أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
058-Suwrah Al-Mujaadalah: Aayah 14
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ تَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مَّا هُم مِّنكُمْ وَلَا مِنْهُمْ وَيَحْلِفُونَ عَلَى الْكَذِبِ وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴿١٤﴾
14. Je, hukuona wale waliofanya urafiki na watu ambao Allaah Ameghadhibika nao, wao si miongoni mwenu na wala si miongoni mwao na wanaapia uongo nao wanajua.
أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٥﴾
15. Allaah Amewaandalia adhabu kali, hakika uovu ulioje waliyokuwa wakiyatenda.
Sababun-Nuzuwl:
ثنا محمد بن جعفر ثنا شعبة عن سماك بن حرب عن سعيد بن جبير عن ابن عباس قال: قال رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم: "يدخل عليكم رجل ينظر بعين شيطان أو بعيني شيطان". قال فدخل رجل أزرق فقال: يا محمد علام سببتني أو شتمتني أو نحو هذا قال وجعل يحلف، قال: ونزلت هذه الآية في المجادلة ((وَيَحْلِفُونَ عَلَى الْكَذِبِ وَهُمْ يَعْلَمُونَ)) والآية الأخرى.
Ametuhadithia Muhammad bin Ja’far, ametuhadithia Shu’bah toka kwa Simaak bin Harb toka kwa Sa’iyd bin Jubayr toka kwa Ibn ‘Abbaas amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atawajieni mtu anayeangalia kwa jicho la shaytwaan au macho mawili ya shaytwaan)). Akasema: Akaingia mtu wa kibuluu akasema: Ee Muhammad! Umenitukania nini au umenitusia nini, au mfano wa hivi. Akasema: Akaendelea kuapa, na ikashuka Aayah hii katika Al-Mujaadalah:
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ تَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مَّا هُم مِّنكُمْ وَلَا مِنْهُمْ وَيَحْلِفُونَ عَلَى الْكَذِبِ وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴿١٤﴾
Je, hukuona wale waliofanya urafiki na watu ambao Allaah Ameghadhibika nao, wao si miongoni mwenu na wala si miongoni mwao na wanaapia uongo nao wanajua.
أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٥﴾
Allaah Amewaandalia adhabu kali, hakika uovu ulioje waliyokuwa wakiyatenda.
Hadiyth hii ameitaja vile vile katika ukurasa wa 267 na ukurasa 350. Al-Haythamiy amesema katika Majma’u Az Zawaaid kuwa Ahmad na Al-Bazzaar wameisimulia, na wapokezi wake wote ni watu wa kuaminika wasio na shaka yoyote, lakini katika Hadiyth hii inaeleza kuwa Rasuli ndiye aliyemwambia (mtu huyo): ((Unanitukania nini wewe na wenzako?)) [Al-Musnad ukurasa wa 267 na 350. Al-Haakim ameikhariji katika Al-Mustadrak katika mjeledi wa pili ukurasa wa 482. Amesema: Hii ni Hadiyth Swahiyh kwa sharti ya Muslim, na wao hawakuikhariji, na Ibn Jariyr katika mjeledi wa pili ukurasa wa 25]
Katika Muwattwa Maalik: Kitaab An Nudhuwr Wal Iymaan:
حَدَّثَنِي يَحْيَى، عَنْ مَالِكٍ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ، أَنَّهَا كَانَتْ تَقُولُ لَغْوُ الْيَمِينِ قَوْلُ الإِنْسَانِ لاَ وَاللَّهِ بَلَى وَاللَّهِ . قَالَ مَالِكٌ أَحْسَنُ مَا سَمِعْتُ فِي هَذَا أَنَّ اللَّغْوَ حَلِفُ الإِنْسَانِ عَلَى الشَّىْءِ يَسْتَيْقِنُ أَنَّهُ كَذَلِكَ ثُمَّ يُوجَدُ عَلَى غَيْرِ ذَلِكَ فَهُوَ اللَّغْوُ . قَالَ مَالِكٌ وَعَقْدُ الْيَمِينِ أَنْ يَحْلِفَ الرَّجُلُ أَنْ لاَ يَبِيعَ ثَوْبَهُ بِعَشَرَةِ دَنَانِيرَ ثُمَّ يَبِيعَهُ بِذَلِكَ أَوْ يَحْلِفَ لَيَضْرِبَنَّ غُلاَمَهُ ثُمَّ لاَ يَضْرِبُهُ وَنَحْوَ هَذَا فَهَذَا الَّذِي يُكَفِّرُ صَاحِبُهُ عَنْ يَمِينِهِ وَلَيْسَ فِي اللَّغْوِ كَفَّارَةٌ . قَالَ مَالِكٌ فَأَمَّا الَّذِي يَحْلِفُ عَلَى الشَّىْءِ وَهُوَ يَعْلَمُ أَنَّهُ آثِمٌ وَيَحْلِفُ عَلَى الْكَذِبِ وَهُوَ يَعْلَمُ لِيُرْضِيَ بِهِ أَحَدًا أَوْ لِيَعْتَذِرَ بِهِ إِلَى مُعْتَذَرٍ إِلَيْهِ أَوْ لِيَقْطَعَ بِهِ مَالاً فَهَذَا أَعْظَمُ مِنْ أَنْ تَكُونَ فِيهِ كَفَّارَةٌ .
Amenihadithia Yahyaa toka kwa Maalik toka kwa Hishaam bin ‘Urwah toka kwa baba yake toka kwa ‘Aaishah Mama wa Waumini kwamba alikuwa anasema: “Laghwu Al-Yamiyn”, ni mtu kusema: “Laa Wa-Allaahi, Balaa Wa-Allaahi” Maalik kasema: Zuri zaidi nililolisikia kuhusiana na hili ni kuwa “Al-Laghw” ni kiapo cha mtu juu ya kitu ambacho ana uhakika kuwa kiko hivyo kisha kinakutwa kinyume na hivyo, basi hiyo ni “Al-Laghwu”. Maalik kasema: Na kufunga kiapo ni mtu kuapa kuwa hatouza nguo yake kwa dinari kumi, kisha akaiuza kwa bei hiyo, au kuapa kuwa lazima atampiga kijana wake, kisha asimpige na mfano wa hivi. Kiapo hichi ndicho ambacho mwapaji hukitolea kafara, lakini katika “Al-Laghw” hakuna kafara. Maalik amesema: Ama yule anayeapia kitu naye anajua kuwa ni mwenye kufanya dhambi, na anaapia la uongo huku anajua ili kumridhisha kwao mtu, au kuomba udhuru kwao kwa mkosewa, au kudhulumu kwao mali, basi hiki ni kikubwa zaidi kuweza hata kuwa na kafara ndani yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni