04-Zuhd Yake: Alikosa Chakula Nyumbani Mwake Hadi Kufikia Miezi Miwili
Kulifikia ukosekanaji wa chakula nyumbani mwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa siku nzima au masiku au hadi miezi kupita! Basi hakika hii pia ni sifa ya Zuhd ya ajabu mno kuimiliki mtu!
وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما ، قَالَ : ذَكَرَ عُمَرُ بْنُ الخَطَّابِ رضي الله عنه ، مَا أَصَابَ النَّاسُ مِنَ الدُّنْيَا ، فَقَالَ : لَقَدْ رَأيْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَظَلُّ الْيَوْمَ يَلْتَوِي مَا يَجِدُ مِنَ الدَّقَلِ مَا يَمْلأ بِهِ بَطْنَهُ . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa An-Nu'maan bin Bashiyr (رضي الله عنهما) ambaye amesema: Alitaja 'Umar bin Al-Khattaab (رضي الله عنه) yale yaliyowafikia watu katika hii dunia, akasema: "Hakika nilimuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akipitisha siku zake akiwa na njaa hana hata tende (hata) mbaya ya kuondoa njaa yake." [Muslim]
Mpaka katika hali yake ya kuaga dunia hakuwa na chakula nyumbani mwake:
عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : تُوفي رسول الله صلى الله عليه وسلم، وَمَا في بَيْتِي مِنْ شَيْءٍ يَأكُلُهُ ذُو كَبِدٍ إِلاَّ شَطْرُ شَعِيرٍ في رَفٍّ لي ، فَأكَلْتُ مِنْهُ حَتَّى طَالَ عَلَيَّ ، فَكِلْتُهُ فَفَنِيَ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها) amesema: "Aliaga dunia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na hakukuwa katika nyumba chakula cha sawa (kwa watu kula) isipokuwa mtama kidogo katika stoo yangu ambao nilikuwa nikiutumia kwa muda. Baadae nilitaka kuupima lakini ukawa umemalizika." [Al-Bukhaariy na Muslim
Bali alikosa chakula nyumbani mwake hadi kufikia siku tatu:
عن عَائِشَة رضي الله عَنْهَا قالت : (مَا شَبِعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ تِبَاعًا مِنْ خُبْزِ بُرٍّ حَتَّى مَضَى لِسَبِيلِهِ) رواه البخاري ومسلم
‘Aaishah (رضي الله عنها) amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupatapo kula mkate wa ngano mpaka kufariki kwake.” [Muslim na wengineo]
Na pia,
فاطِمةَ ناوَلَتْ رسولَ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ كِسْرةً مِن خُبزِ شَعيرٍ، فقال: هذا أوَّلُ طعامٍ أكَلَهُ أبوكِ مِن ثَلاثةِ أيَّامٍ.
Na pia pindi mwanawe Faatwimah (رضي الله عنها) alipompatia kipande cha mkate wa shayiri alisema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Hiki ni chakula cha kwanza baba yako anakula tokea siku tatu.” [Hadiyth ya Anas bin Maalik ameikusanya Imaam Ahmad -Hadiyth Hasan]
Bali kulikosekana chakula nyumbani mwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hadi kufikia miezi!
عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّهَا كَانَتْ تَقُولُ: "وَاللَّهِ يَا ابْنَ أُخْتِي إِنْ كُنَّا لَنَنْظُرُ إِلَى الْهِلاَلِ ثُمَّ الْهِلاَلِ ثُمَّ الْهِلاَلِ ثَلاَثَةَ أَهِلَّةٍ فِي شَهْرَيْنِ وَمَا أُوقِدَ فِي أَبْيَاتِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم نَارٌ" قَالَ: قُلْتُ: يَا خَالَةُ فَمَا كَانَ يُعَيِّشُكُمْ؟ قَالَت: الأَسْوَدَانِ التَّمْرُ وَالْمَاءُ إِلاَّ أَنَّهُ قَدْ كَانَ لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم جِيرَانٌ مِنَ الأَنْصَارِ وَكَانَتْ لَهُمْ مَنَائِحُ فَكَانُوا يُرْسِلُونَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنْ أَلْبَانِهَا فَيَسْقِينَاهُ .
Amehadithia ‘Urwah kuwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) alikuwa akimwambia: “Ee mwana wa dada yangu! Tulikuwa tukiutazama mwandamo wa mwezi, kisha mwezi mwengine kisha mwezi mwengine, miandamo mitatu katika miezi miwili na ilhali katika nyumba za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakujaashwa moto (wa kupikia chakula). (‘Urwaa) Akasema: Nikamuuliza: “Ee Khaalat yangu, je, mliweza kuishi kwa vipi?” Akasema: “Vyeusi viwili: tende na maji isipokuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ana jirani katika Answaariy walikuwa wana mbuzi na walikuwa wakimletea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) maziwa yake akawa anatunywesha.” [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni