Usizidharau ishara hizi 8 za mwanzo za kisukari
Kisukari kinaweza kujijenga pole pole katika mwili wako wakati mwingine bila hata wewe kufahamu nini kinaendelea.
Ni mhimu kwamba unapata elimu hii ya kuzitambuwa dalili za mwanzo za ugonjwa huu mbaya unaotesa mamilioni ya watu kote duniani ili uweze kuudhibiti kabla haijawa shida.
Hakuna dawa ya hospitali ya kuponya ugonjwa huu mpaka sasa. Wagonjwa hulazimika kutumia dawa za kupunguza makali kila siku miaka yao yote na dawa hizo hazitolewi bure.
Hizi ni ishara 8 za mwanzo za kukutokea ugonjwa kisukari aina ya pili.
Ikiwa unatokewa na dalili 2 au 3 au hata zaidi kati ya hizi ni wakati muafaka kufanya kipimo cha kisukari na kuchukuwa hatua za kujikinga kabla hali haijawa mbaya.
Soma hii pia > Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili
Usizidharau ishara hizi 8 za mwanzo za kisukari
1. Kuongezeka kwa kiu
Ukiwa na sukari nyingi kwenye mzunguko wako wa damu inamaanisha figo zako zitalazimishwa kufanya kazi zaidi ya kuchuja hiyo sukari.
Kiwango hicho cha juu cha sukari kwenye damu kinaweza kuzipa kazi za ziada figo na kukusababishia wewe kukojoa mara nyingi ili kuiondoa sukari iliyozidi mwilini.
Matokeo yake ni kuwa utapatwa na kiu iliyozidi kawaida na unaweza ukapungukiwa maji siku nzima.
Ikiwa unajisikia kupatwa na kiu mara kwa mara hata kama unakunywa maji mengi jaribu kupunguza kiasi cha sukari kwenye vyakula vyako na umuone daktari kwa uchunguzi zaidi.
2. Kukojoa mara kwa mara
Kiu iliyozidi na kukojoa mara kwa mara ni vitu vinavyoenda pamoja linapokuja suala la dalili za mwanzo za kisukari.
Sukari iliyozidi kwenye mzunguko wako wa damu ambayo haiwezi kuchujwa na figo hulazimishwa kutoka nje kupitia mkojo.
Kukojoa mara kwa mara wakati wa mchana hata nyakati za usiku ni dalili za ukaidi wa insulini.
3. Uchovu usioisha
Kisukari huleta uchovu kwa namna mbili.
Namna ya kwanza kisukari huleta uchovu ni matokeo ya upungufu wa maji mwilini kitendo ambacho huleta uchovu sugu.
Namna ya pili kisukari huingilia na kuathiri namna mwili wako unavyotumia damu sukari (glukozi) kwa ajili ya kutengeneza nguvu ya mwili.
Uchovu usioisha hata baada ya kuwa umepata usingizi mzuri usiku ni moja kati ya ishara kuu za mwanzo za wewe kuanza kupatwa na ugonjwa wa Kisukari.
4. Kuchelewa kupona vidonda
Ikikutokea ukapatwa na kidonda sehemu yoyote ya mwili unaweza kuona unachelewa sana kupona tofauti na wengine nah ii ni ishara pia ya mwanzo ya ugonjwa wa Kisukari.
Sukari inapozidi mwilini huishusha kinga yako ya mwili na hivyo mwili kuwa na uwezo mdogo wa kujitibu.
Hii ndiyo sababu unapotaka kuongeza kinga yako ya mwili unashauriwa pia uache kunywa soda na juisi zote za dukani na upunguze pia matumizi ya sukari.
Watu wengi wanaoumwa kisukari wanaumwa pia shinikizo la juu la damu.
Shinikizo la juu la damu ni ugonjwa ambao husababisha mishipa ya damu kujikaza au kujipunguza ukubwa wa kipenyo chake kama matokeo ya kupungua kwa mzunguko wa kimiminika mwilini jambo ambalo hufanya uponyaji wa vidonda kuchukuwa muda mrefu.
5. Kupungua kwa uwezo wa macho kuona
Kisukari kitakuweka kwenye njia panda linapokuja suala la uwezo wa macho yako.
Kwa vile shinikizo la juu la damu linaweza kudhuru mishipa ya damu basi mishipa hiyo baadhi yake ndiyo hupeleka damu kwenye macho na kudhurika kwa mishipa hiyo maana yake macho hayawezi kupata viinilishe mhimu kwa ajili yaw ewe uweze kuona vizuri.
Kwahiyo kutoona vizuri, uwezo wa macho kuona kupungua, kuona maluweluwe, kuona vitu viwili katika kimoja, kutoona mbali, mtoto wa jicho na kadharika ni matatizo ya macho ambayo ni dalili za mwanzo za kisukari usizotakiwa kuzipuuza.
Ikiwa umeanza kuona matatizo kwenye uwezo wako wa macho inafaa uonane na daktari haraka kwa uchunguzi zaidi ili kuzuia kuendelea zaidi kwa kisukari mwilini mwako.
Kwa bahati nzuri ni kuwa unapochukuwa hatua za mapema kuzuia, kujikinga na kutibu kisukari unakuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia matatizo ya kuona yanayoweza kupelekea upofu na kuweka sawa usawa wa sukari mwilini mwako.
6. Kubadilika kwa mudi yako
Insulini ni homoni ambayo inafanana kazi zake na homoni zingine kama estrogen, testosterone, na homoni zinazoshugulika na masuala ya njaa (leptin and ghrelin).
Wakati mwili wako unapoacha kutengeneza au kutumia insulini kama inavyotakiwa homoni zako zinaweza kuvurugika na kukuletea mabadiliko ya namna unavyojisikia (mood wings), kujisikia vibaya, kukuletea msongo wa mawazo nk
Ikiwa utaanza kula vizuri, kuwa bize na mazoezi na kudhibiti sukari yako kwa dawa lishe au mitishamba ambazo ni rafiki kwa afya utaanza kuona hali yako ya kujisikia vibaya au tofauti na ulivyokuwa mwanzo inatulia na unarudi kuwa mtu wa kawaida pole pole.
7. Ganzi sehemu mbalimbali mwilini
Ganzi miguuni, mikononi, miguu kuwaka moto na kuchoma choma ni dalili za mwanzo za kisukari.
Watu wanaosumbuliwa na kisukari mara nyingi hupatwa na ganzi.
Ni ishara mishipa yako ya damu haiwasiliani sawa sawa kama mwanzo. Ni ishara sumu na asidi vimezidi mwilini kama matokeo ya sukari kuzidi.
Ikiwa ganzi ni shida katika mwili wako jaribu kufanya kipimo cha kisukari mapema.
Soma hii pia > Dawa ya kuondoa ganzi mwilini
8. Kupenda vyakula na vinywaji vitamu
Kisukari kinaweza kukuletea hamu au kiu ya kutaka kula au kunywa vitu vitamu vitamu kutokana na sababu mbalimbali.
Kwa mfano msongo wa mawazo na kubadilika kwa mudi yako kama matokeo ya kuvurugika kwa homoni zako kunaweza kukupelekea wewe kupenda vitu vitamu kama soda, chokoleti, pipi nk
Jambo hilo hilo la kuvurugika kwa homoni zako linaweza pia kuvuruga homoni yako inayohusika na masuala ya njaa na kukuletea wewe hamu ya kupenda zaidi kula vyakula feki kama chipsi na vyakula vingine vya kwenye makopo (vya dukani na viwandani).
Vile vile ukaidi wa insulini (insulin resistance) kama matokeo ya kisukari unaweza kukuletea wewe tamaa ya kutaka kula kupita kiasi vyakula vya wanga na vyenye utamu ambavyo haraka sana vitapandisha kiasi cha sukari mwilini mwako.
Ikiwa umekuwa unapata hamu sana ya kutaka kula au kunywa vyakula na vinywaji vitamu siku za karibuni nakushauri uweke miadi (appointment) ya kuonana na daktari haraka iwezekanavyo kufanya uchunguzi juu ya uwezekano wa wewe kuwa na kisukari.
Uonapo dalili hizo usizichukulie poa. Chukua hatua mapema kabla hali haijawa mbaya Zaidi.
Ikiwa utahitaji dawa ya asili kwa ajili kutibu kabisa kisukari hasa kisukari aina ya pili, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175
Mimi napatikana Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke. Kama upo Dar Es Salaam
Soma na hii pia > Madhara zaidi ya Kisukari katika mwili
Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;
Usizidharau ishara hizi 8 za mwanzo za kisukari Click To TweetTafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni