Translate
Ijumaa, 1 Novemba 2019
Hiswnul-Muslim: Fadhila Za Kumdhukuru Allaah
00-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! Utangulizi
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ
Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!
00-Utangulizi
بِسْمِ الله الرَّحْمنِ الرَّحِيم
الْحمْدُ لِلَّه وَالصَّلاةُ وَالسِّلامُ عَلى خَاتم الأنْبِيَاء وَالْمُرْسَلِين، الْمَبْعُوثُ رَحْمَةً لِلْعَالَمِين، مُحَمَّد وَعَلى آلِه وَأصْحابِه أجْمَعِين وَمَنْ تَبِعَهُمْ بِإِحْسَانٍ إِلَى يَوْمِ الدِّينِ.
Himdi Anastahiki Allaah, Swalaah na salaam zimfikie Nabiy na Rasuli wa mwisho, aliyetumwa awe rahmah kwa walimwengu, Muhammad, pamoja na ahli zake na Maswahaba zake wote, na wanaowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Malipo.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ﴿١٣﴾
hakika shirki ni dhulma kubwa mno [Luqmaan: 13]
Kinyume ya shirki ni Tawhiyd ambayo ni kumpwekesha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Rubuwbiyyah (Uola) Uluwhiyyah (‘ibaadah) Yake na katika Asmaa na Swifaat (Majina na Sifa nzuri) Zake. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٦٥﴾
Kwa yakini umefunuliwa Wahy na kwa wale walio kabla yako kwamba: “Ukifanya shirki bila shaka zitaporomoka ‘amali zako na bila shaka utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”
بَلِ اللَّـهَ فَاعْبُدْ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ﴿٦٦﴾
Bali Allaah Pekee mwabudu, na uwe miongoni mwa wenye kushukuru. [Az-Zumar: 65-66]
Waislamu wengi wako katika hali ya kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa); wengine wakiwa wanatambua hatari zake, na wengine wakiwa hawatambui kuwa wanamshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), kwa sababu baadhi ya ‘amali zinazotendwa zinaonekana kuwa kama ni nzuri na hali zimeingia shirki ndani yake.
Imaam Muhammad bin ‘Abdil-Al-Wahhaab amesema katika Al-Qawaaid Al-Arba’: “Kwamba washirikina wa zama zetu ni waovu zaidi (shirki zao ni kubwa zaidi) kuliko washirikina wa awali, kwa sababu, wa awali walimshirikisha Allaah katika raha, lakini wakizitakasa ‘Ibaadah zao wakati wa shida. Ama washirikina wa sasa, shirki zao ni wakati wote, wakiwa katika raha au katika shida … na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
فَإِذَا رَكِبُوا فِي الْفُلْكِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ إِذَا هُمْ يُشْرِكُونَ ﴿٦٥﴾
Wanapopanda merikebu humwomba Allaah wakiwa wenye kumtakasia Yeye Dini, lakini Anapowaokoa katika nchi kavu, tahamaki hao wanamshirikisha. [Al-‘Ankabuwt: 65]
Kwa hiyo, kuna umuhimu mkubwa wa Waislamu kujifunza somo hili ili kujitahadharisha na hatari zake ili waweze kufunga milango na njia zote kubwa na ndogo za shirki. Makala hizi In Shaa Allaah zitaweza kutambulisha na kubainisha matendo mengi yanayomshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na namna ya kuyaepuka, ili Muislamu abakie katika amri ya Muumba wake Ambaye Ameamrisha kuabudiwa Yeye Pekee bila ya kumshirikisha. Kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni katika dhambi kubwa mno kama alivyobainisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
عَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ سَأَلْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم: أَيُّ اَلذَّنْبِ أَعْظَمُ؟ قَالَ: ((أَنْ تَجْعَلَ لِلَّهِ نِدًّا, وَهُوَ خَلَقَكَ))
Imepokelewa kutoka kwa ibn Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: “Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): Je, dhambi ipi kubwa mno?” Akasema: ((Kumfanyia Allaah mlinganishi (wa kumshirikisha) na hali Yeye Amekuumba)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
Nukta chache zifuatazo ni mukhtasari wa hatari za kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
1. Shirki inaharibu ‘amali za mtu. Dhambi hii kubwa walitahadharishwa Rasuli wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa ukali mno pale Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaposema:
وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾
Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda. [Al-An’aam: 88]
2. Shirki ni dhambi pekee ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Haisamehe isipokuwa tu mtu akirudi kutubia Kwake. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا﴿١١٦﴾
Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali. [An-Nisaa: 116]
3. Shirki inamtoa mtu nje ya Uislamu!
Imeelezwa shirki kuwa ni miongoni mwa matendo yanayomtoa mtu nje ya Uislamu, kama ilivyo katika Nawaaqidhw Al-Islaam cha Imaam Muhammad ibn Al-Wahhaab (Rahimahu-Allaah).
Na miongoni mwa mengi wanayotenda baadhi ya Waislamu ni kumwendea kahini anayetabiri mambo ya ghayb; elimu ambayo hakuna aijuae isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Hatari ya tendo hili ni kama alivyotahadharisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنِ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ أَتَى كَاهِنًا، فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)) رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ
Imepokewa toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayemkaribia kahini na kuamini anayoyasema basi amekanusha aliyoteremshiwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)) [Abu Daawuwd]
4-Mwenye kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni mwenye hatima mbaya mno ya makazi ya Moto. Ametahadharisha hilo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾
Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.” [Al-Maaidah: 72]
Tunataraji tawfiyq ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) makala hizi ziwazidishie elimu yenye manufaa Waislamu kuhusiana na somo hili na Atuepushe sote kumshirikisha Yeye Subhaanahu wa Ta’aalaa.
38-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):Unyenyekevu Wake: Akichukuwa Ushauri Kwa Maswahaba Zake
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
38-Unyenyekevu Wake: Akichukuwa Ushauri Kwa Maswahaba Zake
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Hakujiona kuwa ni mtu bora kuliko Maswahaba juu ya kuwa yeye ni Rasuli wa Allaah, hivyo alikuwa haamui jambo peke yake bila ya kuchukua ushauri kwa Maswahaba zake. Ameitikia amri ya Rabb Wake pindi Alipomuamrisha afanye hivyo kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوكِّلِينَ ﴿١٥٩﴾
Basi wasamehe na waombee maghfirah na washauri katika mambo. Na unapoazimia basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anapenda wanaotawakali. [Aal-‘Imraan: 159]
Hivyo alipokea ushauri kadhaa kutoka kwa Swahaba zake kama ifuatavyo:
- Mwanzo kabisa alipopewa Unabiy akatumiwa Wahyi kutoka kwa Allaah (عز وجل) alimtaka ushauri Mama wa Waumini Khadiyjah (رضي الله عنها).
- Pia alitaka ushauri kwa Abuu Bakr na ‘Umar (رضي الله عنهما) pindi walipopata matekwa ya vita vya Badr.
- Hubaab bin Mundhir (رضي الله عنه) pia alimshauri katika vita vya Badr kuhusu kujaza visima vyote isipokuwa kimoja tu.
- Salmaan Al-Faarisy (رضي الله عنه) alimshauri kuhusu shimo la vita vya Khandaq (au vita vya Ahzaab).
- Pia alitaka ushauri katika vita vya Khandaq kuhusu mazao ya Madiynah.
- Pia alimtaka ushauri Mama wa Waumini Ummu Salamah (رضي الله عنها) walipokuwa Hudaybiyyah pindi makafiri wa Quraysh walipowazuia kuingia Makkah. Ummu Salamah (رضي الله عنها) Akamshauri Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wajivue Ihraam; wakachinja na wakanyoa nywele zao.
- Na alitaka ushauri kwa Maswahaba zake mara kadhaa nyenginezo na alikuwa mwenyewe akiwaomba wamshauri kama ilivyothibiti katika Hadiyth:
عَنِ الْمِسْوَرِ بْنِ مَخْرَمَةَ، وَمَرْوَانَ بْنِ الْحَكَمِ، يَزِيدُ أَحَدُهُمَا عَلَى صَاحِبِهِ قَالاَ خَرَجَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَامَ الْحُدَيْبِيَةِ فِي بِضْعَ عَشْرَةَ مِائَةً مِنْ أَصْحَابِهِ، فَلَمَّا أَتَى ذَا الْحُلَيْفَةِ قَلَّدَ الْهَدْىَ، وَأَشْعَرَهُ، وَأَحْرَمَ مِنْهَا بِعُمْرَةٍ، وَبَعَثَ عَيْنًا لَهُ مِنْ خُزَاعَةَ، وَسَارَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم حَتَّى كَانَ بِغَدِيرِ الأَشْطَاطِ، أَتَاهُ عَيْنُهُ قَالَ إِنَّ قُرَيْشًا جَمَعُوا لَكَ جُمُوعًا، وَقَدْ جَمَعُوا لَكَ الأَحَابِيشَ، وَهُمْ مُقَاتِلُوكَ وَصَادُّوكَ عَنِ الْبَيْتِ وَمَانِعُوكَ. فَقَالَ " أَشِيرُوا أَيُّهَا النَّاسُ عَلَىَّ، أَتَرَوْنَ أَنْ أَمِيلَ إِلَى عِيَالِهِمْ وَذَرَارِيِّ هَؤُلاَءِ الَّذِينَ يُرِيدُونَ أَنْ يَصُدُّونَا عَنِ الْبَيْتِ، فَإِنْ يَأْتُونَا كَانَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ قَدْ قَطَعَ عَيْنًا مِنَ الْمُشْرِكِينَ، وَإِلاَّ تَرَكْنَاهُمْ مَحْرُوبِينَ ". قَالَ أَبُو بَكْرٍ يَا رَسُولَ اللَّهِ، خَرَجْتَ عَامِدًا لِهَذَا الْبَيْتِ، لاَ تُرِيدُ قَتْلَ أَحَدٍ وَلاَ حَرْبَ أَحَدٍ، فَتَوَجَّهْ لَهُ، فَمَنْ صَدَّنَا عَنْهُ قَاتَلْنَاهُ. قَالَ " امْضُوا عَلَى اسْمِ اللَّهِ ".
Al-Miswaar bin Makhramah na Marwaan bin Hakam (رضي الله عنهما) Wamesema, (mmoja wao kasema zaidi kulikoni swahibu yake) Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka mwaka wa Al-Hudaybiyyah pamoja na Maswahaba wapatao elfu moja. Walipofika Dhul-Hulayfah akamtia kigwe[1] Hady wake (mnyama wa kuchinja kwa ajili ya Hajj), akaingia hapo Ihraam kwa ajili ya ‘Umrah kisha akamtuma mpelelezi kutoka kabila la Khuzaa’ah. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea mpaka akafika (kijiji cha) Ghaadiyr Al-Ashtwaatw. Akamjia mpelelezi wake akasema: “Hakika Maquraysh wamejumuika mjumuiko mkubwa dhidi yako na wamekusanya Wahabashia wawe dhidi yako na watapigana nawe na watakuzuia kuingia Al-Ka’bah.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Akasema: “Nishaurini enyi watu! Je, mnanishauri niangamize ahli zao na vizazi vyao hao watu wanaotaka kutuzia kuingia Al-Ka’bah? Kwani wakitujia kwa (amani) basi Allaah (عزّ وجلّ) Ataangamiza jasusi wa makafiri, laa sivyo tutawaacha katika hali mbaya wakiwa wamesulibiwa.” Abuu Bakr akasema? “Ee Rasuli wa Allaah, umetoka ukiwa na niyyah ya kuzuru Nyumba (Ka’bah) na hutaki kuua mtu wala kupigana vita na mtu. Basi endelea kuiendea (Ka’bah) na yeyote atakayetuzuia kuingia humo tutapigana nao.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Endeleeni kwa Jina la Allaah.” [Al-Bukhaariy]
- Pia aliwataka Maswahaba wamshauri kuhusu kuvunja Al-Ka’bah na kulijenga upya aliposema kuwaambia Maswahaba:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَشِيرُوا عَلَىَّ فِي الْكَعْبَةِ أَنْقُضُهَا ثُمَّ أَبْنِي بِنَاءَهَا أَوْ أُصْلِحُ مَا وَهَى مِنْهَا؟ قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: فَإِنِّي قَدْ فُرِقَ لِي رَأْىٌ فِيهَا أَرَى أَنْ تُصْلِحَ مَا وَهَى مِنْهَا وَتَدَعَ بَيْتًا أَسْلَمَ النَّاسُ عَلَيْهِ وَأَحْجَارًا أَسْلَمَ النَّاسُ عَلَيْهَا وَبُعِثَ عَلَيْهَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم
“Enyi watu! Nishaurini kuhusu Nyumba (Ka’bah). Je, niivunje kisha kuijenga upya kuanzia msingi wake au nitengeneze kilichoharibiwa?” Ibn ‘Abbaas akasema: “Imenijia rai kwamba nnavyoona sawa, ni utengeneze tu (sehemu) ziloharibika na uiache Nyumba (Ka’bah) katika hali yake ile ile pindi watu walipoingia Uislamu (na uache) mawe (katika hali yake ile ile) pindi watu walipoingia Uislamu na katika hali ile ile ulipotumwa (na Allaah) kuja kama Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). [Hadiyth ya ‘Atwaa ameirekodi Imaam Muslim]
[1] Kama kidani cha chuma kwa ajili ya alama kujulikana kuwa ni mnyama wa Hady yaani kuchinjwa katika Hajj.
123-Aayah Na Mafunzo: Kutofautiana ‘Ulamaa Kuhusu Maana Ya Badr
Aayah Na Mafunzo
Aal-‘Imraan
Kutofautiana ‘Ulamaa Kuhusu Maana Ya Badr
Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):
وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ بِبَدْرٍ وَأَنتُمْ أَذِلَّةٌ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٢٣﴾
123. Kwa yakini Alikunusuruni Allaah katika Badr na hali nyinyi mlikuwa (kikosi) dhaifu. Basi mcheni Allaah mpate kushukuru.
Mafunzo:
Kuhusu Badr: Wametofautiana ‘Ulamaa katika maana ya jina hili ‘Badr’ baadhi yao wamesema ni jina la mtu, na baadhi wamesema ni jina la kisima, na imeitwa kwa jina hilo sehemu hiyo baina ya Makkah na Madiynah na sehemu hiyo iko mbali na Madiynah kwa kilometa 150. Na Allaah ni Mjuzi zaidi.
009-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tawbah: Aayah 34 - 35
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
At-Tawbah: Aayah 34 - 35
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۗ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٤﴾
Enyi walioamini! Hakika wengi katika Wanachuoni Marabai wa dini (zao) na Wamonaki wanakula mali za watu kwa batili, na wanazuia njia ya Allaah. Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo.
يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ ۖ هَـٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ﴿٣٥﴾
Siku zitakapopashwa katika Jahannam, na kwazo vikachomwa moto vipaji vyao, na mbavu zao, na migongo yao (wakiambiwa): Haya ndiyo mliyoyarundika kwa ajili ya nafsi zenu. Basi onjeni yale mliyokuwa mkiyarundika. [At-Tawbah: 34-35]
حَدَّثَنَا عَلِيٌّ، سَمِعَ هُشَيْمًا، أَخْبَرَنَا حُصَيْنٌ، عَنْ زَيْدِ بْنِ وَهْبٍ، قَالَ مَرَرْتُ بِالرَّبَذَةِ فَإِذَا أَنَا بِأَبِي، ذَرٍّ رضى الله عنه فَقُلْتُ لَهُ، مَا أَنْزَلَكَ مَنْزِلَكَ هَذَا، قَالَ: كُنْتُ بِالشَّأْمِ، فَاخْتَلَفْتُ أَنَا وَمُعَاوِيَةُ فِي: ((الَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ)). قَالَ مُعَاوِيَةُ: نَزَلَتْ فِي أَهْلِ الْكِتَابِ، فَقُلْتُ: نَزَلَتْ فِينَا وَفِيهِمْ، فَكَانَ بَيْنِي وَبَيْنَهُ فِي ذَاكَ، وَكَتَبَ إِلَى عُثْمَانَ رضى الله عنه يَشْكُونِي، فَكَتَبَ إِلَىَّ عُثْمَانُ أَنِ اقْدَمِ الْمَدِينَةَ، فَقَدِمْتُهَا، فَكَثُرَ عَلَىَّ النَّاسُ حَتَّى كَأَنَّهُمْ لَمْ يَرَوْنِي قَبْلَ ذَلِكَ، فَذَكَرْتُ ذَاكَ لِعُثْمَانَ فَقَالَ لِي: إِنْ شِئْتَ تَنَحَّيْتَ، فَكُنْتَ قَرِيبًا فَذَاكَ الَّذِي أَنْزَلَنِي هَذَا الْمَنْزِلَ، وَلَوْ أَمَّرُوا عَلَىَّ حَبَشِيًّا لَسَمِعْتُ وَأَطَعْتُ.
Ametuhadithia ‘Aliy, amemsikia Hushaym, ametusimulia Huswayn toka kwa Zayd bin Wahb amesema: Nilipita Ar-Rabadhah na mara ghafla nikamwona Abuu Dharr (رضي الله عنه) Nikamuuliza: Nini kimekuleta kuja kuishi huku? Akasema: Nilikuwa Sham, nikazozana mimi na Mu’aawiyah kuhusiana
((وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ))
((Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah)). Mu’aawiyah akasema: Imeteremka kwa Ahlul-Kitaab tu. Nikasema: Imeteremka kwetu na kwao pia. Ukakasi ukawepo kati yangu na yeye katika hilo. Akamwandikia barua ‘Uthmaan (رضي الله عنه) akimlalamikia kuhusu mimi. Naye ‘Uthmaan akaniandikia na kuniamuru niende Madiynah. Nikaenda, na watu wakanizonga (kuniuliza sababu ya kuondoka Sham) kana kwamba hawajawahi kuniona kamwe. Nikamweleza ‘Uthmaan hilo naye akaniambia: Ukitaka achana (na rai yako) uwe karibu. Basi hili ndilo lililonifikisha kuishi hapa, na lau watampa madaraka Mhabeshi (mtumwa) awe kiongozi wangu, basi nitamsikiliza na kumtii. [Al-Bukhaariy]
Na pia,
قَالَ أَحْمَدُ بْنُ شَبِيبِ بْنِ سَعِيدٍ حَدَّثَنَا أَبِي، عَنْ يُونُسَ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ أَسْلَمَ، قَالَ خَرَجْنَا مَعَ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ ـ رضى الله عنهما ـ فَقَالَ أَعْرَابِيٌّ أَخْبِرْنِي قَوْلَ اللَّهِ: ((وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ)) قَالَ ابْنُ عُمَرَ ـ رضى الله عنهما ـ مَنْ كَنَزَهَا فَلَمْ يُؤَدِّ زَكَاتَهَا فَوَيْلٌ لَهُ، إِنَّمَا كَانَ هَذَا قَبْلَ أَنْ تُنْزَلَ الزَّكَاةُ فَلَمَّا أُنْزِلَتْ جَعَلَهَا اللَّهُ طُهْرًا لِلأَمْوَالِ.
Ahmad bin Shabiyb bin Sa’iyd amesema, baba yangu ametuhadithia toka kwa Yuwnus toka kwa Ibn Shihaab toka kwa Khaalid bin Aslam. Amesema: Tulitoka pamoja na ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما) na bedui mmoja akasema: Nielezee Kauli ya Allaah:
((وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ))
((Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah))
Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما) akasema: Mwenye kuzirundika na asitoe Zakaah yake, basi ole wake na adhabu kali. Na hili lilikuwa kabla ya kufaradhishwa Zakaah, na ilipofaradhishwa, Allaah Ameifanya kuwa utakaso kwa mali. [Al-Bukhaari]
Na pia,
حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ حُصَيْنٍ، عَنْ زَيْدِ بْنِ وَهْبٍ، قَالَ مَرَرْتُ عَلَى أَبِي ذَرٍّ بِالرَّبَذَةِ فَقُلْتُ: مَا أَنْزَلَكَ بِهَذِهِ الأَرْضِ؟ قَالَ: كُنَّا بِالشَّأْمِ فَقَرَأْتُ: ((وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ)) قَالَ مُعَاوِيَةُ مَا هَذِهِ فِينَا، مَا هَذِهِ إِلاَّ فِي أَهْلِ الْكِتَابِ. قَالَ قُلْتُ إِنَّهَا لَفِينَا وَفِيهِمْ.
Ametuhadithia Qutaybah bin Sa’iyd, ametuhadithia Jariyr toka kwa Huswayn toka kwa Zayd bin Wahab amesema: Nilimpitia Abuu Dharr huko Ar-Rabadhah nikamuuliza: Kitu gani kimekuleta ardhi hii? Akasema: Tulikuwa Sham, nikasoma:
وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٤﴾
Enyi walioamini! Hakika wengi katika Wanachuoni Marabai wa dini (zao) na Wamonaki wanakula mali za watu kwa batili, na wanazuia njia ya Allaah. Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo.
Na Mu’aawiyah akasema: Hili halituhusu sisi, hili haliwahusu wengine isipokuwa Ahlul-Kitaab. Akasema: Nikasema hakika hili bila shaka linatuhusu sisi na wao pia. [Al-Bukhaariy]
038-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Allaah Anamuunga Anayeunga Kizazi Na Anamkata Anayekata Kizazi
Lu-ulu-un-Manthuwrun
(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)
Hadiyth Ya 38
Allaah Anamuunga Anayeunga Kizazi Na Anamkata Anayekata Kizazi
عَنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها) قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((الرَّحِمُ مُعَلَّقَةٌ بِالْعَرْشِ، تَقُولُ مَنْ وَصَلَنِي وَصَلَهُ اللَّهُ وَمَنْ قَطَعَنِي قَطَعَهُ اللَّهُ)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaisha (رضي الله عنها) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ((Uterasi [fuko la uzazi] limetundikwa katika ‘Arshi, linasema: Anayeniunga Allaah Atamuunga, na anayenikata Allaah Atamkata)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Mafunzo Na Mwongozo:
1. Jina la Allaah (سبحانه وتعالى) Ar-Rahmaan linahusiana na ‘rahm’ yenye maana ya: Uterasi (fuko la uzazi).
2. Allaah (سبحانه وتعالى) Amesisitiza sana kuunga kizazi kinachohusiana kwa damu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالَّذِينَ يَصِلُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ وَيَخَافُونَ سُوءَ الْحِسَابِ ﴿٢١﴾
Na ambao wanaunga yale Aliyoamrisha Allaah kuungwa na wanamkhofu Rabb wao, na wanakhofu hesabu mbaya. [Ar-Ra’d (13: 21)]
3. Mwenye kutaka radhi za Allaah (سبحانه وتعالى) basi aunge kizazi.
4. Hatari ya kukata kizazi; undugu na ujamaa wa uhusiano wa damu ni kukatwa na kulaaniwa na Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema:
فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ﴿٢٢﴾
Basi huenda nyinyi mkigeuka ndio mfanye ufisadi katika ardhi na kukata jamaa zenu wa uhusiano wa damu?
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰ أَبْصَارَهُمْ﴿٢٣﴾
Hao ndio ambao Allaah Amewalaani; Akawafanya viziwi na Akawapofua macho yao. [Muhammad: 22-23]
Rejea pia Al-Baqarah (2: 27).
5. Kukata uzazi; undugu na ujamaa wa uhusiano wa damu, ni miongoni mwa dhambi kubwa kwa vile zinasababisha mtu kupata laana ya Allaah (سبحانه وتعالى).
6. Mwenye kukata kizazi; undugu na ujamaa wa uhusiano wa damu, haingii Jannah kutokana na kauli ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ((Haingii Jannah mwenye kukata udugu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
6. Fadhila kadhaa kwa wenye kuunga undugu zimetajwa katika Hadiyth za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) mojawapo ni sababu ya kuongezewa umri mrefu na kuzidishiwa riziki na baraka: ((Mwenye kupenda kutanuliwa rizki yake, na azidishiwe baraka katika umri wake aunge undugu wake)) [Al-Bukhaariy]
Pia Hadiyth zifuatazo zimetaja fadhila nyinginezo:
((Mwenye kumuamini Allaah na siku ya mwisho amkirimu mgeni wake, na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya mwisho aunge undugu wake)) [Al-Bukhaariy]
Kutoka kwa Abuu Ayuwb Al-Answaariy (رضي الله عنه) kwamba mtu alisema: “Ee Rasuli wa Allaah! Nifahamishe tendo litakaloniingiza Jannah na litakaloniepusha na Moto.” Akasema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ((Umwabudu Allaah wala usimshirikishe na chochote, usimamishe Swalaah utoe Zakaah na uunge undugu)) [Al-Bukhaariy]
7. Kuunga undugu kunahitajia azimio la nguvu ambalo lina faida kwa mwenye kutekeleza. Hadiyth: Alikwenda mtu kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, mimi nina ndugu nawaunga wananikata, nawafanyia wema na wao wananifanyia maovu, nawa mpole kwao wananifanya mjinga. Akasema: ((ikiwa uko kama unavyosema kanakwamba unawalisha majivu ya moto, na hutoacha kuwa unaungwa mkono na Allaah, ukidumu kwa hilo)) [Muslim]
38-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nabiy Pekee Aliyetakwa Afuate Mwongozo Na Vigezo Vya Manabii Wengineo
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
38-Nabiy Pekee Aliyetakwa Afuate Mwongozo Na Vigezo Vya Manabii Wengineo
Allaah (سبحانه وتعالى) Alimuamrisha Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) afuate mwongozo na vigezo vya Manabii wengineo; jambo ambalo hakuna Nabiy mwengine aliyeamrishwa kufanya hivyo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى) baada ya kuwataja Manabii kumi na nane katika Aayah zilizofuatana za Suwrah Al-An’aam:
وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿٨٣﴾
Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliyompa Ibraahiym juu ya watu wake. Tunampandisha cheo Tumtakaye. Hakika Rabb wako ni Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.
وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَارُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٤﴾
Na Tukamtunukia Is-haaq, na Ya’quwb. Wote Tukawahidi. Na Nuwh Tulimhidi kabla. Na katika dhuria wake Daawuwd, na Sulaymaan, na Ayyuwb, na Yuwsuf, na Muwsaa, na Haaruwn. Na hivyo ndivyo Tulipavyo wafanyao ihsaan.
وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلْيَاسَ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٥﴾
Na Zakariyyaa, na Yahyaa, na ‘Iysaa, na Ilyaas. Wote ni miongoni mwa Swalihina.
وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚ وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٨٦﴾
Na Ismaa’iyl, na Al-Yasa’a na Yuwnus, na Luwtw. Na wote Tuliwafadhilisha juu ya walimwengu.
وَمِنْ آبَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوَانِهِمْ ۖ وَاجْتَبَيْنَاهُمْ وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٨٧﴾
Na katika baba zao, na dhuriya wao, na ndugu zao. Na Tukawateua na Tukawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.
ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾
Hiyo ndiyo hidaaya ya Allaah, kwa hiyo, Humwongoza Amtakaye kati ya waja Wake. Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda. [Al-An’aam: 83-88]
Na hii ni dalili ya kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfadhilisha kuliko Manabii wengineo kama alivyosema Imaam As-Sa’dy (رحمه الله):
“Inamaanisha: Fuata nyuma ee Rasuli Mkarimu mwendo wa hawa Manabii waliokhitariwa, na fuata millah zao. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akafuata vigezo vyao akaongoka kwa hidaaya ya Rusuli (wote) wa kabla yake, na akakusanya kila aina ya mazuri yao. Ikamkusanyikia kwake fadhila na khulqa zikawapita walimwengu wote. Akawa Sayyid wa Rusuli wote, na Imaam wa wenye kumcha Allaah, basi Swalaah za Allaah ziwe juu yake pamoja na Manabii wote wengineo. Na kutokana na hivyo, Maswahaba wakatoa dalili kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli mbora kabilsa kuliko wote. [Tafsiyr As-Sa’dy (Uk 263)]
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...