DAWA MBADALA 11 ZINAZOTIBU KUFUNGA CHOO AU CHOO KIGUMU
Tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu ni jambo tunalolikwepa kwenye mazungumzo yetu ya kila siku.
Hata hivyo ni tatizo kubwa katika jamii na mbaya zaidi wengi hawajuwi madhara yake ni nini ya kuendelea kulivumilia tatizo hili.
Kupata choo kigumu au kufunga choo ni ishara ya tatizo lingine baya zaidi mwilini.
Kama kuna jambo unapaswa uliepuke kwa nguvu zote basi ni hili. Kwa afya bora kabisa hakikisha unapata choo kila siku mara 2 hata mara 3.
Choo kilaini siyo kigumu na chenye maumivu.
Wakati mwingine utakapopata tatizo hili naomba usiwe na aibu kulisema wazi hata kwa boss wako ili upate matibabu kwa haraka.
Kufunga choo au kupata choo kigumu ndiyo CHANZO KIKUU CHA UGONJWA WA BAWASIRI kwa waTanzania wengi na hii inachangiwa kwa sehemu kubwa kwa kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi kila siku.
Pamoja na hayo, hakuna ugonjwa rahisi kutibika kama huu ikiwa utaamua kushughulisha kichwa chako kidogo hasa kwa kuangalia unakula na kunywa nini kila siku.
Dawa mbadala 11 zinazotibu kufunga choo au choo kigumu:
1. Mafuta ya Zeituni
Mafuta ya zeituni (olive oil) yanatosha kutibu hili tatizo.
Yana radha nzuri mdomoni na ni dawa pia.
Kama unaweza yafanye pia kama mafuta yako ya kupikia vyakula vyako mbalimbali, mafuta haya huweza kuliwa pia bila kupitishwa kwenye moto na hivyo ni mafuta mazuri kuweka kwenye kachumbari au saladi mbalimabali.
Matumizi: Chukua kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni changanya na kijiko kidogo kimoja cha chai cha maji maji ya limau na unywe asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa bado tupu.
Fanya hivi kila siku mpaka utakapopona.
2. Juisi ya Limau
Juisi ya limau inatumika kutibu tatizo la kupata choo kigumu au kufunga choo.
Chukua maji maji ya limau kutoka katika limau kubwa 3 na uchanganye na juisi ya matunda kupata kikombe kimoja (ml 250) na unywe yote kutwa mara 1 kila siku kwa siku kadhaa mpaka umepona.
Ukiacha hilo la kutibu kufunga choo limau ina vitamini C nyingi na hivyo itakuongezea kinga yako ya mwili kwa haraka zaidi (usizidishe hata hivyo).
3. Mazoezi ya kutembea
Kama unataka kupata choo kilaini na cha kawaida basi jitahidi uwe mtu wa kutembeatembea na si kukaa tu kwenye kiti kutwa nzima.
Maisha yetu ya kisasa na kazi za ofisini zinatulazimisha kuwa watu wa kukaa kwenye kiti masaa mengi wengine huamua tu kukaa kwenye kiti sebureni akiangalia TV asubuhi mpaka jioni!.
Aina hii ya maisha ni hatari zaidi kwa afya zetu kuliko hata madawa ya kulevya.
Jitahidi kila siku uwe unapata muda wa kutembeatembea kwa miguu mpaka dakika 60 au zaidi.
Hii itakusaidia kuondoa tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.
4. Vyakula vya nyuzinyuzi (fiber)
Mara nyingi utasikia watu wakisisitiza juu ya umhimu wa kula vyakula vya asili na vyenye nyuzinyuzi.
Chakula cha asili kina nafasi kubwa katika kuimarisha afya yako kwa ujumla.
Kinachonishangaza ni kuona watu bado wanaendelea kula ugali wa sembe ilihali inajulikana wazi ugali mweupe ndiyo chanzo kikuu cha kupata choo kigumu ikiwemo ugonjwa wa bawasiri.
Ninakusihi sana uanze kula ugali wa dona kuanzia sasa na kuendelea.
Hakikisha pia asilimia 80 ya mlo wako kwa siku ni matunda na mboga za majani.
Matunda kama ndizi na parachichi ni mhimu ule kila siku kadharika tumia unga au mbegu za maboga.
5. Mshubiri (Aloe Vera)
Mshubiri unajulikana wazi kwa kutibu tatizo hili la kufunga choo au kupata choo kigumu.
Ni mhimu utumie mshubiri fresh kabisa kutoka kwenye mmea moja kwa moja kuliko kutumia za dukani au za kwenye makopo.
Usitumie zaidi ya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya shubiri kwa siku.
Matumizi: Changanya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya aloe vera ndani ya kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani (hasa juisi ya parachichi) na unywe yote kutwa mara 1 hasa nyakati za usiku unapokaribia kwenda kulala kwa siku kadhaa au mpaka umepona.
6. Baking soda
Baking soda ni dawa nyingine ya asili nzuri kwa tatizo hili. Inafanya kazi vizuri kwa zaidi ya asilimia 95.
Sababu ya bicarbonate iliyomo ndani yake itakusaidia kupumua nje vizuri gesi au hewa yoyote ilisongamana ndani ya tumbo pia inasaidia kupunguza asidi mwilini.
Baking soda ni ile wamama huitumia katika kupika maandazi au mikate inapatikana katika maduka ya kawaida hata hapo nje kwa Mangi ipo.
Matumizi:
-Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha baking soda ndani ya nusu kikombe cha maji ya uvuguvugu (ml 125) na unywe yote kwa haraka kutwa mara 1 kwa siku 7 hivi au unaweza kuacha siku yoyote kabla kama tatizo litakuwa limeisha.
7. Mtindi
Unahitaji bakteria wazuri zaidi wakati huu unapokabiliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu.
Utahitaji pia kuacha kula vyakula vya kwenye makopo (processed sugars and foods).
Namna rahisi kabisa ya kuhakikisha mwili wako unapata bakteria wazuri ni kwa kutumia mtindi.
Tumia mtindi wowote ule uliotengeneza mwenyewe nyumbani au hata wa dukani (ila wa dukani usiwe umeongezwa vitu vingine ndani yake – sweetened yogurt).
Matumizi: Kunywa kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi wakati wa chakula cha asubuhi na kikombe kingine usiku unapoenda kulala kwa wiki 1 hata 2.
8. Fanya mazoezi ya kusimama na kuchuchumaa (squat)
Fanya mazoezi ya kuchuchumaaa na kusimama (squatting).
Hili ni zoezi mhimu kwa mtu anayesumbuliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.
Fanya kuchuchumaa na kusimama mara 25 na upumzike dakika 1 kisha unaendelea tena unachuchumaa na kusimaa hivyo hivyo mara 25 kwa mizunguko mitano (5 rounds) huku ukipumzika dakika 1 kila baada ya mzunguko mmoja.
Fanya zoezi hili kila siku mara 1 na usizidishe sana, ni mara 25 kwa mizunguko mitano inatosha na uzuri ni kuwa unaweza kufanya zoezi hili mahali popote.
Wakati huo huo unashauriwa kutumia choo cha kuchuchumaa yaani vile vyoo vya zamani na siyo hivi vya kisasa vya kukaa kama vile upo ofisini.
Vyoo hivi vya kukaa ndiyo moja ya vitu vinavyochangia upate pia ugonjwa wa bawasiri (kuota kinyama sehemu ya haja kubwa na kupata maumivu wakati unajisaidia).
9. Matunda
Asilimia 80 ya chakula chacko kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani.
Unapoumwa na hili tatizo pendelea zaidi parachichi, papai na juisi ya ukwaju.
Kula matunda siyo mpaka uumwe au ushauriwe na daktari, fanya kuwa ndiyo tabia yako kila siku na hutakawia kuona mabadiliko makubwa kwa afya yako kwa ujumla.
10. Maji ya Kunywa
Maji ni uhai. Asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Asilimia 85 za ubongo wako ni maji.
Asilimia 94 ya damu yako ni maji. Hakuna maisha bila maji.
Inashangaza sana kuona mtu anamaliza siku nzima au hata siku 2 hajanywa maji!
Kama wewe si mpenzi wa kunywa maji ya kutosha kila siku SAHAU KUWA NA AFYA NZURI MAISHANI MWAKO.
Hakikisha unakunywa maji kila siku lita 2 mpaka 3, kidogo kidogo kutwa nzima bila kusubiri kiu na hutaugua tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu.
11. UKWAJU
Tunda la ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu.
Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.
NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU.
>Nunua ukwaju wako, ukwaju unapatikana kwa wingi sana masokoni na kwenye supermarkets
>Andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu
>Ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe
>Weka asali kwa kiasi unachopendelea pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata radha nzuri zaidi weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa.
>Ukwaju unakusaidia kuyeyusha chakula tumboni na hivyo kukuepusha na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu
Mambo mhimu mengine ya kuzingatia:
-Acha vilevi VYOTE
-Acha vinywaji baridi na juisi zote za dukani
-Acha chai ya rangi na kahawa na vinywaji vingine vyote vyenye kaffeina
-Acha kula vyakula vilivyokobolewa
-Acha kula mkate mweupe
-Acha kula vyakula vigumu
Kama una swali zaidi liulize hapo chini kwenye comment nitakujibu hapa hapa
Mawasiliano yangu ni : WhatsApp +255714800175
Share post hii kwa ajili ya wengine uwapendao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni