Aayah Na Mafunzo
Aal-‘Imraan
Masjid Al-Haraam Ni Ya Kwanza Kuanzishwa Duniani
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾
Hakika nyumba ya awali iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ‘ibaadah) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah), yenye barakah na mwongozo kwa walimwengu. [Aal-'Imraan: 96]
Mafunzo:
Abuu Dharr (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Masjid gani ilijengwa ardhini mwanzo? Akasema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Masjid Al-Haraam (Makkah).” Kisha nikasema: Kishaupi? Akasema: “Masjid Al-Aqswaa (Palestina).” Nikasema: Kuna muda gani baina ya kuwepo Masjid mbili hizo? Akasema: “Miaka arubaini na popote itakapokudiriki Swalaah basi swali hapo pia ardhi ni mahala pa kuswali.” [Al-Bukhaariy na Muslim].
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni