Translate

Alhamisi, 1 Oktoba 2020

019-Aayah Na Mafunzo: Maamrisho Ya Kumtendea Wema Mke Na Kuvumiliana

 

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Maamrisho Ya Kumtendea Wema Mke Na Kuvumiliana

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا النِّسَاءَ كَرْهًا ۖ وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا بِبَعْضِ مَا آتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّـهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا ﴿١٩﴾

Enyi walioamini! Si halali kwenu kurithi wanawake kwa kuwakirihisha. Na wala msiwazuie kwa inda ili mpokonye baadhi ya vile mlivyowapa isipokuwa wakiwa wamefanya uchafu bayana. Na kaeni nao kwa wema. Na mkiwachukia, basi asaa ikiwa mnachukia jambo na Allaah Akalijaalia kuwa lenye khayr nyingi. [An-Nisaa: 19]

 

Mafunzo:

 

Maamrisho ya kumtendea wema mke yametajwa katika Hadiyth kadhaa za  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) miongoni mwazo ni:

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنِ النَّبِيِّ ـ صلى الله عليه وسلم ـ قَالَ ‏ "‏ خَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لأَهْلِهِ وَأَنَا خَيْرُكُمْ لأَهْلِي ‏"‏ ‏ رواه الترمذي

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:  ((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani [ahli])) [Swahiyh Ibn Maajah (1621), Swahiyh At-Targhiyb (1925)].

 

 Na pia,

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:  ((أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا  وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ خُلُقًا)) الترمذي وقال: حديث حسن صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin aliyekamilika iymaan ni aliye na tabia njema kabisa, na wabora wenu ni walio bora kwa wake zao kwa tabia))  [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Swahiyh Hasan]

 

Na kutomchukia: “Muumini mwanaume asimchukue (mke ambaye) ni Muumini, akichukizwa tabia moja, bila shaka ataridhika naye kwa tabia yake nyingine.” [Muslim].

 

Pia Sababun-Nuzuwl: Walikuwa Waarabu zama za Jaahiliyyah pindi anapokufa mwanaume na akaacha mke, basi wale ndugu wa mume wake wanakuwa na haki zaidi kwa mwanamke, na   baadhi yao wakitaka wanamuoa, na wakitaka wanamuozesha, na wakitaka hawamuozeshi, na wao wanakuwa wana haki naye zaidi kuliko hata ndugu zake mwanamke na wazazi wake. Ndipo Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha Aayah hii. [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ameipokea Al-Bukhaary]. 

 

 

 

 

 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...