Translate

Jumanne, 26 Mei 2020

Vyakula vitano vinavyoua nguvu zako za kiume bila wewe kujuwa

VYAKULA VITANO VINAVYOUA NGUVU ZAKO ZA KIUME BILA WEWE KUJUWA

Ulivyo ni kile unachokula na kunywa kila siku.

You are what you eat.

Kama unakula takataka utakuwa takataka na kama unakula vyakula vya afya basi utakuwa afya.

Hakuna upendeleo katika hili!

Kama hujuwi nguvu za kiume ni kitu gani hasa bonyeza kwanza hapa.

Chakula unachokula kina uhusiano wa moja kwa moja na afya yako ya kitandani.

Kwa bahati mbaya wanaume wengi hawajuwi wale nini na wengine hudhani ukiwa na hela basi unatakiwa kula vyakula kwenye mahotel ya kifahari au kula nyama kila siku!

Vyakula vitano vinavyoua nguvu zako za kiume bila wewe kujuwa 1

Vyakula vitano vinavyoua nguvu zako za kiume bila wewe kujuwa;

1. Vilevi

Glasi moja ya mvinyo mwekundu kwa siku inaweza kukusaidia kuimarisha nguvu zako za kiume. Kumbuka nimesema glasi moja kwa siku.

Mwanzoni unapoanza kuwa mlevi unaweza kuhisi kama vile nguvu zako zinaongezeka au unakuwa imara Zaidi lakini kadri unavyoendelea kuwa mlevi ndivyo utakavyopoteza nguvu zako na hamu yako ya kutaka kuhiriki tendo la ndoa.

Pombe inaweza kukuondolea aibu ya kutongoza na ukajikuta umetongoza yoyote hasa wauza bar (bar meds).

Lakini kunywa pombe kupita kiasi kunahusishwa na kushuka kwa homoni ya testosterone na kuiondoa hii homoni kwenye mzunguko wako wa damu na hata kushusha kiwango chake cha uzalishwaji katika mwili.

Pombe pia ikitumika kupita kiasi na kila siku inao uwezo mkubwa wa kulidhuru ini lako.

Ini ni ogani mhimu ili kuondoa sumu mwilini na linapochakaa hivi sababu ya pombe ni vigumu wewe kuendelea kuwa na nguvu za kiume.

Ini pia linahusika na kuziweka sawa homoni mwilini hasa homoni ya estrogen na homoni nyingine iitwayo phytoestrogens ambayo ni estrogen itokanayo na mimea imo kwenye vitu vinavyotumika kutengeneza bia.

Sigara na bangi ni vilevi vingine vinavyoweza kukuletea upungufu wa nguvu za kiume.

Moshi wa sigara na bangi huziba mishipa yako ya damu na kukusababishia mtiririko mbovu wa damu.

Moshi wa sigara na bangi ni sumu katika mwili.

Sumu yoyote lazima ikuletee kushuka kwa nguvu za kiume.

Sumu yoyote lazima ikuletee kushuka kwa nguvu za kiume Click To Tweet

Sigara kwa mfano zimeandikwa kabisa kwenye boksi lake kwamba ni hatari kwa afya yako kwahiyo naomba usinipotezee muda kueleza kuhusu madhara ya sigara kwani yanajulikana na kila mtu.

Kadharika na madawa mengine yote ya kulevya.

Mwanzoni mwa kutumia hivi vilevi unaweza usione madhara au shida yoyote na pengine unaweza kuona faida katika tendo la ndoa ila kadri siku zinavyoenda utakuja kunitafuta nikupe Msamitu.

Sukari ipo karibu kila sehemu na ni vigumu kuipeuka. Ni vigumu umalize siku hujala au kunywa kitu chenye sukari ndani yake!

Sukari ina kawaida ya kuongeza usawa wa homoni iitwayo insulini ambayo inaweza kukusababishia yafuatayo;

a) Mwili wako kuhifadhi mafuta hasa tumboni na kukuletea kitambi,
b) Kisukari,
c) Kupunguza wingi na uimara wa mishipa na
d) Kushusha kiwango cha homoni mhimu katika tendo la ndoa homoni iitwayo testosterone.

Kwa wanaume mafuta yakijaa tumboni yaani ukianza kuwa na kitambi husababisha kuongezeka zaidi kwa homoni nyingine iitwayo estrogen ambayo yenyewe inapozidi kiwango kuliko inavyohitajika huleta tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na mwanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa.

Ni mhimu kwamba unaiondoa sukari kwenye orodha ya vyakula unavyokula kila siku ili kuimarisha nguvu zako za mwili na za kiume kwa ujumla.

Nini mbadala wa sukari?

Kuna mtu anauliza.

Jibu ni asali.

Tumia asali kwenye chochote kinachohitaji sukari na utakuwa na nguvu za kutosha kila siku.

3. Vyakula vya kwenye makopo

Unahimizwa kuendelea kupenda kula vyakula vya asili zaidi na vilivyopikwa nyumbani.

Vyakula vya kwenye makopo yaani vyakula vya dukani au viwandani vingi vina sodium nyingi zaidi ya mwili wako unavyohitaji.

Sodium nyingi husababisha shinikizo la juu la damu na kushuka kwa mtiririko mzuri wa damu sehemu mbali mbali za viungo vya mwili wako.

Baadhi ya vyakula hivyo ni pamoja na juisi zote za viwandani, soda zote, soseji, jibini(cheese), strawberry, tomato sauce, chill sauce, mkate mweupe nk

4. Vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi

Vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (Fried foods) ni vyakula hatari kwa afya ya moyo na afya ya kitandani kwa ujumla.

Hapa shida siyo chakula bali mbinu inayotumika kupika hicho chakula.

Mafuta haya yanayotumika kupika hivi vyakula yanapopata moto yaani yanapounguzwa ili kupika chakula hubadilika na kuwa moja ya mafuta mabaya kabisa kwa afya yako hasa kwa afya ya moyo, saratani na kolesto.

Vyakula hivi pia hupelekea mwili kuongeza uzito na unene kwa haraka sana.

Uzito ukizidi ni rahisi homoni zako kuvurugika na kushuka kwa nguvu za kiume.

Vyakula hivi huziba ateri na mishipa ya damu na kukusababishia damu kutoweza kutiririka kwa uhuru wote kwenda sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kwenye uume wako.

Ili uendelee kuwa na nguvu za kiume utatakiwa kuacha kula vyakula kama chipsi, maandazi na chakula kingine chochote kinachopikwa kwa staili hii ya kuwekwa katikati ya mafuta mengi.

Chipsi hasa za vibandani ni hatari zaidi kuliko hata zile za nyumbani.

Kwenye vibanda vya chipsi mafuta hayabadilishwi hata yawe na rangi gani, yakipungua wananunua mengine na kuongeza juu ya yale yaliyotumika kupika jana na juzi.

Ukichunguza vyombo wanavyopikia hizo chipsi utaona ndani na nje havina tofauti, ndani vyeusi na nje vyeusi pia!

Unaweza kula chipsi mara moja moja hasa nyumbani na mafuta yakishatumika kupikia mara moja yamwagwe yasirudiwe au kuchanganywa mapya na yaliyotumika kabla.

Ukiweza acha kabisa kula chipsi kwa ajili ya kuwa na nguvu za kiume za kutosha na kuepuka saratani ikiwemo saratani ya tezi dume.

5. Vinywaji vyenye kaffeina

Hivi ni vinywaji vinapotumika kwa kiasi vinaweza kuamsha nguvu na hali yako ya kutaka kushiriki tendo la ndoa lakini vinapozidi kiasi hukuletea tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Hivi ni pamoja na chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi zote, energy drinks zote, chokoleti, kokoa nk.

Kikombe kimoja cha kahawa kwa siku hakina ubaya wowote ila ikizidi utanitafuta nikupe Msamitu.

Kaffeina ni kikojoshi (diuretic), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili.

Ukinywa kikombe kimoja cha kahawa tegemea kwenda chooni muda mchache tangu unywe na kutoa mkojo wa ujazo wa vikombe viwili.

Kaffeina ni dawa mojawapo ya kulevya kundi la madawa ya kulevya ya kusisimua (stimulant drugs).

Ndiyo maana ni vigumu sana mtu kuacha kahawa – ni kwa sababu ni dawa ya kulevya pia.

Hata mtu aliyezoea kunywa chai ya rangi kwa miaka mingi siku asipokunywa huona kichwa kinamuuma!

Kaffeina inaweza kukuletea hali ya kuongezeka kwa hamaki katika mwili wako na hamaki ni jambo linaloweza kudhuru nguvu zako za kiume.

Vyakula vingine vinavyoharibu nguvu za kiume ni pamoja na vyakula au bidhaa zitokanazo na soya, viazi pori (beet roots), flaxseed products, dawa za kuongeza nguvu za kiume za kizungu (viagra, cupid, na vidonge vingine vya namna hii), mnanaa (minti), licorice, samaki wa kufugwa, kuku wa kisasa na mayai ya kisasa, popcorn (bisi) nk

Na kuna vingine sitavitaja ili kutoleta taharuki maana kuna vingine ukiambiwa hutaamini bali hivyo kwanza nahisi vinakutosha.

Ikiwa unahitaji dawa ya asili isiyo na madhara kwa ajili ya kuimarisha nguvu zako za kiume niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Vyakula vitano vinavyoua nguvu zako za kiume bila wewe kujuwa Click To Tweet

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

Imesomwa mara 11

Let's block ads! (Why?)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...