from Uislamu Wangu https://ift.tt/2H7atae
via IFTTT

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
08-Swalaah Zetu Hazitimii Ila Baada Kutamka Shahada Mbili Na Kumswalia
Katika Swalaah zetu tunapokaa kikao cha Tashahhud, huwa tunamtaja Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kushuhudia kwamba yeye ni Rasuli wa Allaah na kisha tunamswalia kwa kutamka Swalaah inayojulikana kwa ni Swalaatul-Ibraahimiyyah. Kikako cha Tashahhud ni mojawapo ya nguzo za Swalaah ambayo bila ya kufanya hivyo, Swalaah haitimii.
Tunavyotamaka tashahhud na aina za kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
التَّحِيّـاتُ للهِ وَالصَّلَـواتُ والطَّيِّـبات، السَّلامُ عَلَيـكَ أَيُّهـا النَّبِـيُّ وَرَحْمَـةُ اللهِ وَبَرَكـاتُه، السَّلامُ عَلَيْـنا وَعَلـى عِبـادِكَ الصَّـالِحـين، أَشْـهَدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ الله، وَأَشْـهَدُ أَنَّ مُحَمّـداً عَبْـدُهُ وَرَسـولُه
At-tahiyyaatu liLLaahi, was-swalawaatu, wat-twayyibaatu, Assalaamu ‘alayka ayyuhan-Nnabiyyu warahmatu-Allaahi wa Barakaatuh, Assalaamu ‘alaynaa wa ’alaa ‘IbaadiLLaahis-swaalihiyn. Ash-hadu an-laa ilaaha illa-Allaah wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu
Maamkuzi mema na Rehma na mazuri yote (ni kwa Allaah), amani ziwe juu yako ee Nabiy na Rehma za Allaah na Baraka Zake, amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allaah walio wema. Nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Rasuli Wake. [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (2/311), Muslim (1/301)]
اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـد وَعَلـى آلِ مُحمَّد كَمـا صَلَّيـتَ عَلـى إبْراهـيمَ وَعَلـى آلِ إبْراهـيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد، اللّهُـمَّ بارِكْ عَلـى مُحمَّـد وَعَلـى آلِ مُحمَّـد كَمـا بارِكْتَ عَلـى إبْراهـيمَ وَعَلـى آلِ إبْراهيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد .
Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Swallayta ‘alaa Ibraahiyma wa ‘alaa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd. Allaahumma Baarik ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa aali Muhammad, kamaa Baarakta ‘alaa Ibraahiyma wa ‘alaa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd.
Ee Allaah! Mswalie Muhammad, na jamaa wa Muhammad, kama Ulivyomswalia Ibraahiym na juu ya jamaa zake Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwenye Kusifika Mtukufu. Ee Allaah! Mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na juu ya jamaa zake Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwenye Kusifika Mtukufu. [Hadiyth ya Ka’ab bin ‘Ujrah (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/408)]
اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى أَزْواجِـهِ وَذُرِّيَّـتِه كَمـا صَلَّيْـتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم، وَبارِكْ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى أَزْواجِـهِ وَذُرِّيَّـتِه كَمـا بارِكْتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد
Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa azwaajihi wa dhurriyaatihi, kamaa Swallayta ‘alaa aali Ibraahiyma, wa Baarik ‘alaa Muhammad, wa ’alaa azwaajihi wa dhurriyaatihi, kamaa Baarakta ‘alaa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiyd
Ee Allaah! Mswalie Muhammad na wake zake na kizazi chake, kama Ulivyowaswalia jamaa zake Ibraahiym, na Mbariki Muhammad na wake zake na kizazi chake kama Ulivyowabariki jamaa zake Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwenye Kusifika Mtukufu. [Hadiyth ya Abu Humayd As-Saa’adiy Al-Mundhir (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/407), Muslim (1/306) na tamashi lake]

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
00-Miongoni Mwa Hayaa Zake Alistahi Maswahaabiyaat
Katika Kuwaelekeza Jinsi Ya Kutwaharisha Hedhi
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) alimstahi mwanamke aliyemjia kumuuliza swala la hedhi yake, basi kwa kusitahi, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifunika uso wake baada ya kumjibu mwanamke huyo. Hadiyth inaelezea:
عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ سَأَلَتِ امْرَأَةٌ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَيْفَ تَغْتَسِلُ مِنْ حَيْضَتِهَا قَالَ فَذَكَرَتْ أَنَّهُ عَلَّمَهَا كَيْفَ تَغْتَسِلُ ثُمَّ تَأْخُذُ فِرْصَةً مِنْ مِسْكٍ فَتَطَهَّرُ بِهَا . قَالَتْ كَيْفَ أَتَطَهَّرُ بِهَا قَالَ: ((تَطَهَّرِي بِهَا . سُبْحَانَ اللَّهِ)) . وَاسْتَتَرَ - وَأَشَارَ لَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ بِيَدِهِ عَلَى وَجْهِهِ قَالَ: قَالَتْ عَائِشَةُ وَاجْتَذَبْتُهَا إِلَىَّ وَعَرَفْتُ مَا أَرَادَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَقُلْتُ تَتَبَّعِي بِهَا أَثَرَ الدَّمِ . وَقَالَ ابْنُ أَبِي عُمَرَ فِي رِوَايَتِهِ فَقُلْتُ تَتَبَّعِي بِهَا آثَارَ الدَّمِ .
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Mwanamke alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) vipi kuoga kujitwaharisha baada ya kumaliza hedhi yake. Akataja kuwa alimfundisha vipi kuoga kisha akamwambia achukue kipande cha pamba aweke misk kwa ajili ya kujitwaharisha. Aksema: Vipi nijitwaharishe nacho? Akasema: ((Jitwaharishe nacho Subhaana Allaah!)) (Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akajifunika uso wake. Sufyaan bin ‘Uyaynah akaonyesha jinsi alivyojifunika uso wake. Akasema ‘Aaishah: Nikamvuta mwanamke kwangu kwani nilifahamu alivyokusudia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), nikasema: Pakaza pamba hiyo katika sehemu zenye athari ya damu. Na Ibn ‘Umar katika Hadiyth yake (ametaja maneno ya ‘Aaishah) Pakaza katika sehemu zenye athari ya damu. [Muslim]

Al-Baqarah
Matahadharisho Ya Ribaa Na Adhabu Zake
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿٢٧٨﴾
278. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na acheni yaliyobakia katika ribaa ikiwa nyinyi ni Waumini
Mafunzo:
‘Awn bin Abi Juhayf amehadithia kutoka kwa baba yake kuwa alinunua kijana (mtumwa) anayejua kuumika (hijaamah). Akasema: “Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amekataza (kuchukua) thamani ya damu (malipo yatokanayo na kuumika), na thamani ya mbwa, na chumo la malaya na amemlaani mla ribaa na muwakilishi wake na mtu anayechora (ngozi za watu kwa kutia rangi ndani yake na mchorajwi na mchonga vinyago.” [Al-Bukhaariy]
“Dirhamu ya ribaa anayokula mtu na huku anajua ni mbaya zaidi kuliko kuzini mara thelathini na sita.” [Ahmad]
“Ribaa ina milango 73 iliyo nyepesi na sahali ni mtu kumuoa mamake.” [Al-Haakim]
“Jiepusheni na mambo saba yenye kuangamiza… kula ribaa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
079-An-Naaziaat
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ﴿٤٢﴾
42. Wanakuuliza (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa lini kufika kwake?
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا ﴿٤٣﴾
43. Huna ujuzi wewe hata utaje lolote.
Ibn Jariyr (30/49) amesema: Amenihadithia Ya’quwb bin Ibraahiym amesema: Ametuhadithia Sufyaan bin ‘Uyaynah kutoka kwa Az-Zuhriy kutoka kwa ‘Urwah kutoka kwa ‘Aaishah amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliendelea kuulizia kuhusu Saa hadi Allaah Alipoteremsha:
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا ﴿٤٣﴾
43. Huna ujuzi wewe hata utaje lolote.
Hadiyth imepokewa na Al-Hakam katika Al-Mustadrak (1/5) na Abuu Nu’aym katika Al-Hilyah (7/314) na akasema Al-Hakam Hadiyth hii haikuwepo katika Asw-Swahihayn nayo ni mahfuwdhw Swahiyh juu ya sharti zao wawili. Na akasema ni Swahiyh kwa sharti zao na hawakuipokea kwa sababu Ibn ‘Uyaynah aliifanyia Irsaal kwa mwingine na Al-Khatwiyb (11/321).
Na Al-Haafidhw ameitaja Hadiyth hii ibn Abiy Haatim katika kitabu chake Al-‘Ilal, na akasema nimemsikia Aba Zur’ah na akataja Hadiyth ya Az-Zuhriy kutoka kwa ‘Urwah kutoka kwa ‘Aaishah amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliendelea kuuliza kuhusu Qiyaamah hadi ilipoteremka kwake:
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا ﴿٤٣﴾
43. Huna ujuzi wewe hata utaje lolote.
Na amesema Ibn Jariyr (رحمه الله) :Ametuhadithia Abuu Kurayb, ametuhadithia Waki’y kutoka kwa Ismaa’iyl kutoka kwa Twaariq bin Shihaab amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anaendelea kutaja mambo ya Qiyaamah hadi ilipoteremka:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ﴿٤٢﴾
42. Wanakuuliza (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa lini kufika kwake?
Hadi kauli yake:
مَن يَخْشَاهَا ﴿٤٥﴾
wa yule anayeikhofu.
Adh-Dhahabiy Al-Haythamiy (رحمه الله) amesema: Ameipokea Al-Bazaar na watu wake ni Swahiyh (7/133) kutoka katika Al-Majma’ na akasema Al-Hafidhw Ibn Kathiyr (رحمه الله) katika tafsiyr yake (2/273) baada ya kutaja kwake sanad na isnad hii ni nzuri na yenye nguvu.
Aayah Husika Za Asbaabun-Nuzwul:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ﴿٤٢﴾
42. Wanakuuliza (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa lini kufika kwake?
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا ﴿٤٣﴾
43. Huna ujuzi wewe hata utaje lolote.
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَاهَا ﴿٤٤﴾
44. Kwa Rabb wako ndio kuishia (ujuzi) wake.
إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخْشَاهَا ﴿٤٥﴾
45. Hakika wewe ni muonyaji wa yule anayeikhofu.
كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا ﴿٤٦﴾
46. Siku watakapoiona, watakuwa kama kwamba hawakubaki (duniani) isipokuwa jioni moja au mchana wake.

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)
Hadiyth Ya 10
Mja Atafufuliwa Kwa Kitendo Alichofariki Nacho
عَنْ جَابِرٍ (رضي الله عنه) قَال: قَالَ النَّبِيَّ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((يُبْعَثُ كُلُّ عَبْدٍ عَلَى مَا مَاتَ عَلَيْهِ)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) ambaye amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kila mja atafufuliwa katika hali aliyofia)) [Muslim]
Mafunzo Na Mwongozo
1. Hima ya kutenda mema na kubakia katika istiqaamah (kuthibitika katika Dini) ili kitendo cha mwisho kabla ya kufariki kiwe ni kitendo chema, na kiwe ni kiliwazo siku ya kufufuliwa. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٣٢﴾
Ambao Malaika huwafisha katika hali nzuri (Malaika) watasema: “Salaamun ‘Alaykum!” Amani iwe juu yenu ingieni Jannah kwa yale mliyokuwa mkitenda.” [An-Nahl (16: 32).]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٧﴾
Mwenye kutenda mema miongoni mwa wanamume au wanawake naye ni Muumin, Tutamhuisha uhai mzuri, na bila shaka Tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda. [An-Nahl 16: 97].
Na pia rejea: Al-Hijr (15: 99), Al-‘Imraan (3: 102).
2. Umuhimu wa kupata husnul-khaatimah (mwisho mwema) kabla ya kuaga dunia na sio kuwa katika maasi, khasa pale mtu anapofikia katika umri mkubwa, kwa sababu kuna hatari ya mtu kugeuka kutoka katika twaa’ah (utiifu) na taqwa na kuingia katika maasi kama ilivyothibiti katika Hadiyth:
عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم -وَهُوَ الصَّادِقُ الْمَصْدُوقُ: ((إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَمْ سَعِيدٍ؛ فَوَاَللَّهِ الَّذِي لَا إلَهَ غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُهَا. وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا)) رواه البخاري ومسلم
Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd (رضي الله عنه) ambaye amesema: “Ametusimulia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake). Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema. Wa-Allaahi naapa kwa Yule Ambaye hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye ‘amali za watu wa Jannah hadi ikawa baina yake na Jannah ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja wenu hufanya ‘amali za watu wa motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa Jannah akaingia Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah inayomalizikia: ((…’amali zinahesabika za mwisho)) [Al-Bukhaariy]
3. Kutahadhari kubakia katika taqwa na twaa’ah (utiifu) wa Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Anawajua vyema waja Wake na yaliyomo moyoni Naye ni Mweza wa kugeuza nyoyo zao pindi wanapomuasi. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿٢٤﴾
Enyi walioamini! Muitikieni Allaah na Rasuli Anapokuiteni kwenye yale yenye kukuhuisheni na jueni kwamba Allaah Anaingilia kati baina ya mtu na moyo wake; na kwamba Kwake mtakusanywa. [Al-Anfaal (8: 24)].
4. Umuhimu wa kuomba du’aa ya kuthibitika katika Dini mpaka kufariki. Nayo ni du’aa ambayo alikuwa akiiomba sana Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
اللَّهُمَّ يَا مُقَلِّبَ الْقُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِك
((Allaahuuma Yaa Muqallibal-Quluub Thabbit Qalbiy 'Alaa Diynik – Ee Allaah, ee Mgeuza nyoyo, Thibitisha moyo wangu katika Dini Yako)) [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan]
Na pia kuomba Du’aa ya Nabiy Yuwsuf (عليه السلام)
(اللَّهُمَّ) فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَنتَ وَلِيِّي فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ تَوَفَّنِي مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ ﴿١٠١﴾
(Ee Allaah) Muanzilishi wa mbingu na ardhi. Wewe ni Mlinzi, Msaidizi wangu duniani na Aakhirah. Nifishe hali ya kuwa Muislamu na Unikutanishe na Swalihina.” [Yuwsuf (12: 101)]
5. Hatari ya kutenda maasi yakaja kuwa ndio kitendo cha mwisho cha Muislamu, kwani mauti yanamfikia mtu bila ya taarifa, mfano kupatwa na ajali ukiwa katika kuendesha gari na huku unasikiliza muziki.
6. Kilicho muhimu ni ‘amali za mwisho, basi atakayefanya ‘amali zake kuwa ni bora katika uhai wake wa mwisho atapata bishara njema na kheri Siku ya Qiyaamah, na atakayefanya maovu katika uhai wake wa mwisho atakutana na shari huko Aakhirah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ ۖ فَأَلْقَوُا السَّلَمَ مَا كُنَّا نَعْمَلُ مِن سُوءٍ ۚ بَلَىٰ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٨﴾
Ambao Malaika huwafisha wakiwa wamejidhulumu nafsi zao, watasalimu amri (watasema): “Hatukuwa tukitenda uovu wowote.” (Wataambiwa): “Hapana! Hakika Allaah ni Mjuzi kwa yale mliyokuwa mkitenda.”
فَادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ فَلَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ﴿٢٩﴾
“Basi ingieni milango ya Jahannam ni wenye kudumu humo.” Ni uovu ulioje makazi ya wanaotakabari.
وَقِيلَ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا مَاذَا أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۚ قَالُوا خَيْرًا ۗ لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۚ وَلَدَارُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ ۚ وَلَنِعْمَ دَارُ الْمُتَّقِينَ﴿٣٠﴾
Na wanapoambiwa wale waliokuwa na taqwa: “Nini Ameteremsha Rabb wenu?” Husema: “Kheri.” Kwa wale waliofanya ihsaan katika dunia hii watapata hasanah (mazuri). Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi. Na uzuri ulioje nyumba ya wenye taqwa.
جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ لَهُمْ فِيهَا مَا يَشَاءُونَ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْزِي اللَّـهُ الْمُتَّقِينَ﴿٣١﴾
Jannaat za kudumu milele wataziingia humo, zipitazo chini yake mito. Watapata humo wayatakayo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyowalipa wenye taqwa.
الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٣٢﴾
Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema watasema: “Salaamun ‘Alaykum, (amani iwe juu yenu) ingieni Jannah kwa yale mliyokuwa mkitenda.” [An-Nahl (16: 28-32)]
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Anasema:
إِنَّ الْعَبْدَ لَيَعْمَلُ عَمَلَ أَهْلِ النَّارِ، وَإِنَّهُ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ، وَيَعْمَلُ عَمَلَ أَهْلِ الْجَنَّةِ، وَإِنَّهُ مِنْ أَهْلِ النَّارِ، وَإِنَّمَا الأَعْمَالُ بِالْخَوَاتِيمِ ".
((Hakika mja hutenda ‘amali za watu motoni lakini uhakika akaja kuwa ni mtu wa Jannah, na akaja kutenda ‘amali za watu wa Jannah lakini uhakika akaja kuwa mtu wa motoni. Hakika ‘amali zinahesabika za mwishoni)) [Al-Bukhaariy]
7. Kutochoka wala kulegea katika kufanya mema na kuacha kutenda maovu kwa sababu hakuna anayejua wakati gani atatembelewa na Malakul-Mawt (Malaika wa kutoa roho). Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ وَاخْشَوْا يَوْمًا لَّا يَجْزِي وَالِدٌ عَن وَلَدِهِ وَلَا مَوْلُودٌ هُوَ جَازٍ عَن وَالِدِهِ شَيْئًا ۚ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿٣٣﴾
Enyi watu! Mcheni Rabb wenu, na iogopeni Siku ambayo mzazi hatomfaa mwanawe na wala mwana hatomfaa mzazi wake chochote. Hakika ahadi ya Allaah ni haki; basi usikughururini uhai wa dunia, na wala (shaytwaan) mwenye kughuri asikughururini kuhusu Allaah.
إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾
Hakika Allaah Ana elimu ya Saa (Qiyaamah), na Anateremsha mvua na Anajua yale yaliyomo katika tumbo la uzazi na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Luqmaan 31: 33-34)]

Du’aa Za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Kutaraji Rahmah Ya Allaah Kuomba Utengenezewe Mambo Yako Yote
اللّهُـمَّ رَحْمَتَـكَ أَرْجـو فَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـيْن، وَأَصْلِـحْ لي شَأْنـي كُلَّـه لَا إِلَهَ إِلَّا أنْـت
Allaahumma Rahmatika arjuw falaa takilniy ilaa nafsiy twarfata ‘aynin, wa aswlih liy sha-aniy kullahu, laa ilaaha illaa Anta
Ee Allaah, nataraji rahmah Zako, usinitegemeze kwenye nafsi yangu japo kwa muda wa upepesa jicho, na Unitengenezee mambo yangu yote, hapana Muabudiwa wa haki ila Wewe
[Hadiyth ya Abu Bakr Nafiy’ bin Haarith Ath-Thaqafiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) - Abu Daawuwd (4/324) [5090], Ahmad (5/42), ameipa daraja ya Hasan Al-Albaaniy katika Swahiyh Abi Daawuwd (3/959) ]
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...