أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
054-Al-Qamar Aayah 47-49
Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ ﴿٤٧﴾
Hakika wahalifu wamo katika upotofu na wazimu.
يَوْمَ يُسْحَبُونَ فِي النَّارِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ ذُوقُوا مَسَّ سَقَرَ ﴿٤٨﴾
Siku watakayoburutwa motoni kifudifudi: Onjeni mguso wa moto mkali mno.
إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ ﴿٤٩﴾
Hakika sisi Tumekiumba kila kitu kwa Qadar (majaaliwa). [Al-Qamar: 49]
Sababun-Nuzuwl:
كان مُشركو قريشٍ عندَ رسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم يُخالِفونَه في القدَرِ فنزَلتْ هذه الآيةُ: ((إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ * يَوْمَ يُسْحَبُونَ فِي النَّارِ عَلَى وُجُوهِهِمْ ذُوقُوا مَسَّ سَقَرَ * إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ))
Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kuwa Washirikina wa ki-Quraysh walikuwa wakimpinga Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Al-Qadar. Zikateremka Aayah hizi:
إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ ﴿٤٧﴾
Hakika wahalifu wamo katika upotofu na wazimu.
يَوْمَ يُسْحَبُونَ فِي النَّارِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ ذُوقُوا مَسَّ سَقَرَ ﴿٤٨﴾
Siku watakayoburutwa motoni kifudifudi: Onjeni mguso wa moto mkali mno.
إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ ﴿٤٩﴾
Hakika sisi Tumekiumba kila kitu kwa Qadar (majaaliwa). [Al-Qamar: 49]
[Ibn Hibbaan na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Hibbaan (6139), na As-Silsilah Asw-Swahiyhah (4/53)]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni