Translate

Alhamisi, 3 Septemba 2020

12-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Kuchinja Kwa Niyyah Ya Asiyekuwa Allaah

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

 

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

 

12 -Kuchinja Kwa Niyyah Ya  Asiyekuwa Allaah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaharamisha: 

 

 

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ وَأَن تَسْتَقْسِمُوا بِالْأَزْلَامِ ۚ ذَٰلِكُمْ فِسْقٌ

 

Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa asiyekuwa Allaah katika kuchinjwa kwake, na aliyenyongwa au aliyepigwa akafa, au aliyeporomoka, au aliyepigwa pembe, na aliyeliwa na mnyama mwitu, isipokuwa mliyewahi kumchinja kihalali (kabla ya kufa); na waliochinjwa kwa ajili ya ‘ibaadah ya waabudiwa, na kupiga ramli kwa mishale. Hayo kwenu ni ufasiki. [Al-Maaidah: 3] 

 

 

Sababu kuchinja ni ‘ibaadah tukufu kabisa Ameamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ichinjwe kwa ajili Yake Pekee. 

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake. [Al-Kawthar: 2] 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾

Sema: “Hakika Swalaah yangu, na kuchinja kafaara na ‘ibaadah zangu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu.” [Al-An’aam: 162] 

 

 

Na Rasuli wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) amelaani mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Hadiyth ya ‘Aliy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu): 

 

عَنْ عَلِيِّ بن أبي طالب (رضي الله عنه) قَالَ: حَدَّثَنِي رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) بأرْبَعِ كَلِمَاتٍ: ((لَعَنَ اللَّهُ مَنْ ذَبَحَ لِغَيْرِ اللَّهِ, وَلَعَنَ اللَّهُ مَنْ لَعَنَ وَالِدَيْهِ, وَلَعَنَ اللَّهُ مَنْ آوَى مُحْدِثًا, وَلَعَنَ اللَّهُ مَنح مَنَارَ الأَرْضِ )) 

Imepokewa kutoka kwa ‘Aliy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinihadithia maneno manne: ((Allaah Amemlaani anayechinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, na Allaah Amemlaani anayewalaani wazazi wake, na Allaah Amelaani anayemkaribisha na kumhami mhalifu, na Allaah Amelaani anayemlaani mzazi wake, na Allaah Amelaani anayebadilisha mipaka ya ardhi [anayomiliki])) [Muslim] 

 

 

Pia: 

 

حديث ثَابِتُ بْنُ الضَّحَّاكِ قَالَ : نَذَرَ رَجُلٌ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ يَنْحَرَ إِبِلاً بِبُوَانَةَ فَأَتَى النَّبِىَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: ‏إِنِّى نَذَرْتُ أَنْ أَنْحَرَ إِبِلاً بِبُوَانَةَ. فَقَالَ النَّبِىُّ -صلى الله عليه وسلم : ((هَلْ كَانَ فِيهَا ‏وَثَنٌ مِنْ أَوْثَانِ الْجَاهِلِيَّةِ يُعْبَدُ)) قَالُوا: لاَ. قَالَ: ((هَلْ كَانَ فِيهَا عِيدٌ مِنْ أَعْيَادِهِمْ )) ‏قَالُوا : لاَ. قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((أَوْفِ بِنَذْرِكَ فَإِنَّهُ لاَ وَفَاءَ لِنَذْرٍ ‏فِى مَعْصِيَةِ اللَّهِ وَلاَ فِيمَا لاَ يَمْلِكُ ابْنُ آدَمَ )). وصححه الألباني 

Imepokelewa kutoka kwa Thaabit ibn Adhw-Dhwahhaak (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: “Mtu mmoja aliweka nadhiri kuchinja ngamia sehemu ya Buwaanah. Akaja kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Nimeweka nadhiri kuchinja ngamia Buwaanah”.  Akasema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Je kuliweko masanamu ya kijaahiliyyah (kabla Uislamu) yakiabudiwa?”. Wakasema:  “Hapana” Akasema: ((Je kuliweko sherehe za kijaahiliyyah zikifanywa hapo?)). Wakasema: “Hapana” Rasuli wa Allaahh (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Timiza nadhiri yako, kwani hakuna kutimiza nadhiri katika kumuasi Allaah, wala katika ambayo hayamiliki bin Aadam)). [Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy] 

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah (1/226) wamefutu:  “Kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ni shirki na hukmu ya kichinjo ni hukmu ya nyamafu (mzoga) haijuzu kuliwa nyama yake hata kama imetajwa Jina la Allaah ikiwa imehakiki kuwa imechinjwa ghairi ya Allaah.” 

 

 

Na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema katika Majmuw' Fataawa Ibn ‘Uthaymiyn (2/148):  “Kuchinja kwa ajili kwa ajili ya aisyekuwa Allaah ni shirki kubwa kwa sababu kuchinja ni ‘ibaadah, kwa hiyo anayechinja kwa ajili (niyyah) asiyekuwa Allaah ni mshirikina ambaye shirki yake inamtoa nje ya Uislamu – tunajikinga na Allaah – ikiwa amechinja kwa ajili ya Malaika au kwa ajili ya Nabiy yeyote au kwa ajili ya Khaliyfah yeyote au kwa ajili ya awliyaa (waja wema) au kwa ajili ya Mwanachuoni yeyote. Yote ni kumshirikisha Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa) na inamtoa nje ya Uislamu. Na kuhusu kula nyama ya vichinjo hivyo ni haraam kwa sababu amechinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah na kila kinachochinjwa kwa ajili ya chochote ghairi ya Allaah au amechinjwa juu ya jiwe la madhabahu (mizimwi) ni haraam.”  

 

 

Hadiyth ifuatayo inadhihirisha kwamba hata ikiwa ni kiasi kidogo vipi kitu kinachokurubishwa pasi na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kuchinja, huwa ni shirki na hatari yake humuingiza mtu Motoni:  

 

((دَخَلَ الْجَنَّةَ رَجُلٌ فِي ذُبَاب، وَدَخَلَ النَّار رَجُلٌ فِي ذُبَاب)): قَالُوا: وَكَيْفَ ذَلِكَ يَا رَسُولَ الله؟ قَالَ: ((مَرَّ رَجُلانِ علَى قَوْمٍ لَهُمْ صَنَمٌ لاَ يَجُوزُهُ أحَدٌ حَتَّى يُقَرِّبَ لَهُ شَيْئاً، فَقَالُوا لإَحَدِهِمَا: قَرِّبْ، قَالَ: لَيْسَ عِنْدِي شَيْءٌ أُقَرِّبَهُ، قَالُوا بِه: قَرِّبْ وَلَوْ ذُباَبًا، فَقَرَّبَ ذُبَاباً، فَخَلُّوا سَبِيْلَهُ، فَدَخَلَ النَّارَ، وَقَالُوا لِلآخر: قَرِّبْ، فَقَالَ: مَا كُنْتُ لأُقَرِّبَ لأحَدٍ شَيْئًا دُونَ الله عَزَّ وَجَلَّ. فَضَرَبُوا عُنقَهُ، فَدَخَلَ الْجَنَّةَ)) 

((Mtu mmoja ameingia Jannah kwa nzi, na ameingia Motoni mtu kwa ajili ya nzi)).  Wakasema: Vipi hivyo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: ((Watu wawili walipitia mbele ya watu walikuwa na sanamu lao, hapiti mtu hadi ajikurubishe kwa kuchinja. Wakamwambia mmoja wao: Jikurubishe!  [Chinja!]  Akasema:  Sina kitu cha kujikurubisha. Wakasema: Jikurubishe japo kwa nzi.  Akajikurubisha kwa nzi.  Wakamwachia apite njia akaingia Motoni.  Wakawambia mwengine: Jikurubishe!  Akasema:  Sikuwa najikurubisha [nachinja] kwa yeyote pasi na Allaah ‘Azza wa Jalla. Wakampiga shingo [wakamuua] akaingia Jannah)). [Ahmad, Fataawaa Shaykh Ibn Baaz] 

 

 

Shaykh Fawzaan bin Fawzaan akifafanua Hadiyth hiyo anasema:  

“[Mtu wa kwanza] Ametoa udhuru kutokuwa na kitu. Hakusema “hakika kuchinja pasi na Allaah haijuzu au ni munkari” – Tunajikinga kwa Allaah.  Na hii inafahamika kwamba lau angelikuwa ana  mnyama wa kuchinja angelichinja. Wakamwambia: “Jikurubishe walau kwa nzi!” Akajikurubisha kwa nzi, yaani akafanya hivyo kwa ajili ya sanamu wakamwachia apite njia, akaingia Motoni kwa sababu ya shirki. Amejikurubisha pasi na Allaah, na 'ibra (zingatio) hapa ni niyyah na kusudio wala sio kuhusu kinachochinjwa.  Na kwamba hakuchukia jambo hili wala hakujiepusha nalo, bali ametoa udhuru kutokuwa na kitu na kwa hivyo amengia Motoni – Tunajikinga kwa Allaah. 

 

Na wakamwambia mwengine: “Jikurubishe!” Akasema:  “Sikuwa ni mwenye kuchinja chochote kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ‘Azza wa Jalla.” Amejiepusha na amechukia shirki. Wakampiga shingo yake, kwa maana wamemuua akaingia Jannah kwa sababu ya Tawhiyd. 

 

Hivyo basi katika Hadiyth hii tukufu kuna mafunzo muhimu:  

 

 

Kwanza:  Hadiyth inaruhusu kuelezea habari za ummah zilizopita na kuelezea ilivyothibiti kwa ajili ya kuwaidhi na zingatio. 

 

 

Pili:  Katika Hadiyth kuna dalili ya kuharamishwa kujikurubisha kwa kuchinja pasi na Allaah, na mwenye kujikurubisha pasi na Allaah, atakuwa ametenda shirki kwa sababu mtu aliyeua nzi ameingia Motoni hata ikiwa ni kitu kichafu cha kutemwa (kidogo, duni mno). Na mtu wa pili amechukia shirki na amejiepusha japokuwa ilikuwa ni kitu cha kuchukizwa (duni) akaingia Jannah. 

 

 

Tatu: Kama alivyosema Shaykh (Rahimahu Allaah) kuhusu mas-alah ya niyyah ya 'amali za moyo, japokuwa ni kitu kichafu cha kutemwa (kidogo, duni mno) lakini itambulike kuwa niyyah ni 'amali ya moyo.  

 

 

Nne:  Kama alivyosema Shaykh (Rahimahu Allaah) kuhusu wepesi wa bin Aadam kukaribia Jannah na Moto ni kama alivyosema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Jannah iko karibu zaidi kwa mmoja wenu kuliko nyuzi za viatu vyake, na Moto kama hivyo)). [Al-Bukhaariy]  

 

Huyu amepigwa shingo yake (ameuliwa) akaingia Jannah. Na yule wamemwachia njia akaingia Motoni.   

 

Tano: Kwamba mtu aliyeua  nzi alikuwa Muumini, akaingia Motoni kwa sababu ya kujikurubisha kwake kwa nzi, kwa sababu angelikua kafiri, angeliingia Motoni kwa kufru yake si kwa kujikurubisha kwa nzi. Akadhihirisha kwamba alikuwa Muumini, na mas-alah haya ni khatari sana! 

 

Basi wako wapi wanaochinja kwa ajili ya makaburi, na majini, na mashaytwaan, na kwa ajili ya ardhi, na wachawi?

 

Akaonyesha kwamba shirki kubwa kabisa inamtoa mtu nje ya Dini japokuwa ikiwa ni kitu chepesi. Hivyo basi, suala la Tahwiyd na  ‘Aqiydah hayasamehe hayo.” [Sharh Kitaab At-Tawhiyd – Baab maa jaa-a fiy adhdhab-h li-ghayri-LLaah]  
 

     

 

 



50-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Amepewa Na Amejaaliwa Mambo Kadhaa Ambayo Manabii Wengineo Hawakupewa

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

50-Amepewa Na Amejaaliwa Mambo Kadhaa Ambayo Manabii Wengineo Hawakupewa

Alhidaaya.com

 

 

 

Miongoni mwa mambo ambayo Amejaaliwa na kupewa Nabiy Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم)  pasi na Manabii wengineo ni:

 

 

1-Kujaaliwa Swafu zake (katika Swalaah za Jamaa) kuwa ni kama Swafu za Malaika.

 

 

2-Amehalalishiwa ghanima (ngawira na mateka ya vita).

 

 

3-Amejaaliwa ardhi kuwa ni twahara. Kwa maana yanapokosekana maji ya kutawadhia Waislamu hufanya Tayammum.

 

 

4-Amejaaliwa ardhi kuwa ni Masjid (Msikiti) kwa maana mtu anaweza kuswali popote katika ardhi madamu ni mahali pasafi; anaweza kuswali njiani, darasani, uwanjani na kadhaalika.

 

 

5-Amepewa Jawaami’ul-Kalim’ (mkusanyiko wa maneno machahe lakini yenye maana pana).

 

 

 

6-Ataruhusiwa Ash-Shafaa’’ah (Uombezi) Siku ya Qiyaamah kuwashufai watu na kuwaingiza Jannah.

 

 

7-Ataruhusiwa kuwaingiza Jannah watu elfu sabiini bila ya kuhesabiwa na bila kuadhibiwa; bonyeza kiungo kifuatacho:

 

24-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ameruhusiwa Kuingiza Jannah Watu Sabiini Elfu Katika Ummah Wake

 

 

8-Amenusuriwa kwa kutiwa khofu na kizaazaa katika nyoyo za makafiri; kwa maana Allaah (سبحانه وتعالى) Ametia kiwewe na khofu kubwa katika nyoyo za makafiri hadi waogope kupigana vita au wanyon’gonyee na kushindwa kupigana na Waumini.

 

 

9-Ametumwa kwa Ulimwengu wote, kwani Manabii wengineo walitumwa kwa kaumu zao tu.

 

 

Hadiyth zifuatazo zimethibitisha hayo:

 

 

Kunusuriwa Kwa Kiwewe, Kuhalalishiwa Ghanima, Kupewa Ash-Shafaa’ah, Kutumwa Wa Walimwengu Wote:

 

عن جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أُعْطِيتُ خَمْسًا لَمْ يُعْطَهُنَّ أَحَدٌ قَبْلِي،  نُصِرْتُ بِالرُّعْبِ مَسِيرَةَ شَهْرٍ، وَجُعِلَتْ لِيَ الأَرْضُ مَسْجِدًا وَطَهُورًا، فَأَيُّمَا رَجُلٍ مِنْ أُمَّتِي أَدْرَكَتْهُ الصَّلاَةُ فَلْيُصَلِّ، وَأُحِلَّتْ لِيَ الْمَغَانِمُ وَلَمْ تَحِلَّ لأَحَدٍ قَبْلِي، وَأُعْطِيتُ الشَّفَاعَةَ، وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً، وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ عَامَّةً))

Jaabir bin Abdillaah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nimepewa mambo matano hakupewa yoyote kabla yangu; Nimenusuriwa na (kutiwa) kiwewe (nyoyoni mwa maadui) kwa mwendo wa mwezi. Na nimefanyiwa ardhi kuwa sehemu ya kufanyia ‘ibaadah na kujitwaharishia, basi mtu mtu yeyote katika ummah wangu akifikiwa na Swalaah, aswali. Na nimehalalishiwa ngawira hazikuwa halali kwa yeyote kabla yangu. Na nimepewa shafaa’ah (maombezi Siku ya Qiyaamah). Na alikuwa Nabiy akitumwa kwa watu wake pekee, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.” [Al-Bukhaariy (5011)]  

 

Kupewa Jawaami’ul-Kalimi, Kunusuriwa Kwa Kiwewe, Kuhalalishiwa Ghanima, Kufanyiwa Ardhi Kuwa Ni Twahara Na Masjid, Kutumwa Kwa Walimwengu Wote, Kufanywa Nabiy Wa Mwisho:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَالَ:  ((فُضِّلْتُ عَلَى الأَنْبِيَاءِ بِسِتٍّ:  أُعْطِيتُ جَوَامِعَ الْكَلِمِ، وَنُصِرْتُ بِالرُّعْبِ، وَأُحِلَّتْ لِيَ الْغَنَائِمُ، وَجُعِلَتْ لِيَ الأَرْضُ طَهُورًا وَمَسْجِدًا، وَأُرْسِلْتُ إِلَى الْخَلْقِ كَافَّةً، وَخُتِمَ بِيَ النَّبِيُّونَ))

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraryah (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Nimefadhilishwa juu ya Manabii kwa mambo sita; nimepewa ‘Jawaami’al-Kalimi’  na nimenusuriwa kwa kutiwa kiwewe na khofu (katika nyoyo za maadui) na nimehalalishiwa ghanima  na nimefanyiwa ardhi kuwa kitoharishi na Masjid (mahali pa kuswali), na nimetumwa kwa viumbe wote, na Manabii wamekhitimishwa kwangu))[Muslim]

 

 

Kujaaliwa Swafu Kama Swafu Za Malaikah, Ardhi Kuwa ni Msikiti, Ardhi Kuwa Twahara: 

 

عَنْ حُذَيْفَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ فُضِّلْنَا عَلَى النَّاسِ بِثَلاَثٍ جُعِلَتْ صُفُوفُنَا كَصُفُوفِ الْمَلاَئِكَةِ وَجُعِلَتْ لَنَا الأَرْضُ كُلُّهَا مَسْجِدًا وَجُعِلَتْ تُرْبَتُهَا لَنَا طَهُورًا إِذَا لَمْ نَجِدِ الْمَاءَ ‏"‏ ‏.‏ وَذَكَرَ خَصْلَةً أُخْرَى ‏.‏

 

Imepokelewa kutoka kwa Hudhayfah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Tumefadhilishwa kuliko watu wengine katika mambo matatu: Safu zetu zimefanywa katika safu za Malaika, ardhi yote imefanywa kwetu kuwa Msikiti na mchanga wake umefanywa twahara kwetu ikiwa hakuna maji.” Na akataja fadhila nyengine. [Muslim].

 

Swafu kama za Malaika zimetajwa katika Hadiyth:

 

عَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ، قَالَ خَرَجَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ ‏"‏ مَا لِي أَرَاكُمْ رَافِعِي أَيْدِيكُمْ كَأَنَّهَا أَذْنَابُ خَيْلٍ شُمْسٍ اسْكُنُوا فِي الصَّلاَةِ ‏"‏ ‏.‏ قَالَ ثُمَّ خَرَجَ عَلَيْنَا فَرَآنَا حَلَقًا فَقَالَ ‏"‏ مَا لِي أَرَاكُمْ عِزِينَ ‏"‏ ‏.‏ قَالَ ثُمَّ خَرَجَ عَلَيْنَا فَقَالَ ‏"‏ أَلاَ تَصُفُّونَ كَمَا تَصُفُّ الْمَلاَئِكَةُ عِنْدَ رَبِّهَا ‏"‏ ‏.‏ فَقُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ وَكَيْفَ تَصُفُّ الْمَلاَئِكَةُ عِنْدَ رَبِّهَا قَالَ ‏"‏ يُتِمُّونَ الصُّفُوفَ الأُوَلَ وَيَتَرَاصُّونَ فِي الصَّفِّ ‏"‏ ‏.‏

Imepokelewa toka kwa Jaabir bin Samrah akisema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitutokea akasema: ((Mbona nawaona mnanyanyua mikono yenu kana kwamba ni mikia ya farasi waliochacharika? Tulieni katika Swalaah)). Akasema: Kisha akatutokea akatuona tumejigawa mafungu mafungu akatuambia: ((Kwa nini msipange safu kama wanavyopanga safu Malaika mbele ya Rabb wao?)) Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Ni vipi Malaika wanapanga safu mbele ya Rabb wao? Akasema: ((Wanaikamilisha safu ya kwanza na wanazinyoosha safu zao)). [Muslim, Abuu Daawuwd (661), An-Nasaaiy (2/92), Ibn Maajah (992)].

 

 

 

 



06-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Ilifika Siku Hapakuwa Na Chakula Nyumbani Mwake Isipokuwa Tende Moja Tu!

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

06-Zuhd Yake:

Ilifika Siku Hapakuwa Na Chakula Nyumbani Mwake Isipokuwa Tende Moja Tu!

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Wake zake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) nao walijifunza Zuhd na wakakhiari hata kujikhini wenyewe kwa kidogo mno walichonacho na badala yake wakawapatia Maskini waliokuja kuomba kwao.  Basi pindi mwanamke maskini mmoja alipofika nyumba ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuomba Swadaqah au chakula, alimkuta Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) ambaye hakusita kuigawa tende moja iliyokuwa ndio chakula pekee kilichopatika nyumbani mwake:

 

 

 عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها قَالَتْ: دَخَلَتِ امْرَأَةٌ مَعَهَا ابْنَتَانِ لَهَا تَسْأَلُ، فَلَمْ تَجِدْ عِنْدِي شَيْئًا غَيْرَ تَمْرَةٍ فَأَعْطَيْتُهَا إِيَّاهَا، فَقَسَمَتْهَا بَيْنَ ابْنَتَيْهَا وَلَمْ تَأْكُلْ مِنْهَا، ثُمَّ قَامَتْ فَخَرَجَتْ، فَدَخَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَيْنَا، فَأَخْبَرْتُهُ فَقَالَ:  "‏مَنِ ابْتُلِيَ مِنْ هَذِهِ الْبَنَاتِ بِشَىْءٍ كُنَّ لَهُ سِتْرًا مِنَ النَّارِ"  البخاري و مسلم

Kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) ambaye amesema: “Mama mmoja pamoja na binti zake wawili walikuja kwangu wakiomba (Swadaqah), lakini hakukuta chochote nilichonacho isipokuwa tende moja. Nikampa naye akaigawanya kwa binti zake, naye mwenyewe hakula chochote, kisha akasimama na akaenda zake.  Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaja nami nikampa taarifa hii. Akasema: “Yeyote anayekabiliwa na mtihani kwa binti zake, naye akawakirimu kwa wema, basi mabinti hao watakuwa ni kinga dhidi ya Moto wa Jahannam.” [Al-Bukhariy, Muslim na wengineo]

 

Kujikhini kwa aina hii ni ‘amali njema kabisa Aipendayo Allaah (سبحانه وتعالى) Ambaye Aliteremsha Aayah kwa sababu ya kisa kilichotokea katika nyumba ya Abuu Twalhah Al-Answaariy na mkewe Ummu Sulaym ambao walijikhini kula chakula ilhali wao walikuwa na njaa, lakini badala yake wakawaachia wageni wao wale. Kisa chao hicho kilimfurahisha mno Allaah (سبحانه وتعالى) hadi kwamba Akateremsha Aayah:    

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، ‏.‏ أَنَّ رَجُلاً، مِنَ الأَنْصَارِ بَاتَ بِهِ ضَيْفٌ فَلَمْ يَكُنْ عِنْدَهُ إِلاَّ قُوتُهُ وَقُوتُ صِبْيَانِهِ فَقَالَ لاِمْرَأَتِهِ نَوِّمِي الصِّبْيَةَ وَأَطْفِئِي السِّرَاجَ وَقَرِّبِي لِلضَّيْفِ مَا عِنْدَكِ - قَالَ - فَنَزَلَتْ هَذِهِ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba mtu alilala usiku kama mgeni kwa mtu mmoja katika Answaariy ambaye hakuwa na chakula isipokuwa chakula cha watoto wake akamwambia mkewe: “Laza watoto na zima taa karibisha wageni kwa (chakula) ulichonacho.” Ikateremka kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٩﴾

 Na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wanahitaji. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. [Al-Hashr: 9]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنفِقُوا خَيْرًا لِّأَنفُسِكُمْ ۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿١٦﴾

Basi mcheni Allaah muwezavyo, na sikilizeni; na tiini na toeni (kwa ajili ya Allaah) ni kheri kwa ajili ya nafsi zenu. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. [At-Taghaabun: 16]

 

 

Naye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akatufunza kuwa Iymaan haipatikani isipokuwa mtu ampendelee nduguye kile anachokipendelea nafsi yake:

 

 

عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم) قَالَ: ((لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يُحِبَّ لإِخِيهِ مَا يُحِبُّ لِنَفْسِهِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hatoamini mmoja wenu mpaka ampendelee nduguye anayojipendelea nafsi yake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na huko ndio kufikia wema wa uhakika kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٩٢﴾

Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachotoa basi hakika Allaah kwacho ni Mjuzi. [Aal-’Imraan 92]

 



200-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Ribaatw Fiy SabiliLLaah

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Fadhila Za Ribaatw  Fiy SabiliLLaah

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٢٠٠﴾

200. Enyi walioamini! Subirini na zidini kuvuta subira na bakieni imara na mcheni Allaah ili mpate kufaulu.

 

Mafunzo:

 

Baadhi Ya Maana Ya Ribaatw: 

 

Kwanza:  Kubakia kuchunga mipaka katika Jihaad fiy SabiliLLaah

Pili:          Kubakia katika ‘Ibaadah baina ya Swalaah Na Swalaah ya pili.

 

Fadhila za Ribaatw: Sahl bin Sa’ad (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ar-Ribaatw (Kubakia kuchunga mipaka) kwa ajili ya Allaah siku moja ni bora kuliko dunia na vilivyomo. Na sehemu (ndogo kabisa) ukubwa wa  kuweka fimbo ya mmoja wenu Jannah ni bora kuliko dunia na vilivyomo. Na juhudi ya kutoka jioni anakotoka mja katika njia ya Allaah au asubuhi ni bora kuliko dunia na vilivyomo.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Pia: “Ribaatw ya siku moja na usiku wake ni bora kuliko kufunga mwezi mzima na qiyaam chake (kisimamo cha kuswali usiku), na mtu akifa (akiwa katika ribaatw), ‘amali zake zitaendelea kuandikwa na riziki yake ataendela kupata na atasalimika na fitnah (za kaburi).”  [Muslim].

 

 

 



075-Asbaab Nuzuwl: An-Nahl - Allaah Amepiga Mfano Wa Mja Aliyemilikiwa Hana Uwezo...

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

016-Suwrah An-Nahl Aayah 75 - 76

 

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَمَن رَّزَقْنَاهُ مِنَّا رِزْقًا حَسَنًا فَهُوَ يُنفِقُ مِنْهُ سِرًّا وَجَهْرًا ۖ هَلْ يَسْتَوُونَ ۚ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٧٥﴾

Allaah Amepiga mfano wa mja anayemilikiwa hana uwezo juu ya chochote na (mwengine) ambaye Tumemruzuku kutoka Kwetu riziki nzuri; naye anatoa katika humo kwa siri na dhahiri. Je, wanalingana sawa? AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah!). Bali wengi wao hawajui.

 

 

وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَاهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ ۖ هَلْ يَسْتَوِي هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ ۙ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٧٦﴾

Na Allaah amepiga mfano (mwingine) wa watu wawili; mmoja ni bubu asiye na uwezo juu ya chochote naye ni mzigo kwa bwana wake, popote unapomuelekeza haleti khayr. Je, analingana sawa yeye na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko juu ya njia iliyonyooka? [An-Nahl: 75-76]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

عن ابن عباس في قوله عز وجل ((ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلاً عَبْداً مَمْلُوكاً ..))  قال: نزلت في رجل من قريش وعبده، وفي قوله ((مَثَلًا رَجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لا يَقْدِرُ عَلَى شَيْءٍ)) إلى قوله ((وَهُوَ عَلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ)). قال هو عثمان بن عفان، قال: والأبكم الذي أينما يوجهه لا يأتي بخير، ذاك مولى عثمان بن عفان كان عثمان ينفق عليه ويكفله ويكفيه المؤونة، وكان الآخر يكره الإسلام ويأباه، وينهاه عن الصدقة والمعروف فنزلت فيهما.

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kuhusu Kauli ya Allaah:

ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا  

Allaah Amepiga mfano wa mja anayemilikiwa…

 

Amesema imeteremka kuhusu mtu katika Quraysh na mtumwa wake. 

 

Na kuhusu Kauli Yake:

مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ

Mfano (mwingine) wa watu wawili; mmoja ni bubu asiye na uwezo juu ya chochote…

 

mpaka kauli Yake:

وَهُوَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ

naye yuko juu ya njia iliyonyooka.

 

Amesema: “(Aaliyekusudiwa) huyo ni ‘Uthmaan bin ‘Affaan.”

 

Akasema pia: “Na bubu ambaye popote unapomuelekeza haleti khayr, huyo ni mtumwa wa ‘Uthmaan, alikuwa ‘Uthmaan akimhudumia matumizi yake na kumdhamini, na kumtosheleza chakula chake. Na yule (mtumwa) mwengine (wa Aayah iliyotangulia) alichukia Uislamu na akaukanusha na akimzuia (bwana wake) asitoe Swadaqah na kutokufanya wema, zikateremka (Hizo Aayah) kuhusu wao wawili:

 

[Imaam Al-Muqbil amerekodi Ibn Jariyr (4/151) na watu wake ni watu Swahiyh]

 

Na pia,

 

عن إبراهيم، عن عكرمة، عن ابن عباس قال: نزلت هذه الآية ((ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلاً عَبْداً مَمْلُوكاً لا يَقْدِرُ عَلَى شَيْءٍ )) في هِشَامِ بْنِ عَمْرٍو، وَهُوَ الَّذِي يُنْفِقُ مَالَهُ سِرًّا وَجَهْرًا، وَمَوْلَاهُ أَبُو الْجَوْزَاءِ الَّذِي كَانَ يَنْهَاهُ وَنَزَلَتْ (( وَضَرَبَ اللَّهُ مَثَلاً رَجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لا يَقْدِرُ عَلَى شَيْءٍ )) فَالْأَبْكَمُ مِنْهُمَا الْكَلُّ عَلَى مَوْلَاهُ هُوَ أُسَيْدُ بْنُ أَبِي الْعِيصِ، وَالَّذِي يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَهُوَ عَلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ هُوَ عُثْمَانُ بْنُ عَفَّانَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ

Kutoka kwa Ibraahiym kutoka kwa Ikrimah kutoka kwa Ibn ‘Abbaas amesema: Zimeteremka Aayah hizi mbili:

ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ

Allaah Amepiga mfano wa mja anayemilikiwa hana uwezo juu ya chochote…

 

Kumhusu Hishaam ambaye alikuwa akitoa mali yake kwa siri na kwa dhahiri na  mtumwa wake Abu Al-Jawzaaiy alimzuia asifanye hivyo, basi ikateremka:

 

وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَاهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ ۖ هَلْ يَسْتَوِي هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ ۙ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٧٦﴾

Na Allaah amepiga mfano (mwingine) wa watu wawili; mmoja ni bubu asiye na uwezo juu ya chochote naye ni mzigo kwa bwana wake, popote unapomuelekeza haleti khayr. Je, analingana sawa yeye na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko juu ya njia iliyonyooka? [An-Nahl: 75-76]

 

Na aliyekuwa bubu ni mmojawapo kati ya wawili, na aliye mzigo kwa bwana wake ni Asyad bin Abiy Al-‘Iysw. Na yule ambaye anaamrisha uadilifu naye yuko juu ya njia ya kunyooka ni ‘Uthmaan bin ‘Affaan (رضي الله عنه).

[Abul-Hasan ‘Aliy Ibn Ahmad Al-Waahidi An-Naysaaburiy]

 



050-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Kafiri Analipwa Duniani Aakhirah Hatopata Kitu, Na Muumin Analipwa Duniani Na Aakhirah

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 50

Kafiri Analipwa Duniani Aakhirah Hatopata Kitu,

Na Muumin Analipwa Duniani Na Aakhirah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ أَنَسِ (رضي الله عنه) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال: ((إِنَّ الْكَافِرَ إِذَا عَمِلَ حَسَنَةً أُطْعِمَ بِهَا طُعْمَةً مِنْ الدُّنْيَا، وَأَمَّا الْمُؤْمِنُ فَإِنَّ اللَّهَ يَدَّخِرُ لَهُ حَسَنَاتِهِ فِي الأَخِرَةِ وَيُعْقِبُهُ رِزْقًا فِي الدُّنْيَا عَلَى طَاعَتِهِ)) 

وفي رواية: ((إِنَّ اللَّهَ لاَ يَظْلِمُ مُؤْمِنًا حَسَنَةً يُعْطَى بِهَا فِي الدُّنْيَا وَيُجْزَى بِهَا فِي الأَخِرَةِ.  وَأَمَّا الْكَافِرُ فَيُطْعَمُ بِحَسَنَاتِ مَا عَمِلَ بِهَا لِلَّهِ فِي الدُّنْيَا حَتَّى إِذَا أَفْضَى إِلَى الأَخِرَةِ لَمْ يَكُنْ لَهُ حَسَنَةٌ يُجْزَى بِهَا)) مسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika kafiri anapotenda ‘amali nzuri hulipwa mwonjo duniani. Ama Muumin, Allaah Humwekea mema yake Aakhirah na Anamlipa rizki duniani kwa utiifu wake)).

 

Na katika riwaayah: ((Hakika Allaah Hamdhulumu Muumin kwa mema yake, hupewa duniani [kheri zaidi] na hulipwa Aakhirah. Ama kafiri, huonjeshwa duniani kwa mema yake aliyoyatenda kwa ajili ya Allaah mpaka akifika Aakhirah hatakuwa na jema la kulipwa)). [Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Tofauti kubwa baina ya malipo ya kafiri na Muumin, na Waumini daima ndio watakaofaulu kwa kulipwa mema zaidi.

 

 

2. Vipimo vya Allaah (سبحانه وتعالى) katika kulipa ‘amali kutokana na niyyah na ‘Aqiydah ya mtu.

 

 

3. Kafiri hulipwa mema yake duniani; ima kwa ziada ya mali yake au kukingwa na shari, lakini Aakhirah hana sehemu yoyote. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 مَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ ۖ وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ﴿٢٠﴾

Yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya Aakhirah Tunamzidishia katika mavuno yake; na yeyote yule aliyekuwa anataka mavuno ya dunia, Tutampa humo, lakini Aakhirah hatokuwa na fungu lolote. [Ash-Shuwraa (42: 20)]

 

 [Rejea pia:  Al-Muuminuwn (23: 55-56)].

 

 

 4. Kafiri hata akitenda ‘amali nzuri zenye uzito mno, juhudi zake ni za bure hazina thamani mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى). Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا ﴿١٠٣﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Je, Tukujulisheni wenye kukhasirika mno kwa ‘amali?”

 

الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا ﴿١٠٤﴾

Ni wale ambao wamepoteza juhudi zao katika uhai wa dunia, na huku wao wakidhani kwamba wanapata mazuri kwa matendo yao.

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَلِقَائِهِ فَحَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَزْنًا ﴿١٠٥﴾

Hao ni wale waliozikanusha Aayaat za Rabb wao na kukutana Naye basi zimeporomoka ‘amali zao; hivyo Hatutowasimamishia Siku ya Qiyaamah uzito wowote. 

 

ذَٰلِكَ جَزَاؤُهُمْ جَهَنَّمُ بِمَا كَفَرُوا وَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَرُسُلِي هُزُوًا ﴿١٠٦﴾

Hivyo ndio jazaa yao Jahannam kwa yale waliyoyakufuru na kuchukulia mzaha Aayaat Zangu na Rusuli Wangu. [Al-Kahf (18: 103-106)]

 

[Rejea pia: Al-Israa (17: 18)].

 

 

5. Muumin juhudi zake zinathaminiwa na anapata faida ya kulipwa duniani na Aakhirah malipo mema zaidi. [Rejea: Al-Israa (17: 19-20)].

 

 

6. Allaah (سبحانه وتعالى) Hamdhulumu mja ‘amali yake hata ndogo vipi. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٤٠﴾

Hakika Allaah Hadhulumu hata uzito au chembe (au sisimizi). Na ikiwa ni ‘amali njema Huizidisha na Hutoa kutoka Kwake ujira adhimu.  [An-Nisaa (4: 40)]

 

[Rejea pia: Fusw-swilat (41: 46), Al-Zalzalah (99: 7), Yuwnus (10: 61), Al-Anbiyaa (21: 47)].

 

 

7. Allaah (سبحانه وتعالى) Anamlipa Muumin mara kumi zaidi kwa kitendo kimoja.

 

مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦٠﴾

Atakayekuja kwa ‘amali njema basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo. Na Atakayekuja kwa ovu basi hatolipwa ila mfano wake, nao hawatodhulumiwa. [Al-An’aam (: 160)]

 

 

 



Jumamosi, 29 Agosti 2020

Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30

Mungu anaposema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hamaanishi maarifa ya kutengeneza au kuendesha ndege, ni maarifa ya kawaida tu katika maisha yetu ya kila siku ambayo yanaweza kubadilisha afya na ustawi wetu.

Moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa na viinilishe vingi na mhimu sana kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili ni kitunguu swaumu.

Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum.

Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita.

Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.

Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, virusi, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen’genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.

Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika nchini China mwaka 510 kabla ya Kristo na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Warumi.

Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.

Kuna baadhi ya imani watu wanaamini kitunguu swaumu kina uwezo wa kufukuza hadi wachawi!

Hivyo kama unatokewa unapata usingizi wa usioeleweka au unakabwa kabwa na wachawi hebu jaribu kitunguu swaumu na uniletee mrejesho

Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia.

Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash).

Huko sokoni tayari nimeviona vitunguu swaumu kutoka China na Afrika kusini ambavyo vyenyewe huwa vina punje kubwa nene na huwa rahisi kuvimenya.

Hata hivyo ili upate faida hizi zote hapa chini naendelea kukushauri utumie vitunguu swaumu vyetu vinavyolimwa hapa Tanzania kwani hivyo vya kutoka nje pamoja na kuwa ni rahisi kuvimenya lakini ubora wake si kama ule wa vitunguu vyetu.

Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuipuwa mboga yako toka katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake.

Kama una friza au friji ya kawaida unaweza kumenya vitunguu swaumu hata kilo nzima na kuvitwanga kidogo katika kinu, vifunge vizuri katika bakuli au mfuko wa plastiki na uvihifadhi katika friza au friji na hivyo kila unapopika unachukuwa tu na kukitumia ili kuepuka usumbufu wa kukimenya kila siku.

Unaweza kutumia kitunguu swaumu kwenye chakula chako kila siku, kuna kitunguu swaumu pia katika unga pia katika mfumo wa vidonge

Kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu

Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji au ukichanganye na mtindi kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.

1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja,
2. Kigawanyishe katika punje punje,
3. Chukua punje 6 menya punje moja baada ya nyingine.
4. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu,
5. Meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala au kila baada ya siku 1.

Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe.

Na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

Unaweza kutumia mtindi uliotengeneza mwenyewe nyumbani au hata wa dukani. Binafsi mara nyingi natumia mtindi wa Tanga freshi.

Dozi ni siku ngapi? Unaweza kutumia mpaka utakapochoka mwenyewe. Ni chakula tu kama vilivyo viazi. Unaweza kutumia hata kama huumwi chochote.

Watoto wadogo miaka miwili kwenda juu mpaka miaka 10 unaweza kuwapa punje 2 kwa siku.

Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo wa kuimarisha na kuongeza kinga ya mwili ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti.

Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30

1. Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.

2. Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.

3. Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, fangasi na virusi.

4. Huondoa sumu mwilini jambo ambalo ni mhimu sana ili uwe na kinga nzuri ya mwili

5. Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi. Huwezi kuwa na kinga nzuri ya mwili kama hupati usingizi wa kutosha kila siku.

6. Kinaondoa msongo wa mawazo (stress) na kukufanya uishi miaka mingi. Ni vigumu au ni sawa na haiwezekani uwe na msongo wa mawazo (stress) halafu uwe na kinga nzuri ya mwili.

7. Hutibu kifua kikuu (TB). Ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu.

8. Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine

9. Huzuia kuhara damu (Dysentery)

10. Huondoa Gesi tumboni

11. Hutibu msokoto wa tumbo

12. Hutibu Typhoid

13. Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi

14. Hutibu mafua na malaria

15. Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I

16. Hutibu kipindupindu

17. Hutibu upele

Kwa kutumia kitunguu swaumu tu unaweza kujitibu tatizo la ukurutu na hata upele.

Kitunguu swaumu kina nguvu dhdi ya bakteria na wadudu wengine wanaosababisha maambukizi kwenye ngozi.

Kitunguu swaumu kinaweza kufanya kazi hii kwa namna mbili. Kama utakunywa kitunguu swaumu kinaweza kusaidia kupunguza ukali wa maambukizi na hata kuyazuia kutojirudia. Njia ya pili kitunguu swaumu kinaweza kutengenezwa mafuta na kupakwa juu ya ngozi moja kwa moja.

Kitunguu swaumu kinadhibiti virusi, fangasi, bakteria na vijidudu vingine nyemelezi. Kazi hizi zote zinawezeshwa na kitu mhimu kilichopo kwenye kitunguu swaumu kijulikanacho kama ‘Alicin’.

Ukurutu, chunusi, miwasho, mba, upele na matatizo mengi ya ngozi yanaweza kutibiwa kwa kutunguu swaumu tu

18. Huvunjavunja mawe katika figo

19. Hutibu mba kichwani

20. Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.

21. Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu ya jino

22. Hutibu maumivu ya kichwa

23. Hutibu kizunguzungu

24. Hutibu shinikizo la juu la damu

25. Huzuia saratani mbalimbali

26. Hutibu maumivu ya jongo (gout)

27. Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

28. Huongeza hamu ya kula

29. Huzuia damu kuganda

30. Husaidia kutibu kisukari

31. Husafisha tumbo

32. Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)

Tafiti kadhaa zimeonyesha kitunguu swaumu kuwa na ufanisi mkubwa sana katika kutibu magonjwa kama shinikizo la juu la damu, kolesteroli na magonjwa ya mishipa ya moyo.

Kitunguu swaumu huzuia kujikaza au kuzibika kwa mishipa ya damu.

Kitunguu swaumu pia huongeza msukumo wa damu.

Kama umeambiwa moyo wako umekuwa mkubwa sana au una tatizo lolote kwenye moyo kitunguu swaumu kinaweza kuwa msaada mkubwa kwako

Mhimu : Kitunguu swaumu kinaweza kisipatane na aina nyingi ya dawa za hospitalini sababu ya baadhi ya dawa hizo hukaza mishipa ya damu. Wasiliana na daktari wako kabla ya kuanza kutumia hii dawa

33. Kitunguu swaumu hutibu majipu

Unaweza kutumia kitunguu swaumu pekee au ukikichanganya na kitunguu maji ili kutibu majipu.

Wakati unataka kutibu jipu sehemu yoyote katika mwili wako unaweza kunywa kitunguu swaumu au hata kupakaa mafuta yake juu ya ngozi yenye jipu moja kwa moja.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kitunguu swaumu kina uwezo wa kudhibiti bakteria, uvimbe, na vijidudu mbalimbali nyemelezi katika mwili.

Ule uwezo wake wa kudhibiti uvimbe (anti-inflammatory properties) unakifanya kitunguu swaumu kuwa dawa bora mbadala ya kutibu jipu.

34. Kitunguu swaumu kinatibu korodani zinazovimba

Kuna wanaume wanapatwa na korodani zao kuongezeka ukubwa au zinavimba.

Inaweza kutokea korodani zote 2 zikavimba au korodani moja kati ya mbili ikaongezeka ukubwa na nyingine ikabaki ndogo vile vile.

Tatizo hili (enlarged prostate) linaweza kutibika kwa kutumia kitunguu swaumu tu.

35. Kitunguu swaumu kinatibu Pumu

Kitunguu swaumu kikichanganywa na maji ya moto au maziwa ya moto ni dawa nzuri sana ya kutibu pumu.

Kitunguu swaumu kinao uwezo wa kuondoa msongamano kwenye mapafu na hivyo kuwa msaada mkubwa kwa mtu mwenye pumu.

Kitunguu swaumu kinatibu pumu na kuziondoa kabisa dalili zake haraka.

Angalizo kuhusu kitunguu swaumu:

1. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema usitumie kitunguu swaumu kwa namna hii mpaka umeongea na kukubaliana na daktari wako wa karibu. Pia watoto chini ya miaka miwili wasitumie kitunguu swaumu kwa namna hii.

2. Vile vile kama una presha ya kushuka usitumie kitunguu swaumu kwa namna hii.

3. Harufu mbaya mdomoni baada ya kutumia kitunguu swaumu hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide).

Harufu hii mbaya hata hivyo yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu.

Na nimeshuhudia nikinywa kitunguu swaumu kwenye mtindi hii harufu ni kama haipo kabisa na hata ukijamba haikutokei ile harufu mbaya sana kama ukinywa vitunguu swaumu katika maji

4. Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)

5. Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha

6. Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.

7. Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.

8. Aidha vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa

9. Ukiona kichwa kinauma sana siku 3 au 5 baada ya kuanza kutumia kitunguu swaumu utatakiwa kuacha kukitumia kwa siku 2 au 3 mpaka kichwa kiache kukuuma ndipo uendelee tena na dozi. Na ndiyo sababu napenda utumie kila baada ya siku 1 na siyo kila siku ili kuepuka hili la kuumwa kichwa

Mhimu : Ukiwa na swali lolote kuhusu kitunguu swaumu naomba uulize hapa chini kwenye comment nitakujibu hapa hapa tena.

Soma hii pia 👇

Njia zingine mpya 8 za kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni

Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30 Click To Tweet

Share na wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 14

Let's block ads! (Why?)

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...