أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
017-Asbaab Nuzuwl Suwrah Al-Israa Aayah 59
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا مَنَعَنَا أَن نُّرْسِلَ بِالْآيَاتِ إِلَّا أَن كَذَّبَ بِهَا الْأَوَّلُونَ ۚ وَآتَيْنَا ثَمُودَ النَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُوا بِهَا ۚ وَمَا نُرْسِلُ بِالْآيَاتِ إِلَّا تَخْوِيفًا ﴿٥٩﴾
Na hakuna kinachotuzuia kuleta Aayaat (muujiza) isipokuwa ni kuwa watu wa awali waliikadhibisha. Na Tuliwapa kina Thamuwd ngamia jike kuwa dalili dhahiri lakini wakamdhulumu. Na Hatupeleki Aayaat (miujiza, maonyo) isipokuwa kwa ajili ya kukhofisha. [Al-Israa: 59]
Sababun-Nuzuwl:
عَنْ اِبْن عَبَّاس قَالَ : سَأَلَ أَهْل مَكَّة النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَجْعَل لَهُمْ الصَّفَا ذَهَبًا، وَأَنْ يُنَحِّي عَنْهُمْ الْجِبَال، فَيَزْرَعُوا، فَقِيلَ لَهُ : إِنْ شِئْت أَنْ نَسْتَأْنِي بِهِمْ لَعَلَّنَا نَجَتْنِي مِنْهُمْ، وَإِنْ شِئْت أَنْ نُؤْتِيهِمْ الَّذِي سَأَلُوا، فَإِنْ كَفَرُوا أُهْلِكُوا كَمَا أُهْلِكَ مَنْ قَبْلهمْ، قَالَ : "بَلْ تَسْتَأْتِي بِهِمْ " فَأَنْزَلَ اللَّه : وَمَا مَنَعَنَا أَنْ نُرْسِل بِالْآيَاتِ إِلَّا أَنْ كَذَّبَ بِهَا الْأَوَّلُونَ وَآتَيْنَا ثَمُود النَّاقَة مُبْصِرَة
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas amesema: Watu wa Makkah wamemtaka Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) awajaalie jabali la Swafaa liwe dhahabu na majabali yote yatoweke ili wapate kulima (badala yake katika ardhi hiyo). Akaambiwa: “Ima tuwavumilie kwa wema na tuwape muda zaidi au ukitaka tuwape waliyoyataka, kisha wakikufuru waangamizwe kama walivyoangamizwa wa kabla yao.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Bali wavumilieni kwa wema na wapeni muda zaidi.” Hapo Allaah (عز وجل) Akateremsha:
وَمَا مَنَعَنَا أَن نُّرْسِلَ بِالْآيَاتِ إِلَّا أَن كَذَّبَ بِهَا الْأَوَّلُونَ ۚ وَآتَيْنَا ثَمُودَ النَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُوا بِهَا ۚ وَمَا نُرْسِلُ بِالْآيَاتِ إِلَّا تَخْوِيفًا ﴿٥٩﴾
Na hakuna kinachotuzuia kuleta Aayaat (muujiza) isipokuwa ni kuwa watu wa awali waliikadhibisha. Na Tuliwapa kina Thamuwd ngamia jike kuwa dalili dhahiri lakini wakamdhulumu. Na Hatupeleki Aayaat (miujiza, maonyo) isipokuwa kwa ajili ya kukhofisha.
[Imaam Ahmad, Ibn Jariyr, Al-Haakim]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni