Translate

Alhamisi, 12 Septemba 2019

31-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Akiwahudumia Maswahaba Kama Kuwamiminia Maji Ya Kunywa

 

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

31-Unyenyekevu Wake: Akiwahudumia Maswahaba

Kama Kuwamiminia Maji Ya Kunywa

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Hadiyth ndefu ya Abuu Qataadah kuhusu kisa cha kupitiwa kwao na usingizi Alfajiri …..

 

 

قَالَ: فَانْتَهَيْنَا إِلَى النَّاسِ حِينَ امْتَدَّ النَّهَارُ وَحَمِيَ كُلُّ شَىْءٍ وَهُمْ يَقُولُونَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ: هَلَكْنَا عَطِشْنَا ‏.‏ فَقَالَ: ‏"‏لاَ هُلْكَ عَلَيْكُمْ"‏ ‏.‏ ثُمَّ قَالَ: ‏"‏أَطْلِقُوا لِي غُمَرِي"‏ .‏ قَالَ: وَدَعَا بِالْمِيضَأَةِ فَجَعَلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَصُبُّ وَأَبُو قَتَادَةَ يَسْقِيهِمْ فَلَمْ يَعْدُ أَنْ رَأَى النَّاسُ مَاءً فِي الْمِيضَأَةِ تَكَابُّوا عَلَيْهَا ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ‏"‏أَحْسِنُوا الْمَلأَ كُلُّكُمْ سَيَرْوَى‏"‏.‏ قَالَ: فَفَعَلُوا فَجَعَلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَصُبُّ وَأَسْقِيهِمْ حَتَّى مَا بَقِيَ غَيْرِي وَغَيْرُ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم – قَالَ: ثُمَّ صَبَّ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ لِي: "‏اشْرَبْ "‏‏.‏ فَقُلْتُ: لاَ أَشْرَبُ حَتَّى تَشْرَبَ يَا رَسُولَ اللَّهِ:  قَالَ: "‏إِنَّ سَاقِيَ الْقَوْمِ آخِرُهُمْ شُرْبًا‏"‏ ‏.‏ قَالَ: فَشَرِبْتُ وَشَرِبَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم  قَالَ: فَأَتَى النَّاسُ الْمَاءَ جَامِّينَ رِوَاءً

 

 …(Abuu Qaatadah) akasema:  “Basi tukaendelea mpaka tukawafikia watu (tulioawaacha nyuma), na mchana ukawa umetanda na kila kitu kilishika joto  nao (Maswahaba) wakasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Tumeangamia! Tumebanwa na kiu!” Akasema:  ((Hamtaangamia)) Kisha akasema: ((Nipeni kikombe kodogo changu)).  Kisha akaomba aletewe jagi la maji. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaanza kumimina maji (katika kikombe kidogo) na Abuu Qaatadah akawa anawanyeshwa maji.  Watu walipoona kuwa kuna maji (kidogo) katika jagi, wakalielemea. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Tulieni! Maji yatakutosheni!)). Kisha (Maswahaba) wakaanza kupata (mgao wao) wa maji kwa utulivu (bila ya kudhihirisha kutapatapa) na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaanza kujaza (kifuniko) nami nikaanza kuwamiminia (maji) mpaka ikawa hakuna aliyebakia isipokuwa mimi na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Kisha akajaza (kikombe) maji na akaniambia: ((Kunywa!)) Nikamwambia: “Sitokunywa mpaka unywe wewe Ee Rasuli wa Allaah.” Akasema: ((Anayewamiminia watu hanywi mpaka wa mwisho wao amalize kunywa)). Nikanywa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanywa pia na watu wakafikia mahali pa maji wakiwa wanafuraha na kuridhika...    [Muslim]



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...