Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume
Una elimu au uelewa wa kiasi gani kuhusu mbegu za kiume yaani shahawa?
Kuna uwezekano mkubwa hujawahi kuwa na muda wowote wa kupeleleza au kujifunza mengi kuhusu mbegu zako.
Kama hujawahi kupata shida kutungisha mimba unaweza usiwaze lolote kuhusu mbegu zako na ukaendelea kuzichukulia poa kila siku.
Soma hii pia > Vidonda vya tumbo husababisha upungufu wa nguvu za kiume
Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume
1. Ni nyingi sana
Bao moja linakuwa na mbegu karibu milioni 200 na lina ujazo wa karibu nusu kijiko cha chai.
Kama utazipanga kwa kufuatana mbegu za mshindo mmoja (bao) zinaweza kuchukuwa umbali wa kilomita 9.
Kitu kingine cha kweli na cha kushangaza kuhusu wingi wa mbegu za kiume ni kuwa zimekuwa zikipunguwa kwa wanaume wa viazi vyote mwaka hadi mwaka.
Yaani kama mwanaume wa mwaka 1990 alikuwa na jumla ya mbegu milioni 500 kwa mfano basi kuna uwezekano mkubwa mwanaume wa mwaka 2020 akawa na jumla ya mbegu milioni 450.
Tafiti za hivi karibuni zinataja mambo ya mabadiliko ya mazingira na tabia ya mwanadamu ndiyo vinahusika na kushuka kwa karibu asilimia 50 ya ujazo, wingi na ubora wa mbegu za wanaume katika kipindi cha miongo minne iliyopita.
2. Zina safari ndefu zinapoingia kwa mwanamke
Mbegu za kiume zina safari ndefu sana zinapoingia katika via vya uzazi vya mwanamke.
Kwanza kabisa huingia kwenye mlango wa kizazi (cervix), kasha kwenye mji wa mimba (uterus), na kisha husafiri kupitia mirija ya mayai (fallopian tubes) mpaka kulifikia yai la mwanamke linalosubiri kurutubishwa.
Mbegu chache sana huendelea kuwa hai katika safari hiyo ndefu, nyingi hufa njiani na nyingine huamua kulala au kupumzika njiani na inahitajika mbegu 1 tu katika mbegu milioni 200 anazokojoa mwanaume ili kurutubisha yai na kutunga mimba.
Kuna wakati huwa nakutana na wanaume hata wanawake ninapochat nao WhatsApp huniambia mara tu wakikojoa huona mbegu zao zikitoka nje ya uke kwahiyo wana wasiwasi huenda ndiyo sababu hawapati mtoto!
Kwa faida ya wengi niseme hapa kuwa mbegu za mwanaume hazina sehemu ya kuhifadhiwa katika uke wa mwanamke.
Kama hazijatunga mimba ambapo ni mbegu 1 tu inahitajika katika hizo milioni 200 nyingine zote lazima zitoke
Ndiyo maana ukishiriki tendo la ndoa utaona mkimaliza mwanamke lazima ataenda bafuni kujisafisha sababu lazima zitolewe nje.
Hata kama hataenda bafuni maalumu kwa ajili hiyo, bado wakati wowote hizo mbegu lazima zimtoke anapooga na kujisafisha nk
3. Zinaweza kuendelea kuwa hai kipindi kirefu
Baada ya mbegu kutoka kwa mwanaume akishakuwa amefika kileleni yaani amepiga bao na kuingia katika via vya uzazi vya mwanamke zinaweza kuendelea kuwa hai kwa siku mbili mpaka tano bado zikiwa hai.
Hii ni kutokana na ukweli kuwa mbegu za kiume zinaweza kuendelea kupata viinilishe vyote inavyovihitaji ili kuwa hai zikiwa katika via vya uzazi vya mwanamke.
4. Zina mbio vibaya mno
Wakati mbegu zinatoka katika uume wa mwanaume huwa na spidi kubwa ambayo haiwezi kuelezewa.
Kabla hata ya mwanaume hajafika kileleni yaani hajakojoa au kabla hajapiga bao kiasi fulani cha mbegu (maji maji) huanza kutoka kwenye tundu la uume wake na hili linaweza kutokea mapema tu wakati wa mazungumzo wawili wakiwa chumbani.
Wanaume hawana udhibiti wa hili na wengi hawajuwi muda gani linaweza kutokea.
Hali inaweza kuwa ya kuonekana zaidi hasa kama mwanaume huyo si mtu wa kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara.
Bado wataalamu hawana hitimisho moja kwamba maji maji hayo ya mwanzo yanaweza kuwa na mbegu zinazoweza kutungisha ujauzito.
Kazi kubwa ya maji maji hayo ni kusaidia kulainisha mbegu zitakazokuwa zinatoka wakati wa tendo na kupunguza hali ya uasidi katika mrija unaopitisha mbegu kwenye uume (urethra).
Hii ndiyo sababu mbinu ya kuzuia ujauzito kwa kumwaga nje ina walakini mkubwa na usiitegemee sana katika kuzuia ujauzito kwani kuna uwezekano mwanaume akakumwagia kiasi fulani cha mbegu hata kabla hajafika mshindo wenyewe.
5. Kwa kawaida lazima zitoke
Kuna jambo huwa naulizwa na vijana wa kiume hata baadhi ya wanaume watu wazima kwamba wanapokojoa mkojo wa kawaida au wanapopata choo kikubwa wanaona mbegu zao zikitoka pia na wengi wanashikwa na butwaa na kudhani ni ugonjwa.
Kutokwa na mbegu wakati unakojoa mkojo wa kawaida au unapojisaidia haja kubwa ni ishara unakaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa.
Basi ni hivyo tu siyo ugonjwa.
Bali ikiwa mbegu hizo zinapotoka zinaambatana na maumivu au damu au zina harufu mbaya muone daktari haraka kwa uchunguzi zaidi.
Mwanaume anaweza kutokwa pia na mbegu akiwa usingizini bila hata yeye kujuwa, anaweza kutokewa na ndoto akihisi yupo na mwanamke anashiriki tendo la ndoa na mbegu humtoka kisha lazima ashtuke usingizini na tayari ataona mbegu zimejaa kwenye nguo yake ya ndani.
Mwanaume anaweza pia kutokwa na mbegu akiangalia picha au video za X.
6. Hazipendi joto
Mbegu za kiume yaani shahawa hazipendi joto.
Zinapenda mazingira ya joto yasiyozidi sentigredi 13.
Mji wa Dar Es Salaam mara nyingi una joto la kati ya 20 mpaka 30.
Mwili wa mwanaume unao mfumo wake wa ndani unaosaidia hizi mbegu zisipatwe na joto jingi.
Mwili wa mwanaume una viyoyozi (AC) karibu na korodani ambavyo hutumika kuondoa joto kwenye mfuko wa mbegu za mwanaume.
Hivi viyoyozi (veins) hufanya kazi kama transfoma ya umeme. Joto linapokuwa juu sana hushusha na linapokuwa chini sana hulipandisha ili kubaki katika hali ya sentigredi 13.
Mwanaume pia unatakiwa kuepuka mazingira ya joto sana hasa kutovaa chupi zinazobana sana na ikiwezekana usivae chupi vaa tu suruali peke yake ili kuziwezesha mbegu zako zisiingiliwe na joto na kuziwezesha zibaki na afya.
Mwanaume pia unashauriwa ukikaa au kusimama usipende kubana miguu yako ili kuzipa mbegu zako hewa ya kutosha wakati wote.
7. Zinaweza kuhifadhiwa katika friza
Siyo ice cream tu ndiyo unaweza kuzihifadhi katika friza
Kama unaumwa au una ugonjwa fulani hasa saratani au unahisi miaka kadhaa ijayo mbegu zako zaweza kuwa hazina ubora tena kama ulizo nazo leo, unaweza kuzifadhi katika friza kwa muda upendao wewe na siku ukizihitaji unazichukuwa na kumwekea mwanamke
Sasa tuelewane zipo friza maalumu huko hospitalini au maabara zinazoweza kutunza mbegu hizo bila mwisho (indefinitely) zikihifadhiwa kwenye joto la nyuzi joto -196 hivyo usije ukapiga punyeto sasa na kuzihifadhi wewe kama wewe!
Soma hii pia > Jinsi ya kuacha punyeto
8. Huwa hazifi haraka
Ni uongo kuamini kwamba mbegu za kiume yaani shahawa au manii hufariki mara tu zinapokutana na oksijeni (yaani mara tu zikitoka nje ya mwili wa mwanaume).
Mbegu za mwanaume hufariki zinapokosa maji na haziwezi kurudi tena kuwa hai zinapokuwa hazina umajimaji tena yaani zikikauka.
Maji ni uhai ndugu.
9. Zinapenda kupetiwapetiwa
Mwanaume anao uwezo wa kuchukuwa baadhi ya hatua katika kuishi kwake ili kuziongezea afya mbegu zake.
Mbegu hizi zinapenda kupetiwapetiwa au zinapenda kujariwa, kwa lugha nyepesi ni kuwa zinapenda uwe unazijali.
Kuna vitu ukivifanya vinaweza kusaidia kuongeza ubora wa mbegu zako ikiwemo wingi wake na afya yake kwa ujumla, vitu hivyo ni pamoja na kuacha vilevi, kupunguza msongo wa mawazo (stress), kudhibiti uzito wako, kupata usingizi wa kutosha, kukaa mbali na joto jingi, kukaa mbali na viwanda, kula chakula sahihi, kufanya mazoezi ya viungo nk
Soma hii pia > Vyakula vitano vinavyoua nguvu zako za kiume bila wewe kujuwa
Ikiwa una tatizo lolote kuhusiana na mbegu zako labda zimekuwa chache, hazina afya na uwezo wa kutungisha mimba nk tuwasiliane WhatsApp +255714800175
Mjulishe pia rafiki yako kwenye Twitter naye asome post hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;
Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume Click To TweetTafadhali SHARE post hii na wengine uwapendao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni