Translate

Jumatano, 27 Mei 2020

Dawa ya kisukari inashukiwa kusababisha saratani

Dawa ya kisukari inashukiwa kusababisha saratani

Dawa ya kisukari inashukiwa kusababisha saratani

Dawa maarufu ya kudhibiti kisukari aina ya pili ijulikanayo kama Metformin inachunguzwa na Mamlaka ya chakula na dawa ya Marekani FDA kama inaweza kuwa ina vitu vinavyoweza kusababisha saratani.

Ripoti ya WSB  ya tarehe 9 disemba 2019 inasema Metformin inaweza kuwa na kitu kinachosababisha saratani kijulikanacho kwa kitaalamu kama N-Nitrosodimethylamine kwa kifupi NDMA kwa watumiaji wa dawa hiyo.

Soma hii pia > Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili

Kwa mjibu wa taarifa hiyo Metformin hutumika kwa wagonjwa wa kisukari aina ya pili.

Karibu kila mtu ana hatari ya kupatwa na saratani inayotokana na NDMA kutokana na ukweli kwamba ni aina ya taka inayoweza kupatikana katika maji na vyakula tunavyokula kila siku na ikiwa unakunywa au kula vyakula vyenye taka ya aina hii kuna uwezekano ukapatwa na saratani siku za mbeleni kwa mjibu wa FDA.

Pamoja na dawa hii ya Metformin kufanyiwa utafiti huu kuona kama inaweza kuleta shida ya saratani kwa watumiaji wake, bado wagonjwa wanashauriwa kuendelea kuitumia ili kudhibiti ugonjwa wao wa kisukari.

“Itakuwa ni hatari kwa wagonjwa wa kisukari kuacha kuitumia dawa hii bila kuzungumza kwanza na madaktari wao wa karibu’’ anasema Dr. Janet Woodcock wa mamlaka ya dawa na chakula Marekani – FDA.

Kama unapenda kujuwa mamlaka hii imefikia wapi na uchunguzi huu wapigie simu kwenye namba yao 1-888-463-6332.

Soma hii pia > Usizidharau ishara hizi 8 za mwanzo za kisukari

Je unaumwa kisukari aina ya pili na unahitaji dawa ya asili kwa ajili hiyo? kama ndiyo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Mjulishe pia rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Dawa ya kisukari inashukiwa kusababisha saratani Click To Tweet

Tafadhari SHARE post hii na wengine uwapendao

Imesomwa mara 6

Let's block ads! (Why?)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...