Aayah Na Mafunzo
Aal-‘Imraan
Allaah Anaridhia Mshikamane Kwa Kamba Yake Msifarikiane
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٠٣﴾
103. Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Allaah juu yenu, pale mlipokuwa maadui (kati yenu); kisha Akaunganisha nyoyo zenu, mkawa kwa neema Yake ndugu; na mlikuwa ukingoni mwa shimo la moto Akakuokoeni humo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat Zake mpate kuongoka.
Mafunzo:
Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Anawaridhia mambo matatu na Anachukia kwenu mambo matatu; Anawaridhia mumwabudu Yeye, wala msimshirikishe kwa chochote, na mshikamane nyote na kamba ya Allaah wala msifarikiane. Na anachukia kwenu uvumi, kuuliza sana na kupoteza mali.” [Muslim, na katika riwayaah: “Na muwanasihi wenye kuwatawalia mambo yenu.” Swahiyh Adaab Al-Mufrad (343)].
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni