أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Suwrah Huwd Aayah 114
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ﴿١١٤﴾
Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku; hakika mema yanaondosha maovu. Hivyo ni ukumbusho kwa wanaokumbuka. [Huwd: 114]
Sababun-Nuzuwl:
عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّ رَجُلاً، أَصَابَ مِنَ امْرَأَةٍ قُبْلَةً، فَأَتَى رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَذَكَرَ ذَلِكَ لَهُ فَأُنْزِلَتْ عَلَيْهِ ((وَأَقِمِ الصَّلاَةَ طَرَفَىِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِنَ اللَّيْلِ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ذَلِكَ ذِكْرَى لِلذَّاكِرِينَ)). قَالَ الرَّجُلُ: أَلِيَ هَذِهِ؟ قَالَ: " لِمَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ أُمَّتِي ".
Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) amehadithia: Mwanamume mmoja alimbusu mwanamke (kinyume na Shariy’ah) kisha akaenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kumhadithia. Allaah Akateremsha:
وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ﴿١١٤﴾
Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku; hakika mema yanaondosha maovu. Hivyo ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.
Yule mtu akamuuliza Rasuli wa Allaah: “Je, hii (Aayah) ni kwa ajili yangu?” Akajibu: “Ni kwa ajili ya watakaoitendea kazi katika Ummah wangu.” [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni