Translate

Jumapili, 30 Desemba 2018

Hukumu ya Kuacha mabega wazi kwa mwanamke

Swali: 

Ni ipi hukumu ya mwanamke kuswali na huku ameweka ´Abaa´ah yake juu ya mabega yake? Imenifikia kutoka kwako kwamba katika hali hii swalah yake inabatilika kwa kuwa imefanana na vazi la mwanaume.


Jibu: 


Allaah ndiye Mwenye kutakwa msaada. Mwanamke huyu imepokelewa vilevile kinyume chake katika yale yaliyoenezwa na wanawake kwamba sisi tunasema kwamba ni sawa kwa mwanamke kuvaa ´Abaa´ah juu ya mabega hata kama hilo litafanywa sokoni na madukani. Yote mawili ni makosa.
Sisi tunasema mwanamke kuweka ´Abaa´ah juu ya mabega yake wakati wa swalah hakuna neno. Kwa sababu hili ni jambo lililozoeleka kwa wanawake. Si jambo maalum kwa wanaume peke yao mpaka tuseme kuwa huku ni kujifananisha na wanaume.
Kuhusu mwanamke kuweka ´Abaa´ah yake juu ya mabega masokoni na mbele za watu asifanye hivo. Kwa sababu kule kuweka kwake ´Abaa´ah yake juu ya mabega kunapelekea kufichukua fomu ya mabega yake na shingo yake na kuonyesha kama shingo yake ni ndefu au ni fupi, jambo ambalo ni fitina. 


Iwapo wanawake wataruhusiwa kuweka ´Abaa´ah zao masokoni ni nani ambaye ana uhakika kama mambo hayatokuwa na wanawake wakaanza kutoka masokoni wakiwa na kanzu pasi na ´Abaa´ah? Kwa sababu wanawake mara nyingi wakifunguliwa mlango kidogo basi mlango unakuwa mkubwa. Huenda wakafikia mpaka kuufungua mlango wote na wakaingia kusikokuwa mlango.
Kwa hiyo tunasema kuweka ´Abaa´ah juu ya mabega wakati wa swalah hakuna neno. Hakubatilishi swalah. Ama kutembea nayo masokoni hapana. Kwa sababu kunapelekea katika fitina. Ni njia inayopelekea wanawake kupanuka zaidi katika mavazi.


Marejeo : Al-Liqaa' ash-Shahriy (42) 


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2EX60FQ
via IFTTT

Hukumu ya Mwanamke kuvaa nguo nyeupe

Swali: 


Hadiyth ambayo imependekeza kuvaa mavazi meupe, je, ni kwa wanaume na wanawake? Na je, ni jambo lililopendekezwa hata kwa wanaume?


Jibu


Lilio la dhahiri ni kuwa ni kwa wanaume. 


Kwa dalili ya Hadiyth ya ´Aaishah, ya kwamba aliona wanawake wa Answaar wametoka kwa ajili ya Swalah ya Fajr na walikuwa wamevaa mavazi meusi. Pamoja na haya, sio Haramu kwa mwanamke kuvaa mavazi meupe. Jambo lililo la Haramu kwake ni kujifananisha na wanaume. Kama ilivyokuja katika Swahiyh:
“Allaah Anamlaani mwanaume anayejifananisha na mwanamke; na mwanamke anayejifananisha na mwanaume.”


Na  Allaah  anajua  zaidi


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2EYqqz0
via IFTTT

Hukumu ya Mwanamke Kuvaa Jilbaab na suruali

Swali: 


Ni ipi hukumu ya mwanamke kuvaa ´Abaa´ah ya mapambo, anaweka ´Abaa´ah mabegani na kuvaa suruwali?


Jibu: 


Naam, kwanza kabisa Suruwali haijuzu kwa mwanamke. 


Kwasababu Suruwali sio vazi la mwanamke. 

Mwanamke anatakiwa kuvaa vazi pana, lenye kusitiri na lililo la wasaa. 


Kwahiyo haijuzu kwake kuvaa mavazi ya kubana. 


Suruwali ni vazi la kubana. Haijuzu kwake.
´Abaa´ah la mapambo halijuzu. ´Abaa´ah ni kwa ajili ya kujisitiri. Sio kwa ajili ya kujipamba. ´Abaa´ah halitakiwi kuwa na mapambo na michoro.
Wakati anapotoka ´Abaa´ah anatatakiwa kuliweka juu ya kichwa. Hata hivyo hakuna neno akaliweka mabegani mwake anapokuwa nyumbani au pamoja na wanawake wenzake.


Marejeo : Liqaa'-ul-Jumu´ah bit-Twaa'if

Na  Allaah anajua  zaidi


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2EX5WWC
via IFTTT

Hukumu ya Kula Tonge lilioanguka

Swali: 

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Linapoanguka tonge la mmoja wenu, basi aliondoshe uchafu na alile na wala asimwachie shaytwaan.”At-Tirmidhiy (1862).
Nifanye nini ikiwa  tonge hilo siwezi kuliondosha uchafu?


Jibu: 


Naam, Ikiwa huwezi kuliondosha uchafu na limechanganyikana na uchafu, hakuna la kufanya. 


Lakini hata hivyo liweke sehemu ambayo ni safi kwa ajili ya kuitukuza neema.


Marejeo : Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) 


Na Allaah  anajua  zaidi


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2F0ZvTa
via IFTTT

kunyamaza wakati wa kula ni Sunnah?

Swali: 

Je, ni adabu kunyamaza wakati wa kula?


Jibu: 


Hakuna msingi juu ya hilo. Msingi wakati wa kula na mambo mengine yote ni:
“Yule anayemuamini Allaah na siku ya Mwisho aseme yaliyo na kheri au anyamaze.”
Mambo yanatakiwa kuwa hivyo.


Marejeo : Fataawaa Raabigh (3)


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2SoPL8t
via IFTTT

Hukumu ya kutoelekea Qibla wakati wa kuchinja

Swali: 

Je, inatosha kusema “Bismillaah” bila ya kuelekea Qiblah, au ni lazima kufanya yote mawili (kusema Bismillaah na kuelekea Qiblah)? Kwa kuwa mahala ambapo nafanya kazi ni pafinyu na wala siwezi kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja.
Jibu: 

Kusema “Bismillaah” wakati wa kuchinja ni jambo la wajibu, kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kaamrisha hilo, na namna hii ndivyo alivyoamrisah Mtume (´alayhis-Swalaat was-Salaam). 

Haijuzu mtu kukusudia kuacha kusema “Bismillaah”. 


Mtu anatakiwa kusema wakati wa kuchinja “Bismillaah Allaahu Akbar”. Hii ndio Sunnah. Na lau atasema “Bismillaah” yatosha. 

Haifai kwake kukusudia kuacha kusema “Bismillaah”. Akiiacha kwa kusahau au kwa ujinga wa kutokujua, hakuna neno kwa hilo na kichinjo kitakuwa ni Halali. 

Lakini haifai kwake kuiacha kwa kukusudia. Ama kuelekea Qiblah ni jambo limependekezwa na wala sio la wajibu

Lau atachinja bila ya kuelekea Qiblah, ni sahihi na inajuzu. Lakini kuelekea kwake Qiblah wakati wa kuchinja ndio bora zaidi.


Mhusika : Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

Marejeo : Nuur ´alaad-Darb


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2ApSLuj
via IFTTT

Kuelekea Qibla wakati wa Kuchinja

Swali


Je, ni lazima kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja...?


Jibu


 Kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja sio wajibu

Mtu anaweza kuchinja kichinjwa chake ijapokuwa hakuelekea Qiblah. Lakini wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema kuwa bora zaidi ni mtu aelekee Qiblah. Kwa sababu ni ´ibaadah. 

Lakini hata hivyo hawakusema kuwa ni sharti. Iwapo mtu atachinja kwa kuelekea upande usiokuwa Qiblah ni halali. Sio jambo limechukizwa. Hapana neno. 

Tofauti na wanavosema watu wasiokuwa na elimu. Baadhi yao wanasema kwamba ni lazima kuelekea Qiblah, jambo ambalo si sahihi.


Rejea : Al-Liqaa' ash-Shahriy (42)

from fisabilillaah.com http://bit.ly/2SvU024
via IFTTT

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...