Translate

Alhamisi, 29 Oktoba 2020

18-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aanah Kwa Asiyekuwa Allaah

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم

 

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

 

18- Isti’aanah (Kuomba Msaada) Kwa Asiyekuwa Allaah

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Maana Ya Isti’aanah (kuomba msaada) na dalili zake:

 

Isti’aanah ni kuomba msaada. Na Isti’aanah kwa Allaah ni kuomba katika mambo ya Dini na ya dunia na inajumuisha mja kujidhalilisha kwa Mola wake na kuwa na yakini na kumtegemea Yeye (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Pekee kama Anavyosema:

فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ

basi mwabudu Yeye na tawakali Kwake. [Huwd: 123]

 

 

Na katika Suwratul-Faatihah ambayo inajumuisha aina zote za Tawhiyd, Muislamu anakariri katika Swalaah zake zote:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada. [Al-Faatihah: 5]

 

 

Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

إِيَّاكَ نَعْبُدُ

Inathibitisha Tawhiyd ya ‘Uluwhiyyah (kumpwekesha Allaah katika kumwabudu); yaani aina zote za ‘ibaadah zinahitaji kuelekezwa Kwake Pekee Subhaanahu wa Ta’aala.

 

Na

وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ 

Inathibitisha Tawhiyd ya Ar-Rubuwbiyyah (kumpwekesha Allaah katika Uola) kwa sababu ni kuomba msaada kwa Ar-Rabb (Mola) Ambaye ni Al-Khaaliq (Muumbaji), Ar-Raaziq (Mtoaji rizki), Al-Mudabbir (Mwendeshaji mambo), Al-Maalik (Mwenye kumiliki) Ambaye mambo yote yamo Mikononi Mwake. Kwa hiyo anapaswa Yeye kuombwa mahitaji yetu kama vile Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyomuusia Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ambaye amehadithia:

 

كُنْتُ خَلْفَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يًوْماً، فقال: ((يا غُلامُ، إنِّي أُعَلِّمُكَ كلِماتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجاهَك، إذا سأَلْتَ فاسْأَلِ اللهَ، وإذا اسْتَعنْتَ فاسْتَعِنْ باللهِ، واعْلَمْ أنَّ الأُمَّة  لَوِ اجْتَمَعَتْ على أَنْ يَنْفَعُـوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيْءٍ قدْ كَتَبَهُ اللهُ لَكَ، وإن اجْتَمَعُوا على أن يَضُرَّوكَ بِشيءٍ لَمْ يَضُروكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأقْلامُ وَجَفَّتِ الصُّحُفُ))

Siku moja nilikuwa nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: “Ee kijana! nitakufundisha maneno (ya kufaa); Mhifadhi Allaah (fuata maamrisho Yake na chunga mipaka Yake) Atakuhifadhi.  Muhifadhi Allaah utamkuta mbele yako. Ukiomba, muombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), ukitafuta msaada tafuta kwa Allaah. Tambua kwamba ikiwa ummah mzima utaungana kukunufaisha wewe kwa kitu, basi hutonufaika ila tu kwa kile Alichokwishakuandikia Allaah. Na wakikusanyika kukudhuru kwa chochote, hutodhurika ila tu kwa kile Allaah Alichokwishakukuandikia (kuwa kitakudhuru), kwani kalamu zimeshanyanyuliwa (kila kitu kishaandikwa) na swahifa zimeshakauka.” [At-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Kumuomba bin-Aadam msaada wa jambo ambalo limo katika uwezo wake inafaa kwa dalili zifuatazo katika Qur-aan na Sunnah:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. [Al-Maaidah: 2]

 

Na Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عن أبي هُرَيْرَة رضي اللهُ عنه، عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قال:  "مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيا نَفَّسَ اللهُ عَنْهُ كُرْبَةً من كُرَبِ يوْمِ القيامَةِ، ومَنْ يَسَّرَ على مُعْسِرٍ يَسَّرَ اللهُ عليه في الدنْيا والآخِرَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ الله في الدُّنْيا والآخِرَةِ  واللهُ في عَوْنِ الْعَبْدِ ما كانَ الْعَبْدُ في عَونِ أخيهِ"  

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yeyote atakayemuondoshea shida ya kidunia Muislamu mwenzake, Allaah Atamuondoshea moja katika shida za Siku ya Qiyaamah. Na yeyote yule atakayemsaidia muhitaji (maskini) Allaah Atamsaidia haja zake hapa duniani na Aakhirah. Na yeyote yule atakayemsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri hapa duniani na Aakhirah. Allaah Humsaidia mja wake wakati wote madamu mja (huyo) yungali anamsaidia nduguye (Muislamu).” [Muslim]

 

Pia,   

 

عَنْ عَبْدِ الله بنِ عُمَرَ رَضِيَ الله عَنْهُما، أَنَّ النَّبِيَ صَلَّى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "أَحَبُّ النَّاسِ إِلَى الله أَنْفَعُهُمْ لِلّنَاسِ، وَأَحَبُّ الأَعْمَالِ إِلَى الله سُرُورٌ تُدْخِلُهُ عَلَى مُسْلِمٍ  أَوْ تَكْشِفُ عَنْهُ كُرْبَةً  أَوْ تَقْضِيَ عَنْهُ دَيْناً أَوْ تَطْرُدُ عَنْهُ جُوعاً، وَلأَنْ أَمْشِيَ مَعَ أَخِي المُسْلِمِ فِي حَاجَةٍ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أَعْتَكِفَ فِى هَذَا المَسْجِدِ يعني مسجدَ المدينةِ شهرًا، وَمَنْ كَفَّ غَضَبَهُ سَتَرَ اللهُ عَوْرَتَه وَمَنْ كَظَمَ غَيْظَهُ وَلَوْ شَاءَ أَنْ يُمْضِيَه أَمْضَاهُ مَلأَ اللهُ قَلْبَهُ رَجاءً يَوْمَ القِيَامَةِ وَمَنْ مَشَى مَعَ أَخِيهِ المُسْلِمِ فِى حَاجَةٍ حَتَّى تَتَهَيَّأَ لَهُ أَثْبَتَ اللهُ قَدَمَهُ يَوْمَ تَزِلُّ الأَقْدَامُ وَإِنَّ سُوءَ الخُلُقِ لَيُفْسِدُ العَمَلَ كَمَا يُفْسِدُ الخلُّ العَسَلَ"

‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Mtu ambaye ni kipenzi kabisa kwa Allaah ni yule ambaye ni mbora kabisa katika kunufaisha wenziwe. Na ‘amali zilizokuwa kipenzi kabisa kwa Allaah ('Azza wa Jalla) ni furaha aingizayo kwa Muislamu, au kumuondoshea shida, au kumtimizia deni lake, au kumuondoshea njaa. Na hakika mimi kwenda kumtimizia ndugu yangu haja yake, ni kipenzi kwangu kuliko nikae I’tikaaf (kijifunga katika ‘ibaadah Msikitini) mwezi mzima katika Masjid hii (Masjid Nabawiy). Na atakayeacha ghadhabu zake, basi Allaah Atamsitiri aibu zake. Na atakayezuia ghaydhi (ghadhabu na huzuni moyoni) zake japokuwa haogopi kuzionyesha, lakini anazuia, Allaah Atamjaza moyo wake kwa matumaini Siku ya Qiyaamah. Na atakayetembea na nduguye katika kumtimizia haja mpaka akamsaidia kikamlifu basi Allaah Atamthibitisha miguuu yake Siku ambayo miguu haitothibitika. Hakika khulqu (tabia) mbaya inaharibu ‘amali kama vile siki inavyoharibu asali.” [As-Silsilah Asw-Swahiyhah (906)]

 

Mifano ya mtu kumuomba bin-Aadam mwenziwe;

 

“Ee fulani! Nakuomba unisaidie kunilipia deni langu!”

 

“Ee fulani! Nakuomba unisaidie kunilipia gharama za matibabu ili nitibiwe!”

 

Au kuomba msaada wa mtu kumsimamia kazi yake, kumpatia anachohitaji katika matumizi, au kuomba kushirikiana katika ‘amali za khayr, au kuomba kusaidia jambo lolote la khayr ambalo litampatia thawabu kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kumfanyia wema mwenziwe kama ilivyothibiti katika Hadiyth zilizotangulia.

 

Ama kuomba jambo ambalo halimo katika uwezo wa ki-bin-Aadam hapo huwa ni shirki. Mfano mtu kumuomba mtu amsaidie kupata kizazi, au kumwendea mtabiri amsaidie kumtazamia mambo ya ghayb, au mchawi kumuomba amfanye awe tajiri, au kuwaomba msaada wa riziki walio kaburini au kuwaomba wawaondoshee maradhi n.k.

 

Hizo ni aina za ‘ibaadah zipasazo kuelekezwa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee, kwa hiyo, 'Ibaadah kuielekeza kwa mwengine ni shirki kubwa kabisa kwa sababu ni kumshirikisha Allaah na viumbe Vyake katika mambo ambayo ni Allaah ('Azza wa Jalla) Pekee Mwenye uwezo nayo. Na shirki hii inamtoa mtu nje ya Uislamu kwa dalili kauli ya Allaah (Subahaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿١١٧﴾

 

Na yeyote yule anayeomba du’aa (au kuabudu) pamoja na Allaah muabudiwa mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo; basi hakika hesabu yake iko kwa Rabb wake. Hakika hawafaulu makafiri. [Al-Muuminuwn: 117]

 

 

Ilhali Allaah ('Azza wa Jalla) Ametuamrisha tumuombe Yeye Pekee kama Anavyosema:

 

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ﴿١٨٦﴾

Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah: 186]

 

 

Na Yeye Allaah ('Azza wa Jalla) Ndiye Mwenye kumuondoshea mtu dhiki zake Anapoombwa Yeye Pekee bila ya kumshirikisha, Anasema Allaah (Subahaanahu wa Ta’aalaa):

 

أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٦٢﴾

Au nani Anayemuitika mwenye dhiki mno anapomwomba, na Akamuondoshea ouvu na Akakufanyeni makhalifa wa ardhi? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Ni machache mno mnayokumbuka. [An-Naml: 62]

 

Na pia Akamuamrisha Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumpwekesha na kutokumshirikisha na kwamba hata yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hana uwezo wa kumnufaisha mtu wala kumdhuru wala kumjaalia hidaaya:

 

قُلْ إِنَّمَا أَدْعُو رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِهِ أَحَدًا﴿٢٠﴾

Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi namuomba Rabb wangu na wala simshirikishi na yeyote.”

 

 

قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا﴿٢١﴾

Sema: “Hakika mimi sikumilikieni dhara na wala uongofu.” [Al-Jinn: 20-21]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٦﴾

Na wala usiombe badala ya Allaah visivyokufaa wala visivyokudhuru. Na ukifanya, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.

 

 

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ ۚ يُصِيبُ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚوَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿١٠٧﴾

Na Allaah Akikugusisha dhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye. Na Akikutakia kheri, basi hakuna wa kurudisha fadhila Zake, Anasababisha kumfikia kwayo (fadhila Yake) Amtakaye katika waja Wake. Naye ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Yuwnus: 106-107]

 

 

Na maharamsho mengineyo mengi yanapatikana katika Qur-aan:

 

إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ ۖ فَادْعُوهُمْ فَلْيَسْتَجِيبُوا لَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٩٤﴾

Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah ni waja kama nyinyi. Hebu waiteni wakuitikieni ikiwa nyinyi ni wakweli. [Al-A’raaf: 194]

 

 

Wale ambao wanaombwa, hawawezi kujiondoshea wenyewe madhara wala kujinufaisha Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا ﴿٥٦﴾

Sema: “Iteni wale ambao mnadai (ni waabudiwa) pasi Naye, basi hawamiliki kukuondesheeni dhara na wala kuihamisha (kwa mwengine).” [Al-Israa: 56]

 

 

Na Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ ﴿٢٢﴾

Sema: “Ombeni wale mnaodai kwa dhana (ni waabudiwa) badala ya Allaah, hawamiliki hata uzito wa sisimizi mbinguni wala ardhini, na wala hawana humo ushirika Naye, na wala Yeye (Allaah) Hana msaidizi miongoni mwao.” [Sabaa: 22]

 

 

Hakuna anachokipata yule ambaye anamshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) isipokuwa ni khasara duniani na Aakhirah na kujiweka katika upotofu:

 

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَعْبُدُ اللَّـهَ عَلَىٰ حَرْفٍ ۖ فَإِنْ أَصَابَهُ خَيْرٌ اطْمَأَنَّ بِهِ ۖ وَإِنْ أَصَابَتْهُ فِتْنَةٌ انقَلَبَ عَلَىٰ وَجْهِهِ خَسِرَ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ ﴿١١﴾

Na miongoni mwa watu yuko anayemwabudu Allaah ukingoni. Inapompata kheri, hutumainika kwayo; Na inapompata mtihani hugeuka nyuma juu ya uso wake (kurudia kufru). Amekhasirika duniani na Aakhirah. Hiyo ndiyo khasara bayana.

 

 

يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُ وَمَا لَا يَنفَعُهُ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الضَّلَالُ الْبَعِيدُ ﴿١٢﴾

Humwomba badala ya Allaah ambavyo visivyomdhuru na wala visivyomnufaisha. Huo ndio upotofu wa mbali.

 

يَدْعُو لَمَن ضَرُّهُ أَقْرَبُ مِن نَّفْعِهِ ۚ لَبِئْسَ الْمَوْلَىٰ وَلَبِئْسَ الْعَشِيرُ ﴿١٣﴾

Humwomba yule ambaye dhara yake iko karibu kuliko manufaa yake. Bila shaka ni mlinzi muovu kabisa, na bila shaka ni rafiki muovu kabisa. [Al-Hajj: 11-13]

 

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَن دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ﴿٥﴾

 “Na nani aliyepotoka zaidi kuliko ambaye anayeomba asiyekuwa Allaah ambaye hamuitikii mpaka Siku ya Qiyaamah; nao wala hawatambui  maombi yao.” [Al-Ahqaaf: 5]

 

 

 

Pia, maharamisho kadhaa katika Sunnah za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yameshatangulizwa katika silsilah za maudhui hii ya “Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!”

 

 

 



56-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ummah Wake Utashudhuia Umati Zote Za Nyuma

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

56-Ummah Wake Utashudhuia Umati Zote Za Nyuma

Alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ

Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu. [Al-Baqarah: 143]

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ يَجِيءُ نُوحٌ وَأُمَّتُهُ فَيَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى هَلْ بَلَّغْتَ فَيَقُولُ نَعَمْ، أَىْ رَبِّ‏.‏ فَيَقُولُ لأُمَّتِهِ هَلْ بَلَّغَكُمْ فَيَقُولُونَ لاَ، مَا جَاءَنَا مِنْ نَبِيٍّ‏.‏ فَيَقُولُ لِنُوحٍ مَنْ يَشْهَدُ لَكَ فَيَقُولُ مُحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم وَأُمَّتُهُ، فَنَشْهَدُ أَنَّهُ قَدْ بَلَّغَ، وَهْوَ قَوْلُهُ جَلَّ ذِكْرُهُ ‏(( ‏وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ‏)) وَالْوَسَطُ الْعَدْلُ ‏"‏‏.‏ البخاري

 

Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ataitwa Nuwh Siku ya Qiyaamah ataulizwa: Je, umebalighisha ujumbe? Atasema: Naam. Wataitwa watu wake wataulizwa: Je, alikufikishieni ujumbe? Watasema: Hakutujia mwonyaji wala hakuna aliyetumwa kwetu. Ataulizwa Nuwh: Nani mwenye kukushuhudia hayo? Atasema: Muhammad na Ummah wake.  Akasema: Hiyo ndio maana kauli Yake:

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ  

Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu.  Akasema: “Waswatwaa, maana yake ni uadilifu basi mtatoa ushahidi (kuhusu Nuwh) kubalighisha ujumbe na kisha nitakuwa shahidi wenu.”  [Ahmad (3/32) na Al-Bukhaariy pia kama hivyo (4487)]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَجَاهِدُوا فِي اللَّـهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ ۚ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِن قَبْلُ وَفِي هَـٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ ۚ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللَّـهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ ۖ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ ﴿٧٨﴾

Na fanyeni jihaad katika njia ya Allaah kama inavyostahiki kufanyiwa jihaad. Yeye Ndiye Amekuteueni na Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika Dini. Mila ya baba yenu Ibraahiym. Yeye (Allaah) Ndiye Aliyekuiteni Waislamu hapo zamani na pia katika hii (Qur-aan). Ili Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) awe shahidi juu yenu, nanyi muwe mashahidi juu ya watu.  [Al-Hajj: 78]

 

Imaam As-Sa’diy amesema kuhusu kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ

nanyi muwe mashahidi juu ya watu.  

 

Kwa sababu ya kuwa kwenu Waislamu Ummah bora kabisa uliotoka kwa watu, Ummah wa wastani kwa uadilifu   mtashahudia Rusuli wote kwamba wamebaligisha ujumbe kwa Ummah zao, na mtashuhudia kwa Ummah zote kwamba Rusuli wao wamebalighisha ujumbe kutokana na yale ambayo Allaah Amekujlisheni katika Kitabu Chake (Qur-aan). [Tafsiyr As’Sa’diy]

 

Ummah wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni Ummah bora kabisa ni kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾

110. mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Ahlul-Kitaabi ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wanaoamini na wengi wao ni mafasiki. [Aal-‘Imraan:11]

 

 

 

 



12-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Hakujifakharisha Kwa Mavazi Akakataza Mtu Kujivuna Kwayo

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

12-Zuhd Yake: Hakujifakharisha Kwa Mavazi Akakataza Mtu Kujivuna Kwayo

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kujivuna au kujifakharisha kwa mavazi yake, Hadiyth zfuatazo zinathibitisha:

 

حَدَّثَنَا آدَمُ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ زِيَادٍ، قَالَ سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ، يَقُولُ قَالَ النَّبِيُّ ـ أَوْ قَالَ أَبُو الْقَاسِمِ ـ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي فِي حُلَّةٍ، تُعْجِبُهُ نَفْسُهُ مُرَجِّلٌ جُمَّتَهُ، إِذْ خَسَفَ اللَّهُ بِهِ، فَهْوَ يَتَجَلَّلُ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ ‏"‏‏.‏

Ametuhadithia Aadam, ametuhadithis Muhammad bin Ziyaad, amesema: Nimemsikia Abuu Hurayrah akisema:  Nabiy (Au Abul-Qaasim) (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: “Mtu mmoja alikuwa akitembea na kujiona kwa jinsi alivyokuwa amevaa na jinsi alivyozichana nywele zake, ghafla Allaah Akamdidimiza ardhini, kwa hiyo anaendelea kudidimia mpaka Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Na pia amekataza   kuburuza nguo kwa majivuno:

 

  عَنِ ابْنِ عُمَرَ ـ رضى الله عنهما ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ لاَ يَنْظُرُ اللَّهُ إِلَى مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلاَءَ ‏"‏‏.‏

 

Imepokewa kwa Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما)   kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Hamuangalii mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Na pia,

 

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) anasema kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mtu mmoja alipokuwa anatembea, huku anaburuza nguo yake kwa kibri, alifanywa amezwe na ardhi na ataendelea kudidimia ndani yake mpaka siku ya Qiyaamah” [Al-Bukhaariy]

 



029-Aayah Na Mafunzo: Anayejiua Ataingizwa Motoni Kwa Hali Ile Ile Kujiua

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Anayejiua Ataingizwa Motoni Kwa Hali Ile Ile  Kujiua

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى)

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ ۚ وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ﴿٢٩﴾

Enyi walioamini! Msiliane mali zenu kwa ubatilifu, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana baina yenu. Wala msijiue. Hakika Allaah daima kwenu ni Mwenye kurehemu.

 

وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ عُدْوَانًا وَظُلْمًا فَسَوْفَ نُصْلِيهِ نَارًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾

Na atakayefanya hivyo kwa uadui na dhulma, basi Tutamuingiza motoni. Na hilo kwa Allaah ni mepesi.  [An-Nisaa: 29 - 30]

 

 

Mafunzo:

 

Haramisho la kujiua na tahadharisho la adhabu yake kwamba afanyae hivyo, atakariri kujiua Siku ya Qiyaamah: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yeyote atakayejitupa kutoka mlimani na kujiua, atatupwa motoni milele. Atakayekunywa sumu na kujiua, basi atatupwa motoni na huko atakuwa akiinywa hiyo sumu milele. Atakayejiua kwa kipande cha chuma, atatiwa motoni akiwa na kipande hicho cha chuma akijitwanga nacho tumboni kwake humo motoni milele.” [Muslim].

 

 



085-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Israa: Na Wanakuuliza Kuhusu Roho. Sema: Roho Ni...

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

017-Asbaab Nuzuwl Suwrah Al-Israa Aayah 85

 

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى)

 

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٥﴾

Na wanakuuliza kuhusu roho. Sema: Roho ni katika amri ya Rabb wangu. Na hamkupewa ujuzi isipokuwa kidogo tu. [Al-Israa: 85]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ كُنْتُ أَمْشِي مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي حَرْثٍ بِالْمَدِينَةِ وَهْوَ مُتَّكِئٌ عَلَى عَسِيبٍ، فَمَرَّ بِقَوْمٍ مِنَ الْيَهُودِ فَقَالَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ سَلُوهُ عَنِ الرُّوحِ‏.‏ وَقَالَ بَعْضُهُمْ لاَ تَسْأَلُوهُ عَنِ الرُّوحِ‏.‏ فَسَأَلُوهُ فَقَامَ مُتَوَكِّئًا عَلَى الْعَسِيبِ وَأَنَا خَلْفَهُ، فَظَنَنْتُ أَنَّهُ يُوحَى إِلَيْهِ فَقَالَ ‏((‏وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُمْ مِنَ الْعِلْمِ إِلاَّ قَلِيلاً‏))‏ فَقَالَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ قَدْ قُلْنَا لَكُمْ لاَ تَسْأَلُوهُ‏.‏

 

 

Abdullaah bin Mas’uwd amehadithia: Nilikuwa natembea na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika mashamba ya Madiynah, naye alikuwa  akitembea kwa kuegemea kuti la mtende. Wakapita kundi la Mayahudi wakaambizana wamuulize kuhusu roho. Baadhi yao wakasema: “Msimuulize kuhusu roho.” Lakini wakamuuliza. Akainuka kwa kutegemea kuti la mtende, nami niko nyuma yake, nikidhani kuwa anateremshiwa Wahyi. Kisha akasoma:

 

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٥﴾

Na wanakuuliza kuhusu roho. Sema: Roho ni katika amri ya Rabb wangu. Na hamkupewa ujuzi isipokuwa kidogo tu.

 

Hapo baadhi ya Mayahudi wakasema (kuwaambia wenzao): “Si tulikuambieni kuwa msimuulize (hamkusikia)?”

 

[Al-Bukhaariy – Kitaab At-Tawhiyd]

 

 

Na pia,

 

حَدَّثَنَا قَيْسُ بْنُ حَفْصٍ، قَالَ حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَاحِدِ، قَالَ حَدَّثَنَا الأَعْمَشُ، سُلَيْمَانُ عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ بَيْنَا أَنَا أَمْشِي، مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي خَرِبِ الْمَدِينَةِ، وَهُوَ يَتَوَكَّأُ عَلَى عَسِيبٍ مَعَهُ، فَمَرَّ بِنَفَرٍ مِنَ الْيَهُودِ، فَقَالَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ سَلُوهُ عَنِ الرُّوحِ‏.‏ وَقَالَ بَعْضُهُمْ لاَ تَسْأَلُوهُ لاَ يَجِيءُ فِيهِ بِشَىْءٍ تَكْرَهُونَهُ‏.‏ فَقَالَ بَعْضُهُمْ لَنَسْأَلَنَّهُ‏.‏ فَقَامَ رَجُلٌ مِنْهُمْ فَقَالَ يَا أَبَا الْقَاسِمِ، مَا الرُّوحُ فَسَكَتَ‏.‏ فَقُلْتُ إِنَّهُ يُوحَى إِلَيْهِ‏.‏ فَقُمْتُ، فَلَمَّا انْجَلَى عَنْهُ، قَالَ ‏((‏وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتُيتُمْ مِنَ الْعِلْمِ إِلاَّ قَلِيلاً‏))‏‏.

 

Kutoka kwa ‘Abdullaah amesema:  Tulipokuwa tunatembea na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kupitia magofu ya Madiynah na alikuwa anatembea kwa kuegemea kuti la mtende. Wakapita baadhi ya Mayahudi wakaambizana na wenzao: “Muulizeni kuhusu roho.” Baadhi yao wakasema: “Msimuulize jambo huenda akawapa jibu litakalowachukiza.” Lakini wengine wakasisitiza wakasema: “Tutamuuliza!” Mmoja wao alisimama na aliuliza, “Yaa Abal-Qaasim! Roho ni nini?” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akanyamaza. Nikadhani alikuwa akipokea Wahyi. Kwa hiyo nikasubiri mpaka hali ile (ya kufunuliwa Wahyi) iwe imekwisha. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasoma:

 

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٥﴾

Na wanakuuliza kuhusu roho. Sema: Roho ni katika amri ya Rabb wangu. Na hamkupewa ujuzi isipokuwa kidogo tu. [Al-Israa: 85]

 

[Al-Bukhaariy – Kitaab Al-‘Ilm]

 

 



056-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Masikini Amtazame Aliye Chini Yake Wala Asitazame Aliye Juu Yake

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 56

Masikini Amtazame Aliye Chini Yake Wala Asitazame Aliye Juu Yake

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((انْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ أَسْفَلَ مِنْكُمْ وَلاَ تَنْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ فَوْقَكُمْ فَإِنَّهُ أَجْدَرُ أَنْ لاَ تَزْدَرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ)) متفق عليه وهذا لفظ مسلم.

 وفي رواية البخاري: ((إِذَا نَظَرَ أَحَدُكُمْ إِلَى مَنْ فُضِّلَ عَلَيْهِ فِي الْمَالِ وَالْخَلْقِ فَلْيَنْظُرْ إِلَى مَنْ هُوَ أَسْفَلَ مِنْهُ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mtazameni aliye chini yenu wala msimtazame aliye juu yenu, kwani [kufanya hivyo] ni haki zaidi msije  mkazidharau neema za Allaah juu yenu))[ Al-Bukhaariy na Muslim] Hii ni lafdhi ya Muslim.

 

Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: ((Anapomtazama mmoja wenu aliyefadhilishwa zaidi kwa mali na umbo, basi amtazame aliye chini yake)).

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Hikma ya Allaah (سبحانه وتعالى) kujaaliwa baadhi ya watu matajiri, na baadhi yao masikini na kuwafadhalisha wengine juu ya wengineo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمَنْ أَرَادَ الْآخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ كَانَ سَعْيُهُم مَّشْكُورًا ﴿١٩﴾

Na anayetaka Aakhirah na akaifanyia juhudi inayostahiki kufanyiwa, naye ni Muumin, basi hao juhudi zao ni za kushukuriwa. 

كُلًّا نُّمِدُّ هَـٰؤُلَاءِ وَهَـٰؤُلَاءِ مِنْ عَطَاءِ رَبِّكَ ۚ وَمَا كَانَ عَطَاءُ رَبِّكَ مَحْظُورًا ﴿٢٠﴾

Wote hao Tunawakunjulia; hawa na hao katika hiba za Rabb wako. Na hazikuwa hiba za Rabb wako zenye kuzuiliwa.

انظُرْ كَيْفَ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ وَلَلْآخِرَةُ أَكْبَرُ دَرَجَاتٍ وَأَكْبَرُ تَفْضِيلًا ﴿٢١﴾

Tazama vipi Tunavyowafadhilisha baadhi yao juu ya wengineo. Na bila shaka Aakhirah ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi. [Al-Israa 17: 19-21)]

 

 

2. Ni bora kumtazama aliye chini katika mambo ya mali duniani. Ama mas-alah ya Dini, ni jambo zuri kumtazama aliye juu ili Muislamu apate kujihimiza na kushindana kutenda ‘amali au kujifunza na amfikie nduguye huyo.  Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾

Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).

 

يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَـٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٤﴾

Wanamwamini Allaah na Siku ya Mwisho na wanaamrisha mema na wanakataza munkari na wanakimbilia katika mambo ya kheri, na hao ni miongoni mwa Swalihina.

 

وَمَا يَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَلَن يُكْفَرُوهُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ ﴿١١٥﴾

Na kheri yoyote waifanyayo hawatokanushiwa (thawabu zake).  Na Allaah ni Mjuzi wa wenye taqwa.  [Aal-‘Imraan (3: 113-115)]

 

Rejea pia: Al-Muttwaffifiyn (83: 26), Al-Muuminuwn (23: 60-61).

 

 

3. Kumtazama aliye chini husaidia kukumbuka neema za Allaah (سبحانه وتعالى) na kushukuru kwa majaaliwa.

 

 

4. Haitakiwi kutamani kwa wivu na husda neema alizojaaliwa mwengine, bali ni kumshukuru na kumwomba Allaah (سبحانه وتعالى). Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَلَا تَتَمَنَّوْا مَا فَضَّلَ اللَّـهُ بِهِ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبُوا ۖ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبْنَ ۚوَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٣٢﴾

Wala msitamani ambayo Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wanayo sehemu katika waliyoyachuma, na wanawake wana sehemu katika waliyoyachuma. Na muombeni Allaah fadhila Zake. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa kila kitu. [An-Nisaa (4: 32)]

 

Rejea pia: An-Nahl (16: 71).

 

 

5. Kumtazama aliye juu hupelekea kukufuru neema za Allaah (سبحانه وتعالى).

 

 

 

 

 

 

 



Jumatano, 21 Oktoba 2020

Njia za uzazi wa mpango ndiyo chanzo kushuka umri na saratani ya matiti

Njia za uzazi wa mpango ndiyo chanzo kushuka umri na saratani ya matiti

Njia uzazi wa mpango chanzo kushuka umri saratani ya matiti – Daktari

Aveline Kitomary- Dar es salaam

DAKTARI bingwa wa saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Heleni Makwani, amesema moja ya sababu za umri wa wanawake wanaougua saratani ya matiti kuendelea kushuka, ni matumizi ya njia za uzazi wa mpango katika umri mdogo.

Takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo miaka 10 iliyopita zilieleza ongezeko la ugonjwa, lakini pia umri unaoathirika huku wagonjwa wakiongezeka kutoka 250/300 hadi 900 ikiwa ni mara tatu ya wagonjwa walioonwa katika kipindi cha miaka mitatu.

Licha ya hivyo, wastani wa umri wa waathirika kwa miaka 10 iliyopita ni miaka 64, lakini kwa sasa ni miaka 56, ikiwa ni miaka 7 chini ya umri wa kipindi cha nyuma.

Akizungumza na MTANZANIA wakati wa mahojiano maalumu Dar es Salaam jana, Dk. Makwani alisema sababu nyingine ya umri kushuka ni matumizi ya vyakula vya kusindikwa.

“Mabinti wengi sasa wanatumia vidonge na sindano kama njia ya kuzuia mimba, vidonge hivi na sindano vina vichocheo vya ‘estrogen’ ambayo huweza kusababisha uwezekano wa saratani ya matiti.

“Na ukizingatia hii ‘estrogen’ ni ‘artificial’ – si ya kutengenezwa na mwili, hivyo huongeza wingi wa kichocheo hiki ambao hauhitajiki mwilini na hivyo kwenda kuleta athari kwenye mwili kwa kutengeneza uvimbe ambao huchochewa haraka na ‘estrogen’.

“Wasichana wengi sasa hivi wanatumia dawa za dharura za kuzuia mimba baada ya kufanya mapenzi, hii ni hatari, kingine ni watoto wa kike kupenda zaidi kula vyakula vya kusindikwa, hii pia inaweza kusababisha upataji haraka wa saratani ya matiti,” alibainisha Dk. Makwani.

Alisema wasichana wengi wenye umri mdogo wanaoathirika zaidi ni wale wanaoishi maeneo ya mjini.

“Wasichana wa umri mdogo wakipata saratani ya matiti wana hatari kubwa zaidi kuliko wanawake wanaofikia kikomo cha uzazi,” alisema Dk. Makwani.

Alieleza kuwa hata hivyo uelewa wa jamii unaendelea kuongezeka kwa kadiri siku zinavyoenda kutokana na utoaji elimu kuhusu saratani ya matiti na saratani kwa ujumla.

“Watu wengi wanaelewa dalili mbalimbali na idadi ya wanaojitokeza mapema inaongezeka, watu wameanza kujigundua baada ya kujua dalili za mwanzo hivyo kufanya watu kuanza kuwahi hospitalini,” alisema Dk. Makwani.

Alishauri wasichana kutumia njia ya kitanzi kuliko njia za dawa na sindano ili kuweza kuepuka madhara.

Njia za uzazi wa mpango ndiyo chanzo kushuka umri na saratani ya matiti Click To Tweet
Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 2

Let's block ads! (Why?)

Jumanne, 20 Oktoba 2020

Faida 12 za Siagi ya Karanga

Faida 12 za Siagi ya Karanga

Siagi ya Karanga ni moja ya vitu mhimu jikoni katika nyumba nyingi siku hizi, inapendwa na kila mtu watoto na watu wazima.

Mimi napenda zaidi kuitumia kwenye mkate lakini pia unaweza kuongeza siagi ya karanga kwenye karibu kila mboga ya majani, samaki na kadharika.

Ukiacha radha yake nzuri na tamu, siagi ya karanga ni chakula chenye afya na nguvu nyingi na isiyo na takataka zozote zisizohitajika na mwili.

Kama wewe ni mtu unayependa kutumia vyakula vyenye afya basi hii siyo ya kukosa nyumbani kwako!

Faida 12 za Siagi ya Karanga 1

Faida 12 za Siagi ya Karanga

1. Hukufanya usijisikie njaa kwa muda mrefu

Ni jambo la afya kutumia Siagi ya karanga hasa katika mlo wako wa asubuhi kwa sababu itakufanya ujisikie umeshiba kwa masaa mengi zaidi.

Protini na faiba vilivyomo kwenye siagi ya karanga vinaweza kukupunguzia hamu ya kutaka kula vyakula vingine visivyo vya afya au vyakula feki kwa lugha nyepesi.

2. Bora kwa afya ya Moyo

Usawa wa mafuta yasababishayo kolesto ni mdogo sana ukilinganisha na usawa wa yale mafuta yasiyosababisha kolesto katika siagi ya karanga na hivyo kupunguza uwezekano wa mtu kupatwa na matatizo ya moyo.

Vitamini E ipatikanayo katika siagi ya karanga ni mhimu sana katika afya ya mfumo wako wa upumuwaji.

3. Siagi ina Mafuta safi

Watu wengi huogopa kutumia siagi ya karanga sababu ya kuwa na kiasi kingi cha mafuta. Lakini ukweli ni kuwa mafuta yaliyomo kwenye siagi ya karanga ni mafuta safi ‘healthy fats’.

Asilimia ya mafuta haya yasiyo na kolesto katika siagi ya karanga ni kubwa zaidi na hivyo unaweza kuitumia bila wasiwasi wowote.

4. Ina kiasi kingi cha faiba

Matumizi ya kiasi cha kutosha cha faiba ni mhimu kwa ajili ya ufanyaji kazi mzuri wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Siagi ya karanga ni chanzo kizuri kabisa cha faiba kwa ajili ya mwili.

5. Ina viinilishe vingi mhimu

Siagi ya karanga ina viinilishe vingi na ambavyo ni mhimu sana kwa mwili kama vile faiba, protini, potasiamu, kiuaji sumu, mafuta yenye afya, magnesium na vingine vingi.

Viinilishe hivi ni mhimu kwa ajili ya utengenezaji na uimarishaji wa mifupa, kuimarisha mishipa na kuimarisha kinga ya mwili.

6. Huongeza Nguvu

Siagi ya karanga ina kiasi kingi cha mafuta masafi yasiyoweza kusababisha kolesto/lehemu mwilini (unsaturated fats) na kiasi kingi cha protini, vitu hivi viwili vinafanya kazi ya kuongeza nguvu mwilini.

Siagi ya karanga ina kalori nyingi zitakazokuwezesha ubaki ni mwenye nguvu kutwa nzima.

7. Huzuia kuzeeka mapema

Kwenye siagi ya karanga kuna kitu kinaitwa kwa kitaalamu ‘resveratrol’.

Resveratrol ni kitu mhimu sana katika kuondoa sumu mwilini na hivyo kusaidia kuzuia kansa, matatizo ya moyo na kuzeeka mapema.

8. Husaidia katika mzunguko wa damu

Kwakuwa ni chanzo kizuri cha madini ya chuma, shaba, magnesium, na potasiamu, siagi ya karanga ni nzuri sana katika kuuweka katika usawa mzuri mzunguko wa damu mwilini.

9. Huzuia kansa

Uwezo wa siagi ya karanga katika kuondoa sumu mwilini huzuia matokeo ya matendo ya vijidudu nyemelezi vya magonjwa mwilini.

Wakati faiba kwa uwezo mkubwa husaidia katika kuondoa taka zingine katika mwili hasa kwenye utumbo mdogo na hivyo kuzuia kutokea kwa kansa ya utumbo mdogo.

10. Husaidia mmeng’enyo wa chakula

Siagi ya karanga ina kiasi maridhawa cha vitamin B-3 (Niacin) na manganese vitu ambavyo ni mhimu sana katika kuusaidia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vizuri zaidi.

Manganizi huvisisimua vimeng’enya mhimu ambavyo vinahusika katika uondowaji wa ammonia mbaya.

Manganizi pia huzilinda seli dhidi ya mfadhaiko wa kisakolojia. Niacin ni mhimu sana katika kukuwa na kuendelea kwa seli.

11. Hudhibiti damu sukari

Siagi ya karanga ni mhimu katika kuidhibiti na kuisawazisha damu sukari mwilini kwa sababu ya kiasi kingi cha protini na faiba kilichomo ndani yake.

12. Husaidia katika kujenga mishipa

Kadharika kiasi kingi cha protini kilichomo kwenye siagi ya karanga kinasadikika kuwa na uwezo wa kuongeza nguvu au uwezo wa mwili na kutengeneza nguvu za kiume

Kama unahitaji siagi ya karanga niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 2

Let's block ads! (Why?)

Jumapili, 11 Oktoba 2020

Magonjwa hatari 18 yanayotibika kwa kutumia mbegu za maboga

MAGONJWA HATARI 18 YANAYOTIBIKA KWA KUTUMIA MBEGU ZA MABOGA

Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini kama madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma.

Mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna kama mimi.

Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 18 yafuatayo:

1. UGONJWA WA MOYO

Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo.

Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo.

Mbegu hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wenye ugonjwa wa moyo yenye OMEGA 3.

2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI

Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zink ni kuimarisha kinga ya mwili.

Upungufu wa madini ya zink unaweza kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti, kuishiwa nguvu za kiume, matatizo ya homoni, chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo mengine kadhaa ya kimwili na kiakili.

3. HUONGEZA UWEZO WA MACHO KUONA

Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin, vitu hivi vinavyopatikana katika mbegu za maboga ni mhimu kwa ajili ya nuru ya macho.

Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa ‘melanin’ kimeng’enya mhimu ambacho hutengenezwa kwa asili na miili yetu kwa ajili ya ulinzi wa afya ya macho.

4. KINGA YA KISUKARI

Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoendelea kwa kasi kuwasumbua watu wengi kila pembe ya dunia.

Mbegu za maboga zina vitu vitatu mhimu zaidi ambavyo ni ‘Nicotinic acid’, ‘Trigonelline’ na ‘D-chiro-inositol’ ambavyo husaidia kushusha damu sukari mwilini na kudhibiti kazi za insulini hivyo kuwa kinga na kuleta ahueni kubwa kwa watu wenye kisukari.

Kama unasumbuliwa na kisukari fanya mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na unipe mrejesho hapa.

5. DAWA BORA KABISA YA USINGIZI

Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi.

Kwenye mbegu za maboga kuna vimeng’enya viwili mhimu zaidi ambavyo huhusika na usingizi na afya ya akili moja kwa moja navyo ni ‘L-tryptophan’ na ‘tryptophan’.

Gramu 100 tu za mbegu za maboga zina kiasi cha kutosha cha ‘tryptophan’ mpaka mg 576.

Tryptophan ndiyo inahusika kuleta usingizi wenye utulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress mwilini.

Kwa kuongezea mbegu za maboga zina kiasi kingi cha vitamini za kundi B.

Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi.

Kwahiyo kama una tatizo la kukosa usingizi jaribu kutumia mbegu za maboga na uniletee majibu hapa.

Kumbuka kukosa usingizi mara nyingi huwa ni matokeo ya msongo wa mawazo na kama ulivyoona mbegu hizi zinaondoa pia stress!

Kazi ni kwako ndugu.

6. DAWA BORA YA UVIMBE

Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini sambamba na uvimbe (inflammation).

Kama ujuavyo sehemu kubwa ya vivimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini.

Mbegu za maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara yoyote mabaya hapo baadaye.

Kama unasumbuliwa na uvimbe popote jaribu kutumia mbegu za maboga na utuletee majibu.

Mbegu za maboga pia ni dawa nzuri kwa aina nyingi za kansa mwilini.

7. HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA

Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokanayo na mimea isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama.

Pia zina OMEGA 3.

Mama mjamzito hata unayenyonyesha tumia mbegu za maboga na utakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto.

8. DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME

Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume.

Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini ambayo ni mhimu SANA kwa afya ya tezi dume na husaidia uponyaji wa tatizo la tezi dume moja kuwa kubwa kuliko nyingine tatizo lijukanalo kwa kitaalamu kama ‘benign prostatic hyperplasia’.

Wanaume kazi ni kwenu.

9. ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME

Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado.

Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume?

Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.

Lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili.

Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia

Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako.

Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count).

Ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukimwaga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga hizo.

Magonjwa hatari 18 yanayotibika kwa kutumia mbegu za maboga 1

Mbegu za maboga

10. ZINAONDOA PIA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)

Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi nini madhara ya msongo wa mawazo kiafya.

Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo utaona ni jinsi gani ilivyo mhimu kwako kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa na stress ni hatari zaidi kwa afya yako.

Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao (hormonal imbalance).

Hivyo kama una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti.

Mbegu za maboga zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho ‘tryptophan’ na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo kama ‘serotonin’.

Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa serotonin ni homoni inayohusika na kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mambo yanayohusu njaa.

11. HUZUIA MCHANGA KWENYE KIBOFU CHA MKOJO

Faida nyingine ya kushangaza kuhusu mbegu za maboga kiafya ni ule uwezo wake wa kuzuia mchanga au mawe kwenye kibofu cha mkojo.

Kinachofanya hili liwezekane kupitia mbegu hizi ni kule kuwa na kiasi kingi cha ‘phosphorous’ ambayo ni msaada mkubwa katika kuzuia mawe au mchanga kujilundika katika kibofu cha mkojo.

Pia unashauriwa kuwa unakunywa maji mengi kila siku ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili.

12. HUIMARISHA AFYA YA MIFUPA

Kadri umri unavyoongezeka ndivyo na uwezo na uimara wa mifupa yako unavyopungua.

Imefahamika sasa kuwa madini ya kalsiamu peke yake siyo kitu kinachoimarisha afya ya mifupa.

Kuna madini na vitamini vyngine mhimu ili kuimarisha afya ya mifupa.

Mbegu za maboga ni chanzo kizuri sana cha magnesiamu, Zinki, Vitamini K na viinilishe vingine vingi mhimu katika kuimarisha mifupa na hivyo kuzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).

13. ZINASAIDIA KUWEKA SAWA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU

Shinikizo la juu la damu ni moja magonjwa sababishi ya vifo kwa watu wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo.

Mbegu za maboga ni kitu mhimu kuongezwa katika mlo kwa watu wote wanaosumbuliwa na shinikizo la juu la damu.

Mbegu za maboga zina kiasi kidogo cha sodiamu na zina kiasi kingi cha potasiamu na magnesiamu vitu viwili mhimu katika kuweka sawa shinikizo la damu mwilini.

14. ZINAIMARISHA AFYA YA UBONGO

Kadri unavyoendelea kukua ndivyo na uwezo wa ubongo wako unavyopungua. Hata hivyo bado unayo nafasi ya kuzuia hilo kama utaishi na kula vizuri.

Mbegu za maboga asidi mafuta ya Omega 3 zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘alpha-linolenic acid’ ambazo ni mhimu sana katika kulinda na kustawisha afya ya ubongo.

Vyakula vyenye Omega-3 husaidia kupunguza kasi ya seli za ubongo kuzeeka wakati huo huo vikizuia uharibifu wa seli za ubongo kutokana na vijidudu nyemelezi katika ubongo.

15. ZINAWEKA SAWA Ph YA MWILI

Mwili unaweza kuwa katika hali mbili, ama katika asidi au katika alkaline (Ph). Mwili unapokuwa na asidi nyingi ndipo unapopatwa na magonjwa mengi kirahisi zaidi.

Magonjwa hayo ni pamoja na maumivu ya mifupa, saratani, kisukari, vidonda vya tumbo, kichwa kuuma nk

Hivyo ni mhimu chakula chako kiwe kwa sehemu kubwa ni chakula chenye alkalini na si asidi (tindikali) ili kukusaidia ubaki na Ph (Potential Hydrogen) ya 7.4 mara nyingi.

Kumbuka chochote chini ya 7 Ph ni asidi.

Mbegu za maboga ni moja ya vyakula vizuri zaidi vyenye alkalini ambavyo unatakiwa kuvijumuisha kwenye mlo wako.

16. ZINATIBU TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU

Mbegu za maboga ni chanzo kizuri cha madini ya chuma hivyo kuwa msaada kwa watu wanaosumbuliwa na upungufu wa damu unaosababishwa na kupungua kwa madini ya chuma.

Tafiti zinasema kula vyakula vyenye madini ya chuma kila mara kunasaidia kuongeza madini ya chuma kwa watoto, vijana, wanawake wanaonyenyesha na kwa wamama wajawazito.

Hili linazifanya mbegu hizi kuwa msaada mkubwa kwa wale wanaopata tatizo la upungufu wa damu unaotokana na kupungua kwa madini ya chuma mwilini.

17. ZINASAIDIA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI

Weka pembeni vyakula vyenye sukari nyingi na badala yake tafuna mbegu za maboga.

Kinachotokea hapa ni kuwa mbegu hizi zinao uwezo wa kukuacha ukijisikia umeshiba kwa kipindi kirefu na hivyo kukuondolea hamu ya kutaka kula vyakula vingine feki.

Nyuzi nyuzi nyingi katika mbegu hizi zinazifanya kuwa chakula kizuri kuongezwa kwenye chakula chako cha asubuhi.

Hata hivyo sababu zina protini nyingi iwapo utazidisha kula unaweza kuongezeka uzito na unene badala ya kupungua hivyo uwe makini.

18. ZINARAHISISHA UPONYAJI WA VIDONDA

Mbegu za maboga pia ni msaada mkubwa kwa watu wenye vidonda kwa kuwa zinafanya kazi ya kuponya vidonda kuwa rahisi zaidi sababu zina vitamini A na madini ya zinki kwa wingi.

Kiais kingi cha vitamini A kwenye mbegu za maboga kinaweza kuwa msaada kuhamasisha uponyaji wa vidonda kwa mjibu utafiti mmoja uliofanywa na jarida moja la chuo cha afya ya ngozi nchini Marekani ‘Journal of the American Academy of Dermatology’.

Kwa mjibu wa utafiti, vitamini A ndani ya mwili inaweza kuvutia mfumo wa mwili kujiripea wenyewe ndani kwa ndani bila kuhitaji dawa.

Kama unasumbuliwa na vidonda au kidonda kwa muda mrefu hebu weka mazoea ya kutumia mbegu za maboga mara kwa mara na hutachelewa kuona uponyaji ukifanyika.

Hii ni kweli ukizingatia pia mbegu hizi zinaongeza sana kinga ya mwili.

Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku zao na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi.

Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.

Namna nzuri ya kula mbegu za maboga:

Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 5 hivi na huwa nazichanganya na chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.

Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.

Unaweza pia kuzisaga na mashine maalumu au kuzitwanga katika kinu na utapata unga wake na utumie vijiko vikubwa viwili kutwa mara 1 kwenye kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au katika uji.

Unaweza pia kuchanganya kwenye unga wa lishe wa mtoto

Kama unahitaji mbegu za maboga zilizokaangwa tayari kwa matumizi au ikiwa unahitaji unga wa mbegu za maboga niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175, naweza kukuletea ulipo kwa Dar bila gharama ya nauli, natuma pia mikoani.

Mbegu za maboga ninazouza mimi ninaziandaa kwa usafi wa hali ya juu kabisa na ninazikaanga kidogo sana ili kutopunguza viinilishe vyake na ninaziongezea kidogo chumvi ya mawe ya baharini.

Magonjwa hatari 18 yanayotibika kwa kutumia mbegu za maboga Click To Tweet

Share post hii na wengine uwapendao

Fadhili Paulo
Latest posts by Fadhili Paulo (see all)
Imesomwa mara 23

Let's block ads! (Why?)

Alhamisi, 8 Oktoba 2020

024-Aayah Na Mafunzo: Haramisho La Ndoa Ya Mut’ah

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Haramisho La Ndoa Ya Mut’ah

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

  وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ فَمَا اسْتَمْتَعْتُم بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَاضَيْتُم بِهِ مِن بَعْدِ الْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٢٤﴾

24. Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni shariy’ah ya Allaah kwenu. Na mmehalalishiwa wengineo wasiokuwa hao, mtafute (kuwaoa) kwa mali zenu mkijistahi pasi na kuzini. Basi mliostarehe nao, wapeni mahari yao kuwa ni waajib. Na wala si dhambi kwenu katika mliyoridhiana baada ya yaliyowajibika. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

Mafunzo:

 

Uharamisho wa ndoa ya mut’ah: Sabrah bin Ma’bad Al-Juhniy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba baba yake aliandamana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Fat-hi Makkah akasema: “Enyi watu! Nilikuruhusuni ndoa ya mut’ah hapo mwanzo. Leo Allaah Ameiharamisha mpaka Siku ya Qiyaamah! Basi ikiwa kuna yeyote ambaye ana mke wa ndoa ya mut’ah amwache na wala asichukue chochote katika alichompa.” [Muslim na wengineo].

 

 

 



059-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Israa: Na Hakuna Kinachotuzuia Kuleta Aayaat (Muujiza) Isipokuwa...

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 017-Asbaab Nuzuwl Suwrah Al-Israa Aayah 59

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَمَا مَنَعَنَا أَن نُّرْسِلَ بِالْآيَاتِ إِلَّا أَن كَذَّبَ بِهَا الْأَوَّلُونَ ۚ وَآتَيْنَا ثَمُودَ النَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُوا بِهَا ۚ وَمَا نُرْسِلُ بِالْآيَاتِ إِلَّا تَخْوِيفًا ﴿٥٩﴾

Na hakuna kinachotuzuia kuleta Aayaat (muujiza) isipokuwa ni kuwa watu wa awali waliikadhibisha. Na Tuliwapa kina Thamuwd ngamia jike kuwa dalili dhahiri lakini wakamdhulumu. Na Hatupeleki Aayaat (miujiza, maonyo) isipokuwa kwa ajili ya kukhofisha. [Al-Israa: 59]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

عَنْ اِبْن عَبَّاس  قَالَ : سَأَلَ أَهْل مَكَّة النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَجْعَل لَهُمْ الصَّفَا ذَهَبًا، وَأَنْ يُنَحِّي عَنْهُمْ الْجِبَال، فَيَزْرَعُوا، فَقِيلَ لَهُ : إِنْ شِئْت أَنْ نَسْتَأْنِي بِهِمْ لَعَلَّنَا نَجَتْنِي مِنْهُمْ، وَإِنْ شِئْت أَنْ نُؤْتِيهِمْ الَّذِي سَأَلُوا، فَإِنْ كَفَرُوا أُهْلِكُوا كَمَا أُهْلِكَ مَنْ قَبْلهمْ، قَالَ : "بَلْ تَسْتَأْتِي بِهِمْ  " فَأَنْزَلَ اللَّه وَمَا مَنَعَنَا أَنْ نُرْسِل بِالْآيَاتِ إِلَّا أَنْ كَذَّبَ بِهَا الْأَوَّلُونَ وَآتَيْنَا ثَمُود النَّاقَة مُبْصِرَة

 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas amesema: Watu wa Makkah wamemtaka Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  awajaalie  jabali la Swafaa liwe dhahabu na majabali yote yatoweke ili wapate kulima  (badala yake katika ardhi hiyo). Akaambiwa: “Ima tuwavumilie kwa wema na tuwape muda zaidi au ukitaka tuwape waliyoyataka, kisha wakikufuru waangamizwe kama walivyoangamizwa wa kabla yao.”  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Bali wavumilieni kwa wema na wapeni muda zaidi.” Hapo Allaah (عز وجل) Akateremsha:

 

 وَمَا مَنَعَنَا أَن نُّرْسِلَ بِالْآيَاتِ إِلَّا أَن كَذَّبَ بِهَا الْأَوَّلُونَ ۚ وَآتَيْنَا ثَمُودَ النَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُوا بِهَا ۚ وَمَا نُرْسِلُ بِالْآيَاتِ إِلَّا تَخْوِيفًا ﴿٥٩﴾

Na hakuna kinachotuzuia kuleta Aayaat (muujiza) isipokuwa ni kuwa watu wa awali waliikadhibisha. Na Tuliwapa kina Thamuwd ngamia jike kuwa dalili dhahiri lakini wakamdhulumu. Na Hatupeleki Aayaat (miujiza, maonyo) isipokuwa kwa ajili ya kukhofisha.

[Imaam Ahmad, Ibn Jariyr, Al-Haakim]

 

 



055-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Matendo Ya Aliyeneemeshwa Na Aliye Na Shida Duniani Ndiyo Yenye Kuzingatiwa Aakhirah

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 55

Matendo Ya Aliyeneemeshwa Na Aliye Na Shida Duniani

Ndiyo Yenye Kuzingatiwa Aakhirah

Alhidaaya.com

 

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((يُؤْتَى بِأَنْعَمِ أَهْلِ الدُّنْيَا مِنْ أَهْلِ النَّارِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، فَيُصْبَغُ فِي النَّارِ صَبْغَةً ثُمَّ يُقَالُ: يَا ابْنَ آدَمَ! هَلْ رَأَيْتَ خَيْرًا قَطُّ؟ هَلْ مَرَّ بِكَ نَعِيمٌ قَطُّ؟ فَيَقُولُ لاَ وَاللَّهِ يَا رَبِّ! وَيُؤْتَى بِأَشَدِّ النَّاسِ بُؤْسًا فِي الدُّنْيَا مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ، فَيُصْبَغُ صَبْغَةً فِي الْجَنَّةِ، فَيُقَالُ لَهُ: يَا ابْنَ آدَمَ! هَلْ رَأَيْتَ بُؤْسًا قَطُّ؟ هَلْ مَرَّ بِكَ شِدَّةٌ قَطُّ؟ فَيَقُولُ لاَ وَاللَّهِ يَا رَبِّ مَا مَرَّ بِي بُؤْسٌ قَطُّ ولاَ رَأَيْتُ شِدَّةً قَطُّ)) مسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Siku ya Qiyaamah ataletwa mtu wa motoni katika watu wa dunia aliyeneemeshwa neema nyingi mno, ataingizwa motoni kidogo kisha atatolewa: Ataulizwa: Ee mwana Aadam!  Je, umeona kheri yoyote? Ushawahi kuneemeka aslan? Atajibu: Hapana Wa-Allaahi Rabb wangu! Na ataletwa mtu aliyekuwa ana shida mno duniani katika watu wa Jannah. Ataingizwa Jannah kidogo kisha atatolewa. Ataulizwa: Ee mwana Aadam! Je, umeona shida yoyote? Ushawahi kutaabika aslan? Atajibu: Hapana Wa-Allaahi Rabb wangu! Haikunipitia shida yoyote abadan, wala sikuona taabu yoyote abadan)). [Muslim]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

1. Bishara kwa Muumin masikini kuhusu neema za Jannah yenye kudumu.

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ هُمْ خَيْرُ الْبَرِيَّةِ ﴿٧﴾

Hakika wale walioamini na wakatenda mema, hao ndio wema kabisa wa viumbe.

 

 

جَزَاؤُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًاۖ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ رَبَّهُ ﴿٨﴾

Jazaa yao iko kwa Rabb wao; Jannaat za kudumu milele zipitazo chini yake mito ni wenye kudumu humo abadi. Allaah Ataridhika nao, nao wataridhika Naye; hayo ni kwa yule anayemkhofu Rabb wake.  [Al-Bayyinah (98: 7-8)]

 

 

Rejea pia: Aal-‘Imraan (2: 14-15), At-Tawbah (9: 20-22) (72), Huwd (11: 108), Az-Zukhruf (43: 33-35).

 

 

2. Onyo kwa kafiri au muovu aliyetajiri kwamba Aakhirah kuna adhabu ya kudumu.

 

Rejea: An-Nahl (16: 117), Aal-‘Imraan (3: 197), Luqmaan (31: 23-24).

 

 

3. Aliye na shida, dhiki na taabu yoyote duniani, ni bishara kwake avute subira na atende mema apate starehe ya milele Aakhirah, kwani maisha ya dunia si lolote si chochote. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 وَمَا هَـٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ ۚ وَإِنَّ الدَّارَ الْآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٦٤﴾

Na huu uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni pumbao na mchezo; na hakika Nyumba ya Aakhirah bila shaka hiyo ndiyo yenye uhai wa kweli hasa (wa milele), lau wangelikuwa wanajua! [Al-‘Ankabuwt (29: 64)].

 

 

 4. Funzo kwa mtu muovu aliye na mali, utajiri, na ukwasi kwamba starehe yake na mali haitamfaa kitu au kumuokoa na moto. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ ﴿٨٨﴾

 “Siku hayatofaa mali wa watoto.

 

إِلَّا مَنْ أَتَى اللَّـهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ ﴿٨٩﴾

 “Isipokuwa yule atakayemfikia Allaah na moyo uliosalimika. [Ash-Shu’araa (26: 88-89)].

 

 

Rejea pia: Aal-’Imraan (3: 91), Al-Maaidah (5: 36), Al-Kahf (18: 46).

 

 

5. Maisha ya dunia si lolote si chochote, bali ni starehe ya muda tu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

اعْلَمُوا أَنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَزِينَةٌ وَتَفَاخُرٌ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ ۖ كَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ الْكُفَّارَ نَبَاتُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَكُونُ حُطَامًا ۖ وَفِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٌ ۚ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿٢٠﴾

Jueni kwamba uhai wa dunia ni mchezo na pumbao na mapambo, na kufakharishana baina yenu na kushindana kukithiri katika mali na watoto; ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha yananyweya, basi utayaona yamepiga manjano, kisha yanakuwa mabua yaliyonyauka na kupondekapondeka.  Na Aakhirah kuna adhabu kali, na maghfirah kutoka kwa Allaah na radhi. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni sterehe fupi za kughuri. [Al-Hadiyd (57: 20)]

 

Rejea pia: Aal-‘Imraan (3: 185), Ar-Ra’d (13: 26)].

 

 

6. Muumin ajitahidi kuchuma mema apate Jannah ya Neema na raha tupu.

 

 

7. Umasikini na utajiri duniani ni mtihani tu kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى), hivyo mwana Aadam asidanganyike na maisha yake.

 

 



20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...