Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
03-Zuhd Yake:
Akiomba Du’aa Ya Kujaaliwa Rizqi Ya Kumtosheleza Tu
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akimuomba Allaah (سبحانه وتعالى) rizki ya kumtosheleza tu basi akiomba du’aa:
اللَّهُمَّ اجْعَلْ رِزْقَ آلِ مُحَمَّدٍ قُوتًا
Ee Allaah ijaalie rizki ya Ahl wa Muhammad iwe ya kutosheleza tu.” [Muslim]
Na akataja katika Hadiyth yanayompasa bin Aadam kutosheka nayo:
عن أَبي عمرو ، ويقالُ : أَبو عبدِ الله ، ويقالُ : أَبو ليلى عثمان بن عفان رضي الله عنه : أنَّ النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَيْسَ لاِبْنِ آدَمَ حَقٌّ في سِوَى هذِهِ الخِصَالِ : بَيْتٌ يَسْكُنُهُ ، وَثَوْبٌ يُوارِي عَوْرَتَهُ ، وَجِلْفُ الخُبز وَالماء )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu 'Amru (رضي الله عنه) Inasemwa ni Abu 'Abdillaah, na inasemwa Abu Laylaa 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه) kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Bin Aadam hana haki ya kuwa na zaidi ya vitu aina tatu: nyumba atakayoishi, na mavazi ya kusitiri uchi wake na kipande cha mkate na maji." [At-Tirmidhy, na akasema ni Hadiyth Swahiyh]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni