Chanzo cha ugonjwa wa kisukari aina ya pili
- chanzo cha kisukari mwilini
- nini chanzo cha kisukari
- chanzo cha ugonjwa wa kisukari
- chanzo cha kisukari na dalili zake
- chanzo cha kisukari ni nini
- chanzo cha sukari kushuka
- chanzo cha sukari mwilini
Kisukari ni ugonjwa wa kongosho, wakati uzarishaji wa Insulini au utolewaji wake haufanyi kazi vizuri, na ikiwa hali hii haitadhibitiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa kwenye macho, figo, neva, mishipa ya damu, Ini na moyo.
Kisukari aina ya pili ni wakati ambapo insulini inakuwa huru (insulin-independent) au inapatikana lakini kongosho haliitoi na hivyo dawa (kemikali) lazima itumike kulilazimisha kongosho kutoa insulini.
Aina ya pili ya kisukari huanza kujitokeza kuanzia umri wa miaka 40 na kinachosababisha ni miaka mingi ya kula chakula kisicho sahihi, kutofanya mazoezi na upungufu wa maji na chumvi mwilini.
Kwa bahati mbaya, nyakati hizi tunashuhudia hata watoto wadogo wakipatwa na aina hii ya kisukari.
Watu wenye kisukari cha aina hii ya pili pia huwa na uzito uliozidi (overweight).
Chanzo cha ugonjwa wa kisukari aina ya pili
Chanzo kikuu cha kisukari aina ya pili katika mwili wako ni aina ya nguvu uliyochagua kuitumia zaidi katika kuuendesha mwili wako.
Chanzo kikuu cha kisukari aina ya pili katika mwili wako ni aina ya nguvu uliyochagua kuitumia zaidi katika kuuendesha mwili wako. Click To TweetSoma hii pia > Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili
Mwili una vyanzo vikuu vitatu vya nguvu ambavyo ni;
1. Chanzo kikuu cha kwanza cha nguvu cha mwili ni SUKARI
Hapa ni sukari yenyewe kama ilivyo sukari au vyakula kama vya wanga na protini hubadilishwa na kuwa glukozi au sukari ambayo ndiyo nguvu ya mwili
Ili kuhimili mahitaji ya ubongo, mwili umekuza mfumo maalumu ili kutunza kiasi cha kawaida cha sukari katika mzunguko wa damu.
Hufanya hivyo kwa njia mbili, ya kwanza ni ile ya kusisimua ulaji wa vyakula vyenye protini na wanga ambavyo vitabadilishwa kuwa sukari ikijumuisha pia sukari yenyewe katika mlo.
Wanga mzuri kwako unayeumwa kisukari aina ya pili au kama unataka kujizuia usiuguwe kisukari aina ya pili ni ule ambao haujakobolewa, mfano wanga uliomo kwenye mkate wa ngano ambayo haijakobolewa (brown bread), kwenye ugali wa dona, ule wa kwenye ugali wa mtama, wanga uliomo kwenye mchele wa brown.
Njia ya pili ni ya kubadili wanga na protini toka katika hifadhi ya mwili na kuwa sukari. Njia hii ya pili huitwa kwa kitaalamu kama ‘Gluconeogenesis’, yaani utengenezwaji wa sukari toka katika malighafi zilizohifadhiwa. Utengenezaji wa aina hii ya sukari hufanyika katika Ini.
2. Chanzo cha pili cha nguvu ya mwili ni MAFUTA
Na hiki ndiyo chanzo pekee cha nguvu cha mwili chenye uwezo wa kukupa nguvu nyingi kuliko chanzo kingine chochote cha nguvu cha mwili.
Hivyo mafuta yenyewe ni chanzo cha nguvu chenye uwezo wa kukupa nguvu nyingi kuliko vyanzo vingine viwili vya nguvu vya mwili.
Kwanini mafuta ni mhimu katika kutengeneza nguvu za mwili?
Kila gramu 1 ya mafuta hutoa kalori 9 za nishati(nguvu), kila gramu 1 ya protini au sukari hutoa kalori 4 za nishati(nguvu).
Hii ndiyo sababu mafuta yanapotumika kuzarisha nguvu, mtu hajisikii sana njaa na anakuwa na nguvu nyingi zaidi kuliko kama maji/chumvi au sukari/wanga/protini vikitumika kuzalisha nguvu
Sasa shida ipo hapa. Mwili kamwe hauchagui mafuta kama chanzo chake cha nguvu isipokuwa tu umefanya mazoezi ya viungo au umefunga kula chakula masaa kadhaa.
Mafuta ni mhimu kwako kama ilivyo mhimu pia vyakula vya wanga na protini lakini ni lazima uwe bize na mazoezi ya viungo kila siku ili kupata faida hii adimu ya mazoezi ya viungo kwa nguvu za mwili.
Mafuta nayo yamegawanyika mara mbili. Kuna mafuta mazuri na mafuta mabaya.
Kwa mfano mafuta yanayotumika kupikia chipsi au maandazi au mafuta mengi tunayotumia kupikia majumbani si mafuta mazuri.
Mafuta mazuri kabisa ni yale yenye OMEGA 3 ambayo ni pamoja na mafuta ya nazi, mafuta ya mawese, mafuta ya mbegu za maboga, mafuta ya ufuta, mafuta ya parachichi, mafuta ya zeituni na mafuta ya samaki.
Kama upo bize na mazoezi ya viungo kila siku unaweza kula mafuta yoyote yawe mazuri au mabaya na bado akabaki na afya njema.
Mhimu ni mazoezi bila mazoezi hata hayo mafuta mazuri ukiyatumia bado hutaona faida yoyote.
Kwa mtu mwenye kisukari aina ya pili mazoezi ni lazima.
Kwahiyo umhimu wa kwanza wa maoezi ya viungo katika kuzuia na kutibu kisukari aina ya pili ni kuwa kwanza maoezi yanakuwezesha kuchoma mafuta mwilini ambayo bila mazoezi yangeendelea kujirundika mwilini.
Pili mazoezi yanauwezesha mwili kutumia mafuta kama chanzo chake cha nguvu na siyo nguvu tu bali nguvu mara 2 zaidi tofauti na kama mwili ungetumia sukari au maji na chumvi kutengeneza nguvu.
Mazoezi pia ni mhimu sana kwa mwili katika kuzuia na kutibu tatizo la msongo wa mawazo (stress). .
Shida iliyopo ni kuwa watu wengi linapokuja suala la mazoezi hawakosi visingizio na kisingizio chao kikuu ni kukosa muda wa kufanya mazoezi!.
Ni hatari sana kuwa na watu wa namna hii kwenye jamii yetu.
Unakosaje muda wa mazoezi ndugu? je muda wa kulala unapata? je muda wa kula chakula unapata? je muda wa kwenda bafuni kuoga unapata? je muda wa kukaa bar au kijiweni unapiga stori na washikaji unapata?
Unashindwaje sasa kupata muda wa mazoezi dakika 30 au 40 kwa siku? jibu ni moja tu, wewe ni mvivu na huoni umhimu wowote wa afya yako.
Mazoezi gani sasa ya viungo nifanye ? hilo lazima utauliza.
Jibu fupi ni mazoezi yoyote yanaweza kukusaidia kuepuka kisukari aina ya pili, ila mazoezi ya kukimbia (jogging), kuchuchumaa na kusimama (squatting), pushup, na mazoezi ya kutembea ni mazoezi mazuri sana kwako
Bila kufanya MAZOEZI AU BILA KUFUNGA KULA mwili utaendelea kuchagua SUKARI kama chanzo chake cha nguvu na mafuta yataendelea kujirundika mwilini bila kuwa na faida yoyote na hivyo kukuletea kitambi, manyama uzembe, upungufu wa nguvu za kiume na mwisho kukuletea tatizo la kisukari aina ya pili.
3. Chanzo cha tatu cha nguvu za mwili ni MAJI NA CHUMVI.
Hivi karibuni imegundurika kuwa, mwili unao uwezo wa kutengeneza nguvu kwa kutumia maji (hydroelectric energy), wakati maji peke yake yanapoingia kupitia kuta za seli na kuwasha pampu maalumu za majenereta ya kuzarishia nguvu yaitwayo kwa kitaalamu, ‘cation pumps’,.
Ni kama vile bwawa la umeme linapojengwa karibu na mto mkubwa.
Inajionyesha wazi sasa kwamba ubongo unategemea zaidi nguvu zitokanazo na umeme wa maji hasa katika mifumo yake ya usafirishaji kwenye neva zake kwenda sehemu mbalimbali za mwili.
Hivyo ni vigumu mtu kuishi bila mafuta, chumvi, wanga au sukari.
Chumvi hasa ninayotaka uwe unaitumia ni ile chumvi ya mawe hasa ya baharini ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt).
Unapokuwa katika upungufu wa maji (haunywi ya kutosha), unapokuwa hufanyi mazoezi ya viungo mara kwa mara na unakula vyakula vyenye chumvi kidogo au visivyo na chumvi kabisa, ‘automatikali’ ubongo utapandisha kiwango cha sukari kwenye damu yako.
Chanzo cha ugonjwa wa kisukari aina ya pili
Ukichunguza sana watu wa siku hizi utagunduwa vitu vifuatavyo;
- Wanakula sana vyakula vya wanga na protini
- Hawanywi maji ya kutosha kila siku kwa mjibu wa uzito wao
- Hawanywi maji mpaka wasikie kiu
- Hawatumii chumvi ya kutosha kwenye vyakula vyao
- Hawana muda wa kufanya mazoezi
Chanzo kikuu cha kisukari aina ya pili katika mwili wako ni aina ya nguvu uliyochagua kuitumia zaidi katika kuuendesha mwili wako.
ikiwa mwili una kiasi kidogo cha maji na chumvi, ikiwa hufanyi mazoezi ya viungo ubongo utakuwa unajiendesha kwa karibu ya aslilimia 100 kwa kutumia sukari.
Ikiwa utaanza kuwa bize na mazoezi kila mara, utakunywa maji ya kutosha kila siku na kutumia chumvi ya kutosha kwenye vyakula vyako, mwili utaacha kuchagua sukari kama chanzo chake kikuu cha nguvu na kuanza kuchagua mafuta na maji na chumvi kama vyanzo vyake vingine vya nguvu na ugonjwa wako wa kisukari utaishia hapo.
Ikiwa utahitaji dawa ya asili kwa ajili kutibu kabisa kisukari hasa kisukari aina ya pili, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175
Mimi napatikana Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke.
Soma hii pia > Usizidharau ishara hizi 8 za mwanzo za kisukari
Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni