Aayah Na Mafunzo
Aal-‘Imraan
Tawbah Baada Ya Kuritadi Inakubalika
Anasema Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa):
كَيْفَ يَهْدِي اللَّـهُ قَوْمًا كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُوا أَنَّ الرَّسُولَ حَقٌّ وَجَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٦﴾
86. Vipi Allaah Atawaongoza watu waliokufuru baada ya kuamini kwao na wakashuhudia kwamba Rasuli ni haki na zikawajia hoja bayana? Na Allaah Hawaongozi watu madhalimu.
أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُمْ أَنَّ عَلَيْهِمْ لَعْنَةَ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿٨٧﴾
87. Hao jazaa yao ni kwamba juu yao ipo laana ya Allaah na ya Malaika na ya watu wote.
خَالِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٨٨﴾
88. Wenye kudumu humo hawatopunguziwa adhabu wala hawatopewa muda wa kuakhirishwa adhabu.
إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٨٩﴾
89. Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengenea, basi hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.
Mafunzo:
Aayah hizi (3: 86-89) ziliteremka kuhusu mtu mmoja katika Answaar ambaye alisilimu kisha akaritadi na akaingia katika shirki kisha akajuta kwa hilo tendo lake la kuritadi. Akatuma watu wake ili wamtumie ujimbe wa swali kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa je, hivi anaweza kuleta tawbah kwa tendo lake hilo? Kisha baada ya swali hilo kuulizwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) zikateremka hizo Aayaat, akatumiwa, akasilimu [Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) imepokelewa aathaar hii na Ibn Jariyr, na pia imesimuliwa na Ahmad, Ibn Hibbaan na wengineo na ameiwafiki Adh-Dhahabiy na Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah (3066)].
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni