أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
054-Al-Qamar Aayah 1 -2
Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى):
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿١﴾
Saa imekaribia na mwezi umepasuka.
وَإِن يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ ﴿٢﴾
Na wanapoona Aayah (ishara, dalili) hukengeuka na husema: Sihiri inayoendelea [Al-Qamar: 1-2]
Sababun-Nuzuwl:
عَنْ أَنَسٍ، قَالَ سَأَلَ أَهْلُ مَكَّةَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم آيَةً فَانْشَقَّ الْقَمَرُ بِمَكَّةَ مَرَّتَيْنِ فَنَزَلَت: ((اقتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانْشَقَّ الْقَمَرُ)) إِلَى قَوْلِهِ : ((سحْرٌ مُسْتَمِرٌّ)) يَقُولُ ذَاهِبٌ . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ .
Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba watu wa Makkah walimuomba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) awaletee Aayah (Ishara, muujiza), basi mwezi ukapasuka Makkah mara mbili (Yaani sehemu mbili), kisha ikateremka:
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿١﴾
Saa imekaribia na mwezi umepasuka
Mpaka kauli Yake:
سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ
Sihiri inayoendelea [Al-Qamar: 1-2]
Yaani Sihiri (Uchawi) inayootoweka.
[Amesema Abuu ‘Iysaa (at-Tirmidhiy) Hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Pia,
عن ابن عباس رضي الله عنهما قال كسف القمر على عهد رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم فقالوا: سحر القمر، فنزلت ((اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانْشَقَّ الْقَمَرُ، وَإِنْ يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُسْتَمِرٌّ))
Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba mwezi ulipatwa katika zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) basi (makafiri) wakasema: “Sihiri (uchawi) unaoendelea.” Ikateremka:
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿١﴾
Saa imekaribia na mwezi umepasuka.
وَإِن يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ ﴿٢﴾
Na wanapoona Aayah (ishara, dalili) hukengeuka na husema: Sihiri inayoendelea [Al-Qamar: 1-2]
[Atw-Twabaraniy na Al-Haafidhw Ibn Kathiyr amesema katika Al-Bidaayah Wan-Nihaayah: Isnaad yake ni Jayyid]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni