Translate

Jumanne, 25 Juni 2019

Haijuzu kwa mke kubaki na mume kafiri asiyeswali

Swali


Tatizo langu ni kuhusiana na mume wangu, ni mwanaume ambaye ana mapungufu katika Dini yake, haswali. Na pindi ninapomwita kuswali anakasirika na ananifanyia istihzai. Na anaendelea kuacha Swalah kwa hoja kuwa baba yake alikuwa haswali, hii ndio sababu na yeye haswali. Niliendelea na hali ya kumkumbusha na siku moja akanambia: “Ukiendelea kwa hali hii, mlango uko wazi”, hapo ndio nilifika namuomba Talaka. Na mara ya pili ilikuwa takriban sababu hiyo hiyo. Akanambia: “Usiniongeleshi mpaka siku ya Qiyaamah”. Ipi rai yako kwa mtu huyu na kwa maneno yake aliyosema kwa minasaba miwili, wa kwanza na wa pili? Je, huchukuliwa ni Talaka au nini? Na je, inajuzu kwangu kubaki nae katika hali hii?


Jibu



Mwanaume huyu haijuzu kubaki nae. Maadamu anaacha Swalah kama ulivyosema, kwa hilo anakuwa kafiri. Ikiwa baba yake naye haswali, kaiga kwake. Na wala haijuzu kumuiga kafiri asiyeswali, anatukana Dini, au anafanya kitu miongoni mwa vitu vinavyovunja Uislamu wa mtu au maasi katika maasi ya kumuasi Allaah. Watu wote hawa ni mamoja. Mwanaume huyu ni kafiri na kamuiga kafiri mwenzake kutokana na kauli yake. Na imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba kasema:
“Baina ya mtu na baina ya kufuru na Shirki ni kuacha Swalah.” (Kaipokea Muslim katika Swahiyh yake)
Na kasema (´alayhis-Swalaah was-Salaam):
“Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni Swalah, mwenye kuiacha amekufuru.”

Kauli yenye nguvu katika kauli za wanachuoni ni kwamba, mwenye kuiacha kwa kuzembea na uvivu ni kafiri, hata kama hakupinga uwajibu wake. Na ikiwa mwanaume huyu anapinga uwajibu wake, ni kafiri kwa Ijmaa´. 


Kwa hali yoyote, mwanaume huyu ni mwanaume mbaya na ni kafiri kwa kuacha kwake Swalah kutokana na kauli yenye nguvu ya wanachuoni. Haijuzu kwako kubaki nae. Bali ni wajibu kwako kuachana nae na wala usimpe kitu. Na kauli yake kusema kuwa mlango uko wazi, hii ni kinaya. Ikiwa amekusudia Talaka, anakusudia utoke kwa nia ya Talaka, itakuwa ni Talaka. 


Na ikiwa hakukusudia Talaka, itakuwa sio Talaka. Lakini kwa hali yoyote, hata kama hakukutaliki, haitakikani kwako kubaki nae. 


Bali ni wajibu kwako kumuacha na umuachie [… sauti haiko wazi… ], na watoto wako uwachukue na yeye (mume) hana haki ya (kubaki na) watoto kutokana na ukafiri wake. Wewe ndiye aula zaidi ya watoto wako. 


Ni mwanaume mbaya kwa kumkufuru kwake Allaah (´Azza wa Jalla). Huenda Allaah Akamsamehe. Akitubu nawe bado ungali ndani ya eda, akarejea, akatubu kwa Allaah na akajuta kwa aliyoyafanya na akaanza kuswali, hakuna ubaya kwako kurudi kwake na maadamu ungali ndani ya eda. Ama baada ya eda hapana (kurudi kwake), isipokuwa kwa ndoa mpya.



Na  Allaah  anajua  zaidi


kuvumilia maudhi ya wanawake wanapokuwa wajawazito

Swali: Mimi nilioa na tahamaki mke wangu akaniomba talaka kwa hoja kwamba hakuishi maisha ya starehe vile alivyotarajia. Mimi ni kijana na mwanafunzi vilevile ambaye hali yangu ni ya kawaida. Kuniomba kwake talaka kulikuwa ni pasi na haki na mimi sikuwa na nia ya kumtaliki kwa kuwa alikuwa ni mjamzito. Je, akiniomba talaka ni haki kwangu kurudishiwa mahari? Isitoshe mahari yenyewe ilikuwa ni misaada kutoka kwa watu. Je, ikiwa atanipa mahari hayo nina haki ya kuzitumia au nitatakiwa kuzirudisha kule nilikozichukua pamoja na kuwa mimi ni mwenye madeni tele yasiyojua yeyote isipokuwa Allaah pekee.



Jibu: Katika hali hii mwanaume akiweza kuwa na subira na asimjibu ndio bora zaidi. Hili ni kwa sababu mbili:


Ya kwanza: Baadhi ya wanawake wanapokuwa na mimba wanawachukia waume zao. Wanawachukia waume zao hata kama ameishi naye miaka mingi. Kwa hivyo awe na subira juu yake mpaka yataisha. Huenda akarudi katika hali yake ya kawaida na yakamuondoka yaliyomkereta moyoni mwake.

Ya pili: Huenda baada ya kujifungua akaelewa kuwa anatakiwa kubaki kwa mume wake na hatimaye yakamwondoka yaliyomo moyoni mwake.
Mimi naona kwamba ikiwa amemridhia tabia na dini yake basi awe na subira juu yake na amfanyie wepesi mpaka migogoro iishe. Baada ya yeye kujifungua ataangaliwa kama kweli anaona hawezi kubaki basi ni sawa akaomba haki yake. Mwanamke wa Thaabit bin Qays (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia:
“Ee Mtume wa Allaah! Sina cha kumtia dosari Thaabit bin Qays si katika tabia wala dini. Lakini mimi nachelea kufuru katika Uislamu.”
Kumesemwa tabia na dini. Isitoshe huyu ni miongoni mwa wale ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemshuhudilia Pepo.
Aliposema kuwa anachelea kufuru katika Uislamu bi maana kwamba hawezi. Hapo ndipo alipomwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Je, utaweza kumrudishia bustani yake?” Akajibu: “Ndio.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwita na kumwambia: “Chukua bustani yako na umtaliki.”
Akachukua bustani yake na kumtaliki. Kwa hivyo tunamshauri mwanaume huyu asubiri mpaka pale mwanamke huyu atapojifungua. Huenda vilevile akabadilika baada tu ya kujifungua midhali ameridhika na dini na tabia yake. Vinginevyo mambo yasipobadilika basi hakuna ubaya kwake akamuomba haki yake yote aliyompa kuanzia mahari, zawadi na vinginevyo. 


Ikiwa baadaye atarudi kwake basi hivyo vitu ni vya mwanaume kwa kuwa alivichukua kwa haki. Ikiwa alivichukua kwa haki yake basi yeye ndiye mwenye kuvimiliki. Wakati mwanaume alipovichukua kwa ajili ya ndoa amekuwa ni mwenye kuvimiliki. Vikirudi kwake basi ni miliki yake. Katika hali hii sio wajibu kwake kuvirudisha kwa yule aliyevichukua kutoka kwake.



Rejea al-Liqaa' ash-Shahriy (31)


Kaandika talaka kisha kaichana, je imepita?

Swali: Mimi nimemuoa mwanamke ambaye anaasi amri zangu na wala hanitii kwa kitu. Na daima anatoka nyumbani bila ya idhini yangu nakwenda kufanya baadhi ya kazi ambazo zimenifanya kunighadhibisha na kufikiria kumtaliki. Ikawa nimeandika karatasi ambapo nimeandika kuwa “nimekutaliki Talaka mbili” na nikamtaja kwa jina lake na la baba yake. Wakati huo nilikuwa nyumbani peke yangu na sikuwa na yeyote. Lakini baada ya hapo nikawa nimeichana hiyo karatasi na wala hakuna yeyote aliyejua kilichokipitika wala yeye. Na wakati huo ili-kuwa ni kabla ya miezi mitano. Talaka imepita au hapana?
Jibu: Ndio, zimepita Talaka mbili. Ukimtaliki kwa kuandika au kwa kumtakia, Talaka inakuwa imepita hata kama hukushuhudisha. Lakini umebaki na Talaka moja, ikiwa ulikuwa hujamtaliki kabla ya hapo umebaki na Talaka moja. Unaweza kumrejea, na unaweza kumchumbia tena ikiwa kishatoka ndani ya eda. Muhimu ni kuwa kumebakia Talaka moja, ikiwa ulikuwa hujamtaliki kabla ya Talaka hii uliyoandika.



Muulizaji: Kulikuwa kumeshapita miezi mitano kuanzia muda ule ambapo aliandika. Siatakuwa kishatoka ndani ya eda?
Ibn Baaz: Ndio, mara nyingi ni kuwa atakuwa kishatoka ndani ya eda kwa kupata hedhi au kwa miezi mitatu ikiwa ni eda ya mwanamke aliyokoma hedhi. Isipokuwa tu ikiwa kama ni mjamzito na hajajifungua, ni juu yake (aendelee) kukaa eda.



Muulizaji: Vipi lakini kuhusiana na muda ule tangu aandike karatasi hiyo ya Talaka, ikiwa kwa mfano (alimtaliki) katika Twahara ambayo kamwingilia.
Ibn Baaz: Kauli ya sahihi ni kuwa, ikiwa ni katika Twahara aliyomjamii au ilikuwa ni wakati wa hedhi, kauli ya sahihi ni kuwa (Talaka) haipiti. Tofauti na kauli ya wanachuoni wengi (wanaoonelea kuwa inapita).


Talaka za Bid´ah

Swali


Tumejua kupitia barnamiji hii ya kwamba haipiti Talaka kwa mwenye hedhi na mwenye mimba. Je, ni kuwa haipiti kabisa au inapita baada ya Twahara?



Jibu



Talaka ya mwenye hedhi haipiti kutokana na kauli sahihi (yenye nguvu) ya wanachuoni, tofauti na kauli ya jamhuri. Jamhuri ya wanachuoni wanaona kuwa inapita. Hali kadhalika kwa mwenye nifasi. 


Lakini kauli ya sahihi katika kauli za wanachuoni, na ndio waliokuwa wakifutu baadhi ya Taabi´iyn na Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na akaichagua Shayk-ul-Islaam bin Taymiyyah, mwanafunzi wake Ibn al-Qayyim na kundi katika wanachuoni, kuwa Talaka hii haipiti. Kwa kuwa inakwenda kinyume na Shari´ah ya Allaah, kwa kuwa Allaah Kawekea Shari´ah kumtaliki mwanamke katika hali ya Twahara ya nifasi, hedhi na katika Twahara ambayo mume wake hakumjamii. 


Hii ndio Talaka ya Kishari´ah. Akimtaliki katika hedhi, nifasi au Twahara ambayo amemjamii, Talaka hii ni Bid´ah na wala haipiti kutokana na kauli ya sahihi ya wanachuoni. Kwa Kauli ya Allaah (Jalla wa ´Alaa):
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ
“Ee Nabii! Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda (twahara na si katika hedhi) zao.” (65:01)
Bi maana katika Twahara ya jimaa. Namna hii ndivyo walivyosema wanachuoni kuhusu (maana ya) “watalikini katika wakati wa eda.” Wawe Twahara hawakuingiliwa au wawe na ujauzito. 



Hii ndio Talaka ya katika eda. Ama Talaka ya mjamzito wanachuoni wanaona kuwa inapita, na mwenye kusema kuwa haipiti kakosea. Talaka ya mjamzito inapita kwa wanachuoni, Talaka isiyopita ni ya mwenye hedhi na nifasi na Twahara ambayo mwanamke kaingiliwa na hakujadhihiri mimba yake. 



Talaka hizi (sampuli tatu) hazipiti kutokana na kauli ya sahihi ya wanachuoni, kwa kuwa zinakhalifu na Shari´ah ya Allaah na vile vile ni katika hali ambayo haikuwekwa Talaka kama tulivyotangulia kusema. Na baadhi ya ´Awwaam wanastaajabu na kusema Talaka ya mjamzito haipiti, hili ni kosa. Hii ni katika kauli za ´Awwaam zisizokuwa na asli katika Shari´ah wala maneno ya wanachuoni. Mjamzito Talaka inapita. Ni wajibu kujua hilo.

Rejea Nuur ´alaad-Darb

Na  Allaah anajua  zaidi


Mashahidi katika talaka

                      Mashahidi katika talaka




Allaah (Subhaana wa Ta´ala) amesema kwamba:
فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّـهِ
“atakapokaribia kufikia muda wao, basi wazuieni kwa wema au farikianeni nao kwa wema na mshuhudishe mashahidi wawili wenye uadilifu katika nyinyi na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Allaah. “65:02


Ameamrisha kuwepo mashahidi wakati mume atapomrejea mke. Ummah umeafikiana juu ya kwamba mashahidi wanatakiwa kuwepo. Wako waliosema kwamba maamrisho ni kwa njia ya uwajibu na wengine wamesema maamrisho ni kwa njia ya mapendekezo tu.
Baadhi ya watu wamedhani kuwa ushahidi ni kwa ajili ya talaka na kwamba talaka haipiti isipokuwa mpaka kuwepo mashahidi. Haya yanakwenda kinyume na maafikiano, Qur-aan na Sunnah. Hakuna yeyote katika wanachuoni wanaotambulika aliyesema hivo. Mara ya kwanza talaka iliruhusiwa kwa kuwepo mashahidi. Kuliamrishwa kuwepo kwa mashahidi wakati aliposema:
فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ
“atakapokaribia kufikia muda wao, basi wazuieni kwa wema.”
Makusudio ya mtengamano katika Aayah ni kumwacha pindi eda yake itakapokwisha. Hii sio talaka, kumrejea wala kumuoa. Ni lazima wawepo mashahidi juu ya mambo haya matatu kwa maafikiano ya waislamu.
Hekima ya hilo ni kwamba shaytwaan anaweza kumshawishi mwanaume ambapo akamtaliki mwanamke kwa mara ya tatu na akalificha hilo pasi na yeyote kujua. Matokeo yake mwanamke huyo akabaki kuishi pamoja naye ilihali amekwishaharamika kwake. Ndipo Allaah akaamrisha pindi atapomrejea awashuhudishe mashahidi ili watu wajue ni mara ngapi amemwacha.
Hilo ni tofauti na talaka. Pindi mwanaume atapomtaliki mke wake itawadhihirikia watu ya kwamba sio mwanamke wake tena.


Rejea Kitab Majmuu´-ul-Fataawaa (33/33-34)

Na Allaah  anajua  zaidi


Jumatatu, 24 Juni 2019

POMBOO: Samaki mpole mwenye akili

Naam! Kwa taufiki yake Mola Karima aliyetupa uhai na uzima tumekutana tena katika mfululizo mwengine wa makala zetu hizi za kuwasoma na kujifunza viumbe mbalimbali wa Allah Aliyetukuka.

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Muumba wa kila kitu ndiye peke anayestahiki kuabudiwa katika dunia hii. Yeye ameumba mbingu na ardhi, Jua na Mwezi na wanyama wa bara na baharini, naye ndiye anayewaruzuku. Katika viumbe wote ambao Mwenyezi Mungu amewaumba, zipo dalili na ishara ya kuwa Allah Aliyetukuka peke yake ndie anayestahiki kuabudiwa.

Katika dalili na alama za kumjua Mungu kupitia viumbe vyake, leo nataka ujifunze jambo kumuhusu samaki wa ajabu anayefahamika kwa Jina la pomboo.

Pomboo ni wanyama wa majini wanaofanana sana na nyangumi. Inatajwa kuwa, kuna pomboo takribani aina 40. Pomboo wana ukubwa tofauti, kuanzia urefu wa mita 1.2 – 9.5 na uzito wa kilogramu 40 mpaka tani 10. Viumbe hawa wanapatikana duniani kote, hasa kwenye bahari za kina kifupi.

Pomboo huchangamana sana wao kwa wao, na huweza hata kufikia kundi moja dogo. Makundi hayo yanaweza kuongezeka, hata kufikia pomboo 1,000. Pomboo hutumia milio mbalimbali katika mawasiliano yao, huku wakisaidiana sana hasa pale miongoni mwao wanapokuwemo wagonjwa. Pomboo huweza hata kuwasaidia wenzao kupumua kwa kuwasogeza kwenye usawa wa maji. Huko New Zealand, pomboo waliwahi kuonekana wakilinda jike na ndama wao.

Pomboo wameonekana pia wakiwalinda waogeleaji kwa kuwazunguka katika duara ili wasishambuliwe. Pia wameonekana wakiwakasirisha papa ili kuwafukuza.

Pomboo, mara nyingi, huwa Mara katika makundi. Mara kadhaa, pomboo, hasa dume, wame kuwa wakigombana na hivyo kusababisha kuwa na makovu mengi mwilini mwao. Aghalabu sababu ya kupigana ni kugombania nafasi ya kuwa na jike. Wale wanaoshindwa huenda zao mbali.

Pomboo ni samaki msafi. Hapendi usafi asilani. Ukirusha kitu majini, pomboo yeye hukirudisha nje kwa kukipiga na mkia wake, Midomo ya pomboo imechongoka na vijimeno vyake ni vidogo vidogo sana lakini hatari. Umaarufu wa samaki huyu pengine umechagizwa pia na mahusiano yake na binadamu.

Wataalamu wa elimu ya viumbe wa baharini wanasema, ni vigumu kufa maji kama pomboo yupo eneo hilo kwani samaki huyu anaweza kuja kukuokoa. Akiwepo samaki huyu jirani pia huwezi kudhuriwa na samaki wakali kama papa. Pomboo atakulinda kwa hali na mali.

Inapotokea umedumbukia majini na akakuona, haraka pomboo hukujia sana, kisha atakukumbatia na kwa spidi kubwa atakuwa anakupeleka nchi kavu. Atakapofika jirani atakurusha huko na msaada wake huishia hapo. Ukitua kwenye jiwe, mwamba, michongoma au kwenye mti hiyo ni shauri yako yeye kazi yake kashamaliza

UZAZI

Pomboo hujamiiana kwa vipindi vifupi lakini hufanya mara nyingi nyingi katika muda mfupi. Pomboo hubeba mimba kwa muda wa miezi 11-12, kutegemeana na aina husika. Pomboo huanza kujamiiana katika umri mdogo. Pia, umri hasa wa kukomaa kijinsia hutofautiana kutoka aina moja mpaka nyingine.

Pomboo huzaa mtoto mmoja au wawili, na huyu ni samaki mwenye kasi kubwa ya kusafiri majini. Pomboo hatagi bali anazaa. Pia, pomboo hunyonyesha. Samaki huyu anafanana na mwanadamu katika mambo mengi, ikiwemo kuzaa na kunyonyesha na vilevile kuishi kifamilia.


CHAKULA

Pamoja na kwamba samaki ndiyo chakula chake kikuu, pomboo pia hupendelea zaidi kula pweza na fisi maji. Pomboo hula kwa namna mbalimbali na pia ana mbinu mbalimbali za kushambulia samaki. Namna mojawapo ni ile ya kuwatenga samaki kadhaa kwa kuwazunguka, na kisha kuanza kuwashambulia taratibu. Namna nyingine ni pale pomboo wanapowafukuzia samaki kwenye maji yenye kina kifupi na kisha kuwakamata kwa urahisi.

MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU POMBOO

  • Pomboo ni kiumbe mpole na mwenye akili sana. Inatajwa pia na baadhi ya wataalamu kuwa, baada ya binadamu, viumbe wanaofuata kwa akili ni pomboo pamoja na kunguru.
  • Licha ya upole wake, pomboo ana kasi kubwa sana majini.
  • Kwa kawaida, pomboo hulala upande mmoja tu wa ubongo, huku mwingine ukiendelea kufanya kazi ya kuratibu masuala mengine kama vile kupumua na kujihami na hatari za mazingira yao. Hata hivyo, usingizi wa hatua za mwanzo hutokea katika sehemu zote za ubongo.
  • Pomboo ni samaki anayelindwa na umoja wa mataifa hivyo chunga sana matamanio yako ya kutaka kumla.
  • Pomboo huwasaidia wavuvi katika shughuli zao za uvuaji wa samaki. Kwa mfano, ili wavuvi wapate samaki, pomboo hutumia mkia wake kuwapiga samaki wakubwa. Pomboo hufanya yote haya kwa mapenzi aliyonayo kwa mwanadamu.
  • Inaelezwa na wataalamu wa elimu wa viumbe wa baharini kuwa pomboo ana takriban meno yapatayo 100 mdomoni.
  • Pomboo wana namna yao ya kuwasiliana kwa lugha, tena kwa sauti.


Nifasi na eda ya talaka

                         Nifasi na eda ya talaka



Hukumu za nifasi ni zile zile kama hukumu za hedhi isipokuwa katika mambo yafuatayo:
Jambo la kwanza  Eda inaisha kwa kuzaa na sio kwa nifasi. Talaka ikipitika kabla ya kuzaa basi eda inaisha kwa kuzaa na si kwa nifasi. 


Na ikiwa talaka itapitika baada ya kuzaa, basi itabidi asubiri mpaka pale atapopata hedhi halafu aangalizie hapo.


Jambo la pili  Kipindi cha Ilaa´ kiko pamoja na hedhi na si nifasi. Ilaa´ maana yake ni mume kuapa kuwa hatofanya jimaa na mke wake kabisa au chini chini miezi mine. 


Akifunga kiapo hicho na mke akamtaka wafanye jimaa ambapo akakataa, ana miezi mine kuanzia ile siku alipofunga kiapo. Baada ya muda kutimia atalazimika kufanya naye jimaa. 


La sivyo mke ataomba talaka. Ikiwa ndani ya muda huu atapata nifasi, muda huu hauhesabiki kwa mume. 


Miezi minne hiyo itakuwa ni ya kipekee pasi na nifasi. Tofauti na hedhi ambayo miezi mine hiyo itahesabika kwa mume.



Jambo la tatu Kubaleghe kunajulikana kwa hedhi na si kwa nifasi. Kwa kuwa mwanamke hawezi kushika mimba mpaka amwage usingizini. 

Anabaleghe kwa kumwaga usingizini kabla ya kushika ujauzito.


Jambo la nne Damu ya hedhi ikikatika kisha ikarejea katika ada basi inahesabika bila ya shaka kuwa ni damu ya hedhi. Mfano wa hilo ada ya mwanamke ni kwa siku nane. Baada ya siku nne damu yake ikakatika kwa siku mbili na halafu siku ya saba na ya nane ikarudi tena. Damu hii iliyorudi ni hedhi pasina shaka yoyote na kutathibiti hukumu za hedhi.

Ama kuhusu nifasi, damu ikikatika kabla ya siku arubaini kisha ikarudi tena ndani ya siku arubaini, damu hii itazingatiwa ni yenye kutia shaka. Kwa hivyo itakuwa ni wajibu kwa mwanamke kuswali na kufunga faradhi kwa wakati wake na ni haramu kwake kufanya yale ambayo ni haramu kwa mwanamke mwenye hedhi mbali na mambo ya wajibu. 


Baada ya kutwaharika atalipa zile ´ibaadah alizofanya katika kipindi cha damu hii yenye kutia shaka kama jinsi ni wajibu kwa mwanamke mwenye hedhi kulipa yale yaliyompita. Haya ndio maoni yanayojulikana kwa wanachuoni wa Hanaabilah.

Hata hivyo kauli sahihi ni kuwa maadamu damu inatoka katika kipindi cha nifasi inahesabika kuwa ni nifasi. Vinginevyo ni damu ya hedhi. Damu ikiendelea kutoka pasina kukatika inahesabika kuwa ni damu ya ugonjwa. Haya yanashabihiana na yale Ibn Qudaamah aliyotaja katika “al-Mughniy”[al-Mughniy (1/349).] kutoka kwa Imaam Maalik ambaye amesema:

“Akipata damu siku mbili au tatu baada ya kuwa imekatika, inahesabika kuwa ni nifasi. Vinginevyo ni damu ya hedhi.”

Maoni haya ndio muqtadha wa chaguo la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah. Uhakika wa mambo ni kuwa hakuna damu yenye kutia mashaka. Mambo yote yako wazi wazi kwa kutegemea ujuzi na uelewa wa watu. Qur-aan na Sunnah imebainisha kila kitu. 


Allaah (Subhaanah) hakumuwajibishia yeyote kufunga mara mbili au kufanya Twawaaf mara mbili ikiwa matendo hayo hayakufanywa kimakosa na hapo yakahitajia kurudiliwa. Pindi mja anapofanya kiasi na anavyoweza basi ameitakasa dhimma yake. 


Allaah (Subhaana wa Ta´ala) amesema:


لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake.” (02:286)


فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Basi mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)



Jambo la tano Mwanamke damu yake ikikauka ndani ya ada, inafaa kufanya jimaa na mume wake. Ni jambo ambalo halikuchukizwa kabisa. Hata hivyo ni jambo lenye kuchukiza kufanya naye jimaa akikauka katika damu ya uzazi wake ndani ya siku arubaini. Hii ndio kauli yenye kujulikana katika madhehebu [ya Hanaabilah].
Kauli sahihi ni kuwa haikuchukizwa kabisa kufanya naye jimaa. Hii ndio kauli ya wanachuoni wengi. Machukizo ni hukumu ya Kishari´ah inayohitajia dalili ya Kishari´ah. Hakuna katika masuala haya dalili isipokuwa ile aliyotaja Imaam Ahmad kutoka kwa ´Uthmaan bin Abiyl-´Aasw na kwamba mke wake alimjia ndani ya zile siku arubaini ambapo akasema:
“Usinikaribie.”
Hili halilazimishi kuwa imechukizwa. Huenda alisema hivo kwa njia ya usalama kwa kukhofia kwamba hakuwa na yakini juu ya kutwahatika kwake, damu yake kurudi kwa sababu ya jimaa au sababu nyengineyo na Allaah ndiye anajua zaidi.





20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...