Translate

Alhamisi, 16 Julai 2020

013-Asbaabun-Nuzuwl: Ar-Ra’d

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

013-Suwrah Ar-Ra’d Aayah: 13

 

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَيُسَبِّحُ الرَّعْدُ بِحَمْدِهِ وَالْمَلَائِكَةُ مِنْ خِيفَتِهِ وَيُرْسِلُ الصَّوَاعِقَ فَيُصِيبُ بِهَا مَن يَشَاءُ وَهُمْ يُجَادِلُونَ فِي اللَّـهِ وَهُوَ شَدِيدُ الْمِحَالِ ﴿١٣﴾

Na radi inamsabihi (Allaah) kwa Himidi Zake na Malaika pia kwa kumkhofu, na Anatuma mingurumo ya radi, humsibu kwayo Amtakaye nao huku (makafiri) wakiwa wanabishana kuhusu Allaah Naye ni Mkali na Mwenye nguvu za kuhujumu. [Ar-Ra’d: 13]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

عن أنس بن مالك، أن رسول الله صلى الله عليه وسلم بعث رجلا مرّة إلى رجل من فراعنة العرب، فقال: "اذهب فادعه لي"، فقال:   "يا رسول الله إنه أعتى من ذلك"، قال: "اذهب فادعه لي"، قال: فذهب إليه فقال: " يدعوك رسول الله" قال:  "وما الله أمن ذهب هو أو من فضة أو من نحاس؟" قال فرجع إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم فأخبره، وقال: " قد أخبرتك أنه أعتى من ذلك قال لي كذا وكذا"  فقال : "ارجع إليه الثانية فادعه"، فرجع إليه، فعاد عليه مثل الكلام الأول، فرجع إلى النبيّ صلى الله عليه وسلم فأخبره، فقال: "ارجع إليه"، فرجع الثالثة فأعاد عليه ذلك الكلام، فبينا هو يكلمني إذ بعثت إليه سحابة حيال رأسه فرعدت فوقعت منها صاعقة فذهبت بقحف رأسه، فأنـزل الله تعالى: ((وَيُرْسِلُ الصَّوَاعِقَ فَيُصِيبُ بِهَا مَنْ يَشَاءُ وَهُمْ يُجَادِلُونَ فِي اللَّهِ وَهُوَ شَدِيدُ الْمِحَالِ))

Kutoka kwa Anas bin Maalik amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimtuma mtu amwendee mtu miongoni mwa firauni wa ki-Quraysh, Akamwambia “Nenda uniitie!” Akasema: “Ee Rasuli wa Allaah hakika yeye ni mtu jeuri kuliko hivyo (unavyotegemea kuwa ataitikia)” Akasema: “Nenda ukaniitie!” Akaenda (kwa firauni wa ki-Quraysh) akamwambia: “Rasuli Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anakuita” Akajibu: “Ama Wallahi? Kwani yeye anatokana na dhahabu au fedha au anatokana na shaba?” Akarudi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Nilikuambia kuwa yeye ni jeuri mno kuliko hivyo, kwani ameniambia kadhaa wa kadhaa.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Mwendee tena mara ya pili na mwite.” Akamrudia tena naye yule firauni wa ki-Quraysh akampa maneno yaleyale kama ya mwanzo. akarudi kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamjulisha. Akamwambia: “Mrudie tena.” Akamrudia mara ya tatu naye yule jeuri akampa maneno yaleyale.  Akasema: “Basi pindi alipokuwa akinisemesha akateremshiwa wingu juu ya kichwa chake, mngurumo na radi ikampiga na kumuangusha na kusambaratisha fuvu la kichwa chake, hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:   

وَيُرْسِلُ الصَّوَاعِقَ فَيُصِيبُ بِهَا مَن يَشَاءُ وَهُمْ يُجَادِلُونَ فِي اللَّـهِ وَهُوَ شَدِيدُ الْمِحَالِ ﴿١٣﴾

Anatuma mingurumo ya radi, humsibu kwayo Amtakaye nao huku (makafiri) wakiwa wanabishana kuhusu Allaah Naye ni Mkali na Mwenye nguvu za kuhujumu. [Ar-Ra’d 13]

 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...