Translate

Alhamisi, 29 Agosti 2019

091-Aayah Na Mafunzo: Mtu Wa Motoni Atatamani Kufidia Dhahabu Ya Ujazo Wa Duniani

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Mtu Wa Motoni Atatamani Kufidia Dhahabu Ya Ujazo Wa Duniani

 

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Taa'alaa):

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾

91. Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao dhahabu ya ujazo wa dunia nzima lau wakitaka kujifidia nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru.

 

 

Mafunzo:

 

Anas (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ataitwa mtu katika watu wa Jannah, kisha Allaah Atamuuliza: Ee mwana Aadam! Umeonaje makazi yako? Atasema: Yaa Rabb! Hakika ni makazi bora kabisa. Allaah Atasema: Omba na tamani (utakalo)! Atasema: Hakuna ninaloomba au kutamani isipokuwa Unirudishe duniani nipigane katika njia Yako mara kumi – kutokana fadhila anazoziona za waliokufa mashahidi. Kisha ataletwa mtu katika watu wa motoni Atasema: Ee mwana Aadam! Umeonaje makazi yako? Atasema: Yaa Rabb! Makazi maovu kabisa! Atasema: Je, unataka kufidia Kwangu dhahabu kwa ujazo wa dunia nzima? Atasema: Naam ee Rabbi! Atasema: Umeongopa! Kwani Nilikuomba la chini kuliko hilo na jepesi zaidi wala hukufanya! Atarudishwa motoni.” [Ahmad, As-Silsilah Asw-Swahiyhah (3008), Swahiyh Al-Jaami’ (7996)].

 

 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...