Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
11-Zuhd Yake: Amefariki Hakuacha Mali
وعن عمرو بن الحارث أخي جُوَيْرِيّة بنتِ الحارِث أُمِّ المُؤْمِنِينَ ، رضي الله عنهما ، قَالَ : مَا تَرَكَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عِنْدَ مَوْتِهِ دِيناراً ، وَلاَ دِرْهَماً ، وَلاَ عَبْداً ، وَلاَ أَمَةً ، وَلاَ شَيْئاً إِلاَّ بَغْلَتَهُ الْبَيضَاءَ الَّتي كَانَ يَرْكَبُهَا ، وَسِلاَحَهُ ، وَأرْضاً جَعَلَهَا لاِبْنِ السَّبِيلِ صَدَقَةً . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa 'Amri bin Al-Haarith, kaka yake Juwayriyyah bint Al-Haarith, Mama wa Waumini ambaye amesema: "Hakuacha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati wa kufariki hata dinari moja wala dirhamu wala mjakazi wala kijakazi wala kitu kingine chochote isipokuwa nyumbu wake mweupe aliyekuwa akipanda na silaha zake na ardhi aliyoiacha kama sadaqah kwa wasafiri." [Al-Bukhaariy]
Na alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
لَا نُورَثُ، مَا تَرَكْنَاهُ صَدَقَةٌ
haturithiwi na tunachoacha ni sadaka. [Al-Bukhaariy, Muslim]
وقال عمرو بن الحارث رضي الله عنه : "مَا تَرَكَ النَّبِىُّ صلى الله عليه وسلم إِلاَّ سِلاَحَهُ وَبَغْلَتَهُ الْبَيْضَاءَ ، وَأَرْضًا تَرَكَهَا صَدَقَةً" رواه البخاري
‘Amr bin Al-Haarith (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam hakuacha chochote (baada ya kifo chake) isipokuwa ngao yake, nyumbu wake mweupe, na kipande cha ardhi ambacho alikiacha kwa ajili ya sadaka.” [Al-Bukhaariy]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni