonjwa tayari wamekata tamaa kwamba kuna kupona vidonda vya tumbo na wameamua na wamekubali kuishi na vidonda vya tumbo kama sehemu ya maisha yao.
Pia matumizi ya muda mrefu mrefu au ya mara kwa mara ya baadhi ya dawa za hospitali kama vile ibuprofen au aspirin nayo huchangia kutokea kwa vidonda vya tumbo.
2. Inachukuwa muda kufahamu ni nini hasa unatakiwa kula
Inachukuwa muda kufahamu ni chakula gani hasa unatakiwa kula na ni vyakula vipi hutakiwi kula.
Vyakula vikuu unavyopaswa kupenda kula ni vile vinavyokupeleka kupunguza asidi, gesi na sumu mwilini.
Kumekuwa na mkanganyiko na marumbano ya hapa na pale juu ya nini mgonjwa wa vidonda vya tumbo unaweza kula au usile.
Kwa hapa mimi nilipata somo kuu moja tu nalo ni kuhakikisha asilimia 80 ya chakula chako kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani.
Hii ina maana kwamba kama kwa siku unakula chakula cha uzito wa kg 2 kwa mfano basi kg 1 na gram 80 ziwe ni matunda na mboga za majani na gram 20 tu ndiyo viwe vyakula vingine ambavyo bado ni vyakula rafiki kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo.
Watu wengi tunaposema ule kwa wingi matunda na mboga za majani huwa hawaelewi.
Wanafikiri ni kitendo cha wewe kula wali sahani imejaa halafu umalizie na chungwa au parachichi moja eti ndiyo umekula matunda.
Siyo hivyo.
Inafaa hiyo sahani iliyojaa ugali ndiyo ijae mboga za majani au matunda na ugali uwe ndiyo matonge 10 au 15 tu.
Ili kupata faida hasa kwa upande huu amua na utenge mlo mmoja katika milo yako mitatu kwa siku mlo mmoja uwe ni matunda au mboga za majani pekee.
Ningekushauri mlo wa asubuhi uwe ni matunda tu au juisi ya matunda yenye asali ndani yake na siyo sukari au mlo wako wa usiku uwe ni matunda na mboga mboga za majani tu.
Kama utaweza kupata mboga ya majani unayoweza kuila ikiwa mbichi bila kupikwa katika moto hiyo ndiyo nzuri zaidi kwako.
Wazungu wana mboga nyingi za namna hii ambazo huliwa mbichi hivyo hivyo bila kupikwa.
Nakushauri upande mti wa mlonge nyumbani kwako, majani yake yanaweza kuliwa mabichi na yana vitamini C mara 7 zaidi ya ile ya kwenye chungwa. Ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako kwa siku inakutosha kwenye kachumbali au hata katika juisi ya matunda.
Pia pendelea kula kabeji mbichi mara kwa mara.
Ukifeli hapa kwenye vyakula kupona kwako vidonda vya tumbo itakuwa ni mtihani na utakata tamaa na utaamini vidonda vya tumbo havitibiki jambo ambalo si kweli.
Ukweli ni kwamba hata madaktari wenyewe bado hawafahamu ni kwa vipi baadhi ya vyakula vinasababisha gesi na matatizo ya mmeng’enyo wa chakula.
Ukiacha vyakula au vinywaji, tumbo lenyewe kwa asili huitengeneza hii asidi ili kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi yake ya kumeng’enya chakula.
Kwa ujumla kama una vidonda vya tumbo utalazimika kuacha kabisa vitu kama pombe, sigara, sukari, soda, kahawa, chai ya rangi, vyakula vinavyosindikwa viwandani na vyakula vyenye mafuta mengi.
3. Kufunga kula au kuacha kula ni hatari kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo
Kufunga kula au kuacha kula hakuwezi kukusaidia na pengine kunaweza kukuongezea vidonda zaidi.
Kwa sababu unapoumwa vidonda vya tumbo mawazo yako mengi yanakuwa kwenye kuwaza ule nini na usile nini ili kuhofia madhara yanayoweza kukutokea kuna wakati unaweza kuamua bora usile kabisa chochote.
Huo ni uamuzi mbaya kuliko wote unaweza kuuchukuwa unapoumwa vidonda vya tumbo.
Bila kula chochote au kukaa masaa mengi bila kula tumbo lako linakuwa limebaki kwa sehemu kubwa na asidi tu ambayo inaweza kupelekea kuongezeka zaidi kwa vidonda vya tumbo.
Kula milo midogo midogo mingi na usikae muda mrefu bila kula na wala huhitaji kufunga kula.
Kanuni ni ile ile, matunda na mboga za majani.
4. Usile chakula na kulala wakati huo huo
Usile wakati wa kulala.
Kuna nyumba zingine zina mambo ya ajabu huwezi hata kuamini. Eti mama anaingia jikoni kupika chakula cha usiku saa tatu usiku!
Ukila saa tatu au saa nne usiku utalala saa ngapi?
Kuna mtu akimaliza tu kula anajitupa kitandani kulala.
Kama kweli unaumwa vidonda vya tumbo na umeamua kupona au kuzuia usipatwe na vidonda vya tumbo huwezi kuishi hivyo.
Kama unataka maumivu ukiwa usingizini au maumivu ya vidonda vya tumbo nyakati za usiku basi wewe maliza tu kula na ujitupe kitandani, utaniambia habari yake.
Tangu umekula chakula na unapoenda kulala kuwe na tofauti ya kati ya lisaa limoja hata masaa mawili.
Hivyo kama wewe huwa unaingia kitandani kulala saa tatu usiku basi jitahidi kwenye saa moja kamili au saa moja na nusu jioni uwe tayari umekula.
Na ukishakula usikae chini. Ukimaliza kula tembea tembea kwa miguu hata nusu saa ndiyo utulie.
Kitendo cha kumaliza kula na ukaamua kutembea tembea huusaidia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi yake kwa kiwango chake cha juu kabisa na kwa ufanisi mkubwa.
Unapomaliza kula na kujitupa kitandani unauzuia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi yake vizui na utaambulia maumivu zaidi ya vidonda.
Kwa kipande hiki napenda kuongeza pia kama utaweza kuwa unakula chakula chako huku umesimama na ukimaliza hukai chini unatembea tembea kama nusu saa hivi wewe unaweza kupona haraka zaidi vidonda vya tumbo.
Unapokuwa umekaa mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula unakuwa unafanya kazi chini ya kiwango na pengine gesi na asidi vinaweza kujitengeneza kirahisi kwa njia hiyo ya kukaa kwenye kiti au chini muda mwingi.
5. Usiwaze sana kuhusu vyakula vyenye asidi
Mara nyingi sana nakutana na comment zinazouliza je mwenye vidonda vya tumbo anaweza kutumia limau? Ndimu? Tangawizi? Kitunguu swaumu? Machungwa ? na mengine mengi ya namna hiyo.
Na wengine wanaweza hadi kukujaji na kukuona hujuwi lolote kwa sababu umemwambia ale chakula fulani ambacho daktari wake alimwambia asile.
Kwa sehemu kubwa tumbo lenyewe huitengeneza hii asidi hata kama utakula vizuri kiasi gani.
Matokeo ya mwisho kabisa ya asidi ni saratani.
Ndiyo maana unakutana na mtu hajawahi kuvuta sigara wala kunywa pombe na anaugua saratani fulani!
Nimekutana na wachungaji wanaumwa saratani, wachungaji hata mashehe wanaumwa bawasiri na kadharika na watu hawa ni wale wapo makini sana juu ya nini wale na nini wasile au kunywa.
Wanawake wengi sana wanaumwa saratani ya matiti na wengi wao hawajawahi kutumia kilevi chochote.
Kwahiyo unakutana na mtu hapa anauliza eti mwenye vidonda vya tumbo anaruhusiwa kutumia limau? Ukimjibu ndiyo anakuona wewe hujuwi kitu kutokana na alivyoaminishwa na daktari wake.
Ni msitu mkubwa. Hivyo mpendwa kuwa mpole.
Limau kwa mfano lina vitamini C ambayo ni mhimu sana kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.
Limau linapokuwa nje ya mwili ni asidi lakini kile wewe hufahamu ni kuwa limau linapofika chini tumboni hubadilika na kuwa alkalini tena alkalini ile nzuri kuliko hata ya kwenye mboga za majani au matunda mengine.
Kwahiyo usiwe bize sana kukariri hiki ni asidi na hiki siyo asidi kwa sababu tumbo lenyewe kwa asili lazima liizalishe hii asidi ili mfumo wake wa mmeng’enyo wa chakula uweze kufanya kazi yake.
Uwe ni mtu uliye tayari kujifunza > open minded.
Endelea kupenda kula zaidi matunda na mboga za majani huku ukiepuka kukaa chini au kwenye kiti masaa mengi
Usiwaze sana kuhusu vyakula vyenye asidi.
6. Usiidharau stress (msongo wa mawazo)
Kuna uhusiano kati ya msongo wa mawazo na vidonda vya tumbo na kila kimoja kinaweza kumleta mwenzake.
Msongo wa mawazo (stress) unaweza kuleta vidonda vya tumbo na vidonda vya tumbo vinaweza kuleta msongo wa mawazo.
Jambo baya na la kipuuzi kabisa unaweza kufanya unapoumwa vidonda vya tumbo ni kuwa na stress.
Kwahiyo jikaguwe na ujipeleleze ni kitu gani hasa ndiyo sababu ya wewe kuwa na msongo wa mawazo na ukiondowe hicho kwenye maisha yako bila kujali ni nini au ni nani.
Usiiuguze stress wala usikubali kuishi nayo.
Haijalishi itakugharimu nini, uamuzi mzuri kabisa unaweza kuufanya kwenye maisha yako ni kuamua kuishi maisha ya amani na utulivu bila msongo wowote wa mawazo usio na kichwa wala miguu.
Kumbuka maisha ni mafupi na maisha ni yako na hii dunia ni kubwa sana ina mahitaji ya kumtosha kila mtu ni wewe tu kuamua kubadilika na kufungua akili zako.
Usijifungie kwenye boksi.
Lolote linalokusibu lina suluhisho lake.
Ongea na watu, kaa na watu.
Kwa kawaida hata kama hupendi au hutaki mwili wenyewe utaelekeza nguvu kushughurika na stress kwa sababu ni jambo linalohitaji kutokuwepo.
Sasa hizi nguvu ambazo mwili wako unazielekeza kushughulika na stress ndiyo hizo hizo zingetumika kuutibu mwili dhidi ya vidonda vya tumbo.
Uamuzi unabaki kuwa kwako.
Kwamba wewe ushughulike na stress na mwili ushughulike na uponyaji au wewe ushughulike na uponyaji jambo ambalo huliwezi na mwili ushughulike na stress.
Upe mwili uwezo wake wa asili wa kujitibu kwa kuamua kujitenga mbali na msongo wa mawazo.
Kumbuka duniani tunapita na tuna muda mchache sana wa kuwa hapa.
Ishi vizuri kwa amani, furaha na upendo.
Jiunge na Group langu la Afya Kila Siku kwenye WhatsApp kwa ada ya sh 5000 tu kwa mwezi, nitafute WhatsApp +255714800175 na utakuwa karibu na mimi masaa 24
Kama unapenda kujifunza mambo mengine zaidi kuhusu vidonda vya tumbo bonyeza hapa
Kama unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kutibu kabisa vidonda vya tumbo nipigie simu au niachie ujumbe WhatsApp +255714800175
Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;
Kama wewe ni mvivu kusoma pita hivi kwanza nenda ka-like mapicha ya rafiki zako wengine huko kwenye facebook.
Siku hizi tunaambiwa mtu mmoja kati ya watu watatu atakuwa na mojawapo ya aina za saratani, miaka 65 iliyopita ilikuwa mtu mmoja kati ya watu elfu kumi.
Saratani ni nini?
Saratani ni mgawanyiko usio sawa na usiodhibitika wa seli na kuunda uvimbe unaovamia na kuzidhuru tishu.
Seli za Saratani husambaa kupitia mikondo ya damu au kupitia vungu (cavities) mbalimbali za mwili na kuunda uvimbe wa pili katika sehemu nyingine za mwili.
Saratani inaweza kushambulia karibu katika kila tishu yeyote ya mwili.
Bado hakuna uhakika wa moja kwa moja wa nini kinachosababisha kansa ingawa inajulikana wazi kuwa, kuwa karibu na baadhi ya vitu (kemikali) kunaweza pelekea saratani.
Tuna seli za ngozi, seli za Ini, seli za ubongo, seli za mapafu, seli za misuli, seli za mifupa na kadharika.
Seli hizi tofauti zinatujia toka kwa kinasaba (DNA) chetu ambacho kinamiliki maagizo (blue print) juu ya aina gani ya seli itengenezwe.
Wakati baadhi ya vitu (kemikali) vimechukuliwa ndani ya mwili kupitia ngozi au hewa tunayopumua au kwa njia ya chakula, miili yetu inaweza kuvihimili vingi ya hivyo vitu kabla ya safari ya mwisho kuingia kwenye vinasaba vyetu na kusababisha seli zisizo za kawaida kutengenezwa na kupelekea kile tunachokiita SARATANI.
Miili yetu lazima iachwe katika hali ya ualikalini kidogo na siyo katika asidi kabisa isipokuwa kwa kipindi cha muda mfupi, kinyume chake madhara lazima yatatokea kwenye tishu, ogani, seli na mwisho kwenye kinasaba ambako seli hutengenezwa.
Kuna namna tatu ambazo zimebuniwa ili kuishughurikia asidi: mfumo wa mkojo, mapafu na tumbo.
Mfumo wetu wa mkojo hupitisha asidi nje ya mwili.
Mapafu yetu huchukua ndani oksijeni na kutoa nje gesi ya kabonidayoksaidi (co2) ambayo ni asidi.
Hii ndiyo njia namba moja miili yetu iwezavyo kuitoa asidi ambayo ni taka za seli.
Tumboni mwetu ndimo haidrokloriki asidi hutengenezwa na kuhifadhiwa ikisubiri kutumika wakati chakula kinaliwa.
Haidrokloriki asidi hii inahitajika na mwili ili kuuwezesha mwili kuyatumia madini yanayopatikana kwenye vyakula tulavyo.
Baada ya hii haidrokloriki asidi kuwa imeandaliwa (opened up the food), valvu ya chini ya tumbo itajifungua na chakula huenda ndani mwanzoni mwa utumbo mdogo ambako asidi hupunguzwa makali (neutralized) na bikaboneti toka katika kongosho.
Ikiwa asidi hii haikurekebishwa vya kutosha na baadhi ya asidi inaingia katika utumbo mdogo, asidi hiyo itaziathiri seli za tishu na kwa kipindi cha muda mrefu itaathiri kinasaba na unapata kuzarisha seli zisizo za kawaida na kupelekea kansa ya utumbo mdogo (intestinal cancer).
Wakati asidi hii inaingia kwenye mkondo wa damu ikitokea kwenye utumbo mdogo hupelekwa kwenye ini ambako damu husafishwa na asidi hurekebishwa.
Ini letu haliwezi kuhimili kiasi kingi cha asidi inapotokea tunakunywa kiasi kingi cha vinywaji vyenye kabonidayoksaidi (the carbonation), ni kiasi kidogo kinachopatikana katika soda, bia na shampanye (champagne).
Ubongo wetu unatambua damu hiyo yenye asidi nyingi lazima irekebishwe kwa haraka, hivyo utaamuru kalsiamu itolewe toka katika mifupa yetu ili kuirekebisha damu hiyo.
Ukopaji huu wa kalsiamu kutoka katika mifupa kama hautalipwa kwa wakati, utapelekea matatizo mengine ya kiafya kama vile ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).
Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH (potential hydrogen). Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.
Unaweza kukinunua kipimo cha PH na kupima Ph ya mate na mkojo, hii itakupa mwelekeo wa namna gani unafanya kuitunza 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.
Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.
Haidrojeni ina chaji chanya (+), wakati alkalini ina chaji hasi (-).
Kila mtu anapaswa kula zaidi vyakula vyenye alkalini (matunda na mboga za majani) na kunywa vinywaji vyenye asidi chache, alkalini nyingi kama juisi ya limau, ya chungwa, ya zabibu na maji halisi.
Maeneo ndani ya mwili ambayo hayana mtiririko wa moja kwa moja wa damu yanaweza kupatwa na asidi kwa urahisi zaidi.
Tishu zitaisajiri asidi hiyo na kihisio maalumu (special sensor) ambacho kitapeleka ujumbe kwenye ubongo kama MAUMIVU.
Kunakokuwa na damu chache au hakuna mtiririko wa moja kwa moja wa damu kama vile kwenye maungio, katileji na uti wa mgongo, maeneo haya yanaweza kupungukiwa kwa urahisi madini, chumvi, maji na elektrolaiti na kusababisha misuli iliyo karibu nayo kufanya kazi zaidi ya uwezo wake na kusababisha uwezekano wa kukakamaa kwa mishipa, madhara kwenye misuli na kwenye mafundo (ligaments).
Maumivu ambayo hayakusababishwa na jeraha au ajari, ni kiashiria kuwa tishu, ogani, maungio na seli vina asidi iliyozidi ambayo inahitaji kufanywa alkalini.
Kwa kunywa glasi moja (ml 250) ya maji halisi na kuchukua kipande cha chumvi ya baharini, kutapunguza kama siyo kuondoa kabisa maumivu.
Jaribu hii kwa kunywa glasi moja ya maji na kisha kuiweka chumvi mwishoni mwa ulimi wako na kuiacha iyeyuke kwa dakika na kisha isafishe kwenda chini na glasi ya pili ya maji.
Kitendo hiki kitabadili PH ya damu, tishu, ogani na seli ndani ya mwili.
Asilimia 94 ya damu ni maji, ubongo wetu una zaidi ya asilimia 85 za maji, na tishu zetu laini zina asilimia 75 ya maji.
Tunatumia maji kupumua nje, kila masaa 24 tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumua tu nje.
Chukua kioo, hemea juu ya kioo, utaona ukungu (maji).
Kumbuka kuwa hali hiyo ya uasidi wa tishu, ogani, na seli, mwisho itaingia kwenye kinasaba (DNA) chetu na kubadili mpangilio (codes) na kusababisha seli mbovu kutengenezwa ambazo tunaziita ‘SARATANI’.
Saratani inaweza kuishi katika mazingira ya uasidi na uanaerobiki, yaani katika upungufu wa oksijeni pekee.
Ikiwa kinga yako ya mwili inafanya kazi vizuri, itakuwa na seli nyeupe za damu ambazo zinaweza kutengeneza oksijeni na kuitoa ‘haidrojeni peroksaidi’ kama inavyohitajiwa kuzuia kutengenezwa kwa seli za kansa.
Wakati mtu anapokuwa katika upungufu wa maji na chumvi (out of balance in cells), mwili utajifunguwa na kuizarisha histamini ili kujiwezesha kuiweka upya seli katika usawa wake, kupiga chafya ni angalizo kuwa histamini imeamushwa.
Moja kati ya madhara ya histamini ni kuisimamisha seli nyeupe ambayo hutengeneza haidrojeni peroksaidi kwenye mfumo wetu wa kinga ya mwili.
Kwa sababu ya biashara kuunda vyakula vyetu vyote maalumu na vinywaji vyenye radha mpya, radha nzuri na nguvu ya kutosha kwa kutumia kafeina toka katika mimea na mitishamba kama vile ginseng kuisisimua tezi ya adreno, kunasababisha Ini kutoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa.
Hakuna nguvu iliyomo kwenye kafeina au ginseng.
Kuna majina mengine mengi ya visisimuaji hivi kama vile, kokwa za guru, kokwa za cola na mfalme wa yote ni guarana.
Mbegu za guarana zina kiasi cha kafeina mara tatu zaidi ya zile za kahawa, na hawatakiwi kuliorodhesha neno kafeina kwenye vifungashio (packages) au kontena.
Ungaunga wa guarana hutumika kutengeneza vidonge vya kupunguza uzito kwa sababu kafeina itazisambaratisha hisia za njaa, lakini hakuna mahala neno kafeina linaonekana kwenye kifungashio.
Kuna mimea, kokwa na kemikali nyingi ambazo zitaisisimua tezi ya adreno na kusababisha ini kuitoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa au hata kuitengeneza toka tishu za mwili wenyewe.
Kafeina kama kikojoshi, huyalazimisha maji kukimbia nje ya mwili kwa haraka na kuziacha seli bila muda wa kutosha kuyatumia maji hayo, maji yanapokimbia kwa haraka nje ya mwili huyakimbiza pia madini mhimu nje ya miili yetu.
Nguvu safi katika mwili wa binadamu huja kutoka katika maji/chumvi na potasiamu ambavyo huwasha pampu za majenereta machache yaitwayo kwa kitaalamu ‘cation pumps’, umeme wake huifadhiwa katika beteri ziitwazo “Adenosine Triphosphate”(ATP) na “Guanosine Triphosphate”(GTP).
Aina nyingine ya nguvu kwa mwili inatokana na sukari.
Inahitajika sukari zaidi kuzarisha kiasi sawa cha nguvu izarishwayo kwa maji/chumvi na potasiamu, ni kama vile umeme wa maji (haidroelectric power) dhidi ya umeme uzarishwao kwa makaa ya mawe.
Wakati sukari inapochomwa kuzarisha nguvu, huzarisha taka nyingi zaidi (oxidation) zinazohitaji vidhibiti zaidi vya taka hizo (anti-oxidants) ili kuirekebisha hali hiyo ya taka za sumu.
Ikiwa huna tabia ya kupenda kula matunda na mboga za majani vya kutosha, basi Ini lazima lizitumie asidi amino zenye umhimu sana kama vidhibiti vya taka hizo.
Tunapokula vyakula vya asidi vilivyoongezwa utamu kama kemikali na kemikali vihifadhio, jumlisha vinywaji ambavyo ni asidi na vimeongezwa utamu kama kemikali; vitakuwa vikiuandaa mwili kupata ‘Saratani’.
Moja ya sababu kuu kwanini unatakiwa kula matunda na mboga za majani kwa wingi ni kuwa vyakula hivi ni alkalini, wakati nyama, kuku, samaki, nyama ya nguruwe, pasta (tambi) mayai na vyakula vingine karibu vyote ni asidi.
Watu wetu siku hizi tunakula vyakula ambavyo vimekwisha andaliwa (fast food) na hatutumii vyakula vyenye alkalini ya kutosha.
Kumbuka kuwa kabonidayoksaidi ni asidi pia kama ilivyo kwa kahawa, chai na pombe ambavyo huathiri PH ya damu na tishu.
Madawa na wewe, kwa mjibu wa dr.Earl mindell, mwandishi wa kitabu; ‘Earl mindell’s new vitamin bible’ (zaidi ya nakala milioni 10), anasema katika ukurasa wa 414 wa kitabu hicho kuwa ‘kafeina ni dawa yenye nguvu kubwa, uwezekano ni kuwa, hauifurahii tu kahawa au cola yako ya kila siku, bali umekuwa mtegemezi (addicted) kwavyo’.
Kafeina inafanya kazi moja kwa moja kwenye mfumo mkuu wa fahamu (central nervous system).
Inakupa hisia safi kwa haraka na kupunguza uchovu.
Inasisimuwa pia kutolewa kwa sukari iliyokuwa imehifadhiwa kwenye Ini ambayo inatumika kama kiinuzi (lift) kwa kahawa, cola na chokoleti (The caffeine big three), lakini faida hizi zinaweza kuzidiwa uzito na hasara zake.
Utolewaji wa sukari iliyokuwa imehifadhiwa, kunapelekea mfadhaiko mkubwa kwenye mfumo wa dharura wa mwili.
Unaposhitushwa kidogo tu, unakuwa na nguvu za haraka kushughurika na tatizo (hamaki).
Hali hii hatimaye inaweza pelekea kukauka kwa tezi ya adreno kutakakosababisha damu chache yenye sukari (hypoglycemia), udhaifu, na kuumwa sana iwapo sukari haitachukuliwa mapema kupandisha juu damu sukari.
Pia dalili za uchovu sugu zinaweza kujitokeza kwa sababu mwili utakuwa umelazimishwa kutengeneza sukari toka katika tishu, mishipa na umbile lake wenyewe.
Kitendo hiki huitwa kwa kitaalamu kama ‘Gluco-neogenesis’, yaani kutengenezwa upya kwa sukari toka katika hifadhi ya mwili na kisha toka katika tishu, mishipa na umbile lake wenyewe (mwili).
Imethibitika pia kuwa kafeina imekuwa ikiingilia na kuathiri unakilishaji wa kinasaba (DNA), namna ambavyo seli mpya hutengenezwa.
Kafeina inaweza kusababisha upotevu toka mwilini wa vitamini nyingi za kundi B, kundi C, zinki, potasiamu na madini mengine.
Kahawa huongeza hali ya uasidi kwenye utumbo mdogo.
Kafeina inaweza kusababisha msukosuko ndani ya mwili.
Kafeina siyo kwamba tu huimaliza nguvu iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ubongo, bali pia huzuia mfumo vimeng’enya katika kutengeneza kumbukumbu kwenye ubongo.
Jarida moja la afya la Uingereza, ‘The British Medical Journal Lancet’, limeripoti uhusiano mkubwa uliopo baina ya utumiaji wa kahawa na kansa ya kibofu cha mkojo na kupungua kwa uzarishaji wa mkojo.
Kituo cha sayansi kwa masirahi ya umma (Center for science in public interest) kimewashauri kinamama wajawazito kukaa mbali na kafeina kwa kuwa tafiti zimeonesha kwamba kiasi cha kafeina kilichomo kwenye vikombe 4 vya kahawa kwa siku kinaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua kama yalivyoonwa katika majaribio kwa wanyama.
Kunywa maji kunahitaji kiasi cha chumvi kuchukuliwa pia ili kuzirekebisha taka (haidrojeni) kutokana na maji kutotumika kwenye seli.
Haidrojeni ni asidi.
Damu yetu ina chumvi na kongosho letu lazima liwe na chumvi ili kuitumia kutengeneza bikaboneti inayotumika kurekebisha asidi ndani ya tumbo.
Siku hizi vyakula vyetu vingi vinazarishwa kwa kutumia mbolea kemikali na kupuliziwa tena kemikali ili kudhibiti wadudu waharibifu.
Tunatumia kemikali kali kwenye vyakula vyetu ili kuvihifadhi kwa matumizi ya baadaye.
Miili yetu lazima ishughurike na kemikali hizi kila siku.
Siku hizi, kemikali zinazotumika kuongeza utamu kwenye vyakula zinasababisha matatizo makubwa kwenye miili yetu kwa sababu zina radha ya utamu lakini hazina sukari.
Sukari ni asidi, lakini kemikali zinazotumika badala ya sukari zinasababisha madhara zaidi ya sukari halisi.
Baadhi ya kemikali hizi kali zipatikanazo kwenye vyakula vyetu nyakati hizi zinabaki na kujishikiza kwenye utumbo mdogo na kuendelea kurundikana na hivyo kuufanya utumbo usifanye kazi zake vema.
Ini letu pia litazishikilia baadhi ya kemikali hizi kali ambazo zinaingia kwenye damu na kujaribu kuzirekebisha kadiri liwezavyo.
Ini litaendelea kuzihifadhi kemikali nyingi kadiri liwezavyo mpaka litakaposhindwa na kuamua kuzitupa tena kwenye mkondo wa damu na kwenda kwenye kila seli mwilini.
Kwa sababu hii, ndiyo maana watu wengi siku hizi wanatumia dawa rafiki na vifaa maalumu kusafisha utumbo mdogo na Ini kila mara ili kuziondoa taka hizi na uzito zinazoongezeka tumboni.
Kisha mtu analazimika kuwa mwangarifu sana kuepuka vyakula ambavyo vina kemikali kali nyingi.
Damu yote hupita kwenye Ini na amino asidi zinatumika kuzirekebisha sumu ambazo huliingia Ini.
Wakati Ini linapokuwa katika upungufu wa amino asidi hizi, litalazimika kukopa baadhi toka katika ogani zingine kama vile Kongosho.
Kitendo cha kongosho kukopwa amino asidi zake kutapelekea matatizo mengine kwenye kongosho kama vile kisukari, na uwezekano wa kutokea kwa saratani ya kongosho (pancreatic cancer) ikiwa amino asidi zilizokopwa hazikurudishwa kwa wakati ili kuliwezesha kongosho kuendelea na kazi zake vizuri.
Miili yetu ilisanifiwa kula vyakula halisi vya asili (fresh natural grown food) au kula nyama iliyouliwa wakati huo huo (fresh live kill).
Kwa njia za kijenetiki, siku hizi tumebadili vyakula vyetu ili kupata mavuno mengi.
Tunawalisha wanyama wetu vitu (kemikali) ili kuwafanya wakue haraka na kuongezeka uzito kwa haraka.
Tumekuwa wafugaji wa samaki pia ili kukidhi mahitaji na kuepukana na bei kubwa zitokanazo na gharama za kutumia meli za uvuvi na matatizo ya hali ya hewa.
Siku hizi sote tunaharaka katika kila jambo, hatuna muda wa kutosha, kila kitu ni mwendokasi, kitu kinachotusababishia wengi wetu kutokula mlo kamili wenye matunda halisi na mboga za majani.
Masaa 24 kwa siku seli ndani ya mwili zinaunguza kaboni kama mafuta ili kutuacha katika hali joto ya nyuzi joto 37.5.
Unapochoma kitu chochote, kinatoa nje taka moshi.
Taka zote hizo toka katika seli zote za mwili, lazima zirekebishwe kwa muda wa masaa yote 24 kwa msaada wa matunda na mboga za majani.
Asidi amino zina umhimu mkubwa kwa afya bora.
Ubongo wetu lazima upate kusambaziwa asidi amino kila siku ili ufanye kazi.
Ini haliwezi kufanya kazi vizuri bila uwepo wa asidi amino.
Mishipa yetu lazima iwe na amino asidi, kila seli kwenye mwili wa binadamu inazihitaji amino asidi au asidi ambazo zimetengenezwa toka asidi amino ndani ya mwili.
Deoxyribonucleic acid (DNA), Ribonucleic acid (RNA) na Decosahexaenoic acid (DHA), zote ni asidi.
Tunapopumua katika hewa iliyochafuliwa kama vile moshi wa magari au tunapovuta sigara miili yetu lazima izitumie asidi amino hizi kuirekebisha sumu hiyo kadiri iwezekanavyo.
Gari huyaunguza mafuta ya kaboni kwa kutumia oksijeni na kutoa nje taka (moshi) ziitwazo ‘kabonimonoksaidi’.
Moto wa kuni pia huzarisha moshi.
Hata uchomaji wa mafuta safi huzarisha taka ziitwazo kabonimonoksaidi.
Kwa hiyo mtu anapoamua kuvuta sigara, anakuwa ameamua kuvuta ndani kabonimonoksaidi ambayo ni sumu kwa mwili wa binadamu.
Uvutaji wa sigara pia unasababisha upungufu wa oksijeni mwilini, hii inamaanisha kuwa baadhi ya seli ndani ya mwili hazipati oksijeni ya kutosha na zinapatwa na asidi toka katika kabonimonoksaidi.
Kitendo hiki kitapelekea siku moja kutokea kwa SARATANI katika sehemu dhaifu za mwili.
Watu wengine hawajawahi kuvuta sigara tangu wazaliwe lakini wamepatwa na saratani ya matiti pia saratani ya mapafu na saratani nyinginezo.
Kila mwili wa kila mtu lazima ukope asidi amino na hivyo kupunguza usambazwaji mzuri wa oksijeni kwenye baadhi ya sehemu za mwili ili kukutetea uendelee, kwa matumaini kuwa utaupa mwili unachokihitaji siku za mbeleni ili kuyarudishia maeneo yaliyokopwa amino asidi zake.
Unajiuliza kwanini watu wanavuta?
Wote wanajibu kuwa wanaifurahia.
Unaenda kufa kwa sababu fulani kwa namna fulani.
Kuvuta kunawafanya wajisikie vema.
Wakati mtu anajaribu kuvuta sigara kwa mara ya kwanza, mapafu yake hujifunga na atakohoa kwakuwa mapafu yanajaribu kuitoa kwa haraka hewa iliyochafuliwa (moshi).
Lakini atakapojaribu ‘puff’ ya pili, mwili wake utaitoa kemikali iitwayo ‘endorphinsi’ ili kumuwezesha kuhimili (kuvumilia maumivu) moshi huo mpaka atakapopata hewa safi kupumua.
Ni kemikali hii ambayo mwili unaitoa ndiyo inayomfanya mtu kuwa mtegemezi (addicted) wa kuvuta.
Kutolewa huku kwa endorphinsi kunamfanya mtu kujisikia ‘super’.
Endorphinsi hutolewa pia wakati mama anajifungua kwa sababu ya maumivu.
Kwa kawaida ni ngumu sana kwa mwanamke kuacha kuvuta au kuacha kilevi chochote kuliko kwa mwanaume kwa sababu wanawake wana kiasi kingi cha endorphinsi kuliko wanaume.
Endorphinsi ni homoni ambayo huusaidia mwili kuvumilia maumivu.
Unywaji pombe pia unaweza kupelekea baadhi ya miili kuitoa endorphinsi na kumpelekea mtu huyo kuwa mtegemezi wa POMBE.
Moshi unaweza kunukia vizuri, lakini kamwe hauwezi kuwa mzuri kwa afya zetu.
Vinukizi vingi (air fresheners) vinatumia kemikali kali ambazo si nzuri kwetu, baadhi ya mishumaa pia ina kemikali hizo.
Mtu anapaswa kuwa makini na kusoma maelekezo ya kwenye vidandiko vya bidhaa ili kujua ni nini anakula, kunywa, kunusa au anaongeza kwenye ngozi yake.
Inashauriwa pia kuepuka kubaki katika mkao mmoja kwa muda mrefu iwe ni kukaa au kusimama.
Watu wengi kutokana na kazi wanazofanya wanalazimika kubaki wamekaa au kusimama tu kwa masaa mengi kwa siku jambo ambalo ni hatari kwa afya kwa kuwa asidi hujikusanya hivyo kwa urahisi zaidi.
Yapo mazoezi maalumu ya kufanya kila mara kwa watu wa kazi za aina hiyo ili kurudishia damu katika mfumo na hivyo kutoa nje taka za asidi.
Ukiamua kuacha kunywa vinywaji vyenye kafeina na kula chokoleti; na kisha kunywa maji nusu ya uzito wao katika aunsi na kuchukua robotatu gramu za chumvi kwa kila aunsi 16 (ml 500) za maji na kuongeza matunda na mboga za majani zaidi kwenye milo yako na kufanya mazoezi, saratani yako itaisha na mwili wako utajiripea wenyewe.
Je unasumbuliwa na saratani yoyote na unahitaji dawa ya asili kwa ajili hiyo na isiyo na madhara? nipigie simu au niachie ujumbe WhatsApp +255714800175
Jiunge na Group langu la Afya Kila Siku kwenye WhatsApp kwa ada ya sh 5000 tu kwa mwezi, nitafute WhatsApp +255714800175 na utakuwa karibu na mimi masaa 24
Tafadhari SHARE kwa ajili ya wengine
Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ofisi yangu inaitwa TUMAINI ALL NATURAL STORE, ipo Mwanagati Kitunda Ilala Dar Es Salaam.
Kama unahitaji kuonana na mimi uso kwa uso weka miadi (appointment) kwa kunipigia simu au niachie ujumbe WhatsApp 0714800175.
Pia kama una semina au kongamano lolote na unahitaji mzungumzaji hasa kwa upande wa afya hususani tiba asili, tuwasiliane napatikana.