Translate

Jumatano, 27 Mei 2020

Dawa ya kisukari inashukiwa kusababisha saratani

Dawa ya kisukari inashukiwa kusababisha saratani

Dawa ya kisukari inashukiwa kusababisha saratani

Dawa maarufu ya kudhibiti kisukari aina ya pili ijulikanayo kama Metformin inachunguzwa na Mamlaka ya chakula na dawa ya Marekani FDA kama inaweza kuwa ina vitu vinavyoweza kusababisha saratani.

Ripoti ya WSB  ya tarehe 9 disemba 2019 inasema Metformin inaweza kuwa na kitu kinachosababisha saratani kijulikanacho kwa kitaalamu kama N-Nitrosodimethylamine kwa kifupi NDMA kwa watumiaji wa dawa hiyo.

Soma hii pia > Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili

Kwa mjibu wa taarifa hiyo Metformin hutumika kwa wagonjwa wa kisukari aina ya pili.

Karibu kila mtu ana hatari ya kupatwa na saratani inayotokana na NDMA kutokana na ukweli kwamba ni aina ya taka inayoweza kupatikana katika maji na vyakula tunavyokula kila siku na ikiwa unakunywa au kula vyakula vyenye taka ya aina hii kuna uwezekano ukapatwa na saratani siku za mbeleni kwa mjibu wa FDA.

Pamoja na dawa hii ya Metformin kufanyiwa utafiti huu kuona kama inaweza kuleta shida ya saratani kwa watumiaji wake, bado wagonjwa wanashauriwa kuendelea kuitumia ili kudhibiti ugonjwa wao wa kisukari.

“Itakuwa ni hatari kwa wagonjwa wa kisukari kuacha kuitumia dawa hii bila kuzungumza kwanza na madaktari wao wa karibu’’ anasema Dr. Janet Woodcock wa mamlaka ya dawa na chakula Marekani – FDA.

Kama unapenda kujuwa mamlaka hii imefikia wapi na uchunguzi huu wapigie simu kwenye namba yao 1-888-463-6332.

Soma hii pia > Usizidharau ishara hizi 8 za mwanzo za kisukari

Je unaumwa kisukari aina ya pili na unahitaji dawa ya asili kwa ajili hiyo? kama ndiyo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Mjulishe pia rafiki yako kwenye twitter naye asome post hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Dawa ya kisukari inashukiwa kusababisha saratani Click To Tweet

Tafadhari SHARE post hii na wengine uwapendao

Imesomwa mara 6

Let's block ads! (Why?)

Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume

Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume

Una elimu au uelewa wa kiasi gani kuhusu mbegu za kiume yaani shahawa?

Kuna uwezekano mkubwa hujawahi kuwa na muda wowote wa kupeleleza au kujifunza mengi kuhusu mbegu zako.

Kama hujawahi kupata shida kutungisha mimba unaweza usiwaze lolote kuhusu mbegu zako na ukaendelea kuzichukulia poa kila siku.

Soma hii pia > Vidonda vya tumbo husababisha upungufu wa nguvu za kiume

Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume

Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume

1. Ni nyingi sana

Bao moja linakuwa na mbegu karibu milioni 200 na lina ujazo wa karibu nusu kijiko cha chai.

Kama utazipanga kwa kufuatana mbegu za mshindo mmoja (bao) zinaweza kuchukuwa umbali wa kilomita 9.

Kitu kingine cha kweli na cha kushangaza kuhusu wingi wa mbegu za kiume ni kuwa zimekuwa zikipunguwa kwa wanaume wa viazi vyote mwaka hadi mwaka.

Yaani kama mwanaume wa mwaka 1990 alikuwa na jumla ya mbegu milioni 500 kwa mfano basi kuna uwezekano mkubwa mwanaume wa mwaka 2020 akawa na jumla ya mbegu milioni 450.

Tafiti za hivi karibuni zinataja mambo ya mabadiliko ya mazingira na tabia ya mwanadamu ndiyo vinahusika na kushuka kwa karibu asilimia 50 ya ujazo, wingi na ubora wa mbegu za wanaume katika kipindi cha miongo minne iliyopita.

2. Zina safari ndefu zinapoingia kwa mwanamke

Mbegu za kiume zina safari ndefu sana zinapoingia katika via vya uzazi vya mwanamke.

Kwanza kabisa huingia kwenye mlango wa kizazi (cervix), kasha kwenye mji wa mimba (uterus), na kisha husafiri kupitia mirija ya mayai (fallopian tubes) mpaka kulifikia yai la mwanamke linalosubiri kurutubishwa.

Mbegu chache sana huendelea kuwa hai katika safari hiyo ndefu, nyingi hufa njiani na nyingine huamua kulala au kupumzika njiani na inahitajika mbegu 1 tu katika mbegu milioni 200 anazokojoa mwanaume ili kurutubisha yai na kutunga mimba.

Kuna wakati huwa nakutana na wanaume hata wanawake ninapochat nao WhatsApp huniambia mara tu wakikojoa huona mbegu zao zikitoka nje ya uke kwahiyo wana wasiwasi huenda ndiyo sababu hawapati mtoto!

Kwa faida ya wengi niseme hapa kuwa mbegu za mwanaume hazina sehemu ya kuhifadhiwa katika uke wa mwanamke.

Kama hazijatunga mimba ambapo ni mbegu 1 tu inahitajika katika hizo milioni 200 nyingine zote lazima zitoke

Ndiyo maana ukishiriki tendo la ndoa utaona mkimaliza mwanamke lazima ataenda bafuni kujisafisha sababu lazima zitolewe nje.

Hata kama hataenda bafuni maalumu kwa ajili hiyo, bado wakati wowote hizo mbegu lazima zimtoke anapooga na kujisafisha nk

3. Zinaweza kuendelea kuwa hai kipindi kirefu

Baada ya mbegu kutoka kwa mwanaume akishakuwa amefika kileleni yaani amepiga bao na kuingia katika via vya uzazi vya mwanamke zinaweza kuendelea kuwa hai kwa siku mbili mpaka tano bado zikiwa hai.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa mbegu za kiume zinaweza kuendelea kupata viinilishe vyote inavyovihitaji ili kuwa hai zikiwa katika via vya uzazi vya mwanamke.

4. Zina mbio vibaya mno

Wakati mbegu zinatoka katika uume wa mwanaume huwa na spidi kubwa ambayo haiwezi kuelezewa.

Kabla hata ya mwanaume hajafika kileleni yaani hajakojoa au kabla hajapiga bao kiasi fulani cha mbegu (maji maji) huanza kutoka kwenye tundu la uume wake na hili linaweza kutokea mapema tu wakati wa mazungumzo wawili wakiwa chumbani.

Wanaume hawana udhibiti wa hili na wengi hawajuwi muda gani linaweza kutokea.

Hali inaweza kuwa ya kuonekana zaidi hasa kama mwanaume huyo si mtu wa kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara.

Bado wataalamu hawana hitimisho moja kwamba maji maji hayo ya mwanzo yanaweza kuwa na mbegu zinazoweza kutungisha ujauzito.

Kazi kubwa ya maji maji hayo ni kusaidia kulainisha mbegu zitakazokuwa zinatoka wakati wa tendo na kupunguza hali ya uasidi katika mrija unaopitisha mbegu kwenye uume (urethra).

Hii ndiyo sababu mbinu ya kuzuia ujauzito kwa kumwaga nje ina walakini mkubwa na usiitegemee sana katika kuzuia ujauzito kwani kuna uwezekano mwanaume akakumwagia kiasi fulani cha mbegu hata kabla hajafika mshindo wenyewe.

5. Kwa kawaida lazima zitoke

Kuna jambo huwa naulizwa na vijana wa kiume hata baadhi ya wanaume watu wazima kwamba wanapokojoa mkojo wa kawaida au wanapopata choo kikubwa wanaona mbegu zao zikitoka pia na wengi wanashikwa na butwaa na kudhani ni ugonjwa.

Kutokwa na mbegu wakati unakojoa mkojo wa kawaida au unapojisaidia haja kubwa ni ishara unakaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa.

Basi ni hivyo tu siyo ugonjwa.

Bali ikiwa mbegu hizo zinapotoka zinaambatana na maumivu au damu au zina harufu mbaya muone daktari haraka kwa uchunguzi zaidi.

Mwanaume anaweza kutokwa pia na mbegu akiwa usingizini bila hata yeye kujuwa, anaweza kutokewa na ndoto akihisi yupo na mwanamke anashiriki tendo la ndoa na mbegu humtoka kisha lazima ashtuke usingizini na tayari ataona mbegu zimejaa kwenye nguo yake ya ndani.

Mwanaume anaweza pia kutokwa na mbegu akiangalia picha au video za X.

6. Hazipendi joto

Mbegu za kiume yaani shahawa hazipendi joto.

Zinapenda mazingira ya joto yasiyozidi sentigredi 13.

Mji wa Dar Es Salaam mara nyingi una joto la kati ya 20 mpaka 30.

Mwili wa mwanaume unao mfumo wake wa ndani unaosaidia hizi mbegu zisipatwe na joto jingi.

Mwili wa mwanaume una viyoyozi (AC) karibu na korodani ambavyo hutumika kuondoa joto kwenye mfuko wa mbegu za mwanaume.

Hivi viyoyozi (veins) hufanya kazi kama transfoma ya umeme. Joto linapokuwa juu sana hushusha na linapokuwa chini sana hulipandisha ili kubaki katika hali ya sentigredi 13.

Mwanaume pia unatakiwa kuepuka mazingira ya joto sana hasa kutovaa chupi zinazobana sana na ikiwezekana usivae chupi vaa tu suruali peke yake ili kuziwezesha mbegu zako zisiingiliwe na joto na kuziwezesha zibaki na afya.

Mwanaume pia unashauriwa ukikaa au kusimama usipende kubana miguu yako ili kuzipa mbegu zako hewa ya kutosha wakati wote.

7. Zinaweza kuhifadhiwa katika friza

Siyo ice cream tu ndiyo unaweza kuzihifadhi katika friza

Kama unaumwa au una ugonjwa fulani hasa saratani au unahisi miaka kadhaa ijayo mbegu zako zaweza kuwa hazina ubora tena kama ulizo nazo leo, unaweza kuzifadhi katika friza kwa muda upendao wewe na siku ukizihitaji unazichukuwa na kumwekea mwanamke

Sasa tuelewane zipo friza maalumu huko hospitalini au maabara zinazoweza kutunza mbegu hizo bila mwisho (indefinitely) zikihifadhiwa kwenye joto la nyuzi joto -196 hivyo usije ukapiga punyeto sasa na kuzihifadhi wewe kama wewe!

Soma hii pia > Jinsi ya kuacha punyeto

8. Huwa hazifi haraka

Ni uongo kuamini kwamba mbegu za kiume yaani shahawa au manii hufariki mara tu zinapokutana na oksijeni (yaani mara tu zikitoka nje ya mwili wa mwanaume).

Mbegu za mwanaume hufariki zinapokosa maji na haziwezi kurudi tena kuwa hai zinapokuwa hazina umajimaji tena yaani zikikauka.

Maji ni uhai ndugu.

9. Zinapenda kupetiwapetiwa

Mwanaume anao uwezo wa kuchukuwa baadhi ya hatua katika kuishi kwake ili kuziongezea afya mbegu zake.

Mbegu hizi zinapenda kupetiwapetiwa au zinapenda kujariwa, kwa lugha nyepesi ni kuwa zinapenda uwe unazijali.

Kuna vitu ukivifanya vinaweza kusaidia kuongeza ubora wa mbegu zako ikiwemo wingi wake na afya yake kwa ujumla, vitu hivyo ni pamoja na kuacha vilevi, kupunguza msongo wa mawazo (stress), kudhibiti uzito wako, kupata usingizi wa kutosha, kukaa mbali na joto jingi, kukaa mbali na viwanda, kula chakula sahihi, kufanya mazoezi ya viungo nk

Soma hii pia > Vyakula vitano vinavyoua nguvu zako za kiume bila wewe kujuwa

Ikiwa una tatizo lolote kuhusiana na mbegu zako labda zimekuwa chache, hazina afya na uwezo wa kutungisha mimba nk tuwasiliane WhatsApp +255714800175

Mjulishe pia rafiki yako kwenye Twitter naye asome post hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Mambo 9 ya kushangaza na usiyoyajuwa kuhusu mbegu za kiume Click To Tweet

Tafadhali SHARE post hii na wengine uwapendao

Imesomwa mara 61

Let's block ads! (Why?)

Jumanne, 26 Mei 2020

Vyakula vitano vinavyoua nguvu zako za kiume bila wewe kujuwa

VYAKULA VITANO VINAVYOUA NGUVU ZAKO ZA KIUME BILA WEWE KUJUWA

Ulivyo ni kile unachokula na kunywa kila siku.

You are what you eat.

Kama unakula takataka utakuwa takataka na kama unakula vyakula vya afya basi utakuwa afya.

Hakuna upendeleo katika hili!

Kama hujuwi nguvu za kiume ni kitu gani hasa bonyeza kwanza hapa.

Chakula unachokula kina uhusiano wa moja kwa moja na afya yako ya kitandani.

Kwa bahati mbaya wanaume wengi hawajuwi wale nini na wengine hudhani ukiwa na hela basi unatakiwa kula vyakula kwenye mahotel ya kifahari au kula nyama kila siku!

Vyakula vitano vinavyoua nguvu zako za kiume bila wewe kujuwa 1

Vyakula vitano vinavyoua nguvu zako za kiume bila wewe kujuwa;

1. Vilevi

Glasi moja ya mvinyo mwekundu kwa siku inaweza kukusaidia kuimarisha nguvu zako za kiume. Kumbuka nimesema glasi moja kwa siku.

Mwanzoni unapoanza kuwa mlevi unaweza kuhisi kama vile nguvu zako zinaongezeka au unakuwa imara Zaidi lakini kadri unavyoendelea kuwa mlevi ndivyo utakavyopoteza nguvu zako na hamu yako ya kutaka kuhiriki tendo la ndoa.

Pombe inaweza kukuondolea aibu ya kutongoza na ukajikuta umetongoza yoyote hasa wauza bar (bar meds).

Lakini kunywa pombe kupita kiasi kunahusishwa na kushuka kwa homoni ya testosterone na kuiondoa hii homoni kwenye mzunguko wako wa damu na hata kushusha kiwango chake cha uzalishwaji katika mwili.

Pombe pia ikitumika kupita kiasi na kila siku inao uwezo mkubwa wa kulidhuru ini lako.

Ini ni ogani mhimu ili kuondoa sumu mwilini na linapochakaa hivi sababu ya pombe ni vigumu wewe kuendelea kuwa na nguvu za kiume.

Ini pia linahusika na kuziweka sawa homoni mwilini hasa homoni ya estrogen na homoni nyingine iitwayo phytoestrogens ambayo ni estrogen itokanayo na mimea imo kwenye vitu vinavyotumika kutengeneza bia.

Sigara na bangi ni vilevi vingine vinavyoweza kukuletea upungufu wa nguvu za kiume.

Moshi wa sigara na bangi huziba mishipa yako ya damu na kukusababishia mtiririko mbovu wa damu.

Moshi wa sigara na bangi ni sumu katika mwili.

Sumu yoyote lazima ikuletee kushuka kwa nguvu za kiume.

Sumu yoyote lazima ikuletee kushuka kwa nguvu za kiume Click To Tweet

Sigara kwa mfano zimeandikwa kabisa kwenye boksi lake kwamba ni hatari kwa afya yako kwahiyo naomba usinipotezee muda kueleza kuhusu madhara ya sigara kwani yanajulikana na kila mtu.

Kadharika na madawa mengine yote ya kulevya.

Mwanzoni mwa kutumia hivi vilevi unaweza usione madhara au shida yoyote na pengine unaweza kuona faida katika tendo la ndoa ila kadri siku zinavyoenda utakuja kunitafuta nikupe Msamitu.

Sukari ipo karibu kila sehemu na ni vigumu kuipeuka. Ni vigumu umalize siku hujala au kunywa kitu chenye sukari ndani yake!

Sukari ina kawaida ya kuongeza usawa wa homoni iitwayo insulini ambayo inaweza kukusababishia yafuatayo;

a) Mwili wako kuhifadhi mafuta hasa tumboni na kukuletea kitambi,
b) Kisukari,
c) Kupunguza wingi na uimara wa mishipa na
d) Kushusha kiwango cha homoni mhimu katika tendo la ndoa homoni iitwayo testosterone.

Kwa wanaume mafuta yakijaa tumboni yaani ukianza kuwa na kitambi husababisha kuongezeka zaidi kwa homoni nyingine iitwayo estrogen ambayo yenyewe inapozidi kiwango kuliko inavyohitajika huleta tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na mwanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa.

Ni mhimu kwamba unaiondoa sukari kwenye orodha ya vyakula unavyokula kila siku ili kuimarisha nguvu zako za mwili na za kiume kwa ujumla.

Nini mbadala wa sukari?

Kuna mtu anauliza.

Jibu ni asali.

Tumia asali kwenye chochote kinachohitaji sukari na utakuwa na nguvu za kutosha kila siku.

3. Vyakula vya kwenye makopo

Unahimizwa kuendelea kupenda kula vyakula vya asili zaidi na vilivyopikwa nyumbani.

Vyakula vya kwenye makopo yaani vyakula vya dukani au viwandani vingi vina sodium nyingi zaidi ya mwili wako unavyohitaji.

Sodium nyingi husababisha shinikizo la juu la damu na kushuka kwa mtiririko mzuri wa damu sehemu mbali mbali za viungo vya mwili wako.

Baadhi ya vyakula hivyo ni pamoja na juisi zote za viwandani, soda zote, soseji, jibini(cheese), strawberry, tomato sauce, chill sauce, mkate mweupe nk

4. Vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi

Vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (Fried foods) ni vyakula hatari kwa afya ya moyo na afya ya kitandani kwa ujumla.

Hapa shida siyo chakula bali mbinu inayotumika kupika hicho chakula.

Mafuta haya yanayotumika kupika hivi vyakula yanapopata moto yaani yanapounguzwa ili kupika chakula hubadilika na kuwa moja ya mafuta mabaya kabisa kwa afya yako hasa kwa afya ya moyo, saratani na kolesto.

Vyakula hivi pia hupelekea mwili kuongeza uzito na unene kwa haraka sana.

Uzito ukizidi ni rahisi homoni zako kuvurugika na kushuka kwa nguvu za kiume.

Vyakula hivi huziba ateri na mishipa ya damu na kukusababishia damu kutoweza kutiririka kwa uhuru wote kwenda sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kwenye uume wako.

Ili uendelee kuwa na nguvu za kiume utatakiwa kuacha kula vyakula kama chipsi, maandazi na chakula kingine chochote kinachopikwa kwa staili hii ya kuwekwa katikati ya mafuta mengi.

Chipsi hasa za vibandani ni hatari zaidi kuliko hata zile za nyumbani.

Kwenye vibanda vya chipsi mafuta hayabadilishwi hata yawe na rangi gani, yakipungua wananunua mengine na kuongeza juu ya yale yaliyotumika kupika jana na juzi.

Ukichunguza vyombo wanavyopikia hizo chipsi utaona ndani na nje havina tofauti, ndani vyeusi na nje vyeusi pia!

Unaweza kula chipsi mara moja moja hasa nyumbani na mafuta yakishatumika kupikia mara moja yamwagwe yasirudiwe au kuchanganywa mapya na yaliyotumika kabla.

Ukiweza acha kabisa kula chipsi kwa ajili ya kuwa na nguvu za kiume za kutosha na kuepuka saratani ikiwemo saratani ya tezi dume.

5. Vinywaji vyenye kaffeina

Hivi ni vinywaji vinapotumika kwa kiasi vinaweza kuamsha nguvu na hali yako ya kutaka kushiriki tendo la ndoa lakini vinapozidi kiasi hukuletea tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Hivi ni pamoja na chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi zote, energy drinks zote, chokoleti, kokoa nk.

Kikombe kimoja cha kahawa kwa siku hakina ubaya wowote ila ikizidi utanitafuta nikupe Msamitu.

Kaffeina ni kikojoshi (diuretic), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili.

Ukinywa kikombe kimoja cha kahawa tegemea kwenda chooni muda mchache tangu unywe na kutoa mkojo wa ujazo wa vikombe viwili.

Kaffeina ni dawa mojawapo ya kulevya kundi la madawa ya kulevya ya kusisimua (stimulant drugs).

Ndiyo maana ni vigumu sana mtu kuacha kahawa – ni kwa sababu ni dawa ya kulevya pia.

Hata mtu aliyezoea kunywa chai ya rangi kwa miaka mingi siku asipokunywa huona kichwa kinamuuma!

Kaffeina inaweza kukuletea hali ya kuongezeka kwa hamaki katika mwili wako na hamaki ni jambo linaloweza kudhuru nguvu zako za kiume.

Vyakula vingine vinavyoharibu nguvu za kiume ni pamoja na vyakula au bidhaa zitokanazo na soya, viazi pori (beet roots), flaxseed products, dawa za kuongeza nguvu za kiume za kizungu (viagra, cupid, na vidonge vingine vya namna hii), mnanaa (minti), licorice, samaki wa kufugwa, kuku wa kisasa na mayai ya kisasa, popcorn (bisi) nk

Na kuna vingine sitavitaja ili kutoleta taharuki maana kuna vingine ukiambiwa hutaamini bali hivyo kwanza nahisi vinakutosha.

Ikiwa unahitaji dawa ya asili isiyo na madhara kwa ajili ya kuimarisha nguvu zako za kiume niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome post kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Vyakula vitano vinavyoua nguvu zako za kiume bila wewe kujuwa Click To Tweet

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

Imesomwa mara 11

Let's block ads! (Why?)

Jumatatu, 18 Mei 2020

Chanzo cha ugonjwa wa kisukari aina ya pili

Chanzo cha ugonjwa wa kisukari aina ya pili

  • chanzo cha kisukari mwilini
  • nini chanzo cha kisukari
  • chanzo cha ugonjwa wa kisukari
  • chanzo cha kisukari na dalili zake
  • chanzo cha kisukari ni nini
  • chanzo cha sukari kushuka
  • chanzo cha sukari mwilini

Chanzo cha ugonjwa wa kisukari aina ya pili

Kisukari ni ugonjwa wa kongosho, wakati uzarishaji wa Insulini au utolewaji wake haufanyi kazi vizuri, na ikiwa hali hii haitadhibitiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa kwenye macho, figo, neva, mishipa ya damu, Ini na moyo.

Kisukari aina ya pili ni wakati ambapo insulini inakuwa huru (insulin-independent) au inapatikana lakini kongosho haliitoi na hivyo dawa (kemikali) lazima itumike kulilazimisha kongosho kutoa insulini.

Aina ya pili ya kisukari huanza kujitokeza kuanzia umri wa miaka 40 na kinachosababisha ni miaka mingi ya kula chakula kisicho sahihi, kutofanya mazoezi na upungufu wa maji na chumvi mwilini.

Kwa bahati mbaya, nyakati hizi tunashuhudia hata watoto wadogo wakipatwa na aina hii ya kisukari.

Watu wenye kisukari cha aina hii ya pili pia huwa na uzito uliozidi (overweight).

Chanzo cha ugonjwa wa kisukari aina ya pili

Chanzo kikuu cha kisukari aina ya pili katika mwili wako ni aina ya nguvu uliyochagua kuitumia zaidi katika kuuendesha mwili wako.

Chanzo kikuu cha kisukari aina ya pili katika mwili wako ni aina ya nguvu uliyochagua kuitumia zaidi katika kuuendesha mwili wako. Click To Tweet

Soma hii pia > Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili

Mwili una vyanzo vikuu vitatu vya nguvu ambavyo ni;

1. Chanzo kikuu cha kwanza cha nguvu cha mwili ni SUKARI

Hapa ni sukari yenyewe kama ilivyo sukari au vyakula kama vya wanga na protini hubadilishwa na kuwa glukozi au sukari ambayo ndiyo nguvu ya mwili

Ili kuhimili mahitaji ya ubongo, mwili umekuza mfumo maalumu ili kutunza kiasi cha kawaida cha sukari katika mzunguko wa damu.

Hufanya hivyo kwa njia mbili, ya kwanza ni ile ya kusisimua ulaji wa vyakula vyenye protini na wanga ambavyo vitabadilishwa kuwa sukari ikijumuisha pia sukari yenyewe katika mlo.

Wanga mzuri kwako unayeumwa kisukari aina ya pili au kama unataka kujizuia usiuguwe kisukari aina ya pili ni ule ambao haujakobolewa, mfano wanga uliomo kwenye mkate wa ngano ambayo haijakobolewa (brown bread), kwenye ugali wa dona, ule wa kwenye ugali wa mtama, wanga uliomo kwenye mchele wa brown.

Njia ya pili ni ya kubadili wanga na protini toka katika hifadhi ya mwili na kuwa sukari. Njia hii ya pili huitwa kwa kitaalamu kama ‘Gluconeogenesis’, yaani utengenezwaji wa sukari toka katika malighafi zilizohifadhiwa. Utengenezaji wa aina hii ya sukari hufanyika katika Ini.

2. Chanzo cha pili cha nguvu ya mwili ni MAFUTA

Na hiki ndiyo chanzo pekee cha nguvu cha mwili chenye uwezo wa kukupa nguvu nyingi kuliko chanzo kingine chochote cha nguvu cha mwili.

Hivyo mafuta yenyewe ni chanzo cha nguvu chenye uwezo wa kukupa nguvu nyingi kuliko vyanzo vingine viwili vya nguvu vya mwili.

Kwanini mafuta ni mhimu katika kutengeneza nguvu za mwili?

Kila gramu 1 ya mafuta hutoa kalori 9 za nishati(nguvu), kila gramu 1 ya protini au sukari hutoa kalori 4 za nishati(nguvu).

Hii ndiyo sababu mafuta yanapotumika kuzarisha nguvu, mtu hajisikii sana njaa na anakuwa na nguvu nyingi zaidi kuliko kama maji/chumvi au sukari/wanga/protini vikitumika kuzalisha nguvu

Sasa shida ipo hapa. Mwili kamwe hauchagui mafuta kama chanzo chake cha nguvu isipokuwa tu umefanya mazoezi ya viungo au umefunga kula chakula masaa kadhaa.

Mafuta ni mhimu kwako kama ilivyo mhimu pia vyakula vya wanga na protini lakini ni lazima uwe bize na mazoezi ya viungo kila siku ili kupata faida hii adimu ya mazoezi ya viungo kwa nguvu za mwili.

Mafuta nayo yamegawanyika mara mbili. Kuna mafuta mazuri na mafuta mabaya.

Kwa mfano mafuta yanayotumika kupikia chipsi au maandazi au mafuta mengi tunayotumia kupikia majumbani si mafuta mazuri.

Mafuta mazuri kabisa ni yale yenye OMEGA 3 ambayo ni pamoja na mafuta ya nazi, mafuta ya mawese, mafuta ya mbegu za maboga, mafuta ya ufuta, mafuta ya parachichi, mafuta ya zeituni na mafuta ya samaki.

Kama upo bize na mazoezi ya viungo kila siku unaweza kula mafuta yoyote yawe mazuri au mabaya na bado akabaki na afya njema.

Mhimu ni mazoezi bila mazoezi hata hayo mafuta mazuri ukiyatumia bado hutaona faida yoyote.

Kwa mtu mwenye kisukari aina ya pili mazoezi ni lazima.

Kwahiyo umhimu wa kwanza wa maoezi ya viungo katika kuzuia na kutibu kisukari aina ya pili ni kuwa kwanza maoezi yanakuwezesha kuchoma mafuta mwilini ambayo bila mazoezi yangeendelea kujirundika mwilini.

Pili mazoezi yanauwezesha mwili kutumia mafuta kama chanzo chake cha nguvu na siyo nguvu tu bali nguvu mara 2 zaidi tofauti na kama mwili ungetumia sukari au maji na chumvi kutengeneza nguvu.

Mazoezi pia ni mhimu sana kwa mwili katika kuzuia na kutibu tatizo la msongo wa mawazo (stress). .

Shida iliyopo ni kuwa watu wengi linapokuja suala la mazoezi hawakosi visingizio na kisingizio chao kikuu ni kukosa muda wa kufanya mazoezi!.

Ni hatari sana kuwa na watu wa namna hii kwenye jamii yetu.

Unakosaje muda wa mazoezi ndugu? je muda wa kulala unapata? je muda wa kula chakula unapata? je muda wa kwenda bafuni kuoga unapata? je muda wa kukaa bar au kijiweni unapiga stori na washikaji unapata?

Unashindwaje sasa kupata muda wa mazoezi dakika 30 au 40 kwa siku? jibu ni moja tu, wewe ni mvivu na huoni umhimu wowote wa afya yako.

Mazoezi gani sasa ya viungo nifanye ? hilo lazima utauliza.

Jibu fupi ni mazoezi yoyote yanaweza kukusaidia kuepuka kisukari aina ya pili, ila mazoezi ya kukimbia (jogging), kuchuchumaa na kusimama (squatting), pushup, na mazoezi ya kutembea ni mazoezi mazuri sana kwako

Bila kufanya MAZOEZI AU BILA KUFUNGA KULA mwili utaendelea kuchagua SUKARI kama chanzo chake cha nguvu na mafuta yataendelea kujirundika mwilini bila kuwa na faida yoyote na hivyo kukuletea kitambi, manyama uzembe, upungufu wa nguvu za kiume na mwisho kukuletea tatizo la kisukari aina ya pili.

3. Chanzo cha tatu cha nguvu za mwili ni MAJI NA CHUMVI.

Hivi karibuni imegundurika kuwa, mwili unao uwezo wa kutengeneza nguvu kwa kutumia maji (hydroelectric energy), wakati maji peke yake yanapoingia kupitia kuta za seli na kuwasha pampu maalumu za majenereta ya kuzarishia nguvu yaitwayo kwa kitaalamu, ‘cation pumps’,.

Ni kama vile bwawa la umeme linapojengwa karibu na mto mkubwa.

Inajionyesha wazi sasa kwamba ubongo unategemea zaidi nguvu zitokanazo na umeme wa maji hasa katika mifumo yake ya usafirishaji kwenye neva zake kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Hivyo ni vigumu mtu kuishi bila mafuta, chumvi, wanga au sukari.

Chumvi hasa ninayotaka uwe unaitumia ni ile chumvi ya mawe hasa ya baharini ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt).

Unapokuwa katika upungufu wa maji (haunywi ya kutosha), unapokuwa hufanyi mazoezi ya viungo mara kwa mara na unakula vyakula vyenye chumvi kidogo au visivyo na chumvi kabisa, ‘automatikali’ ubongo utapandisha kiwango cha sukari kwenye damu yako.

Chanzo cha ugonjwa wa kisukari aina ya pili

Ukichunguza sana watu wa siku hizi utagunduwa vitu vifuatavyo;

  1. Wanakula sana vyakula vya wanga na protini
  2. Hawanywi maji ya kutosha kila siku kwa mjibu wa uzito wao
  3. Hawanywi maji mpaka wasikie kiu
  4. Hawatumii chumvi ya kutosha kwenye vyakula vyao
  5. Hawana muda wa kufanya mazoezi

Chanzo kikuu cha kisukari aina ya pili katika mwili wako ni aina ya nguvu uliyochagua kuitumia zaidi katika kuuendesha mwili wako.

ikiwa mwili una kiasi kidogo cha maji na chumvi, ikiwa hufanyi mazoezi ya viungo ubongo utakuwa unajiendesha kwa karibu ya aslilimia 100 kwa kutumia sukari.

Ikiwa utaanza kuwa bize na mazoezi kila mara, utakunywa maji ya kutosha kila siku na kutumia chumvi ya kutosha kwenye vyakula vyako, mwili utaacha kuchagua sukari kama chanzo chake kikuu cha nguvu na kuanza kuchagua mafuta na maji na chumvi kama vyanzo vyake vingine vya nguvu na ugonjwa wako wa kisukari utaishia hapo.

Ikiwa utahitaji dawa ya asili kwa ajili kutibu kabisa kisukari hasa kisukari aina ya pili, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Mimi napatikana Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke.

Soma hii pia > Usizidharau ishara hizi 8 za mwanzo za kisukari

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

Imesomwa mara 13

Let's block ads! (Why?)

Alhamisi, 14 Mei 2020

Usizidharau ishara hizi 8 za mwanzo za kisukari

Usizidharau ishara hizi 8 za mwanzo za kisukari

Kisukari kinaweza kujijenga pole pole katika mwili wako wakati mwingine bila hata wewe kufahamu nini kinaendelea.

Ni mhimu kwamba unapata elimu hii ya kuzitambuwa dalili za mwanzo za ugonjwa huu mbaya unaotesa mamilioni ya watu kote duniani ili uweze kuudhibiti kabla haijawa shida.

Hakuna dawa ya hospitali ya kuponya ugonjwa huu mpaka sasa. Wagonjwa hulazimika kutumia dawa za kupunguza makali kila siku miaka yao yote na dawa hizo hazitolewi bure.

Hizi ni ishara 8 za mwanzo za kukutokea ugonjwa kisukari aina ya pili.

Ikiwa unatokewa na dalili 2 au 3 au hata zaidi kati ya hizi ni wakati muafaka kufanya kipimo cha kisukari na kuchukuwa hatua za kujikinga kabla hali haijawa mbaya.

Soma hii pia > Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili

Dalili za kisukari

Usizidharau ishara hizi 8 za mwanzo za kisukari

1. Kuongezeka kwa kiu

Ukiwa na sukari nyingi kwenye mzunguko wako wa damu inamaanisha figo zako zitalazimishwa kufanya kazi zaidi ya kuchuja hiyo sukari.

Kiwango hicho cha juu cha sukari kwenye damu kinaweza kuzipa kazi za ziada figo na kukusababishia wewe kukojoa mara nyingi ili kuiondoa sukari iliyozidi mwilini.

Matokeo yake ni kuwa utapatwa na kiu iliyozidi kawaida na unaweza ukapungukiwa maji siku nzima.

Ikiwa unajisikia kupatwa na kiu mara kwa mara hata kama unakunywa maji mengi jaribu kupunguza kiasi cha sukari kwenye vyakula vyako na umuone daktari kwa uchunguzi zaidi.

2. Kukojoa mara kwa mara

Kiu iliyozidi na kukojoa mara kwa mara ni vitu vinavyoenda pamoja linapokuja suala la dalili za mwanzo za kisukari.

Sukari iliyozidi kwenye mzunguko wako wa damu ambayo haiwezi kuchujwa na figo hulazimishwa kutoka nje kupitia mkojo.

Kukojoa mara kwa mara wakati wa mchana hata nyakati za usiku ni dalili za ukaidi wa insulini.

3. Uchovu usioisha

Kisukari huleta uchovu kwa namna mbili.

Namna ya kwanza kisukari huleta uchovu ni matokeo ya upungufu wa maji mwilini kitendo ambacho huleta uchovu sugu.

Namna ya pili kisukari huingilia na kuathiri namna mwili wako unavyotumia damu sukari (glukozi) kwa ajili ya kutengeneza nguvu ya mwili.

Uchovu usioisha hata baada ya kuwa umepata usingizi mzuri usiku ni moja kati ya ishara kuu za mwanzo za wewe kuanza kupatwa na ugonjwa wa Kisukari.

4. Kuchelewa kupona vidonda

Ikikutokea ukapatwa na kidonda sehemu yoyote ya mwili unaweza kuona unachelewa sana kupona tofauti na wengine nah ii ni ishara pia ya mwanzo ya ugonjwa wa Kisukari.

Sukari inapozidi mwilini huishusha kinga yako ya mwili na hivyo mwili kuwa na uwezo mdogo wa kujitibu.

Hii ndiyo sababu unapotaka kuongeza kinga yako ya mwili unashauriwa pia uache kunywa soda na juisi zote za dukani na upunguze pia matumizi ya sukari.

Watu wengi wanaoumwa kisukari wanaumwa pia shinikizo la juu la damu.

Shinikizo la juu la damu ni ugonjwa ambao husababisha mishipa ya damu kujikaza au kujipunguza ukubwa wa kipenyo chake kama matokeo ya kupungua kwa mzunguko wa kimiminika mwilini jambo ambalo hufanya uponyaji wa vidonda kuchukuwa muda mrefu.

5. Kupungua kwa uwezo wa macho kuona

Kisukari kitakuweka kwenye njia panda linapokuja suala la uwezo wa macho yako.

Kwa vile shinikizo la juu la damu linaweza kudhuru mishipa ya damu basi mishipa hiyo baadhi yake ndiyo hupeleka damu kwenye macho na kudhurika kwa mishipa hiyo maana yake macho hayawezi kupata viinilishe mhimu kwa ajili yaw ewe uweze kuona vizuri.

Kwahiyo kutoona vizuri, uwezo wa macho kuona kupungua, kuona maluweluwe, kuona vitu viwili katika kimoja, kutoona mbali, mtoto wa jicho na kadharika ni matatizo ya macho ambayo ni dalili za mwanzo za kisukari usizotakiwa kuzipuuza.

Ikiwa umeanza kuona matatizo kwenye uwezo wako wa macho inafaa uonane na daktari haraka kwa uchunguzi zaidi ili kuzuia kuendelea zaidi kwa kisukari mwilini mwako.

Kwa bahati nzuri ni kuwa unapochukuwa hatua za mapema kuzuia, kujikinga na kutibu kisukari unakuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia matatizo ya kuona yanayoweza kupelekea upofu na kuweka sawa usawa wa sukari mwilini mwako.

6. Kubadilika kwa mudi yako

Insulini ni homoni ambayo inafanana kazi zake na homoni zingine kama estrogen, testosterone, na homoni zinazoshugulika na masuala ya njaa (leptin and ghrelin).

Wakati mwili wako unapoacha kutengeneza au kutumia insulini kama inavyotakiwa homoni zako zinaweza kuvurugika na kukuletea mabadiliko ya namna unavyojisikia (mood wings), kujisikia vibaya, kukuletea msongo wa mawazo nk

Ikiwa utaanza kula vizuri, kuwa bize na mazoezi na kudhibiti sukari yako kwa dawa lishe au mitishamba ambazo ni rafiki kwa afya utaanza kuona hali yako ya kujisikia vibaya au tofauti na ulivyokuwa mwanzo inatulia na unarudi kuwa mtu wa kawaida pole pole.

7. Ganzi sehemu mbalimbali mwilini

Ganzi miguuni, mikononi, miguu kuwaka moto na kuchoma choma ni dalili za mwanzo za kisukari.

Watu wanaosumbuliwa na kisukari mara nyingi hupatwa na ganzi.

Ni ishara mishipa yako ya damu haiwasiliani sawa sawa kama mwanzo. Ni ishara sumu na asidi vimezidi mwilini kama matokeo ya sukari kuzidi.

Ikiwa ganzi ni shida katika mwili wako jaribu kufanya kipimo cha kisukari mapema.

Soma hii pia > Dawa ya kuondoa ganzi mwilini

8. Kupenda vyakula na vinywaji vitamu

Kisukari kinaweza kukuletea hamu au kiu ya kutaka kula au kunywa vitu vitamu vitamu kutokana na sababu mbalimbali.

Kwa mfano msongo wa mawazo na kubadilika kwa mudi yako  kama matokeo ya kuvurugika kwa homoni zako kunaweza kukupelekea wewe kupenda vitu vitamu kama soda, chokoleti, pipi nk

Jambo hilo hilo la kuvurugika kwa homoni zako linaweza pia kuvuruga homoni yako inayohusika na masuala ya njaa na kukuletea wewe hamu ya kupenda zaidi kula vyakula feki kama chipsi na vyakula vingine vya kwenye makopo (vya dukani na viwandani).

Vile vile ukaidi wa insulini (insulin resistance) kama matokeo ya kisukari unaweza kukuletea wewe tamaa ya kutaka kula kupita kiasi vyakula vya wanga na vyenye utamu ambavyo haraka sana vitapandisha kiasi cha sukari mwilini mwako.

Ikiwa umekuwa unapata hamu sana ya kutaka kula au kunywa vyakula na vinywaji vitamu siku za karibuni nakushauri uweke miadi (appointment) ya kuonana na daktari haraka iwezekanavyo kufanya uchunguzi juu ya uwezekano wa wewe kuwa na kisukari.

Uonapo dalili hizo usizichukulie poa. Chukua hatua mapema kabla hali haijawa mbaya Zaidi.

Ikiwa utahitaji dawa ya asili kwa ajili kutibu kabisa kisukari hasa kisukari aina ya pili, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Mimi napatikana Victoria Home Remedy ipo Sigara Yombo Vituka Temeke. Kama upo Dar Es Salaam

Soma na hii pia > Madhara zaidi ya Kisukari katika mwili

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Usizidharau ishara hizi 8 za mwanzo za kisukari Click To Tweet

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

Imesomwa mara 1

Let's block ads! (Why?)

[unable to retrieve full-text content]

Jumapili, 10 Mei 2020

Sababu za wanaume kukosa hamu ya tendo la ndoa

SABABU ZA WANAUME KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA

Ni matumaini yangu umzima wa afya

Leo katika mada yangu hii, nataka kuzungumzia zaidi sababu za wanaume wengi kukosa hamu ya tendo la ndoa.

Kama ilivyo matatizo mengine, tatizo la kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa huwakumba na wanaume vilevile ila siyo kwa kiwango kikubwa kama ilivyo kwa wanawake.

Katika makala haya, tutaangalia kwa kina sababu za tatizo hili kwa wanaume na athari zake.

Mwili wa mwanadamu uliumbwa na matamanio na si mabaya kama mwenye mwili atakuwa na uwezo wa kujitawala.

Wanaume wengi huvutiwa zaidi na hisia za kushiriki tendo la ndoa kwa kuona baadhi ya maungo kwa wanawake, kusikia sauti na hata migusano.

Kuna wanaume ambao wapo tu, ilimradi siku zinakwenda, hawapati hamu ya kushiriki tendo la ndoa na wanajiona kama ndiyo wamefanikiwa kujitawala, kumbe ni wagonjwa.

Habari njema ni kwamba, licha ya tatizo hilo kuwasumbua wengi, kuna mambo unayoweza kuyafanya kupunguza ukubwa wa tatizo hili au kuliondoa kabisa kwa kutumia mimea tiba na matunda tiba.

Unachotakiwa kufanya, kama umejaribu kutumia njia mbalimbali kuondoa tatizo hili bila mafanikio, basi wahi mapema kwa wataalamu ukafanyiwe uchunguzi.

Baadhi ya wanaume wanamini kuwa, hamu ya kufanya tendo la ndoa inapungua kadiri umri wa mwanaume unavyoongezeka. Kuna idadi kubwa ya wanaume ambao hamu yao ya kufanya tendo la ndoa imebaki vilevile hata umri wao kuwa mkubwa.

UKUBWA WA TATIZO KATIKA JAMII

Kwanza tuanze kwa kutazama ukubwa wa tatizo hili. Idadi ya wanaume wanaoridhika kuishi na tatizo hili ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya wanawake.

Hata hivyo, tatizo la wanaume kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa limekuwa ni chanzo kikubwa katika kuleta migogoro katika familia.

Wanaume kwa kawaida ni wabishi na huwa hawapendi kuaibika hivyo mtu anaweza akawa na tatizo lakini asipende mwenza wake ajue kama analo ambapo kumbe kama angeliweka bayana angepata ushauri wa namna ya kulitatua.

Pamoja na kwamba tatizo hili halijitokezi sana kwa wanaume ukilinganisha na wanawake, inakadiriwa kuwa asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wana tatizo hili. Ni sawa na uwiano wa mwanaume mmoja mwenye tatizo hili katika kila wanaume sita au saba. Idadi ya wanawake wenye tatizo hili ni mara mbili ya wanaume.

WANAUME WANAKEREKA ZAIDI

Tatizo hili huwakera zaidi wanaume kuliko wanawake kwa sababu wanaume huchukulia urijali kama sehemu ya ukamilifu wa mwanaume na wanakosa raha wanapoona wana upungufu kuhusu mambo ya mapenzi tofauti na wanawake.

Kukosa hamu ya tendo la ndoa

SABABU AU CHANZO KIKUU CHA TATIZO

Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa wanaume linaweza kusababishwa na vitu vingi.

Sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile, kisaikolojia au za mchanganyiko wa vitu hivyo viwili. Hebu tuone baadhi ya vyanzo vya tatizo hili.

1. Ugomvi baina ya wanandoa

Uhusiano kati ya mwanaume na mwanamke ambao ni wanandoa una mchango mkubwa katika kujenga au kubomoa matamanio ya mwanaume.

Kama kutakuwa na matatizo ya uhusiano kama vile ugomvi kati ya wawili hao, kuna mchango mkubwa katika kusababisha tatizo la mwanaume kukosa hamu ya tendo la ndoa.

Ni vyema ukajihoji kama uhusiano wako na mwenza wako upo sawasawa.

Soma hii pia > Jinsi ya kuacha punyeto

2. Kuzoeana

Mara nyingine mwanaume anaweza akawa katika uhusiano kwa muda mrefu kiasi ambacho amemzoea mwanamke hali inayosababisha mwanaume huyo kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Hili nalo hutokea mara nyingi.

3. Madawa ya kulevya

Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia huweza kuleta tatizo hili la mwanaume kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Madawa yanayochangia tatizo hili ni ya High blood pressure, ya kuondoa msongo wa mawazo, yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa Testosterone. Mfano, Cimetidine, Finasteride na Cyproterone.

4. Kuvurugika kwa homoni

Tumeshaona kuwa, upungufu wa homoni inayoitwa Testosterone inasababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Matatizo mengine katika mfumo wa homoni huchangia tatizo hili.

Kama Thyroid haitoi homoni za kutosha, tatizo hili huweza kutokea ingawa mchango wa Thyroid katika tatizo hili ni mdogo sana.

Thyroid ni tezi ya kuzalisha homoni iliyopo katika eneo la shingo.

5. Umri

Kiwango cha Testosterone katika mwili wa mwanaume hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadiri anavyozidi kuwa na umri mkubwa.

Mara nyingi kuanzia miaka 50 na kuendelea. Homoni ya msingi sana kuhusiana na masuala ya mapenzi huitwa Testosterone.

Kwa mwanaume homoni hii hutolewa kwa kiwango kikubwa na korodani na kwa mwanamke hutolewa na Ovari.

Homoni ikipungua katika mwili wa binadamu, humfanya apoteze hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Kiwango cha Testosterone kikishuka sana katika mwili wa mwanaume huyu humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.

6. Uchovu

Wakati mwingine uchovu husababisha mwanaume kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Na ikiwa mwanaume atasongwa na shughuli nyingi zinazochosha mwili, hamu ya kushiriki tendo la ndoa huanza kupungua na ikizidi, baadaye mwanaume atakosa kabisa hamu ya kushiriki tendo na atahitaji uangalizi mkubwa ili arejee katika hali ya kawaida.

Vilevile kukosa mpango mzuri wa shughuli zako za kila siku na kujaribu kulazimisha kufanya mapenzi katikati ya ratiba yako iliyojaa huchangia kukosa hamu ya kufanya tendo.

Soma hii pia > Jinsi uchovu sugu unavyoleta upungufu wa nguvu za kiume

7. Msongo wa mawazo (stress)

Msongo ni ugonjwa wa hali ya kuwa na mawazo makali ya muda mrefu ya kukukosesha raha hali inayosababisha kushindwa kuyafanya mambo yako ya kawaida kiufanisi.

Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha pamoja na matamanio yako ya kimapenzi.

Soma hii pia > Namna msongo wa mawazo unavyoleta tatizo la kuwahi kufika kileleni

Mjulishe rafiki yako kwenye twitter naye asome ujumbe huu kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Sababu za wanaume kukosa hamu ya tendo la ndoa Click To Tweet

Share post hii na wengine uwapendao

Imesomwa mara 59

Let's block ads! (Why?)

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...