Translate

Alhamisi, 29 Oktoba 2020

12-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Hakujifakharisha Kwa Mavazi Akakataza Mtu Kujivuna Kwayo

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

12-Zuhd Yake: Hakujifakharisha Kwa Mavazi Akakataza Mtu Kujivuna Kwayo

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kujivuna au kujifakharisha kwa mavazi yake, Hadiyth zfuatazo zinathibitisha:

 

حَدَّثَنَا آدَمُ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ زِيَادٍ، قَالَ سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ، يَقُولُ قَالَ النَّبِيُّ ـ أَوْ قَالَ أَبُو الْقَاسِمِ ـ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي فِي حُلَّةٍ، تُعْجِبُهُ نَفْسُهُ مُرَجِّلٌ جُمَّتَهُ، إِذْ خَسَفَ اللَّهُ بِهِ، فَهْوَ يَتَجَلَّلُ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ ‏"‏‏.‏

Ametuhadithia Aadam, ametuhadithis Muhammad bin Ziyaad, amesema: Nimemsikia Abuu Hurayrah akisema:  Nabiy (Au Abul-Qaasim) (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: “Mtu mmoja alikuwa akitembea na kujiona kwa jinsi alivyokuwa amevaa na jinsi alivyozichana nywele zake, ghafla Allaah Akamdidimiza ardhini, kwa hiyo anaendelea kudidimia mpaka Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Na pia amekataza   kuburuza nguo kwa majivuno:

 

  عَنِ ابْنِ عُمَرَ ـ رضى الله عنهما ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ لاَ يَنْظُرُ اللَّهُ إِلَى مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلاَءَ ‏"‏‏.‏

 

Imepokewa kwa Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما)   kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Hamuangalii mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Na pia,

 

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) anasema kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mtu mmoja alipokuwa anatembea, huku anaburuza nguo yake kwa kibri, alifanywa amezwe na ardhi na ataendelea kudidimia ndani yake mpaka siku ya Qiyaamah” [Al-Bukhaariy]

 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...